Saturday, February 14, 2015

WAJUMBE WA ALAT RUVUMA WATEMBELEA KITUO CHA KILIMO NALIENDELE MKOANI MTWARA


Katibu tawala wa mkoa wa Mtwara,Yusuf Matumbo akizungumza na wajumbe wa jumuiya ya serikali za mitaa(Alat)mkoa wa Ruvumna wakati wa ziara ya wajumbe hao kutembelea mkoani humo kujifunza namna ya kilimo cha korosho na mazao mengine ya biashara.
Mtafiti wa zao la korosho kutoka kituo cha kilimo Naliendele mkoani Mtwara,Ramadhan Bashiru (kulia) akiwaonesha mche wa korosho baadhi ya wajumbe wa jumuiya ya serikali za mitaa(Alat)wa mkoa wa Ruvuma walipotembelea katika kituo hicho kujifunza kilimo cha kilimo bora cha korosho hivi karibuni.
Wajumbe wa jumuiya ya serikali za mitaa(Alat)mkoa wa Ruvuma wakimsikilimza mtaalamu wa kilimo cha korosho kutoka kituo cha kilimo cha Naliendele mkoani Mtwara,Bi Joan Kasuga (kushoto) juu ya kilimo bora cha korosho,kufuatia ziara ya wajumbe hao kutembelea kituo hicho kwa lemngo la kujifunza kilimo bora cha zao hilo.
Mtafiti wa zao la muhogo kutoka kituo cha kilimo cha Naliendele mkoani Mtwara Abdala Nyapuka (kulia) akiwaonesha wajumbe wa Alat mkoa wa Ruvuma aina moja wapo ya muhogo unaozalishwa katika kituo hicho.kufuatia ziara ya mafunzo ya wajumbe hao mkoani Mtwara kujifunza namna ya kilimo bora cha korosho na mazao mengine ya biashara.
Katibu wa jumuiya za serikali za mitaa(Alat)mkoa wa Ruvuma Musa Zungiza akiazungumza na wajumbe wa jumuiya hiyo juzi katika u8kumbiu wa halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani humo,kushoto ni mwenyekiti wa jumuiya hiyo Oddo Mwisho.
Mwenyekiti wa jumuiya ya serikali za mitaa(Alat) mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho akiangali chupa yenye wadudu waharibifu wa korosho katika kituo cha kilimo cha Naliendele mkoani Mtwara,alipoongoza ujumbe wa wajumbe hao kutembelea mkoani Mtwara hivi karibuni.Picha na Muhidin Amri wa Globu ya Jamii,Ruvuma.
Chanzo: Michuzi Blog

Chuo cha Utafiti Naliendele kiini cha mafaniko ya kilimo cha korosho

Tanzania imeweza kupiga hatua katika uzalishaji wa zao la korosho kutokana na Elimu iliyotolewa kwa wakulima na wataalamu wa utafiti wa kilimo cha Korosho na Magonjwa ya  Korosho kutoka chuo  Naliendele kilichopo mkoani Mtwara.

Dr. Louis Kasuga ameyasema hayo katika semina ya ufufuaji wa mikorosho iliyotelekezwa,  semina inayo jumuisha mikoa 3 ya mbeya,Njombe , na Ruvuma kwa kueleza mafanikio yaliyo patikana baada ya utafiti.

Dr Louis Kasuga amesema  uzalishaji wa korosho kwa Tanzania nzima mwaka 1974-1975 ulikuwa tani 145,000lakini kutokana na magonjwa mbalimbali na kuhama bila mpango kiasi kilishuka hadi kufikia tani 16,000 kwa mwaka kwa katika  Tanzania Nzima

Dr louis Kasuga mtaalamu wa utafiti wa magonjwa ya korosho amesema baada ya juhudi za serekari kufanya utafiti na kubaini chanzo  cha matatizo iliweza kuongeza uzalishaji wa korosho kutoka tani 16,000 kwa mwaka hadi kufikia tani 158,000 kwa mwaka

Wakulima wa Zao la korosho kutoka mikoa ya Njombe ,Mbeya na Ruvuma wamesema kinachosababisha kuzorota kwa zao la korosho ni kuchelewa kwa pembejeo na ukosefu wa masoko na bei ya uhakika.

Mgeni Rasmi katika semina hiyo Kasimu Andrew Maswaga amesema wakulima wajue kuwa kilimo ni ajira kama walivyo ajiliwa watu wengine Serikarini kuna kupanda na kushuka.

Katika Tanzania kuna Miti ya mikorosho ipatayo 40,000,000 na katika miti hiyo ipo mingine ambayo imeshambuliwa na magonjwa , asilimia 80%  ya miti ya mikorosho ili pandwa mwaka 1950  jambo linalosababisha kupungua kwa uzalishaji, kampeni zimeanza za kupanda miche mipya ya ya kisasa pamoja na pandikizi matawi ya kisasa.

JIPATIE MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2014 NA QT HAPA

                                 Na Chalila kibuda Globu ya Jamii
Shule za sekondari binafsi zaongoza 10 bora matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana

Akizungumza na waandisha wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es salaam. Katibu mtendaji wa baraza la mitihani nchini (NECTA) Dk Charles Msonde amesema katika matokeo ya kidato cha nne ya mitihani wa mwaka jana umeongwzeka kwa asilimia 12.67 ikilinganishwa na mwaka jana 2013

Katika matokeo hayo msichana wa shule ya sekondari ya Baobab, Nyakaho
   1. Mrungu ndio aliyeongoza mtihani huo na kufatia na wavulana

Shule za sekondari za St Fransis ya mkoani Mbeya wanafunzi sita na Feza wanafunzi Nane na kufanya shule hizo kuingia katika kumi (10) bora kwa kutoa idadi wanafunzi wengi ikilinganishwa na shule zingine

Msonde amesema matokeo hayo yatatoka na mfumo mpya wa GPA kwa kuangalia masomosaba hivyo hivyo ufaulu umetokan na mfumo huo


DCB YANG^ARISHA KONGAMANO LA WAJASIRIAMALI DAR

 Meneja masoko wa bidhaa wa Benki ya biashara ya Dar es salaam(DCM),Boyd Mwaisame akitoa maelezo kwa wateja waliohudhuria kongamano la Wajasiriamaali. kwenye viwanja vya makumbusho Dar es salaam namna Benki hiyo inavyo endesha huduma zake kadhaa,ikiwemo huduma za akiba,DCB Mobile,DCB jirani na utaratibu wa jinsi ya kukopa na masharti ya huduma za mikopo hasa SGL. na Super SGI


Friday, February 13, 2015

Mkutano wa Kujadili Mkakati wa Maendeleo wa Sekta ya Mifugo nchini Kenya

Dkt . Titus Mlengeya Kamani (Mb)  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Akishiriki  Kwenye Mkutano wa Mawaziri Wenye Dhamana ya Sekta ya Mifugo.KujadiliMkakati wa Maendeleo wa Sekta ya Mifugo Afrika kwa Kipindi cha 2015-2035 (The Livestock Development Strategy for Africa -LiDeSa 2015-2035).  Katika ukumbi wa Mikutano wa AU-IBR Nairobi, Kenya

Imetolewa na wizara ya ufugaji

Tangazo la Kujiunga na Mafunzo Maalum ya Stashahada ya Teknolojia ya Maziwa

Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) inatangaza nafasi za mafunzo ya Kozi Maalum ya Stashahada ya Teknolojia ya Maziwa itakayotolewa kwenye Kampasi ya Tengeru, Arusha kuanzia mwezi Februari hadi Jula 2015, Kwa maelezo zaidi tembelea link hapo chini



BAAZI YA MATREKTA NA VIFAA VYA KILIMO VINAVYO SAMBAZWA NA SUMA JKT

Matrekta ya nayo sambazwa na suma JKT






AIRTEL YATOSHA KUFANYA DROO YA WIKI YA PILI YA PROMOSHENI YA AIRTEL YATOSHA ZAIDI



Viongozi wa Airtel wakiongea na  waandishi wa habari kuhusu promosheni hiyo ya wiki ya pili ya Airtel yatosha zaidi

Thursday, February 12, 2015

MBOLEA YA ASILI INAYOTOKANA NA MAGUGU MAJI

Hii ni aina ya mbolea ya asili isiyokuwa na madhara yoyote kwa binadamu na wanyama. Mbolea hii hutengenezwa kwa kuvundika mimea ya baharini au maotea ya majini.

seaweedAina hii ya mbolea inafaa kutumika kwa kuchanganya na viua wadudu vyovyote ambavyo ni asidi au basickwani utendaji kazi wake hauwezi kupote endapo itachanganywa.

Viambata vya mbolea

Mbolea hii ina vichocheo vya mimea ambavyo ni vya asili kama Auxins,  Cytokins na Gibberellins ambavyo hivi ni homoni za mimea ya asili yenye uwezo mkubwa wa kufanya mazao yaweze kumea vizuri na hatimaye kutoa mavuno mazuri Mbolea hii pia ina madini zaidi ya sabini ambayo yana uwezo mkubwa wa kustawisha na kuimarisha mazao kwa kiwango cha juu.

Kazi za mbolea hii

1. Inaongeza uwezo wa mmea kuweza kufyonza madini na virutubisho mbali mbali kutoka kwenye udongo na pia kutoa mizizi kwa haraka.
2. Mbolea hii pia inaongeza uwezo wa mimea kujitengenezea chakula chake yenyewe.
3. Ina uwezo wa kusaidia uhifadhi wa unyevu nyevu katika udongo kwa muda mrefu.
4. Inafanya mmea uweze kuhimili hali ya ukame, ubaridi pamoja na magonjwa mbalimbali.
5. Inafanya mmea uweze kuota mapema kuongeza wingi wa mizizi na mimea kuwa na afya
6. Inaongeza kiwango cha mavuno ya mazao yako.
7. Inaongeza muda wa matunda au mazao kukaa muda mrefu baada ya mavuno kama ikitumiwa siku kumi kabla ya kuvuna.

Unaweza kulima kabichi msimu wote wa mwaka. Soko lake ni la uhakika katika kipindi chote na ni muhimu kwa afya. Pia, linaweza kutumika kama malisho ya mifugo

Kabichi ni moja ya mazao yaliyomo katika jamii ya mimea inayojumuisha mimea ya kaulifulawa (cauliflower ), kabichi ya kichina na kale. Kwa kawaida kabichi hupandwa kwa msimu mmoja, lakini iwapo itakuzwa kwa ajili ya kutoa mbegu hukuzwa zaidi ya msimu mmoja. Endapo inalimwa sehemu yenye maji ya kutosha, inaweza kulimwa msimu wote wa mwaka. Kichwa cha kabichi kinapofunga vizuri, hutumika kama chakula na huvunwa baada ya kufunga na kukomaa vizuri.

Mizizi: Mizizi ya kabichi hutawanyika ardhini vizuri. Kwa kawaida, huenda chini kiasi cha sentimita ishirini (20 sm), na hujitawanya kwa kiasi cha sentimita sabini na tano (75sm).


Shina: Shina la mmea wa kabichi huwa na rangi ya kijani au zambarau. Hii hutegemeana na aina ya kabichi, na kwa kawaida ni fupi.


Hali ya hewa: Kabichi hustawi vyema katika sehemu yenye hali ya baridi, hali ya joto jingi haifai kwa kabichi kwa kuwa huathiri uotaji na ukuaji wake. Joto jingi pia husababisha kulegea kwa vichwa vilivyofunga. Zao hili hustawi vema katika maeneo yenye mwinuko wa zaidi ya mita 100 toka usawa wa bahari.

Udongo: Zao hili linaweza kustawishwa kwenye udongo wa aina yoyote mradi tu udongo huo usiwe na chumvichumvi nyingi na usiotuhamisha maji. Udongo wa kichanga na ule usio na rutuba ya kutosha husababisha kabichi kukomaa upesi na kuzaa kabichi hafifu zenye vichwa vidogo.

Kitalu: Kitalu ni muhimu katika uzalishji wa zao hili. Ni vema kutengeneza matuta yenye upana wa mita moja, na urefu wowote kulingana na matakwa ya mkulima. Mbolea za samadi na zenye asili ya chokaa zichanganywe vizuri kwenye udongo. Kiasi cha gramu 500 za mbegu huhitajika kwa hekta moja.  Katika upandaji kwenye kitalu ni vizuri kutengeneza mistari katika tuta, umbali toka mstari hadi mstari uwe sentimita ishirini (20). Udongo kiasi kidogo utumike katika kufunika mbegu.

Baada ya mbegu kuota ni vizuri kupunguza baadhi ya miche na uwe katika kipimo cha sentimita 2-3 toka mche hadi mche. Hii itasaidia kuwa na miche mifupi na yenye nguvu. Inafaa kunyeshea kitalu mara moja au mbili kwa siku na katika sehemu za joto ni vizuri kuweka kivuli katika matuta. Katika wiki ya tatu, hadi wiki ya nne, ni vyema kuondoa kivuli kidogo kidogo huku ukipunguza unyeshaji. Hali hii itasaidia miche isipate mshtuko wa uhamishaji shambani.

ZALISHA MATANGO UPATE KUBORESHA KIPATO KWA MDA MFUPI

Matango (cucumber) ni zao muhimu katika mazao ya mboga na matunda nchini Tanzania na hata nje ya Tanzania.

 Hili ni zao la biashara, pia chakula. Zao hili hustawi na kulimwa kwa wingi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Pwani.
Cucumber

Matumizi:  Matango hutumika kama tunda, ijapokuwa ni aina ya mboga na huongeza vitamin A, C na maji mwilini. Pia, tango linaweza kutumiwa kama saladi wakati wa mlo.


Hali ya hewa: Matango hustawi kwenye hali ya joto, hali kadhali kwenye sehemu yenye joto kidogo pia hustawi. Matango yanahitaji joto wastani wa nyuzi joto 20°C – 25°C. Zao hili pia huhitaji maji kwa wingi, ingawa unyevu ukizidi husababisha magonjwa kwenye majani na maua.


Udongo:  Kwa ustawi mzuri wa matango, udongo unatakiwa kuwa na rutuba ya kutosha, na chachu ya kuanzia 5.5 hadi 6.7, mwinuko unaotakiwa ni kuanzia mita 1000-1200 kutoka usawa wa bahari.

Tofauti na ilivyo mazao mengine, matango hayahitaji mwanga mkali sana kwa kuwa husababisha maua dume kuzaliwa, hivyo kuathiri uzalishaji wa idadi ya matunda ya matango. Mwanga kidogo husababisha maua jike kuchanua kwa wingi kuongeza kiwango cha mazao. Mwanga unapokuwa mwingi, inabidi kutumia neti au aina nyingine ya vizuizi ili kupunguza mwanga, ambapo pia itasaidia kulinda mmea dhidi ya upepo mkali ambao unaweza kuharibu maua na matunda, au mmea kwa ujumla.


UTUNZAJI WA UDONGO KWA AJILI YA KILIMO

Utunzaji wa udongo unategemeana kwa kiasi kikubwa na mazingira ya kibiolojia. Kazi kubwa ya baadhi ya viumbe hai waliomo kwenye udongo, ni kumeng’enya mabaki ya mimea na viumbe hai wengine. Mtiririko huu hufanya uwepo wa nguvu, virutubisho, na hewa ya kaboni, ambavyo kwa pamoja hutengeneza rutuba kwenye udongo.

Utunzaji wa rutuba ya udongo unaongozwa na filosofia hii ‘Lisha udongo ili nao ulishe mimea.’ Udongo wenye rutuba utazalisha mimea yenye afya inayoweza kukabiliana na magonjwa. Uzalishaji wa mazao kwa njia za asili uhakikisha kunakuwepo uzalishaji wa kutosha bila ya kutumia pembejeo za ziada isipokuwa matandazo, mboji na bila kutifua udongo mara kwa mara. Ongezeko la malighafi za asili husaidia kuimarisha udongo na kufanya kuwepo kwa virutubisho vya kutosha.


KILIMO BORA CHA MANANASI

Zao la mananasi hulimwa sana hapa nchini maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Geita, Mwanza, Tanga, MtwaraLindi na maeneo mengine. Zao hili lina kiasi kikubwa cha vitamini A na B na kiasi kidogo cha vitamini C, pia kuna madini kama potasiam, kalsiam, chuma na magnesiam

HALI YA HEWA
Manansi hustawi sana ukanda wa pwani usawa usiozini mita 900 toka usawa wa bahari ambapo kuna mvua nyingi kiasi cha milimita 1500 na unyevu wa kutosha, pia unaweza kupanda kwenye maeneo yenye mvua chache lakini kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji, Hali ya joto ni kuanzia sentigredi 15 - 32, huwa haya stahimili baridi

UDONGO
Udongo wenye rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji ndi unaofaa kwa ajili ya kilimo cha mananasi, unaweza kutumia samadi au mbole vunde ili kuongezea rutuba ya udongo wako. 

MSIMU
Kwa ukanda wa pwani wenye mvua mbili kwa mwaka upandaji wa mananasi huanza mara baada ya mvua za kwanza kuanza, ni vizuri kupanda kwa muda mfupi ili uzaaji usipishane sana na pia kusaidia kupata mvua za kutosha kabla ya msimu kuisha.

UPANDAJI
Tumia miche ya aina moja na yenye umri sawa ili huduma zifanane na pia uzaaji uwe wa mpangilio, umbali toka mmea hadi mmea ni sentimeta 30 na mstari hadi mstari ni sentimeta 60, na umbali kila baada ya mistari miwili miwili ni sentimeta 90
Kwa ekari moja unaweza kupanda miche 25,200 na kwa hekta moja unaweza kupanda miche 44,000. ili mananasi yako yastawi vizuri basi tengeneza kama mtaro mdogo na kwenye mitaro ndio upande mananasi yako, hii husaidia kupata unyevu zaidi 

MBOLEA
Kwa wale wanaotumia mbolea za viwandani, ni vizuri kutumia NPK na DAP ambazo utaweka miezi miwili baada ya kupanda na miezi 12 baada ya kupanda baada ya hapo hautahitaji mbolea tena, lakini ni vizuri zaidi kama utatumia mbolea za asili

WADUDU
Wadudu wanaoshambulia mananasi ni aina ya mealybug ambao huondolewa kwa kupulizia dawa kama dume na karate.

Ugonjwa wa kuoza moyo wa miche unaweza kuzuiwa kwa kupiga dawa za copper oxychloride au kwa kuzamisha miche kwenye dawa za fungasi (fungicides)kabla ya kupandwa shambani

UVUNAJI
Mananasi huwa tayari kuvunwa miezi 18  mpaka 24 baada ya kupandwa kutegemeana na mbegu na matunzo ikiwemo kiasi cha mvua, mbolea na unyevu shambani, Uvunaji  hufanyika kwa kutumia visu na vibebeo maalum kuhakikisha ubora wa zao hili

WASIRA AAGIZA WADAU WA SUKARA KUINGIZA SOKONI BIDHAA HIYO BADALA YA KUIFUNGIA GHALANI

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh Stephen Masatu Wasira amekutana na wadau wa sukari na kutoa tamko la serikali kuhusiana na kupanda kwa sukari hapa Nchini Mh Wasira amewaangiza wazalishaji na wafanya biashara wa sukari hapa Nchini kuingiza sukari badala ya kuiweka kwenye maghala ili kushusha bei ya bidhaa hiyo muhimu Agizo hilo la Wazili limekuja muda mfupi baada ya kupanda ghafla kwa bei ya sukari kutoka shilingi 1700/= iliyo kuwa ikiuzwa awali hadi shilingi 3000/= kwa kilo


Waziri wa kilimo Chakula na ushirikiano Mh Stephen Wasira na Naibu wake (kushoto) Mh Godfrey zambi , Bi Sophia Kaduma katibu mkuu kulia na Dkt Yamungu kayandabila (kushoto) wakifuatilia kwa makini mjadala baina yao na wazalishaji na wafanya biashara wa sukari katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa kilimo

FAIDA YA TUNDA LA PARACHICHI - PEA (AVOCADO)


Ndani ya tunda hili kuna maji kiasi kidogo sana ukilinganisha na matunda mengine lakini kuna mafuta mengi na unaweza kuchanganya kula na tunda lingine kama vile apple, ndizi, chungwa au hata maziwa kwa kutengeneza juisi.


TINDIKALILicha ya kuwa na mafuta parachichi lina tindikali (acid) mbalimbali ikiwemo inayojulikana kama amino ambayo husaidia sana kukinga na kutibu maradhi katika mwili wa binadamu. Tunda hili pia lina protini ya kiwango cha juu.Pia kuna tindikali inayoitwa oleic acid kwenye parachichi ambayo husaidia kukinga magonjwa ya moyo, kiharusi na kansa.




Wednesday, February 11, 2015

RAIS KIKWETE AKAGUA KILIMO CHA KAHAWA MBINGA

D92A6133
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miche bora ya kahawa mkulima mdogo Bi Dorothea Komba wakati alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam katika kijiji cha Lipokela wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma leo.Kampuni ya Olam imepanga kutoa jumla ya miche milioni tatu kwa wakulima wadogo elfu mbili katika vijiji vinne vinavyozunguka shamba hilo katika kipindi cha miaka mitano ili kuwashirikisha kuzalisha kahawa bora.



KILIMO BORA CHA ALIZETI

Alizeti hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara, na Rukwa. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. 

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA UZALISHAJIKuchagua aina bora ya mbegu • Chagua aina bora ya mbegu inayovumilia magonjwa, wadudu, inayotoa mazao mengi na kiwango kikubwa cha mafuta.• Vilevile chagua aina ya mbegu ambayo hukomaa kwa wakati mmoja ili kurahisisha uvunaji.
 

 KUWEKA MBOLEA • Rutubisha udongo kwa kutumia mbolea za mboji na samadi ili kupata mazao mengi na bora.
  

KUDHIBITI WADUDU NA MAGONJWA Alizeti hushambuliwa na magonjwa ya majani, mizizi na masuke ambayo husababisha upungufu wa mavuno. Hivyo ni muhimu kuyadhibiti ili kupata mavuno mengi na bora. Pia ndege hupunguza mavuno kwa kiasi cha asilimia 50 au zaidi. Njia ya kudhibiti ndege ni kwa kuwafukuza na kupanda mbegu zinazokomaa mapema.
 


MAELEZO YA MSINGI KUHUSU KILIMO CHA MBOGA MBOGA-Vegetables


Mboga ni mmea au sehemu yoyote ya mmea inayoweza kuliwa na binadamu ambayo haina sukari kama matunda. Mboga huweza kuliwa zikiwa zimepikwa na mara nyingi huwekewa chumvi ili kuongeza ladha na pia huweza kuliwa zikiwa mbichi kwa mfano kwenye kachumbari. Mboga ni sehemu muhimu sana katika mlo uliokamilika, hii imesababisha ukuaji wa kasi wa soko la mboga na upandaji wa mboga katika maeneo mengi ya mijini na vijijini.
Sehemu za mmea ambazo zinaweza kutumika kama mboga

I. Majani
Mboga nyingi hutoka kwenye majani ya mimea. Mara nyingi haya majani huwa ya rangi ya kijani kwasababu ya kutengeneza chakula cha mmea kutoka kwenye mionzi ya jua na huwa na virutubisho vingi muhimu katika mwili wa binadamu kwa vile vitamin. Miongoni mwa majani ambayo huliwa kama mboga ni Kabichi, Spinach, Chinese, Mchicha na figiri.

II. Mizizi
Mizizi ya baadhi ya mimea ni mboga nzuri na ina virutubisho kama vile vitamin A ambayo huimarisha macho na kuongeza uwezo wa kuona. Miongoni mwa mizizi ambayo huliwa kama mboga ni karoti.

III. Tunda
Tunda kwa maana ya kibustani ni sehemu ya mmea ambayo hubeba mbegu na inalika ikiwa mbichi au imepikwa. Mfano wa mimea ambayo sehemu ya tunda ni mboga ni kama vile nyanya, matango, bilinganya na bamia.

IV. Bulb (Tunguu)
Hii ni sehemu ya mmea ambayo hukua chini ya ardhi kwa mfano vitunguu (maji na swaumu). Mboga za aina hii ni muhimu sana katika mwili wa binadamu kwani husaidia kusafisha damu na huongeza ladha na harufu nzuri katika chakula.

V. Tuber (Kiazi)
Hii ni aina ya mboga ambayo ni mzizi unaohifadhi chakula cha mmea. Aina hii ya mboga husaidia kujaza tumbo na kufanya usihisi njaa haraka. Mfano wake ni viazi (mviringo na vitamu).

VI. Nyinginezo
Sehemu nyingine za mmea ambazo hutumika kama mboga ni pamoja na jicho la ua (cauliflower), mbegu (kunde na maharage), shina (tangawizi), chipukizo/kimea (majani ya kunde, soybean).
Mfano wa mboga mboga

i) Bilinganya ii) kabichi iii) karoti iv) Mchicha
Umuhimu wa vyakula vya jamii ya mboga mboga mwilini
Watu hushauriwa kula vyakula vya jamii ya mboga mboga kwa wingi. Sababu kubwa ni kutokana na faida za kiafya ambazo huletwa kutoka kwenye mboga mboga ambazo haziwezi kupatikana kutoka kwenye vyanzo vingine. Mboga zina vitamins na madini (minerals) kama vile potassium, vitamin A & C hupatikana kwa wingi kwenye mboga mboga na huhitajika mwilini kila siku ili kuusaidia kuwa na afya na kuweza kukinga au kuzuia maradhi. Virutubisho vingine husaidia kukinga moyo na figo dhidi ya maradhi na huzuia kansa.
Kanuni bora za ukuzaji wa mboga mboga

1. Kuchagua eneo
Katika kuchagua eneo kwaajili ya kupanda mboga ni muhimu kuzingatia vitu vifuatafvyo;
 Mwinuko: Eneo lisiwe kwenye mwinuko mkali kwa sababu husababisha mmomonyoko wa udongo. Endapo sehemu itakuwa na mwinuko, tengeneza makingamaji ili kuzuia mmomonyoko.
 Udongo: Chagua udongo ambao una rotuba na wenye uwezo wa kupitisha maji kwa urahisi.
 Chanzo cha maji: Eneo la Bustani liwe karibu na maji ya kudumu au chanzo cha maji ili kurahisisha umwagiliaji na maji yasiwe na chumvi nyingi kwani huathiri ukuaji wa mimea.
 Kitalu: Kisiwe mahali palipo na kivuli kingi kwani husababisha mimea kutokupata mwangaza wa jua na kushindwa kutengeneza chakula hivyo kuwa dhaifu.
 Kuzuia upepo mkali: Upepo mkali huharibu mimea, kuvunja majani na matawi na husafirisha vimelea vya ugonjwa na wadudu. Eneo la Bustani lioteshwe miti mipakani ili kuzuia upepo mkali.


2. Kutayarisha shamba
Wakati wa kulima ni muhimu kukatua udongo katika kina cha kutosha, mabonge yalainishwe ili kurahisisha upitaji wa maji na hewa katika udongo. Wakati wa kiangazi, tengeneza matuta yaliyodidimia kidogo ili kufanya maji yaweze kukaa kwenye udongo na wakati wa masika matuta yainuliwe kidogo toka kwenye usawa wa ardhi ili kuzuia maji yasituame.

3. Kutumia mbegu bora
Mbegu bora ni zile zilizokomaa na kukauka vizuri, ambazo hazijashambuliwa na magonjwa au wadudu na zenye uwezo wa kuota vizuri zikipandwa. Inashauriwa kununua mbegu kutoka kwa wakala halali.

4. Kuotesha na kupanda mboga
Kina cha kuotesha mbegu kinategemea na ukubwa wa mbegu yenyewe. Mbegu ndogo, hupandwa katika kina kifupi zaidi kuliko mbegu kubwa. Baadhi ya mbegu huoteshwa kwanza kwenye kitalu kisha mche huhamishiwa bustanini au shambani.

5. Kumwagilia maji
Hakikisha udongo una unyevu nyevu wa kutosha wakati wote na mmea unapata maji. Epuka kumwagilia maji mengi sana kwani husababisha miche au mbegu kuoza.

6. Kuweka kivuli na matandazo
Utandazaji wa majani makavu na uwekaji wa kivuli ni muhimu ili kuzuia jua linaloweza kunyausha miche. Matandazo huhifadhi unyevu, joto la udongo na hupunguza palizi ya mara kwa mara.

7. Matumizi ya mbolea
Mboga hustawi vizuri zaidi katika udongo uliowekwa samadi, mboji au mbolea vunde ya kutosha huwekwa kwenye udongo kabla ya kupanda au kupandikiza mimea. Debe moja huhitajika kwenye tuta lenye upana wa mita moja. Mbolea huuongezea mmea virutubisho na kuufanya ukue na kuzaa vizuri.

8. Kubadilisha mazao
Utaratibu huu ni ule wa kuacha kupanda mfululizo aina ile ile ya zao katika eneo moja. Inashauriwa kubadilisha aina ya zao ili kusaidia kupunguza kuenea kwa magonjwa na wadudu na pia kuhifadhi rotuba ya udongo.

9. Matunzo mengineyo
Kupalilia na kukatia mimea pale inapohitajika ni muhimu sana kwani magugu hufanya mimea isikue vizuri kwa kutumia virutubisho kutoka kwenye udongo.
10. Kuvuna
Mboga nyingi za majani hutakiwa kuvunwa kabla hazijakomaa sana. Baada ya kuvuna, inashauriwa kuweka mboga kwenye eneo safi na salama ili kuweza kuzuia magonjwa yatokanayo na vyakula. Kumbuka kuosha mboga kabla ya kula au kupika.

Posted bd elias and vai

RAISI KIKWETE AKAGUA SHAMBA LA ZABIBU ZAMWINO MKOA DODOMA

Raisi Jakaya Kikwete na Mama Salma wakikagua la kilimo cha zabibu la SACCOS ya kilili cha Chalangali wilyani ambalo hutumia umwagiliaji wa matone chamwino mkoani Dodoma
                                   (PICHA NA IKULU0
                      

posted by Elias @vai

Tuesday, February 10, 2015

VIONGOZI WA KANISA LA ANGLIcANA WATEMBELEA SHAMBA LA WAZIRI MKUU ZUZU DODOMA KUJIFUNZA KILIMO CHA ZABIBU NA EMBE




Waziri mkuu,mizengo pinda akiwaonesha viongozi wa kanisa la Anglikana kutembelea shamba lake la zabibu lililopo Zuzu Dodoma February 9,2015 maana ya viongozi hao kutembelea shamba hilp ni kujifunza na kuwa na lengo la kuanzisha shamba linalofanana na hilo dodoma Askofu Dickson chilongani wa Dayosisi ya Dodoma (kushoto) Askofu Maimbo Madolwa wa Dayosisi ya Tanga (wapili kushoto)na wa kulia ni Bi. Canon,Johnson Chinyongole ambaye ni katibu Mkuu wa kanisa hilo

Waziri Mkuu M izengo Pinda akiwaonesha viongozi wa kanisa la Anglican kutembelea shamba lake la zabibu lililopo Zuzu Dodoma

                                               (PICHA NA IKULU)

Posted by elius

KILIMO BORA CHA MAHINDI

Mahindi ni chakula muhimu na ni aina ya nafaka katika mataifa ya Afrika yaliyomo kusini mwa jangwa la Sahara. Ni chakula cha matumizi ya nyumbani kwa idadi ya watu inayokadiriwa kuwa asilimia 50. Ni chanzo muhimu cha madini na kuongeza nguvu mwilini, protini, madini ya chuma (iron) vitamini na madini mengine asilia.Waafrika hutumia mahindi kwa njia mbalimbali – (uji, ugali na pombe). Na mahindi ya kuchoma. Kila sehemu ya mmea wa mahindi ina thamani kiuchumi : punje, majani, shina na magunzi huweza kutoa kiasi kikubwa cha bidhaa nyinginezo zilizo chakula na zisizokuwa chakula.

Vile vile mahindi ni chakula muhimu cha mifugo (ng’ombe) na huhifadiwa kama silage. Pia mabaki ya mimea na nafaka na pia hutumika viwandani kutengeneza wanga na mafuta. 
Mahitaji ya mahindi katika hali ya hewa, udongo na Mahindi ni mimea ambayo hustahimili mabadiliko mengi ya hali ya hewa na humea katika maeneo mengi tofauti. Kuna aina nyingi za mahindi yanayotofautiana katika muda wa kukomaa, mahindi huwa na ustahimili mkubwa kwa mabadiliko katika kiwango cha joto. Mahindi haswa huwa mimea ya maeneo ya joto ambako unyevu ni wa kutosha. Mmea huu unahitaji kiwango cha joto cha kila siku cha nyuzi joto 20º ili umee vyema. Joto la juu sana kwa mazao mazuri ni kama nyuzi joto 30º. Hupandwa sana katika sehemu zilizo katika kimo cha mita 3000 kutoka bahari hadi kwenye ukanda wa pwani. mahindi yaweza kupandwa kama chakula cha mifugo. 


Monday, February 9, 2015

MIGOMBA - KANUNI ZA KILIMO BORA

Hapa Tanzania kilimo cha migomba kimekuwepo Kwa miaka mingi. Kilimo hiki ni maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika kama chakula kikuu kwa baadhi ya mikoa kama vile Kagera, Kilimanjaro na Mbeya na hivyo kulifanya muhimu, kufuatia mazao ya mahindi, mpunga, mtama, muhogo,viazi na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharage.
Zao la ndizi linaweza kuwa moja kati ya mazao ya biashara iwapo litazalishwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hilo, ikwa ni pamoja na kupanda aina bora ya migomba inayozaa ndizi zinazotambulika katika masoko ya kimataifa.

ASILI YA MIGOMBA
Asili ya migomba ni nchi za Malaysia na India ambazo ziko Kusini Mashariki mwa Asia. Migomba inayolimwa sasa imetokana na migomba ijulikanayo kama Musa balbisiana ambayo asili yake ni India, na Musa acuminata ambayo asili yake ni Malaysia. Kutoka Malaysia na India migomba ilifika Afrika Mashariki katika karne ya tano



Sunday, February 8, 2015

KILIMO CHA EMBE


(picha:croppak blog)

KILIMO CHA EMBE

Zao la embe hustawi vizuri katika maeneo ya tambarare na miinuko kati ya futi 0-600 usawa wa bahari. Kiwango cha wastani cha mvua inayohitajika kwa kilimo cha embe ni mililita 650 hadi 1850 kwa mwaka. Miembe hustawi katika udongo wenye uchachu (ph) kati ya 5.5 na 7.2. udongo wenye chachu zaidi huwa na upungufu wa madini mbalimbali ikiwemo Zinki, Chuma, Fosforas na Kalsham.

KUANDAA MASHIMO

Kuchimba mashimo mapana kutafanya udongo uwe laini ili kusaidia mizizi kuzaliwa kwa wingi, upana wa shimo uwe sentimita 60x60 upana kwa urefu, kwa maeneo yenye udongo mgumu na miamba ya mawe kipimo kiwe sentimita 100x100 upana na urefu. Uchimbaji wa mashimo uwe wa kutengeneza udongo katika
sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni udongo wa juu wa kina cha sentimita 30 na sehemu ya pili ni udongo sentimita zilizobaki za kina cha shimo.



KILIMO BORA CHA MPUNGA CHA UMWAGILIAJI


Maandalizi sahihi ya shamba ni jambo la msingi katika kuboresha kilimo cha umwagiliaji wa mpunga. shamba lisipoandaliwa vema husababisha mbinu bora zinazoshauriwa kutoonyesha matokeo katika kiwango kinachotarajiwa hasa katika uzalishaji. Kimsingi maandalizi ya shamba yanatakiwa yafanyike kwa usahihi
na kwa wakati katika mtiririko unaotakiwa. Zifuatazo ni hatua saba muhimu na za msingi katika kilimo cha mpunga
1. KUSAFISHA SHAMBA
Safisha shamba mapema kabla ya msimu kuanza. Kusanya na kuangamiza visiki na takataka nyingine zote. Masalia ya mazao yanaweza kutumika kutengeneza mbolea ya mboji. Inapobidi tumia moto kwa uangalifu sana maana moto unaweza kuharibu mazingira, unaua wadudu rafiki, unaharibu udongo na kuteketeza mboji.

2. KULIMA
Kulima husaidia kupunguza kiasi cha magugu, huruhusu mzunguko mzuri wa hewa na maji, hurahisisha mizizi kupenya na kuchanganya masalia ya mazao kwenye ardhi. Wakati wa kulima uangalifu unahitajika ili kuzuia kuharibu usawa wa ardhi. Kina cha kulima kiwe kati ya sentimeta 10 na 15. Ili kurahisisha na kuharakisha kazi ya kulima ni vema kutumia zana/mashine rahisi kama Trekta la mkono na wanyamakazi