Tanzania imeweza kupiga hatua katika uzalishaji wa zao la korosho kutokana na Elimu iliyotolewa kwa wakulima na wataalamu wa utafiti wa kilimo cha Korosho na Magonjwa ya Korosho kutoka chuo Naliendele kilichopo mkoani Mtwara.
Dr. Louis Kasuga ameyasema hayo katika semina ya ufufuaji wa mikorosho iliyotelekezwa, semina inayo jumuisha mikoa 3 ya mbeya,Njombe , na Ruvuma kwa kueleza mafanikio yaliyo patikana baada ya utafiti.
Dr Louis Kasuga amesema uzalishaji wa korosho kwa Tanzania nzima mwaka 1974-1975 ulikuwa tani 145,000lakini kutokana na magonjwa mbalimbali na kuhama bila mpango kiasi kilishuka hadi kufikia tani 16,000 kwa mwaka kwa katika Tanzania Nzima
Dr louis Kasuga mtaalamu wa utafiti wa magonjwa ya korosho amesema baada ya juhudi za serekari kufanya utafiti na kubaini chanzo cha matatizo iliweza kuongeza uzalishaji wa korosho kutoka tani 16,000 kwa mwaka hadi kufikia tani 158,000 kwa mwaka
Wakulima wa Zao la korosho kutoka mikoa ya Njombe ,Mbeya na Ruvuma wamesema kinachosababisha kuzorota kwa zao la korosho ni kuchelewa kwa pembejeo na ukosefu wa masoko na bei ya uhakika.
Mgeni Rasmi katika semina hiyo Kasimu Andrew Maswaga amesema wakulima wajue kuwa kilimo ni ajira kama walivyo ajiliwa watu wengine Serikarini kuna kupanda na kushuka.
Katika Tanzania kuna Miti ya mikorosho ipatayo 40,000,000 na katika miti hiyo ipo mingine ambayo imeshambuliwa na magonjwa , asilimia 80% ya miti ya mikorosho ili pandwa mwaka 1950 jambo linalosababisha kupungua kwa uzalishaji, kampeni zimeanza za kupanda miche mipya ya ya kisasa pamoja na pandikizi matawi ya kisasa.
No comments:
Post a Comment