Monday, March 16, 2015

UTUNZAJI WA BWAWA LA SAMAKI

UTUNZAJI WA BWAWA LA SAMAKI
Bwawa la samaki linahitaji matunzo ya mara kwa mara ili kuhakikisha linakaa katika hali inayostahili kuwawezesha samaki kuzailiana au kustawi vizuri. Bwawa lisipopewa matunzo mazuri linaweza pelekea wadudu wa magonjwa kujitokeza na kukuletea hasara kubwa sana katika ufugaji wako. Tafsiri ya wafugaji wengi wa samaki ni kwamba ukishatengeneza bwawa basi kinachofuata ni manufaa ya haraka na bwawa litadumu milele bila hata ya kulifanyia matengenezo madogo madogo. Dhana hii ni potofu wala hakuna ukweli wowote, bwawa linahitaji uangalizi wa karibu sana ili kama kuna tatizo lililojitokeza liweze kurekebishwa kwa wakati. Bwawa linaweza kubomoka kingo zake, kuvujisha maji, kujaa matope au kuota miti ndani.Hakikisha unaliangalia bwawa lako kwa kina ili kubaini kama kuna matatizo kwenye bwawa lako. Fanya marekebisho mara moja unapoyabaini ili kulifanya liendelee kuwa katika hali ya ubora na kulifanya lidumu kwa muda mrefu. Yafuatayo ni mambo ya kuangalia kwenye bwawa;

-Hakikisha ukingo/ukuta wa bwawa haujabomolewa na maji na kama umebomolewa urekebishwe haraka.-Kwa mabwawa yaliyotengenezwa kwa kingo za udongo ni vizuri kupanda majani juu ya kingo/kuta hizo ili kuzifanya ziwe imara na hivyo zisibomolewe na maji kwa urahisi na mmonyoko wa udongo.
-Angalia kama kuna majani/nyasi zinazoota kuelekea au ndani ya bwawa na kama zipo ziondolewe kwa kuzikata. Hakikisha kuwa bwawa lako halina magugu maji kwani haya hupunguza uzalishaji wa chakula cha asili cha samaki kwa kuondoa rutuba majini na kuweka kivuli.-Kama kuna miti yenye matawi yaliyoelekea juu ya bwawa, basi matawi hayo yakatwe ili kuzuia majani ya miti kuangukia ndani ya bwawa.-Angalia kama kuna sehemu inavujisha maji na kama ipo izibwe mara moja kabla haijawa kubwa. Fanya hivyo kwa kuangalia pia kina cha maji kama kinapungua kwa haraka.-Kina cha maji kinaweza kupungua kwa bwawa kujaa matope au mchanga, kama kina kimepungua kwa sababu ya matope ni vema matope yakapunguzwa kwa kuyaondoa na kuyatumia kurutubishia shamba.-Ondoa kama kuna uchafu wowote unaoelea ili kuepuka usije ziba mrija wa kutolea maji nje-Pia angalia mirija ya kuingiza na kutolea maji kama inafanya kazi vizuri, kama inatatizo mfano imezibwa na mawe, matope au uchafu mwingine lilekebishwe.-Tazama namna samaki wanavyokula, je wanakula kawaida, wanachangamka? Kama siyo, na kama wanatafuta hewa nje ya maji basi hewa ndani ya maji ni ndogo. Acha kuwalisha na kuweka mbolea na ruhusu maji safi kuingia ndani ya bwawa hadi pale samaki watakapo rudia hali yao ya kawaida. Kama bado angalia kama kuna dalili ya ugonjwa wowote.-Angalia kama kuna dalili ya wanyama wanaoweza kula au dhuru samaki wanaokuja kwenye bwawa kwa kuangalia walimokanyaga, kasha chukua tahadhari.Jambo jingine la kuangalia ni ubora wa maji yaliyoko na yanayoingia kwenye bwawa la samaki. Ubora wa maji ni kitu muhimu sana kwa ukuaji na afya ya samaki. Baadhi ya sifa ya maji kwa ajili ya samaki kama ifuatavyo:i.Hewa ya oksijeni
Endelea kusoma kwa kubonyeza HAPA

No comments:

Post a Comment