Sifa za mnyama mwenye afya (Ng'ombe, mbuzi na kondoo)
i. Mchangamfu wakati wote macho maang’avu huku mkia na masikio vikimsaidia kufukuza inzi
ii. Kula na kucheua, kunywa maji vizuri kila siku
iii. Kuonyesha ushirikiano na kutembea pamoja kwenye kundi
iv. Kutembea vizuri
v. Anastuka na kukimbia anapostuliwa na mnyama hatari anapomkaribia kamaa vile mbwa mwitu, fisi, chui, simba.
vi. Mwili wake una uwezo mkubwa wa kukibadili chakula anachokula kutoa mazao ya kutosha kama vile maziwa.
vii. Anaonekana mwenye nguvu na kwa wale wanaoendelea kukuna wanaongezeka uzito kwa muda mfupi
viii. Kwa mnyama anayekamuliwa mara kwa mara kupiga kelele za kumtafuta mtoto wake,kiwele huwa kimejaamaziwa, chuchu huwa wakati mwingine zimetanuka upande kwa ajili ya kujaa maziwa
ix. Ngozi ya mnyama husisimka mara kwa mara wadudu wapomtambaa
x. Kwa madume, huwa wana hamu ya kuwapanda majike wanaoingia kwenye joto.
Miili yao hujengeka vizuri. Pumbu hujengeka na kukaa vizuri kwenye nafasi yake
(yaani katikati ya miguu)
xi. Pua na midomo huwa na unyevu unyevu wakati wote.
xii. Ngozi kuwa na ulaini unaotakiwa na manyoya hung’aa.
xiii. Kwa kawaida unapo mkaribia mnyama endapo amekaa chini ni lazima atanyanyuka
Dalili za Mnyama anayeumwa
i. Hukosa hamu ya kula na kunywa maji
ii. Mwili kunyong’onyea na kuonekana mchovu
iii. Mnyama kutembea pole pole na kwa taabu na mara nyingi hujitega na wenzake
iv. Pua zake na midomo huonekana kukauka.
v. Kupunguka kwa kiwango cha uzalishaji kama vile maziwa. Kwa madume huduwaa na kuinamisha shingochini na kukosa hamu ya kuwapanda majike wanaoingia kwenye joto.
Vyanzo vya magonjwa
Magonjwa mengi ya mifugo husambazwa na vijidudu ambao huingia kwenye mfumo wa damu na kusababishahoma na baadae madhara makubwa. Mangonjwa mengi ya mifugo husababishwa na vyanzo kutoka nje ya mwili wa mnyama mfano mazingira machafu anayoishi mnyama, vitu vinavyopelekea vidonda (Vitu vyenye ncha kali) husababisha vidonda ambapo vimelea vinaweza kukaa.Pia mnyama anaweza kupata ugonjwa kutokana na hali zandani ya mwili kama upungufu wa lishe, mfano: madini, na na magonjwa ya kulithi.
Mfano wa wadudu hao ni;
1. Vimelea (bacteria)
Mfano wa magonjwa yanayosababishwa na bacteria ni chambavu, Blackquarter, Kimeta, Kifua kikuuu, brucellosis (ugonjwa wa kutupa mimba) na ugonjwa wa kiwele.Ng’ombe dume huvimba mapumbu.
2. Virusi (virus) Otatis
Mfano wa magonjwa yanayosababishwa na virusi ni kichaa cha mbwa (Rabies), Ugonjwa wa midomo,miguu (foot and mouth disease) na Sotoka (Rinderpest)
3. Protozoa
Magonjwa yanayo sababishwa na protozoa ni kama ndigana baridi, ndigana kali, ndigana mkojo damu, ndiganamaji moyo na nagana.
Angalizo:
Magonjwa yote ya Ndigana husambazwa na makupe, wakati ugonjwa wa nagana husambazwa na ndorobo.
4. Lishe duni
Upungufu wa viinilishe katika chakula cha mifugo husababisha madhara katika mwili kama ifuatavyo;
i. Husababisha majike kutopata joto mapema
ii. Ndama kuzaliwa na viungo visivyo komaa
iii. Upungufu wa uzalishaji maziwa
iv. Kiwango cha uzalishaji kushuka
5. Vidonda/michubuko
Kupitia vidonda au michubuko, wadudu wasababishao magomjwa huweza kuingia mwilini kwa mnyama
6. Magonjwa ya kurithi
Kama mmoja wa wazazi ana ugonjwa wa kurithi basi kuna uwezekano mkubwa kwa mmoja wa ndamawatakaozaliwa kurithi ugonjwa huo
Magonjwa yanayoenezwa na kupe (Maelezo zaidi soma UKURASA wa magonjwa)
1. Ndigana kali
Dalili zake
i. Homa kali hadi nyuzi joto 42c
ii. Povu kutoka mdomoni na puani
iii. Kuhara choo kilichochanganyikana na kamasi na damu iv. Tezi kuvimba sana na zenye joto
v. Kuacha kula
vi. Ukungu kwenye macho
vii. Kifo baada ya wiki moja hadi mbili
Tiba
Butalex, Parvexon, tiba iambatane na sindano moja ya kuondoa uvimbe kwenye mapafu kama hali hiyo tayari imeshajitokeza. Tumia Multivitamin ili kuongeza hamu ya kula na Raxis ili kuondoa maji kwenye mapafu.
Kinga/zuia
Zingatia uogeshaji sahihi na Chanjo ya ECF
2. Ndigana baridi (Anaplasmosis)
Dalili zake
i. Homa hadi nyuzi joto 42C
ii. Kukosa hamu ya chakula
iii. Choo kigumu na makamasi na harufu mbaya iv. Kifo baada ya siku 8 hadi 10
Tiba
i. Antibiotic kama vile Oxytetracycline ii. Imizol.
Kinga
Zingatia uogeshaji sahihi
3. Ndigana mkojo damu (Babesiosis) ugonjwa wa kukojoa damu
Dalili zake
i. Mkojo kuwa na rangi ya damu isiyokolea zambarau ii. Mkojo hutoka kidogo kidogo na kwa muda mrefu
iii. Homa hadi nyuzi joto 40C
iv. Kuacha kula
v. Choo kigumu au kuhara wakati mwingine
vi. Kifo baada ya wiki 1
Tiba
Berenil ikisaidiwa na antibiotics za sindano kama vile oxytetracycline (OTC) pia tumia
Multivitamin kuongeza hamu ya kula.
Kinga
Zingatia uogeshaji sahihi
4. Ndigana maji moyo (heart water)
Dalili zake
i. Kizunguzungu na kuanguka, ii. Kifo baada ya siku 2
Tiba
Antibiotics za sindano kama vile oxytetracycline. Kumbuka tiba lazima ifanywe mapema iwezekanavyo
Kinga/kuzuia
Zingatia uogeshaji sahihi
CHANZO NI: FARM-AFRICA TANZANIA
No comments:
Post a Comment