Friday, March 20, 2015

Ufugaji Bora wa Kwale, Na faida ya Bidhaa zitokanazo na KWALE

Ufugaji wa KWALE ni njia bora na rahisi sana kwa mfugaji yeyote aliyetayari kukuza kipato chake kwa haraka sana na kwa kiwango cha juu.

KWALE ni jamii ya ndege ambao kwa sasa wanafugwa majumbani na wanaotaga mayai kama kuku ama bata na kwa wingi sana. Ndege hawa ni wadogo 280gm - 300gm, Wanarangi ya brown, nyeusi au hata nyeupe yenye miraba na madoa ya rangi ya ugondo au kijivu. Manyoya yao pia yana rangi ya brown au nyeupe na yenye madoa yanayovutia. 

Kutaga na kuatamia

KWALE dume humpanda jike kwa muda kidogo, Hapo jike anakuwa tayari kutaga na hutaga mayai 290 hadi 310 kwa mwaka (hii hulingana na lishe nzuri atakayopatiwa).
Mayai ya KWALE huatamiwa kwa siku 18 na huanza kuanguliwa vifaranga kwa muda wa siku 2, kuanzia siku ya 18 na hadi 20.
Njia bora ya kutotolesha mayai ya KWALE ni kwa kutumia incubator ambapo mayai huatamiwa kwa wingi ndani ya siku 18.

BRN yaanza kuwanufaisha wakulima wa umwagiliaji


Wakulima katika skimu 78 za umwagiliaji nchini, wameanza kunufaika na Mpango wa matokeo makubwa sasa kwaajili ya kilimo shadidi cha zao la mpunga kwa kulima eneo dogo na kuvuna mazao mengi. 

Mratibu wa kilimo shadidi kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt KISSA KAJIGILI amesema shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo - UNDP kwa kushirikiana na serikali wamedhamiria kuboresha kilimo kupitia kilimo shadidi. 

Tayari kilimo shadidi kimekuwa mkombozi kwa baadhi ya nchi barani afrika ambazo wakulima wan chi hizo,ikiwemo nchi za madagaska, Burkinafasso, Mali na zingine nyingi,nchini hapa wakulima katika skimu za umwagiliaji mkoani Morogoro, Arusha na hatimaye mkoani Mbeya,tayari wamefikiwa.

serikali yaomba wakulima kuhama katika vyanzo vya maji

Waziri wa maji prof JUMANNE MAGHEMBE
Waziri wa maji prof JUMANNE MAGHEMBE ameagiza kuwa watu wanaoishi au kulima katika vyanzo vya maji waondoke ili kutekeleza sheria ya maji ya mwaka 2009 inayoeleza kuwa shughuli zozote za kibinadamu zisifanyike katika vyanzo ili viwe endelevu . 


Akizungumza na wakazi wa vijiji vya MUMAGUNGA, LIGAMBA na KITARAMAKA wilayani BUNDA mkoani MARA kwa nyakati tofauti, waziri MAGHEMBE amesema serekali haitawafumbia macho watu watakaokaidi agizo hilo na kuagiza viongozi kusimamia utekelezaji wake. 



Awali akimkaribisha Mgeni rasmi, mkuu wa wilaya BUNDA JOSHUA MIRUMBE ameeleza kuwa Halmashauri ipo katika hatua za mwisho kukamilisha miradi miwili ya maji ambapo hadi kufikia Desemba mwaka huu zaidi ya asilimia 58 ya wakazi wa BUNDA watakuwa wamepata maji safi na salama. 



Katika ziara hiyo prof MAGHEMBE amezindua miradi miwili ya maji iliyogharimu zaidi milioni mia saba na kuwaeleza wananchi kuwa miradi hiyo ni mali yao hivyo wailinde.

Serikali yaanza kutwaa baadhi ya hati za umiliki wa mashamba ya wawekezaji


Serikali imeamua kutwaa baadhi ya hati za umiliki wa mashamba ya wawekezaji katika Bonde la KIRUSIX wilayani BABATI mkoani MANYARA ili zifanyiwe kazi upya. 

Akizungumza na wakazi wa kijiji cha KIRUSIX Mkuu wawilaya ya BABATI, CRISPIN MEELA amesema hatua hiyo inalenga kutatua migogoro ya ardhi ya muda mrefu baina ya wananchi na wawekezaji walioko katika eneo hilo. 

Wakaazi wa Kijiji cha KIRUSIX, wilayani BABATI, mkoani MANYARA, wamesema kuwa migogoro ya ardhi katika Bonde la KIRUSIX baina ya wawekezaji na wananchi imedumu kwa zaidi ya miaka 40 na wameiomba serikali itatue misuguano hiyo inayotishia amani na usalama katika eneo hilo 

Mkuu wa wilaya ya BABATI, CRISPIN MEELA, amesema kuwa kuendelea kwa migogoro hiyo kumesababishwa na baadhi ya watu waliokuwa wakinufaika nayo kwa namna moja au nyingine na kwamba sasa serikali imeamua kwa dhati kuimaliza migogoro hiyo 

Hata hivyo Mkuu huyo wa wilaya ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya, CRISPIN MEELA, amekemea tabia ya baadhi ya watu wanaochoma mali, kuiba na kuharibu mashamba ya wawekezaji kwa kisingizio cha migogoro iliyoko katika Bonde la Kirusix 

Wakaazi hao wameelezea kuridhishwa na uamuzi wa serikali na kumpongeza mkuu huyo mpya wa wilaya ya BABATI kwa ujasiri wake na kusema ukweli kuhusu mambo yanayotokea katika Bonde hilo 

Migogoro ya ardhi katika bonde la KIRUSIX, Imesababisha hasara kubwa baada ya mali za wawekezaji zenye thamani ya zaidi ya shilingi BILIONI 4 kuchomwa moto na watu wasio fahamika huku ikishuhudiwa watu wawili wakipoteza maisha

Thursday, March 19, 2015

UMUHIMU WA CHANJO KWA MIFUGO

Na Nassor S. Mohammed
Mifugo ni rasilimali ambayo huwapa faida kubwa wafugaji na wananchi. Ili mifugo itoe mazao yenye tija inahitaji kupatiwa huduma bora za malisho, maji, kinga na tiba za maradhi. Maradhi ni moja kati ya matatatizo yanayozorotesha sekta ya ufugaji na kupunguza uzalishaji. Katika kukabiliana na changamoto hiyo hatua za kuyadhibiti maradhi zinachukuliwa duniani kote ili kuimarisha ufugaji na kupata tija.
Chanjo
Chanjo ni mchanganyiko maalum wenye vijidudu ambavyo vimepunguzwa nguvu ili visilete madhara kwa wanyama au watu waliochanjwa. Hii ni njia mojawapo inayotumika katika kudhibiti maradhi duniani. Asili ya chanjo ilitokana na ugunduzi wa mwanasayansi wa Uingereza Bw. Edward Jenner katika karne ya 18 ambapo aligundua kwamba wahudumu wa ng’ombe hawakupata ugonjwa aina ya ndui (small pox) kutokana na kuwa na vijidudu vya ugonjwa wa ndui za ng’ombe (cow pox) hali ya kuwa maeneo mengine wasiokuwa wahudumu wa ng’ombe waligundulika kuwa na ugonjwa huo.
Chanjo husababisha mwili wa mnyama au binadamu kuandaa askari (vikinga mwili ni antibody) ambao hukaa mwilini kwa muda maalum na huukinga mwili kukabiliana na
vijidudu vya maradhi. Aidha, chanjo ikipungua nguvu inahitajika wanyama wachanjwe tena kwa muda maalum uliopendekezwa kutokana na aina ya chanjo au mnyama.
Aina za chanjo

Miongoni mwa chanjo maarufu zinazotumika kwa mifugo ni; Hitcher B1, LaSota, S19/ Rev- 1 strain, Blanthrax, Rabisin, Tetanus Toxoid, Newcastle Disease vaccine EDS – 76 + ND + IBD, Fowl pox, Clon CL/76 strain, Canine distemper, Marek’s disease
vaccine, Foot and Mouth Disease, Gumboro, Mahepe/Mdondo/Kideri, Ndui, Pepopunda, Kimeta, Chambavu, Ugonjwa wa kutupa mimba kwa ng’ombe, Ugonjwa wa mapafu wa ng’ombe na mbuzi, Ugonjwa wa bonde la ufa, Ugonjwa wa ngozi (Lumpy skin, Streptothricosis, Warts, Mange) Ugonjwa wa miguu na midomo,
Maradhi yanayochanjwa na muda unaopendekezwa
-Chanjo ya Gumboro kwa kuku wachanga mara moja katika uhai wake;
-Chanjo ya Mahepe/Mdondo/Kideri kwa kuku mara mbili katika uhai wake;
-Chanjo ya Ndui kwa kuku na ng’ombe mara moja;
-Chanjo ya ugonjwa wa kutupa mimba kwa ng’ombe mara moja kwa mwaka;
-Chanjo ya ugonjwa wa Kimeta kwa ng’ombe kila mwaka;
-Chanjo ya ugonjwa wa Chambavu kwa ng’ombe kila mwaka;
-Chanjo ya ugonjwa wa pepopunda (Tetenasi ) kwa ng’ombe kila mwaka;
-Chanjo ya ugonjwa wa ngozi kwa ng’ombe, mbuzi na kondoo kila mwaka;
-Chanjo ya ugonjwa wa miguu na midomo kwa ng’ombe kila mwaka;
-Chanjo ya ugonjwa wa homa ya mapafu kwa ng’ombe na mbuzi kila mwaka;
-Chanjo ya Kichaa cha mbwa kwa mbwa kila mwaka;
-Chanjo ya ugonjwa wa matumbo hasa kwa mbwa wadogo pia unaweza kuchanja kwa wakubwa kila mwaka;
-Chanjo ya Ugonjwa wa sotoka kwa ng’ombe kila mwaka;
-Chanjo ya ugonjwa wa bonde la Ufa kwa ng’ombe;
-Chanjo ya ugonjwa wa Farasi kwa farasi kila mwaka.
Wanyama wanaochanjwa
Wanyama hao ni pamoja na ng’ombe, mbuzi kondoo, nyati, ngamia, mbwa, paka, farasi na jamii ya ndege wakiwemo kuku wa aina zote wa mayai nyama na wa kienyeji.
4
Faida za Chanjo
• Chanjo hudhibiti magonjwa yanayosababishwa na vimelea vya aina ya virusi, bektiria, rikesia na protozoa;
• Chanjo huongeza uwezo wa mnyama kujikinga na maradhi;
• Chanjo hulinda afya ya mifugo baada ya lishe bora na;
• Chanjo hudhibiti magonjwa yasiyoweza kutibika.
Njia na sehemu za kuchanja
• Kupitia mdomoni kwa magonjwa ya mahepe/mdondo/kideri, Gumboro kwa kuku;
• Kwenye bawa kwa ugonjwa wa ndui kwa kuku;
• Chini ya ngozi kwa magonjwa kama ya ngozi.
Mambo ya kuzingatia katika uchanjaji
Chanjo zihifadhiwe kwenye hali ya ubaridi na zisiwekwe kwenye joto au mwanga wa jua, wanyama wanaochanjwa ni lazima wawe na afya nzuri na hawajaambukizwa magonjwa yaliyokusudiwa kuchanjwa. Inashauriwa chanjo zifanywe na wataalamu wa mifugo au wafugaji waliopewa mafunzo ya kuchanja.
Chanjo zinaweza kuleta madhara ikiwa zitatumiwa wakati muda wake wa matumizi umekwisha (expired).
Aidha, chanjo zenye vijidudu vilivyohai zinaweza kuambukiza maradhi kwa wanyama waliochanjwa.
‘KINGA NI BORA KULIKO TIBA’

MKUU WA MKOA WA RUKWA AONANA NA WATAFITI KUTOKA TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO UYOLE MBEYA KUJADILI KUINUA KILIMO CHA NGANO MKOANI RUKWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na watafiti kutoka taasisi ya Utafiti wa Kilimo Uyole iliyopo Mkoani Mbeya walipomtembelea ofisini kwake leo kutambulisha mpango wa SARD (Strategic Agriculture Reseach Development) unaodhaminiwa na Benki ya Maendeleo 
ya Afrika ADB (Africa Development Bank). Mpango huo una lengo la kupunguza utegemezi wa chakula nchini kwa kuongeza uzalishaji wa vyakula mbalimbali ikiwemo zao la ngano ambalo ni sehemu ya mradi huo Mkoani Rukwa. Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alisisitiza juu upatikanaji wa masoko ya kudumu kwa mazao yatakayozalishwa katika mpango huo badala ya kuwekeza nguvu katika uzalishaji pekee. 
Ndugu Anthony langa mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Uyole Jijini Mbeya ambae pia ni Mratibu wa Utafiti wa Zao la Ngano Tanzania akizungumza katika kikao hicho. Amesema mpango huo utahusisha wakulima na vikundi vya wakulima ambao watapatiwa elimu na kuwezeshwa mikopo mbalimbali ya 
kuendeleza kilimo cha ngano Mkoani Rukwa. 
Mkutano ukiwa 

Kikwete ataka kilimo kutumia teknolojia mpya

Na Ibrahim Yamola, Mwananchi

Posted  Jumatano,Januari29  2014  saa 24:0 AM
KWA UFUPI
Alisema uhifadhi wa vyakula katika maghala hauridhishi, kutokana na asilimia 30 ya mazao yanayohifadhiwa huharibika jambo ambalo linaweza kuepukika likitafutiwa ufumbuzi.Rais Kikwete alisema bila kuviwezesha vituo vya utafiti na kuwatumia wataalamu wengi wa kilimo kama mabwana na mabibishamba, sekta hiyo haitapiga hatua.
Alikuwa akifungua mkutano wa wadau wa kilimo na biashara kutoka nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya, jana.
Alisema uhifadhi wa vyakula katika maghala hauridhishi, kutokana na asilimia 30 ya mazao yanayohifadhiwa huharibika jambo ambalo linaweza kuepukika likitafutiwa ufumbuzi.
“Tunatakiwa kutumia ugunduzi wa teknolojia mpya zinazogunduliwa ndani na nje ya nchi kwa vitendo, ili kusaidia kuboresha kilimo nchini jambo ambalo linawezekana tukiamua hasa kwa kushirikiana na wadau wengine,” alisema Rais Kikwete.
Alisema wakulima wengi hususan wadogo wanatakiwa kupewa elimu jinsi ya kulima mazao ambayo yanaendana na udongo wa eneo husika, kazi ambayo inatakiwa kufanywa na mabwana na mabibishamba na wadau wa kilimo.
“Pia, rasilimali fedha na watu katika vituo vyetu vya utafiti wa kilimo vinahitaji kuongezewa nguvu, ili kufanya tafiti nyingi na zitakazoweza kusaidia kutatua matatizo,” alisema.
yanayowakumba wakulima wengi.”

KIWANDA KIPYA CHA KUZALISHA MBEGU BORA ZA MAHINDI JIJINI ARUSHA

Kampuni ya mbegu ya Seedco imezindua kiwanda kipya cha kuzalisha mbegu bora za mahindi na nafaka nyingine kitakachowasaidia wakulima kulima kilimo chenye tija na kupata mazao mengi.
Uzinduzi huo uliongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula Godifrey Zambi ambaye alifungua rasmi kiwanda hicho ,Amesema kuwa tasnia ya mbegu ni tasnia muhimu katika ukuaji wa sekta ya kilimo hiyo amewataka wazalishaji mbegu kuongeza tija ili kukuza kilimo.
Ameeleza kuwa kampuni hiyo imetimiza matakwa ya serikali kwa kwa kuandaa na kuzalisha mbegu nchini badala ya kuagiza kutoka nje na kuzilipia kwa fedha za kigeni .
"Mbegu hizi zinazoandaliwa na kuzalishwa ndani ya nchi zinasambazwa kwa bei rahisi na wakulima wanazipata kwa bei rahisi tofauti na zile zinazoagizwa kutoka nje bei yake huwa juu" Alisema Waziri huyo
Mwakilishi wa Bodi ya Seedco,Profesa Kalunde Simbuge amesema kuwa mbegu hizo bora zinazozalishwa na kiwanda hicho zitawasaidia wakulima kuzalisha chakula cha kutosha na ziada kwa ajili ya kuuza na kujipatia kipato.
Profesa Kalunde anafafanua kuwa wakulima wana jukumu kubwa la kuilisha jamii hivyo wanahitaji mbegu bora zinazoendana na mazingira yao.
Mkulima kutoka Wilaya ya Hai Joel Nkya amesema kuwa ufunguzi wa kiwanda hicho utakidhi mahitaji ya mbegu bora hasa kwa wakulima walioko vijijini.Amewashauri wakulima wenzake kuacha kuona kuwa mbegu halisi ni ghali na kuingia kwenye mtego wa kuuziwa mbegu feki kwa bei rahisi.

Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula Godifrey Zambi Akiongozana na Viongozi wa kampuni ya mbegu ya Seedco ,kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Seedco Frank Wenga ,wakwanza kulia ni Afisa Mauzo Mwandamizi wa kampuni hiyo mkoa wa Manyara Kasim Nyaki na Mwenyekiti wa Seed Co-Afrika Mashariki- Bw. Mike Ndorro wapili kulia .Katika uzinduzi wa kiwanda chao kipya uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula Godifrey Zambi akiweka gunia kwenye mashine ya kusafisha mbegu katika uzinduzi wa kiwanda kipya cha kuzalisha mbegu kilichopo kata ya Kisongo wilaya ya Monduli Mkoani Arusha ,wakwanza mstari wa mbele ni Afisa Mauzo Mwandamizi wa kampuni hiyo mkoa wa Manyara Kasim Nyaki.Picha na Ferdinand Shayo

Monday, March 16, 2015

UTAMBUZI WA MWANZO WA MAGONJWA YA MIFUGO (WANAOCHEUA)

Sifa za mnyama mwenye afya (Ng'ombe, mbuzi na kondoo)
i. Mchangamfu wakati wote macho maang’avu huku mkia na masikio vikimsaidia kufukuza inzi
ii. Kula na kucheua, kunywa maji vizuri kila siku
iii. Kuonyesha ushirikiano na kutembea pamoja kwenye kundi
iv. Kutembea vizuri
v. Anastuka na kukimbia anapostuliwa na mnyama hatari anapomkaribia kamaa vile mbwa mwitu, fisi, chui, simba.
vi. Mwili wake una uwezo mkubwa wa kukibadili chakula anachokula kutoa mazao ya kutosha kama vile maziwa.
vii. Anaonekana mwenye nguvu na kwa wale wanaoendelea kukuna wanaongezeka uzito kwa muda mfupi
viii. Kwa mnyama anayekamuliwa mara kwa mara kupiga kelele za kumtafuta mtoto wake,kiwele huwa kimejaamaziwa, chuchu huwa wakati mwingine zimetanuka upande kwa ajili ya kujaa maziwa
ix. Ngozi ya mnyama husisimka mara kwa mara wadudu wapomtambaa
x. Kwa madume, huwa wana hamu ya kuwapanda majike wanaoingia kwenye joto.
Miili yao hujengeka vizuri. Pumbu hujengeka na kukaa vizuri kwenye nafasi yake
(yaani katikati ya miguu)
xi. Pua na midomo huwa na unyevu unyevu wakati wote.
xii. Ngozi kuwa na ulaini unaotakiwa na manyoya hung’aa.
xiii. Kwa kawaida unapo mkaribia mnyama endapo amekaa chini ni lazima atanyanyuka
Dalili za Mnyama anayeumwa


ULEAJI WA VIFARANGA VYA KUKU SIKU YA 1 HADI WIKI YA 5

UtanguliziKwa kawaida au katika hali halisi, kazi ya kulea vifaranga hufanywa na kuku mwenyewe. Hivyo ili kulea vifaranga, mfugaji ni lazima aige  kuku  anavyofanya.  Ikumbukwe kuwa vifaranga husumbuliwa zaidi na hali mbaya ya hewa, magonjwa mbalimbali, kukosa chakula kisichofaa na kukosa uangalizi wa karibu.Ni lazima  vifaranga waangaliwe kwa  kuwapatia nyumba yenye joto,  chakula kinachofaa na  maji safi, kuwakinga dhidi  ya magonjwa masumbufu kwenye eneo husika na  kuwatibu wanapougua. Mfugaji anayefanikiwa ni yule anayelea vifaranga wenye afya nzuri  ambao hatimaye hutoa mazao mengi yanayompa faida.Wafugaji wengi  vijijini wamezoea kumwachia mama kuku kufuga vifaranga wake kwa muda mrefu hadi  wajitegemee. Njia hii humchelewesha kuku  kurudia kutaga na  hivyo  kupata vifaranga wachache zaidi  kwa  mwaka.  Lakini vifaranga vikiondolewa kwa  kuku  mapema, kama  majuma matano hivi baada ya kuanguliwa, na  wakatunzwa na  mfugaji,  kuku  hutaga mapema na idadi ya kuku kwa mfugaji  huongezeka haraka ndani ya kipindi kifupi.Mwongozo huu  unaeleza jinsi ya  kufuga vifaranga vizuri  ili hatimaye mfugaji  apate faida Zaidi.
Sehemu ya KwanzaNyumba ya kulelea Vifaranga

Ukipenda kujenga nyumba ya vifaranga itafaa ufikirie yafuatayo:-a          Nyumba ya  vifaranga iwe karibu na  nyumba yako  mwenyewe ili uweze kuwakagua vifaranga wako mara kwa mara.b)   Ijengwe hatua 20 au zaidi mbali na nyumba ya kuku wakubwa, hii ni kinga  mojawapo ya kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa.c)   Nyumba ya  vifaranga isiruhusu ubaridi au  unyevu au  wanyama waharibifu kuingia.Lakini nyumba iingize hewa na mwanga wa kutosha kila wakati.d)   Nyumba iwe na  eneo la kutosha ili vifaranga wapate nafasi ya  kutembea kutafuta chakula na maji bila kubanana.e)   Ijengwe kwenye sehemu  isiyoelekea upepo  unaotoka  kwenye nyumba  ya  kuku wakubwa.  Tahadhari hii husaidia vifaranga kuepukana na magonjwa yanayoenezwa na upepo.
Ukubwa  wa Nyumba
Endelea kusoma  HAPA kwa kubonyeza namba 6


UTUNZAJI WA BWAWA LA SAMAKI

UTUNZAJI WA BWAWA LA SAMAKI
Bwawa la samaki linahitaji matunzo ya mara kwa mara ili kuhakikisha linakaa katika hali inayostahili kuwawezesha samaki kuzailiana au kustawi vizuri. Bwawa lisipopewa matunzo mazuri linaweza pelekea wadudu wa magonjwa kujitokeza na kukuletea hasara kubwa sana katika ufugaji wako. Tafsiri ya wafugaji wengi wa samaki ni kwamba ukishatengeneza bwawa basi kinachofuata ni manufaa ya haraka na bwawa litadumu milele bila hata ya kulifanyia matengenezo madogo madogo. Dhana hii ni potofu wala hakuna ukweli wowote, bwawa linahitaji uangalizi wa karibu sana ili kama kuna tatizo lililojitokeza liweze kurekebishwa kwa wakati. Bwawa linaweza kubomoka kingo zake, kuvujisha maji, kujaa matope au kuota miti ndani.Hakikisha unaliangalia bwawa lako kwa kina ili kubaini kama kuna matatizo kwenye bwawa lako. Fanya marekebisho mara moja unapoyabaini ili kulifanya liendelee kuwa katika hali ya ubora na kulifanya lidumu kwa muda mrefu. Yafuatayo ni mambo ya kuangalia kwenye bwawa;

-Hakikisha ukingo/ukuta wa bwawa haujabomolewa na maji na kama umebomolewa urekebishwe haraka.-Kwa mabwawa yaliyotengenezwa kwa kingo za udongo ni vizuri kupanda majani juu ya kingo/kuta hizo ili kuzifanya ziwe imara na hivyo zisibomolewe na maji kwa urahisi na mmonyoko wa udongo.
-Angalia kama kuna majani/nyasi zinazoota kuelekea au ndani ya bwawa na kama zipo ziondolewe kwa kuzikata. Hakikisha kuwa bwawa lako halina magugu maji kwani haya hupunguza uzalishaji wa chakula cha asili cha samaki kwa kuondoa rutuba majini na kuweka kivuli.-Kama kuna miti yenye matawi yaliyoelekea juu ya bwawa, basi matawi hayo yakatwe ili kuzuia majani ya miti kuangukia ndani ya bwawa.-Angalia kama kuna sehemu inavujisha maji na kama ipo izibwe mara moja kabla haijawa kubwa. Fanya hivyo kwa kuangalia pia kina cha maji kama kinapungua kwa haraka.-Kina cha maji kinaweza kupungua kwa bwawa kujaa matope au mchanga, kama kina kimepungua kwa sababu ya matope ni vema matope yakapunguzwa kwa kuyaondoa na kuyatumia kurutubishia shamba.-Ondoa kama kuna uchafu wowote unaoelea ili kuepuka usije ziba mrija wa kutolea maji nje-Pia angalia mirija ya kuingiza na kutolea maji kama inafanya kazi vizuri, kama inatatizo mfano imezibwa na mawe, matope au uchafu mwingine lilekebishwe.-Tazama namna samaki wanavyokula, je wanakula kawaida, wanachangamka? Kama siyo, na kama wanatafuta hewa nje ya maji basi hewa ndani ya maji ni ndogo. Acha kuwalisha na kuweka mbolea na ruhusu maji safi kuingia ndani ya bwawa hadi pale samaki watakapo rudia hali yao ya kawaida. Kama bado angalia kama kuna dalili ya ugonjwa wowote.-Angalia kama kuna dalili ya wanyama wanaoweza kula au dhuru samaki wanaokuja kwenye bwawa kwa kuangalia walimokanyaga, kasha chukua tahadhari.Jambo jingine la kuangalia ni ubora wa maji yaliyoko na yanayoingia kwenye bwawa la samaki. Ubora wa maji ni kitu muhimu sana kwa ukuaji na afya ya samaki. Baadhi ya sifa ya maji kwa ajili ya samaki kama ifuatavyo:i.Hewa ya oksijeni
Endelea kusoma kwa kubonyeza HAPA

KUANDAA NA KUSAFIRISHA MAYAI YA KUKU WA KIENYEJI

Kutunza mayai kabla ya kuyasafirisha
Mayai ya kuku wa kienyeji yakiwa kwenye kiota
Ukiamua kufuga kuku wako wa asili kwa ajili ya kupata mayai ya kuuza, kumbuka kuzingatia mambo yafuatayo: -Usiyaache mayai ndani ya viota kutagia kwa muda mrefu. Yaokote mayai mara kwa mara kutegemeana na utagaji, ili kuepuka kuharibiwa kwa mayai na kuku wenyewe. Mayai yasipohifadhiwa vizuri ni rahisikuharibika. Hivyo ni muhimu yahifadhiwe vyema kabla hayajapelekwa sokoni.-Fanya yafuatayo ili mayai yawe salama:  =Yatenge mayai yenye nyufa, yatumiwe nyumbani kwa kula.  =Kama yamechafuka ondoa uchafu kwa mikono mikavu. Usiyaoshe kwa majiyataharibika upesi, hutaweza kuyahiifadhi kwa muda mrefu. =Yahifadhiwe sehemu isiyokuwa na joto
Kusafirisha mayai 

Mayai yanayosafirishwa yawekwe kwenye chano (tray) za kubebea mayai na kuwekwa kwenye makasha (boksi) kwa utaratibu ufuatao:-• Mayai yapangwe kwenye chano sehemu iliyochongoka ikiwa inaangalia chini• Chano zipangwe ndani ya kasha kwa mpango unaokubalika• Kasha liwe na ukubwa unaolingana na chano kuepusha mtikitisiko• Kasha liruhusu mzunguko wa hewa• Kasha liwe imaraKama hakuna chano ndani ya mazingira yako, yapakie mayai katika chombo imara kwakuyachanganya na pumba ya mpunga au kitu chochote laini kuzuia yasivujike. 

Mayai kwenye chano (tray) tayari kwa kusafirisha

CHANZO: Rural Livelihood Development Company 

MPAPAI (Carica papaya) DAWA YA KUTIBU MAGONJWA YA MIFUGO

Asili ya mpapai ni Amerika ya Kati. Matunda, majani na utomvu wake hutumiwa kama dawa maeneo mbalimbali ya dunia, matunda na utomvu wake umekuwa ukitumika kutengeneza bombe na waini. Mpapayi una viini hai vingi lakini hivi viwili ni muhimu kwa kutibu magonjwa na kusaidia mmeng’enyo wa chakula ufanyike vizuri: chymopapain and papain. Kiasi cha viini hai hivi hutofautiana kwenye matunda, utomvu, majani na mizizi lakini pia kutegemeana na umri wa mti na njia ya kutengeneza dawa yenyewe.
Matumizi kwa mifugo

-Kutibu magonjwa ya bakteria: Matawi na mbegu za mpapai vina uwezo wa kutibu magonjwa yanayoenezwa na bakteria hawa: Staphylococcus aureua, Escherichia coli, Salmonella typhi na Bacillus subtilis.-Kutibu magonjwa ya fangasi: Utomvu wa mpapai unauwezo wa kutibu fangasi inayoenezwa na Candida albicans-Magonjwa ya minyoo:Unga wa mbegu za mpapai unauwezo wa kutibu minyoo ya umbwa inayojulikana kamaDirofilaria immitis (inayoshambulia moyo). Wapewe dozi ya milligram 60 kwa kila kilo moja ya uzito wa mbwa kwa muda wa siku 30. Minyoo mingine pia inaweza kutibiwa na mmea wa mpapai kama Ascaris suum kwa nguruwe katika dozi kati ya milligram 4-8 kwa kila kilo moja ya uzito wa nguruwe kwa muda wa siku 7. Utibuji wa minyoo kwa mifugo ndiyo kivutiuo kwa wafugaji.
-Mpapai pia unauwezo wa kusaidia mnyama aharishe ili kutoa kitu ambacho hakifai tumboni.Kwa binadamu mmea huu umekuwa ukitumika sehemu mbalimbali kutibu magonwa/matatizo yafuatayo: Kuharisha na kuharisha damu, magonjwa ya figo, ini, kichaa, mafua, homa, kuongeza utoaji wa maziwa, matatizo ya mmeng’enyo wa chakula, vidonda na asthma.

KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA MBUZI NA KONDOO

Mbuzi na kondoo wanaweza kufugwa kwa gharama nafuu na kuishi katika mazingira magumu kama ya maradhi na ukame ikilinganishwa na ng’ombe. Kutokana na umbile lao dogo wanaweza kufugwa katika eneo dogo na pia wanaweza kuhudumiwa na familia yenye nguvukazi na kipato kidogo. Uzao wa muda mfupi unamwezesha mfugaji kupata mbuzi/kondoo wengi kwa kipindi kifupi.
Wanyama hao hufugwa kwa ajili ya nyama, maziwa, ngozi, sufu na mazao mengine kwa matumizi ya familia na kuongeza kipato. Ufugaji bora wa mbuzi na kondoo uzingatie kanuni zifuatazo:-
i) Wafugwe kwenye banda au zizi bora,
ii) Wachaguliwe kutokana na sifa za koo/aina na lengo la uzalishaji (nyama, maziwa au sufu),
iii) Wapatiwe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili,
iv) Kuzingatia mbinu za kudhibiti magonjwa kama inavyoshauriwa na mtaalam wa mifugo,
v) Kuweka na kutunza kumbukumbu sahihi za uzalishaji; na
vi) Kuzalisha nyama, maziwa au sufu yenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko
Zizi au Banda la Mbuzi/Kondoo
Mbuzi/kondoo wanaweza kufugwa katika mifumo ya huria, shadidi na kwa kutumia njia zote mbili. Zizi hutumika katika mfumo huria ambapo mbuzi/kondoo huchungwa wakati wa mchana na kurejeshwa zizini wakati wa usiku. Zizi bora ni lile lenye sifa zifuatazo:-