KILIMO BORA CHA MUHOGO
O
· UANDAAJI WA SHAMBA
Zao la muhogo ni muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia chakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani
Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750 - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.
MBEGU BORA ZA MUHOGO
i. Mbegu bora za muhogoMpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimathibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji. ·
1 . Kiroba - Huzaa tani 25 – 30 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.
MBINU BORA ZA KILIMO CHA MUHOGShamba liandaliwe kabla ya msimu wa kuanza. Uandaaji wa shamba bora hufuata hatua zifuatazo:- Kufyeka shamba- Kung’a na kuchoma visiki- Kulima na kutengeneza matuta
- · UCHAGUZI WA MBEGU BORA ZA KUPANDA
Mbegu zinatakiwa zisiwe na magojwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamelomaa vizuri.
Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo:- Kulaza ardhini (Horizontal)- Kusimamisha wima (Vertcal)- Kuinamisha ( Inclined/Slunted)
- · UREFU WA KIPANDE CHA SHINA CHA KUPANDA:
Inashauriwa urefu uwe sm 30; lakini urefu wa kipande cha kupanda unategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande, inashauriwa kipande kiwe na macho (4 – 6).
Kwa upandaji wa shamba muhogo tupu, shina hadi shina ni mita 1 na mstari hadi mstari ni mita 1.Kwa shamba la mchanganyiko na mazao mengine, inategemeana na zao linalochanganywa; mstari hadi mstari ni mita 2 – mita 4 na shina hadi shina ni mita
- Palizi ya kwanza ifanyike mapema (mwezi 1) baada ya kupanda ili kuepukana na maguguyanayochipua haraka baada ya mvua kunyesha. Ndani ya miezi mine ya mwanzo mihogo haitakiwi kuwa na magugu ili kuepuka ushindni wa mahitaji muhimu (mwanga, mbolea, maji, n.k) kati ya muhugo na magugu.- Palizi hufanyika kwa kutumi jebe la mkono au dawa ya kuuwa magugu.- Wakati mwingine udhibiti wa magugu kufanyika kwa kutumia majani kwa kutandazwa juu ya udongo.- Plaizi hufanyika mara 2 – 3 hadi muhugo kukomaa.
Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.
Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu mbili:- Kurahisisha/kuharakisha ukaushaji- Kuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za mihogo- Kuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe.
Njia bora za usindikaji- Kwa kutumia mashine aina ya GraterHii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.- Kwa kutumia mashine aina ya chipper- Mashine hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa hasa kwa ajili ya mihogo mitamu/baridi.
- Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza unga- Unga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na ungawa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.kPia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga.
No comments:
Post a Comment