Friday, April 10, 2015

Wafanyabiashara wagoma kununua mazao ya kilimo

Wafanyabiashara wagoma kununua mazao ya kilimo


Wafanyabiashara wagoma kununua mazao ya kilimo
Wafanyabiashara ya mazao ya kilimo wilayani mpwapwa wamegoma kununua mazao mbali mbali kutoka kwa wakulima kutokana na kile wanachodai kuwa tabia ya viongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kupandisha tozo za ushuru wa mazao kiholela bila kuwashirikisha.

Mgomo huo umekuja mara baada ya Halmashauri ya MPWAPWA kupandisha ushuru wa mazao kutoka shilingi elfu moja hadi elfu tano kwa gunia moja la mahindi na shilingi elfu moja hadi tatu kwa mazao mengine hali ambayo imezua malalamiko kutoka kwa wakulima.

NJOMBE waanza kutumia mbegu mpya za viazi mviringo

NJOMBE waanza kutumia mbegu mpya za viazi mviringo
Mbegu Bora Nne za Viazi Mviringo zimeanza kutumika katika wilaya ya WANGING’OMBE, Mkoani NJOMBE, kufuatia utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, UYOLE, na kubaini kuwa mbegu hizo ni bora kwa kilimo.

Afisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya hiyo , HENRY VAHAYE amesema wakulima wamekuwa na mwitiko katika matumizi ya mbegu hizo ambazo zinatajwa kuhimili magonjwambalimbali ya mazao.

Watalaam wa kilimo katika Halmashauri ya wilaya Mpya ya Wanging’ombe, wamesema kugunduliwa kwa mbegu hizo Nne za Viazi Mviringo,yawezekana ikawa suluhisho la adui Umaskini katika wilaya hii Mpya.

Pamoja na Mbegu hizo mpya za Viazi Mviringo ambazo zimeanza kutumiwa na wakulima wa wilaya tano za mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya, inadaiwa magonjwa mengine yamedhibitiwa isipokuwa Ugonjwa wa Mnyauko ambao umekuwa ni sumu kwa mimea ya mizizi nchini.

HANANG watakiwa kupanga matumizi bora ya ardhi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Dkt. MARY NAGU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Dkt. MARY NAGU, amevitaka vijiji vyote wilayani HANANG mkoani MANYARA, kupanga matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro miongoni mwa makundi mbalimbali katika jamii

Dkt. NAGU ametoa wito huo wakati wa ziara yake katika vijiji vipya vilivyosajiliwa mwaka jana na kuwataka wananchi kushirikiana na viongozi wao kudumisha amani miongoni mwao.

Waziri NAGU amewaeleza wananchi hao kuwa uamuzi wa serikali wa kuanzisha vijiji vingi zaidi umelenga kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi.

Hata hivyo ameonya kuwa bila kupanga matumizi bora ya ardhi katika vijiji ili kuyapanga makundi mbalimbali yaweze kuishi kwa usalama, upendo na mshikamano, maendeleo ya haraka yaliyokusudiwa hayawezi kufikiwa kwa wakati.

Viongozi wa vijiji hivyo kwa upande wao, wameiomba serikali na Mbunge huyo wa Jimbo la HANANG, kuwasaidia kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika maeneo yao ikiwemo maji, elimu na baadhi ya barabara za vijiji.

Katika ziara hiyo pia ambayo mpaka sasa imehusisha vijiji vipya 30, DOKTA NAGU amewahimiza wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, kujiunga katika mfuko wa afya ya jamii-CHF ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya wilayani humo pamoja na kuipigia kura katiba inayopendekezwa wakati utakapofika.

Wednesday, April 8, 2015

ULIMAJI WA VITALU VYA BUSTANI BIASHARA RAHISI YENYE FAIDA



ULIMAJI WA VITALU VYA BUSTANI BIASHARA RAHISI YENYE FAIDA

ULIMAJI WA VITALU VYA BUSTANI BIASHARA RAHISI YENYE FAIDA
Katika falsafa ya Kilimo kwanza nchini Tanzania, baadhi ya watanzania wengi wameitikia kauli hiyo na baadhi ya wafanya biashara na wakulima mbalimbali kusahau suala la ulimaji na utunzaji wa vitalu Bustani kama Maua, miche ya matunda, miti, nyanya na mazao yoyote ya bustani ni biashara rahisi na yenye faida.
Ukulima wa vitalu vya Bustani ni biashara ambayo inafanya vizuri na kupata mwitikio mkubwa katika nchi mbalimbali hususani Kenya nchi jirani na Tanzania ambapo wanawake wamewekeza katika biashara hii na kupata mafanikio kwa urahisi kama mwanamama Loyce ambaye pia ni msomkama anavyvo elezea katika kidokezo hapo chini.
Aidha teknolojia hii ni chanya kwa watanzania kuanza kuitumia kwani Tanzania ni nchi yenye rutuba nzuri kwa kilimo na asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima wakitegemea kilimo kama uti wa Mgongo. Hata hivyo Njia Mpya inalitazama suala hili kwa jicho pana na faida kwa mkulima au mfanyabiashara wa ulimaji na utunzaji wa vitalu na kuiona ni fursa muhimu kwa mfanyabiashara kupitia njia hii kupata kipato na hatimaye kupunguza na kuondoa kabisa umasikini katika familia na nchi kwa ujumla. Kuna maadui watatu ambao ni hatari sana kwa maendeleo katika jamii nao ni “Umasikini, Ujinga na Maradhi” ni wakati sasa wa kupambana na umasikini huu tujitokeze na kuiona fursa hii. Biashara hii haibagui wanaume wala wanawake 

Vijana waaswa kutumia Fursa wazipatazo

WAZIRI wa habari vijana utamaduni na michezo FENELLA MKANGARA
WAZIRI wa habari vijana utamaduni na michezo FENELLA MKANGARA,amewashauri vijana kote nchini kuwa wabunifu na kutumia fursa zinazojitokeza mbele yao ili kujiletea maaendeleo

Hayo ameyasema katika mkusanyiko wa magari hamsini na pikipi 10 za vijana wa BONGO RIDE wakiwa tayari kufanya msafara unaotwa BONGO CHARITY CRUIZE kutoka DAR hadi MORO.

mkurugenzi wa makapuni ya TSN GROUP, FAROUQ BAGHOZA anaeleza kwa nini amedhamini msafara huo kuwa ni kuwaleta vijana pamoja na kuibuwa vipaji vya vijana hapa nchini.

Msafara huo wa MAGARI na PIKIPIKI kutoka DAR HADI MOROGORO, utatembelea kikundi cha watu wanaoshi na virusi vya ukimwi mkoani morogoro,WAVUMO ili kujua shida zao na kuzitafutia ufumbuzi.

Monday, April 6, 2015

Mkutano wa Sita wa Baraza la mwaka la wadau wa Tasnia ya Nyama Tanzania

Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania anawatangazia wadau wote wa Tasnia ya Nyama nchini kwamba kutakuwa na Mkutano wa Baraza la Mwaka hivi karibuniMsajili wa Bodi ya Nyama Tanzania anawaalika  kuhudhulia Mkutano wa Baraza la Mwaka la Wadau wa Tasnia ya Nyama hapa nchini ambao utafanyika tarehe 15/04/2015 na 16/04/2015,katika hoteli ya Glonency 88, saa 2:30 asubuhi. Wajumbe wa Mkutano huu ni wadau wote walioteuliwa na Mhe. Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwa mujibu wa Sheria ya Nyama Na. 10 ya Mwaka 2006 kutoka:-
  1. Mamlaka zote za Serikali za Mitaa za Tanzania Bara,
  2. Taasisi za Serikali, Wizara na Idara za Serikali.
  3.  Asasi za kiraiya zenye maslahi na tasnia ya nyama
Taarifa ya tarehe na mahali utakapofanyika mkutano huu zitatolewa baadae.

Aidha, wadau wenye nia ya kushiriki kwa lengo la kubadilishana na uzoefu kwenye tasnia na hawako kwenye orodha tajwa hapo juu wawasiliane na Msaji wa Bodi ya Nyama Tanzania.

Agriculture - Tanzania

Agriculture is the leading sector of the economy of Tanzania. Apart from providing food, agriculture remains the country's main source of income for the rural population, which forms 80% of the total population and employs 70% of the active labour force of the population. It contributes about 50% of the GDP and about 75% of the foreign exchange earnings. In Tanzania Agriculture is dominated by smallholder farmers with farm sizes ranging between 1 hectare and 3 hectares. Most of these smallholders use the hand hoe as the main cultivating tool. Ox ploughs are used by about twenty percent of the farmers and about ten per cent use tractors.
A wide variety of crops can be grown in Tanzania due to its wide climatic variation and agro-ecological conditions. Area cultivated for food production makes up the bigger part of land under crop production. Maize and rice are principal food crops as well as commercial crops, while cassava and bananas are important subsistence crops. Traditional export crops of Tanzania are coffee, cotton, tea, sisal and cashew nuts. Other widely grown crops include beans, sorghum, millet, sweet potatoes and various types of oil seeds. A wide variety of fruits, vegetables and flowers are also grown in Tanzania.

Wilaya ya Kwimba yakabiliwa na Njaa


Wilaya ya KWIMBA mkoani MWANZA inahitaji msaada wa zaidi ya Tani Elfu Kumi za chakula ili iweza kukabilina na tatizo la njaa ambalo limeikumba wilaya hiyo. 

Mkuu wa wilaya ya KWIMBA - PILI MOSHI amethibitisha wilaya hiyo kuhitaji msaada wa haraka wa chakula kufuatia hali ya ukame uliosababisha kukauka kwa mazao mbalimbali. 

Mkuu wa wilaya hiyo ya KWIMBA alikua akitoa taarifa hiyo kwa wajumbe wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi – CCM wilayani KWIMBA, viongozi pamoja na watendaji wa serikali wa wilaya hiyo.