Serikali imeamua kutwaa baadhi ya hati za umiliki wa mashamba ya wawekezaji katika Bonde la KIRUSIX wilayani BABATI mkoani MANYARA ili zifanyiwe kazi upya.
Akizungumza na wakazi wa kijiji cha KIRUSIX Mkuu wawilaya ya BABATI, CRISPIN MEELA amesema hatua hiyo inalenga kutatua migogoro ya ardhi ya muda mrefu baina ya wananchi na wawekezaji walioko katika eneo hilo.
Wakaazi wa Kijiji cha KIRUSIX, wilayani BABATI, mkoani MANYARA, wamesema kuwa migogoro ya ardhi katika Bonde la KIRUSIX baina ya wawekezaji na wananchi imedumu kwa zaidi ya miaka 40 na wameiomba serikali itatue misuguano hiyo inayotishia amani na usalama katika eneo hilo
Mkuu wa wilaya ya BABATI, CRISPIN MEELA, amesema kuwa kuendelea kwa migogoro hiyo kumesababishwa na baadhi ya watu waliokuwa wakinufaika nayo kwa namna moja au nyingine na kwamba sasa serikali imeamua kwa dhati kuimaliza migogoro hiyo
Hata hivyo Mkuu huyo wa wilaya ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya, CRISPIN MEELA, amekemea tabia ya baadhi ya watu wanaochoma mali, kuiba na kuharibu mashamba ya wawekezaji kwa kisingizio cha migogoro iliyoko katika Bonde la Kirusix
Wakaazi hao wameelezea kuridhishwa na uamuzi wa serikali na kumpongeza mkuu huyo mpya wa wilaya ya BABATI kwa ujasiri wake na kusema ukweli kuhusu mambo yanayotokea katika Bonde hilo
Migogoro ya ardhi katika bonde la KIRUSIX, Imesababisha hasara kubwa baada ya mali za wawekezaji zenye thamani ya zaidi ya shilingi BILIONI 4 kuchomwa moto na watu wasio fahamika huku ikishuhudiwa watu wawili wakipoteza maisha
No comments:
Post a Comment