UtanguliziKwa kawaida au katika hali halisi, kazi ya kulea vifaranga hufanywa na kuku mwenyewe. Hivyo ili kulea vifaranga, mfugaji ni lazima aige kuku anavyofanya. Ikumbukwe kuwa vifaranga husumbuliwa zaidi na hali mbaya ya hewa, magonjwa mbalimbali, kukosa chakula kisichofaa na kukosa uangalizi wa karibu.Ni lazima vifaranga waangaliwe kwa kuwapatia nyumba yenye joto, chakula kinachofaa na maji safi, kuwakinga dhidi ya magonjwa masumbufu kwenye eneo husika na kuwatibu wanapougua. Mfugaji anayefanikiwa ni yule anayelea vifaranga wenye afya nzuri ambao hatimaye hutoa mazao mengi yanayompa faida.Wafugaji wengi vijijini wamezoea kumwachia mama kuku kufuga vifaranga wake kwa muda mrefu hadi wajitegemee. Njia hii humchelewesha kuku kurudia kutaga na hivyo kupata vifaranga wachache zaidi kwa mwaka. Lakini vifaranga vikiondolewa kwa kuku mapema, kama majuma matano hivi baada ya kuanguliwa, na wakatunzwa na mfugaji, kuku hutaga mapema na idadi ya kuku kwa mfugaji huongezeka haraka ndani ya kipindi kifupi.Mwongozo huu unaeleza jinsi ya kufuga vifaranga vizuri ili hatimaye mfugaji apate faida Zaidi.
Sehemu ya KwanzaNyumba ya kulelea Vifaranga
Ukipenda kujenga nyumba ya vifaranga itafaa ufikirie yafuatayo:-a Nyumba ya vifaranga iwe karibu na nyumba yako mwenyewe ili uweze kuwakagua vifaranga wako mara kwa mara.b) Ijengwe hatua 20 au zaidi mbali na nyumba ya kuku wakubwa, hii ni kinga mojawapo ya kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa.c) Nyumba ya vifaranga isiruhusu ubaridi au unyevu au wanyama waharibifu kuingia.Lakini nyumba iingize hewa na mwanga wa kutosha kila wakati.d) Nyumba iwe na eneo la kutosha ili vifaranga wapate nafasi ya kutembea kutafuta chakula na maji bila kubanana.e) Ijengwe kwenye sehemu isiyoelekea upepo unaotoka kwenye nyumba ya kuku wakubwa. Tahadhari hii husaidia vifaranga kuepukana na magonjwa yanayoenezwa na upepo.
Ukubwa wa Nyumba
Endelea kusoma HAPA kwa kubonyeza namba 6
Monday, March 16, 2015
ULEAJI WA VIFARANGA VYA KUKU SIKU YA 1 HADI WIKI YA 5
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment