Saturday, February 21, 2015
UBWIRI UNGA - UGONJWA MKUU WA MIKOROSHO
Moja ya matatizo makubwa ya uzalishaji wa zao la korosho ni ugonjwa wa Ubwiri unga.Ugonjwa huu unasababishwa na vimelea aina ya uyoga (fungus) viitwavyo Oidium anacardii. Ugonjwa huu ni muhimu sana, kiasi kwamba kama haukuthibitiwa, unaweza kupunguza mavuno kwa zaidi ya asilimia 70. Ugonjwa huu umeenea katika mikoa yote inayolima zao hili Tanzania. Hapo awali ugonjwa huu ulikuwa unaitwa kwa jina la“ukungu” kutokana na uhusiano wake mkubwa na haliya hewa ya ukungu (litabwe kwa Kimakonde) unaoonekana alfajiri/asubuhi katika miezi ya Juni - Septemba. Hivyo basi, jina la Ubwiri unga linatumika sasa ili kuwawezesha wakulima wasichanganye vitu hivyo viwili.
MASHAMBULIZI
Ugonjwa huu unashambulia maeneo yote machanga na teketeke katika mti wa mkorosho, hasa machipukizi, majani, maua, mabibo na korosho changa (tegu). Athari kubwa ya ugonjwa huu inatokana na mashambulizi ya maua, ambayo hushindwa kufunguka na kuwezesha chavua kufanya kazi yake, hatimaye hunyauka na kukauka.
SUKUMA VUTA -Njia bora ya kupambana na kiwavi mshambulia mabua ya mahindi (maize stalk borer)
Kiwavi anayeshambulia mabua ya mahindi anajulikana pia kama maize stalk borer(Sesamia fusca) kiwavi huyu hutokana na vipepeo weupe wanao onekana kwenye mashamba ya mahindi, vipepeo hawa hutaga na baada ya mayai yao kuanguliwa ndipo viwavi hawa waharibifu hutokea na kuanza kushambulia mahindi shambani
Viwavi hawa hushambulia katikati ya mabua na kusababisha mmea kudumaa na kisha kufa, hali huwa mbaya zaidi kama mashambulizi yatatokea wakati mimea ikiwa bado michanga maana mkulima hatavuna kabisa katika mimea iliyoshambuliwa na pia hupunguza mavuno kwenye mimea iliyokomaa na kutoa mbelewele
Njia hii ya sukuma vuta ni njia yenye mafanikio kwa asilimia kupambana na viwavi hawa kama utafuata maelekezo kwa usahihi, na hii itakusaidia kupambana na viwavi hawa kwa njia ya kibaiolojia bila kutumia kemikali zozote shambani mwako
Ilikupambana na viwavi hawa waharibifu kwenye shamba lako la mahindi, panda mimea ya desmodium kila baada ya mistari mitano ya mahindi, desmodiuM husaidia kufukuzavipepeo na viwavi kutokana na harufu yake kali na wakati huo huo kuongeza nitrjeni kwenye udongo shambaniPanda majani aina ya napier kuzunguka shamba lako, kwani majani haya huwavutia pia vipepeo na viwavi hawa waharibifu, wakati desmodium inawafukuza nje ya shamba lako viwavi hawa, majani ya napier yanakuwa yanawavuta nje ya shamba lako na ndio maana njia hii ya kibaiolojia hiutwa SUKUMA VUTA
NG'OMBE ALIYE KWENYE JOTO - JINSI YA KUMTAMBUA
Kwa kawaida ng'ombe jike aliyebalehe huingia kwenye joto kila baada ya siku 14 - 24 au wastani wa siku 21 kama hatapandwa na kushika mimba, hii hutegemea na aina ya ng'ombe, mazingira, lishe na hali ya hewa. kuna masaa kati ya 6 - 10 kabla hajaingia vizuri kwenye joto (pre heat) na joto lenyewe huchukua kati ya masaa 4 - 30 pia kutegemeana na aina ya ng'ombe, mazingira, lishe na hali ya hewa na yai hupevuka kwa wastani wa masaa 10 - 12 baadae
Kama utataka kumpandisha ng'ombe jike wako kwa kutumia madume bora ya kuazima au kwa kutumia kupandisha kwa njia ya chupa, basi ni muhimu kuzijua dalili kuu ambazo huonekana ng'ombe jike anapokuwa kwenye joto, dalili hizi zinaweza kuonekana kabla ya joto, wakati wa joto ana hata baada ja joto kupita kidogo, kwa hiyo ni muhimu kuzitambua mara zinapoanza ili usiweze kupitiliza na kulikosa joto halisi
DALILI KUU
- Sehemu ya nje ya kizazi/uke huwa kubwa zaidi kama imeumuka na kutuna zaidi ya ile saizi yake ya kawaida.
- Sehemu ya nje ya kizazi/uke huwa na rangi nyekundu inayoelekea kukooza zaidi ya kawaida yake.
- Ute ute hutoka kwenye kizazi na huwa mzito wenye kunata nata.
- Ng'ombe huwa hatulii, mwenye kuzunguka zunguka na hata kulia lia zaidi ya kawaida yake.
- Ingawa ni jike lakini pia hujaribu kuyapanda majike mengine yaliyopo bandani, kana kuna mabanda mengine zaidi, ukimuhamisha hali hii ya kuwapanda wenzie hizi.
- Hunyanyua nyanyua mkia na kwenye ncha mkia huwa imevurugika (rough)
- Ukimgandamiza mgongoni kwa kutumia mikono sehemu ya nyuma kabisa karibu na mkia hutulia na kusikilizia kama anapandwa, mwanzo hatatulia ila ukifikia wakati sahihi atatulia na hapo ndipo unapoweza kumuwekea mbegu kwa njia ya chupa na kama unatumia dume lenyewe litatambua hali hii kwa hiyo ukiona dalili tu zinaanza mpeleke kwa dume na lenyewe litapanda kwa wakati sahihi.
KILIMO BORA CHA KARANGA
Karanga ni mojawapo ya mazao yanayotoa mafuta. Katika Tanzania zao hili hustawi zaid katika mikoa ya Kusini Mashariki, Dodoma na Morogoro. Pamoja na kutoa mafuta vile vile zao hutumika kwa njia nyingine mbali mbali, nazo ni pamoja na:
1. Chakula cha wanyama (Mashudu na majani)
2. Kurutubisha ardhi
3. Chakula cha binadamu (Confectionary)
Kwa ujumla zao hili hutumika na wakulima kama zao la biashara.
HALI YA HEWA
Karanga hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye miinuko chini ya mita 1500, toka usawa wa bahari katika Tanzania, na hustawi zaidi katika maeneo ambayo yanapata mvua za wastani wa mm 750 hadi mm 1200 kwa mwaka.
Vile vile karanga hustawi vizuri kwenye udongo wa kichanga, inashauriwa kutopanda karanga kwenye udongo mzito (mfinyanzi) hii ni kutokana na sababu kwamba, karanga hazistawi kwenye sehemu zinazo simama maji, na udongo mzito huleta hasara wakati wa uvunaji.
KILIMO BORA CHA VIAZI VITAMU
Watu wengi wamekuwa wakiulizia umuhimu wa madini kwenye udongo na namna ya asili ya kuongezea kosefu wa madini kama potasiam, fosforas, kalsiam na mengineyo, njia rahisi ya kuongeza baadhi ya madini kwenye udongo ni kwakutumia majivu
UMUHIMU
Majivu yanakiwango cha wastani wa madini kifuatacho potasiam 5% - 7%, kalsiam 25% - 50%, fosforas 1.5% - 2% na madini mengine kwa kiasi kidogo pia mabaki mabaki ya chenga za mkaa kwenye majivu pia yanasaidia kwenye kunyonya baadhi ya sumu kwenye ardhi, kumbuka mkaa ni kaboni halisi (pure carbon)
KIASI CHA KUTUMIA
Kiasi cha kilo 2.5 mpaka 5 kitumike kwenye eneo la mita za mraba 33 au futi 100 za mraba, na majivu yamwagwe wiki 3 - 4 kabla ya kupanda kitu chochote ardhini.
MADHARA
Kila kitu kikitumiwa zaidi ya kiasi kina madhara na majivu pia yana madhara kwenye udongo kwa sababu yana hali ya kuwa alkaline zaidi (10 - 12 pH) kwa sababu baadhi ya mchanganyiko wake hauyayuki kwenye maji, kama utahitaji kuongezea kwenye mimea yenye upungufu wa madini kama fosforas na potasiam basi hakikisha majivu hayagusi mashina kwani yanaweza kuuungua haya kama mimea ni michanga.
Pia majivu yanan kiasi kidogo sana cha naitrojeni ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya mmea wowote ule, kwa hiyo hakikisha pia unatumia vyanzo vingine kwa ajili ya naitrojeni, vyanzo kama mimea jamii ya mikunde, marejea, lukina, na alfal
-KILIMO BORA CHA MATUFAA - APPLES
Viazi vitamu ni moja kati ya mazao makuu ya mizizi nchini Tanzania ambalo hulimwa kwa ajili ya chakula. Zao hili ni moja kati ya mazao ya kinga ya njaa kutokana na sifa yake ya kuvumilia ukame. Zao la viazi vitamu, asilia yake ni Amerika ya Kati na ya Kusini. Nchini Tanzania, zao hili hulimwa zaidi katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Morogoro,Kagera,Arusha na Ruvuma.
Matumizi
Viazi vitamu hutumika kama chakula kwa kutayarishwa katika njia mbalimbali kama vichembe, na Matobolwa. Pia Unga wa viazi vitamu hutumika kutengeneza vyakula kama keki, maandazi, kalimati na tambi. Majani ya viazi huliwa kama mboga pia hutumika katika kutayarisha mboji.
Aina za viazi vitamu
Kuna aina nyingi za viazi vitamu zinazolimwa ulimwenguni. Hapa nchini Tanzania aina zinazolimwa zaidi ni Ukerewe, Simama, Kakamega, Karoti C, Mwananjemu, Ali mtumwa mayai, Mavuno, Pananzala, Kibakuli, Sinia,Vumilia na Polista
Uzalishaji
Zao hili hustawi maeneo mengi Nchini Tanzania. Viazi hustawi vizuri katika maeneo ya tambarare yenye udongo tifutifu, unaoruhusu maji kupenya kwa urahisi. Udongo wa mfinyazi na wenye kokoto nyingi haufai kwani huzuia mizizi kupenya na kupanuka.
Shamba jipya litayarishwe vizuri kwa kufyeka vichaka na kung’oa visiki. Majani yafukiwe wakati wa kutengeneza matuta ili kuongeza rutuba ya udongo.
Viazi vipandwe kwa kutumia Marando yenye urefu wa sentimita 30 kwa mavuno bora. Inashauriwa kutumia sehemu ya juu ya shina kwa mavuno zaidi. Marando yapandwe katika umbali wa sentimita 25 hadi 30 kutoka mmea hadi mmea na sentimita 60 hadi 75 kutoka tuta hadi tuta. Viazi pia vyaweza kupandwa kwa kutumia viazi vyenye afya vyenye uzito wa kati ya gramu 20 hadi 30. Hata hivyo inashauriwa kutumia marando ili kupata mavuno zaidi na kuepuka kuenea kwa magonjwa.
Kutunza shamba
Ni muhimu kupalilia viazi vitamu katika miezi miwili ya mwanzo ili kuupa mmea nguvu ya kutambaa vizuri. Baada ya muda huo, viazi huweza kufunika ardhi na hivyo huzuia uotaji wa magugu.
Viazi hushambuliwa na wadudu mbalimbali wakiwemo kipepeo, mbawa kavu, fukusi na minyoo fundo.Pia hushambuliwa na magonjwa yakiwemo magonjwa yanayotokana na virusi kama Sweet Potato Chlorotic Stunt virus (SPCSV). Magonjwa na wadudu yaweza kudhibitiwa kwa kuzingatia usafi wa shamba, kubadilisha mazao, na kuzingatia udhibiti sango.
Uvunaji
Viazi vitamu huwa tayari kuvunwa miezi mitatu hadi minne tangu kupanda kutegemea hali ya hewa. Viazi vinaweza kuvunwa kidogo kidogo kwa kutumia mikono, vijiti, jembe, au rato kadri vinavyohitajika. Aidha inashauriwa viazi visiachwe ardhini muda mrefu bila kuvunwa kwani vitakomaa sana na kuwa na nyuzi, na hivyo kuharibu ubora wake. Pia kuacha viazi muda mrefu hukaribisha mashambulizi ya wadudu kama fukusi na kuoza. Kwa maeneo makubwa zaidi, inashauriwa kutumia mashine ya kukokotwa na ng’ombe. Uvunaji ufanywe kwa uangalifu ili kuhakikisha viazi visikatwekatwe wala kuchubuliwa wakati wa kuvuna.
Mavuno ya viazi hutofautiana kulingana na aina, hali ya hewa, na udongo. Mavuno ya viazi yanakadiriwa kufikia tani 20 kwa hekta
Matumizi
Viazi vitamu hutumika kama chakula kwa kutayarishwa katika njia mbalimbali kama vichembe, na Matobolwa. Pia Unga wa viazi vitamu hutumika kutengeneza vyakula kama keki, maandazi, kalimati na tambi. Majani ya viazi huliwa kama mboga pia hutumika katika kutayarisha mboji.
Aina za viazi vitamu
Kuna aina nyingi za viazi vitamu zinazolimwa ulimwenguni. Hapa nchini Tanzania aina zinazolimwa zaidi ni Ukerewe, Simama, Kakamega, Karoti C, Mwananjemu, Ali mtumwa mayai, Mavuno, Pananzala, Kibakuli, Sinia,Vumilia na Polista
Uzalishaji
Zao hili hustawi maeneo mengi Nchini Tanzania. Viazi hustawi vizuri katika maeneo ya tambarare yenye udongo tifutifu, unaoruhusu maji kupenya kwa urahisi. Udongo wa mfinyazi na wenye kokoto nyingi haufai kwani huzuia mizizi kupenya na kupanuka.
Shamba jipya litayarishwe vizuri kwa kufyeka vichaka na kung’oa visiki. Majani yafukiwe wakati wa kutengeneza matuta ili kuongeza rutuba ya udongo.
Viazi vipandwe kwa kutumia Marando yenye urefu wa sentimita 30 kwa mavuno bora. Inashauriwa kutumia sehemu ya juu ya shina kwa mavuno zaidi. Marando yapandwe katika umbali wa sentimita 25 hadi 30 kutoka mmea hadi mmea na sentimita 60 hadi 75 kutoka tuta hadi tuta. Viazi pia vyaweza kupandwa kwa kutumia viazi vyenye afya vyenye uzito wa kati ya gramu 20 hadi 30. Hata hivyo inashauriwa kutumia marando ili kupata mavuno zaidi na kuepuka kuenea kwa magonjwa.
Kutunza shamba
Ni muhimu kupalilia viazi vitamu katika miezi miwili ya mwanzo ili kuupa mmea nguvu ya kutambaa vizuri. Baada ya muda huo, viazi huweza kufunika ardhi na hivyo huzuia uotaji wa magugu.
Viazi hushambuliwa na wadudu mbalimbali wakiwemo kipepeo, mbawa kavu, fukusi na minyoo fundo.Pia hushambuliwa na magonjwa yakiwemo magonjwa yanayotokana na virusi kama Sweet Potato Chlorotic Stunt virus (SPCSV). Magonjwa na wadudu yaweza kudhibitiwa kwa kuzingatia usafi wa shamba, kubadilisha mazao, na kuzingatia udhibiti sango.
Uvunaji
Viazi vitamu huwa tayari kuvunwa miezi mitatu hadi minne tangu kupanda kutegemea hali ya hewa. Viazi vinaweza kuvunwa kidogo kidogo kwa kutumia mikono, vijiti, jembe, au rato kadri vinavyohitajika. Aidha inashauriwa viazi visiachwe ardhini muda mrefu bila kuvunwa kwani vitakomaa sana na kuwa na nyuzi, na hivyo kuharibu ubora wake. Pia kuacha viazi muda mrefu hukaribisha mashambulizi ya wadudu kama fukusi na kuoza. Kwa maeneo makubwa zaidi, inashauriwa kutumia mashine ya kukokotwa na ng’ombe. Uvunaji ufanywe kwa uangalifu ili kuhakikisha viazi visikatwekatwe wala kuchubuliwa wakati wa kuvuna.
Mavuno ya viazi hutofautiana kulingana na aina, hali ya hewa, na udongo. Mavuno ya viazi yanakadiriwa kufikia tani 20 kwa hekta
Friday, February 20, 2015
Soya zao lenye manufaa lukuki kwa jamii
Soya zao lenye manufaa lukuki kwa jamii
Maharagwe ya soya ni moja ya mazao muhimu katika jamii ya mikunde katika nyanja za uzalishaji wa kibiashara kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha protini (35-40%). Soya inatumika katika kuandaa vyakula vinavyoliwa vikiwa vibichi, vinavyovundikwa na vyakula nikavu, mfano maziwa, tofu, mchuzi pamoja na kimea.
Hali ya hewa, udongo na maji
Soya hulimwa katika ukanda wa Ikweta. Soya hukomaa katika kipindi cha siku 180 (miezi 6) lakini inaweza kuwa na baadhi zinazokomaa mapema zaidi. Joto chini ya nyuzi joto 21 na juu ya 32 inaweza kuathiri ushavushaji na utengenezaji wa viriba. Na joto zaidi ya nyuzi 40 ni hasara kwa uzalishaji wa mbegu.
Endapo maji yanapatikana, Soya inaweza kulimwa kwa kipindi chote cha mwaka. Soya huhitaji milimita 400-500 za maji kwa msimu ili kupata mazao bora. Kiwango cha juu cha unyevu kinahitajika sana wakati wa kuota, kuchanua na kuunda viriba. Hata hivyo majira ya kiangazi ni muhimu kwa ajili ya kukomaza. Soya inaweza kuvumilia maji yaliyotuama lakini mvua ikizidi ni tatizo kubwa kwa uzalishaji wa mbegu.
ZIFAHAMU MBEGU BORA ZA MAHARAGE
Na. Josephine MkudeNi vema kwa wakulima kuzingatia mbegu bora katika kilimo ili kupata mazao bora yatakayowapa faida baada ya mavuno. Kituo cha Utafiti wa Kilimo Selian Arusha ambacho ni makao makuu ya utafiti ya kanda ya Kaskazini kwa miaka mingi imekuwa ikitafiti aina bora za maharage ambazo hutoa mazao mengi, ambazo pia zinastahimaaili ukame na magonjwa. Kwa kufuata kanuni bora za kilimo wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji wa zao la maharage kwa kutumia mbegu bora kama vile Jesica, Lyamungu na Selian. Mbegu hizi zimeshasambazwa kwa wakulima na wanazitumia kwa uzalishaji
KILIMO CHA MICHUNGWA NA MACHENZA
Ndugu Ali Kalufya alitaka kujua kwa kina ukuliama wa michungwa na jamii yake, aliuliza swali hili katika mtandao wa Dada Subi nami najaribu kumweleza haya...
Michungwa na Jamii yake hustawi zaidi ukanda wa pwani wenye joto kiasi, mvua nyingi na udongo wenye rutuba, kwa Tanzania mikoa kama Pwani, Dar es salaam, Tanga, Mtwara, Lindi, na Morogoro ni maarufu kwa kilimo hiki
MBEGU
Kwa kuanzia unakusanya mbegu za mlimao kutoka katika malimao yaliyokomaa na ikiwezekana yawe yameiva yakiwa mtini, kausha mbegu zake na kisha unaweza kutolea ganda la nje ili ziweze kuota vizuri.
KITALU
Mwaga mbegu zako kwenye kitali na uzifukie kwa udongo kiasi cha nusu sentimeta, mwagia maji kilasiku na baada ya wiki 3 - 6 mbegu zitaanza kuchipua,
MICHE YA MILIMAO TAYARI KWA KUUNGWA
Michungwa na Jamii yake hustawi zaidi ukanda wa pwani wenye joto kiasi, mvua nyingi na udongo wenye rutuba, kwa Tanzania mikoa kama Pwani, Dar es salaam, Tanga, Mtwara, Lindi, na Morogoro ni maarufu kwa kilimo hiki
MBEGU
Kwa kuanzia unakusanya mbegu za mlimao kutoka katika malimao yaliyokomaa na ikiwezekana yawe yameiva yakiwa mtini, kausha mbegu zake na kisha unaweza kutolea ganda la nje ili ziweze kuota vizuri.
KITALU
Mwaga mbegu zako kwenye kitali na uzifukie kwa udongo kiasi cha nusu sentimeta, mwagia maji kilasiku na baada ya wiki 3 - 6 mbegu zitaanza kuchipua,
MICHE YA MILIMAO TAYARI KWA KUUNGWA
WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA ZIARANI KATIKA JIMBO LA ISIMANI NA KALENGA MKOANI IRINGA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua matrekta madogo maarufu kwa jina la Power Tiller yanayotumika katika shamba la kilimo cha umwagiliaji la Magozi katika jimbo la Ismani wakati alipolitembelea shamba hilo akiwa katika ziara ya mkoawa Iringa Februari 19, 2015. Watatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza.
Thursday, February 19, 2015
UKOSEFU WA WATAALAMU MBALI MBALI KATIKA SEKTA YA KILIMO CHA MIWA NI KIKWAZO KIKUBWA KWA WAKULIMA WA MIWA KILOMBERO
UKOSEFU WA WATAALAMU MBALI MBALI TATIZO KWA WAKULIMA WA MIWA KILOMBEROUkosefu wa Wataalamu wa Uchumi , Mizani na Sheria ni baadhi ya changamoto zinazovikabili vyama vya Wakulima wa Miwa katika Bonde la Kilombero.Akizungumza katika mahojiano na mwandishi wetu Katibu wa Chama Cha Wakulima wa Miwa cha Msolwa Ujamaa (MUCGA) Modestus Chitemi amesema ili kuwezesha ongezeko la bei kwa Wakulima kwa Uwiano kama ilivyo kwa Nchi Jirani Wataalamu zaidi wanahitajika.Akitolea mfano wa Nchi ya Malawi, Bwana Chitemi amesema kuwa Wakulima wa Miwa waNchi hiyo wana uwiano wa kupata asilimia Sitini (60) wakati Viwanda vya Sukari vinapata asilimia Arobaini(40).Ameongeza kuwa kutokuwepo kwa mgao na Ruzuku ya pembejeo kutoka Serikalini katika zao la Miwa ingawa Mahitaji ya mbolea na dawa za magugu ni makubwa sana ni changamoto nyingine inayoikabili vyama vya Wakulima wa Miwa katika Bonde laKilombero
Mfanyakazi katika shamba la miwa akiendelea na zoezi la ukataji miwa..(picha juu)Changamoto nyingine ni ukosefu wa Mtaji kuanzisha na kuendeleza Kilimo cha bega kwa bega na Umwagiliaji na kukosa kasi kubwa ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara na mifereji mashambani.Mbali ya changamoto hizo katibu huyo amesema kuwa Ajira kwa Wananchi, Idadi ya Wakulima na pato la Mkulima, limeongezeka baada ya ubinafsishaji wa Viwanda na matumizi ya mfumo Mauzo ya miwa kwa uwiano wa mapato.
Shamba la miwa wilayani kilombero..
KILIMO BORA CHA MUHOGO
O
· UANDAAJI WA SHAMBA
Zao la muhogo ni muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia chakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani
Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750 - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.
MBEGU BORA ZA MUHOGO
i. Mbegu bora za muhogoMpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimathibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji. ·
1 . Kiroba - Huzaa tani 25 – 30 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.
Wednesday, February 18, 2015
UGONJWA HATARI WA MAHINDI WAINGIA NCHINI TANZANI.
UGONJWA HATARI WA MAHINDI WAINGIA NCHINI TANZANIA
Ugonjwa hatari unaoshambulia mahindi na kusababisha saratani kwa binadamu umeingia nchini na wakulima sasa wametahadharishwa kutokula mahindi hayo wala unga ambao haujakobolewa.
Mahindi yaliyoathiriwa na ugonjwa huo huota 'fungus' ambao ina sumu inayoitwa 'Aflatoxin' ambayo inaweza kusababisha madhara kwa wanyama na binadamu hususan ugonjwa wa saratani. Mbali na kutikisa mikoa kadhaa na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima, ugonjwa huo ambao umeanzia nchini Kenya unaendelea kusambaa kwa kasi na sasa umeingia pia nchini Uganda.
Awali ugonjwa huo uliripotiwa kuzikumba wilaya za Babati mkoani Manyara na Meatu mkoani Shinyanga tu, lakini sasa umesambaa hadi katika mikoa jirani ikiwamo Kilimanjaro
.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Leonidas Gama jana alilithibitishia gazeti hili kuwa mkoa wake umekumbwa na ugonjwa huo na tayari umesambaa katika wilaya tatu; Moshi Vijijini, Siha na Hai. "Ni kweli baadhi ya wilaya zimekumbwa na ugonjwa huo, bahati mbaya sana hauna tiba na unasambaa kwa kasi... Wataalamu wanaendelea kuwaelimisha wakulima kutambua dalili zake," alisema Gama.
Gama alisema endapo mkulima atabaini shamba lake kushambuliwa na ugonjwa huo katika hatua za awali, anachotakiwa kufanya ni kung'oa mimea yote ya mahindi na kuichoma moto.
Mkuu wa Wilaya ya Hai, Novatus Makunga alisema takriban hekari 14 zimeshambuliwa na ugonjwa huo katika shamba la Watawa wa Kanisa Katoliki Mailisita na shamba la mkulima wa Lambo. Alisema tayari wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Selian (SARI) ya Jijini Arusha wamefika wilayani humo na kutoa tahadhari kwa wakulima juu ya athari za ugonjwa huo. Mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi, John Bennett anayemiliki mgahawa wa Golden Shower aliitaka Serikali kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara na kuchukua tahadhari.
"Utajuaje unga wa dona haukutokana na hayo mahindi au pumba ya chakula cha mifugo hayakutokana na hayo? Hili jambo ni zito sana si la kufanyia utani hata kidogo"alisema Bennett.
Mkulima wa Kijiji cha Kikavu Chini wilayani Hai, Justine Mvungi alisema wataalamu kutoka SARI wamewataka kuchoma moto miche ya mahindi ambayo watagundua imeshambuliwa.
"Wametuambia takriban shamba likishambuliwa, tung'oe mahindi hayo na kuyachoma moto, wametuambia kama tulishavuna basi tukoboe mahindi hayo maana kiini chake kina madhara,"alisema.
"Aliongeza kusema" hata tukikoboa mahindi tumeambiwa zile pumba zake tusiipe mifugo kwa sababu itaathirika... Ugonjwa huu wa mmea wa mahindi umeleta taharuki kubwa kwa wakulima na wananchi
WAJASIRIAMALI, WASANII NA WANAHABARI WALIOSHIRIKI KWENYE MAONYESHO YA UTAMADUNI NCHINI OMAN, WAREJEA NCHINI
Naibu waziri wa Habari na utambaduni Utalii na Michezo Zanzibar .Bi Hindi Hamadi Khamisi akiwa uwanjani wa ndege wa kimataifa Zanzibar wa Abeid Karume akisubiri kuwasili kwa wajasiliamali,Wasanii na Waandishi wa habari waliokuwa nchini Omani kw ajili ya maonesho ya Tamasha la Utamaduni yaliofanyika
wajasiriamali na waandishi wa Habari wliopata nafasi ya kwenda Oman kwa ajili ya kutangaza utamaduni wao wakipokelewa na Naibu Waziri waHabari utamaduni Utalii na michezo Zanzibar.
Naibu Waziri wa Habari utamaduni utalii utamaduni na michezo Zanzibar Bi Hindi Hamadi wa mwanzo kulia akiwasalimia wasanii hao baada ya kuwasalimia uwanjani hapo
WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA AFUNGUA MKUTANO WA NNE WA WADAU WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF MJINI DODOMA
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda (Kushoto) akizindua huduma mpya itolewayo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ya Fao la Uzazi, mwanzoni mwa mkutano mkuu wa wadau na wanachama wa Mfuko huo mjini Dodoma jana. Wanaoshuhudia kutoka kulia, ni naibu waziri wa fedha, Adam Malima, Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko huo, GHeorge Yambesi, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, na mkuu wa mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Nne wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ulioanza leo mjini Dodoma.
KNCU WAINGIZA MTAMBO MPYA WA KUKOBOLEA KAHAWA
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.
CHAMA Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa zao la Kahawa mkoani Kilimanjaro KNCU (1984) Ltd kimetumia kiasi cha dola laki 9.48 kununua mtambo wa kukobolea Kahawa kutoka kampuni ya Pinhalense ya Brazil.
Ununuzi wa Mtambo huo wa kisasa unafanyika ikiwa ni sehemu ya maazimio ya mkutano mkuu wa KNCU uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana wajumbe wakiazimia kufanyika juhudi za makusudi ili kukinusuru kiwanda hicho ambacho kilielekea kufa.
Katika hali ya kukiokoa kiwanda hicho,bodi ya kampuni ya kukoboa kahawa ya Tanganyika (TCCCo) ililazimika kuuza sehemu ya mali zake ili kukinusuru na madeni yanayokikabili baada ya kupata hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 2 .
Tanzania Daima Jumatano ilifika katika kiwanda hicho juzi na kushuhudia sehemu za mtambo huo unaotajwa kuwa wa kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati zikishushwa toka katika magari matano.
Meneja wa TCCCO, Endrew Kleruu, alisema ujio wa mitambo hiyo utasaidia kupunguza upotefu wa Kahawa ,ikiwa ni pamoja na kuongeza ubora wa uzalishaji unaoendana na viwango vya ubora katika soko la Kimataifa.
Alisema mitambo hiyo yenye uwezo wa kuzalisha tani sita kwa saa moja itasaidia kuwapunguzia wakulima wa zao hilo gharama za uzalishaji kutokana na uwezo wake wa kutumia umeme mdogo wa Kilo Voti 30 hadi 35 tofauti na mtambo wa zamani ambao ulikuwa unazalisha tani nne tu kwa saa huku ukitumia zaidi ya Kilo Voti 100 ya umeme.
Kleruu aliwataka wakulima wa zao la Kahawa kuongeza juhudi katika kilimo cha zao hilo chenye tija ili kukidhi hitaji la Kahawa yenye ubora wakati wa uendeshaji wa mtambo huo mpya .
Kwa upande wake meneja wa usambazaji vifaa wa kampuni ya Brazafric Enterprizes Ltd, Salim Mghweno,alisema kuwa ufungaji wa mtambo huo utatumia miezi miwili ambapo matarajio ni hadi kufikia msimu wa uzalishaji wa Kahawa ufungaji wa mtambo huo utakuwa umekamilika.
Alisema kukamilika kwa ufungwaji wa mtambo huo kutasaidia ongezeko la kiwango cha zao hilo ukilinganisha na mtambo wa zamani ambao Kahawa iliyokobolewa ilipungua kiwango licha ya ukubwa wa mitambo ambayo pia imeelezwa kuwa ni chakavu. Mwisho.
Tuesday, February 17, 2015
FAIDA ZA TIKITI MAJI KIAFYA
Baadhi ya vyakula vimekuwa vikifurahisha pale vinapoliwa, tikiti maji ni miongoni mwa vyakula hivyo. Kwanza ule mchanganyiko wa rangi zake hulifanya sio tu kuvutia bali kuwa kama ua lililochanua juu ya meza ya mlaji husika.
Kama vile haitoshi tunda hili limejaaliwa virutubisho kadha wa kadha vyenye faida kubwa katika afya ya mwanadamu.
Licha ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado zile 8% zilizobaki zina faida kubwa sana kiafya jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi.
Zifuatazo ni baadhi tu ya faida chache kati ya nyingi za tunda hili la tikiti maji:
Tikiti maji ni chanzo kizuri cha vitamini. Katika tunda hilo kuna Vitamin A, inayosaidia kuboresha afya ya macho na pia kuondosha sumu mwilini; Vitamin C, inayosaidia kuboresha kinga, kuponya majeraha, kukinga uharifu wa seli, kuboresha afya meno na fizi; na vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha protini kuwa nishati.
Tunda la tikiti maji lina kiwango kikubwa cha lycopene kuliko tunda lolote au mboga za majani.
Ikiwa familia yako inaishi kwenye eneo lisilo na vyanzo vya madini ya potasium, unaweza kuwapa tikiti badala yake. Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.
Halikadhalika tunda hili huweza kukuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu.
Tikiti pia lina amino asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenye mishipa yake.
Sifa ya kipekee iliyopo katika tunda hili, ni ule uwezo wake wa kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwa kunywa juisi yake iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda yake na mbegu zake, kutaisadia kabisa kuondoa tatizo hilo.
Kwa kawaida tunda hili huliwa pejke yake au kwa kuchanganya na matunda mengine. Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya afya ya vyakula kila kitu kwenye tikiti maji kina faida kiafya ukianzia kwenye majani tunda na hata nyama yake.
Monday, February 16, 2015
Bata mzinga: Njia mpya ya ujasiriamali
Ili kuzaliana na kumpatia mfugaji faida, bata mzinga wanahitaji matunzo ya hali ya juu. Kwa kawaida bata mzinga hula chakula kingi kuliko kuku. Bei yake ni ghali zaidi.
Kabla ya kuanza ufugaji wa bata mzinga ni lazima kuhakikisha una chakula cha kutosha kwa sababu ulishaji wa ndege hawa kadri wanavyokua huwa na gharama kubwa zaidi. Ni muhimu pia kujifunza kwa undani na kufahamu namna ya kutunza vifaranga wa bata mzinga kwa kuwa hufa kwa urahisi sana. Pia, unapaswa kujikita kutafuta soko kwa sababu wanapokuwa ni vigumu kuwatunza kwa muda mrefu kutokana na ukubwa wa gharama ya chakula.
Wafugaji wachache kati ya wengi waliojaribu kuwafuga ndege hawa na kufanikiwa hata kufikia malengo yao ni kutokana na kuzingatia lishe kamili. Pamoja na hayo, wapo wafugaji ambao walishindwa kutokana na magonjwa pamoja na gharama ya utunzaji.
WAZIRI MKUU AHIMIZA KILIMO BORA CHA MAZAO MBADALA YA BIASHARA
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka wakazi wa wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi walime mazao mbadala ya biashara kama alizeti, karanga na ufuta kwa sababu yanachukua muda mfupi na hivyo kuleta kipato cha haraka.Ametoa wito huo wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nsenkwa mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye zahanati ya kijiji hicho akiwa katika siku ya pili ya ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani Mlele, mkoani Katavi.
Aliwataka wakazi hao waangalie ufugaji nyuki kama fursa ya kwa sababu mkoa huo umejaliwa kuwa na misitu mingi na unaweza kuongeza kipato cha mkoa wao. “Asali ni dawa, asali ni chakula, asali ni biashara na ina soko hapa nchini hadi nje ya nchi. Changamkieni fursa hii, ongezeni uzalishaji wa asali na nta,” aliongeza. Aliwashauri pia waangalie uwezekano wa kulima miembe ya kisasa kwa sababu inazaa kwa wingi na katika kipindi kifupi mno. “Hii miembe yenu inazaa maembe 10-20 kwa mwaka lakini ya kisasa inazaa hadi maembe 10,000, ikiwa chinichini tu,” alisema.
Akihimiza kanuni bora za kilimo, Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Mlele aliwataka waachane na kilimo cha matuta na badala yake watumie kilimo cha sesa. “Ekari moja ya mahindi inapaswa ikupatie magunia 20-25 ya mahindi, sasa wewe unalima ekari tatu na kuvuna magunia 10, sababu kubwa ni nafasi zinazopotea kwenye miraba ya matuta, alisema. “Ni lazima tuondokane na kilimo hiki kwa sababu hakina tija na tenakinatumia nguvu nyingi na kupoteza eneo kubwa ambalo lingetumika kupanda mazao,” alisisitiza.
Akihimiza kanuni bora za kilimo, Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Mlele aliwataka waachane na kilimo cha matuta na badala yake watumie kilimo cha sesa. “Ekari moja ya mahindi inapaswa ikupatie magunia 20-25 ya mahindi, sasa wewe unalima ekari tatu na kuvuna magunia 10, sababu kubwa ni nafasi zinazopotea kwenye miraba ya matuta, alisema. “Ni lazima tuondokane na kilimo hiki kwa sababu hakina tija na tenakinatumia nguvu nyingi na kupoteza eneo kubwa ambalo lingetumika kupanda mazao,” alisisitiza.
Subscribe to:
Posts (Atom)