Friday, March 20, 2015

Ufugaji Bora wa Kwale, Na faida ya Bidhaa zitokanazo na KWALE

Ufugaji wa KWALE ni njia bora na rahisi sana kwa mfugaji yeyote aliyetayari kukuza kipato chake kwa haraka sana na kwa kiwango cha juu.

KWALE ni jamii ya ndege ambao kwa sasa wanafugwa majumbani na wanaotaga mayai kama kuku ama bata na kwa wingi sana. Ndege hawa ni wadogo 280gm - 300gm, Wanarangi ya brown, nyeusi au hata nyeupe yenye miraba na madoa ya rangi ya ugondo au kijivu. Manyoya yao pia yana rangi ya brown au nyeupe na yenye madoa yanayovutia. 

Kutaga na kuatamia

KWALE dume humpanda jike kwa muda kidogo, Hapo jike anakuwa tayari kutaga na hutaga mayai 290 hadi 310 kwa mwaka (hii hulingana na lishe nzuri atakayopatiwa).
Mayai ya KWALE huatamiwa kwa siku 18 na huanza kuanguliwa vifaranga kwa muda wa siku 2, kuanzia siku ya 18 na hadi 20.
Njia bora ya kutotolesha mayai ya KWALE ni kwa kutumia incubator ambapo mayai huatamiwa kwa wingi ndani ya siku 18.


Utunzaji wa vifaranga na chakula

Siku 1 – 7
Vifaranga wapatiwe chakula “STARTER PELLET” na maji masafi ya kutosha. Siku ya 1 wawekee ‘GLUCOSE’ kwenye maji, Packet moja kwa lita 20 za maji, na siku ya pili hadi ya tano wawekee Amin Total kwenye maji, Wape maji pekee siku ya sita na siku ya saba wapatie chanjo ya Newcastle. Utawapatia joto kwa njia ya umeme kwa ‘BULB’ mbili (2) za 200watts kwa kila vifaranga 300, ama unaweza kuweka taa ya ‘Energy Server’ pamoja na jiko la mkaa uliofunikwa na majivu ambao utakidhi kuwapatia joto sawia kwa masaa 24 kwa siku 7. (Majivu yanasaidia moto kukaa kwa muda mrefu)

Banda/box lako liwe la ukubwa wa 1.5m x 1.5m (au eneo la ukubwa huo ndani mwa banda kubwa la kufugia kuku) lazima uzingatie usalama wa vifaranga dhidi ya panya, paka au vicheche. Unatakiwa kuweka ‘magazeti au mabox’ chini kwenye sakafu yatakayosaidia usafi. Kwa week ya kwanza chakula kitawekwa chini na tunashauri utumie chakula cha pellet ili kusaidia vifaranga wasiteleze na kuathiri miguu. 
NOTE: Weka goroli au mawe kwenye drinkers zako ili kuzuia vifaranga wasizame ndani ya (drinkers) maji na kufa.


Siku 8-14
Vifaranga wataendelea kupewa chakula “STARTER PELLET” na maji safi. Wataendelea kuhitaji ‘mwanga’ wa kutosha muda wote na joto la wastani bulb 2 za watts 100 au moja ya watts 200 

Siku 15-21
Uhitaji wa joto utapungua, ila ni kipindi ambacho wanakula chakula zaidi kwa ajili ya kukua. Ni vizuri waendelee kupata taa ili kupata mwangaza utakayowawezesha kula mchana na usiku.

Siku 21 na Kuendelea
KWALE wako hawatahitaji joto tena wawekee taa tu za energy server kipindi cha usiku, wape chakula na maji ya kutosha zaidi kwa ajili ya kukua. 

UTAGAJI MAYAI
WEEK YA SITA
Wiki ya sita kuelekea ya saba KWALE wako wataanza kutaga mayai kila siku, kwa wastani KWALE mmoja hutaga mayai 300 kwa mwaka. 

Magonjwa

KWALE ni ndege wenye kinga kubwa na ni vigumu sana kushambuliwa na magonjwa kama kuku na mara wanapougua ni rahisi sana kutibika. Magonjwa yanayoweza kuwapata KWALE ni typhoid, mafua na kuharisha .

Tiba za asili
Waweza kuwatibu vifaranga au KWALE wako kwa kutumia njia ya asili ambayo pia ni rahisi, gharama nafuu na bora zaidi kuliko kutumia madawa yaliyochanganywa na kemikali na yenye gharama.
Vifuatazo ni vitu vya asili vinavyotumika kutibu magonjwa mbali mbali kwa KWALE na yanayopatikana kwa wingi katika maeneo ya mfugaji. Madawa haya hutumika kwa kiwango cha wastani na hayana kipimo maalum kwani hata ukiyazidisha hayana madhara.

· Mwarobaini na Aloe Vera: Madawa haya hutumika kutibu kuharisha damu pamoja na mafua kwa vifaranga vya KWALE. Chukua kiasi kidogo cha mwarubaini kisha twanga vizuri kupata maji maji. Kamua maji yale, kisha weka katika maji uliyoandaa kuwanywesha vifaranga wako. Kata vipande vidogovidogo vya aloe vera (jani moja laweza kutosha) na tia katika maji yaliyochanganywa na mwarobaini, kisha wapatie vifaranga wanywe (Aloe Vera itaendelea kujikamua yenyewe ikiwa ndani ya maji huku vifaranga wakiendele kunywa).

· Kitunguu swaumu: Hii hutumika kukinga na kutibu vifaranga vya KWALE wanaosumbuliwa na kuharisha damu. Unachukua kitunguu swaumu na kuondoa maganda ya nje kisha kusafisha na kukata vipande vidogo sana, na kuwawekea kama chakula. Vifaranga wanapenda sana vitunguu hivyo na watakula kwa kasi kama chakula lakini ni tiba tayari. Unaweza kuwapatia kila siku hadi watakapo pona.

· Maziwa:Maziwa yanayotokana na ng’ombe pia hutumika kutibu ugonjwa wa kuhara pamoja na kuwapa nguvu KWALE waliolegea. Mnyweshwe maziwa hayo KWALE anayeumwa bila kuyachemsha na umnyweshe maziwa ya kutosha kiasi cha kushiba. Unamnywesha mara tatu kwa siku. Hakikisha maziwa unayotumia yanatoka kwa ng’ombe wanaotibiwa kila mara.


Angalizo
Siyo lazima KWALE waugue ndipo uwapatie tiba hizi. Hakikisha unawapa tiba kabla hata hawajaugua hivyo utawakinga na magonjwa hayo. Waweza kuchanganya madawa hayo yote kwa wakati mmoja kwani hayana madhara.
Endapo madawa ya asili hayapatikani katika eneo la mfugaji basi waweza kuwatibu KWALE kwa madawa yafuatayo ambapo vipimo huelezwa moja kwa moja kwa maandishi katika madawa hayo au kuelezwa na muuzaji pale utakaponunulia; Amprolium kwa ugonjwa wa kuharisha damu (Coccidiosis), Fluban,Coridix au Doxyco kutibu mafua (Coryza) na Esb3,Trisulmycine au Trimazine hutumika kwa homa ya matumbo (Typhoid). 


Chanjo

Siku ya 7 lazima vifaranga wapatiwe chanjo ya “kideri/mdondo
(respiratory & digestive diseases) kwa dawa inayoitwa ‘newcastle’. Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi na pia husababishwa na virusi kwa njia ya hewa.

Siku ya 14 lazima wapewe chanjo ya “gumboro”. Chanzo cha
maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi na pia husababishwa na virusi kwa njia ya hewa.

Siku ya 21 lazima warudie chanjo ya “Newcastle (aina ya IBDL)”. Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi na pia husababishwa na virusi kwa njia ya hewa.

Siku ya 35 lazima wapate chanjo ya “Ndui”.

Soko
Mayai ya KWALE ni bidhaa adimu sana hapa nchini kwa kuwa ni wafugaji wachache waliojikita katika ufugaji huu, Ufuatao ni muhtasari wa wastani wa bei ya bidhaa za KWALE sokoni 


  1. Trei ya (mayai 30) ya KWALE inauzwa shilingi 30,000 .
  2. Kifaranga wa KWALE wa siku moja anauzwa shilingi 2500 – 3000
  3. KWALE wa week 4 (mwezi mmoja) anauzwa kwa shilingi 10,000– 12,000
  4. KWALE aliyeanza kutotoa (week 6) huuzwa shillingi 20,000 – 25,000
  5. KWALE kwa aliyekomaa kwa ajili ya kitoweo huuzwa kwa shilingi 25,000
  6. DROPING za KWALE huuzwa kwa shilingi 10,000 kwa 50kg kwa wafugaji wa samaki


Soko la KWALE liko juu sana kwa mayai na nyama. KWALE pia hutofautiana bei kwa jike na dume.
Mayai yake pia huuzwa kwa bei nzuri sana. Yai moja huuzwa kuanzia 8,000 hadi 12,000 kwa wakati wowote ule.

Faida

MAYAI YA KWALE

UTANGULIZI
Mayai yaKWALE yameonekana kuwa chanzo muhimu sana cha Vitamini A, B1, B2, B6, B12 NA Vitamini D, chuma, kopa, magnesiamu, zinki, shaba, fosforas na virutubishi vidogovidogo vingine muhimu, madini na aside ya amino, ambayo ni sababu mayai haya hupendekeza kwa ajili ya matumizi ya mara kwa mara ya binadamu. Mayai ya KWALE yamejulikana kuwa bidhaa bora ya tiba za asili. Watumiaji wa Tiba asili huko China wamekuwa wakitumia mayai ya KWALE kama tiba kwa mamia ya miaka na kupata matokeo mazuri ya kustaajabisha kwa jinsi mayai haya ya KWALE yanavyoanza kupatikana katika masoko, watu zaidi wanaonyesha nia ya kutumia mayai hayo kama dawa ya asili.
Faida za Kiafya zitokanazo na ulaji wa Mayai ya KWALE

Yanaaminika kuwa na nguvu sana katika mwili wa binadamu hasa katika kujenga mfumo wa kinga ya mwili. Wataalamu wa tiba kwa njia ya asili ya matibabu hudai kwamba mayai yak wale yamekuwa na athari chanya juu ya watu wenye matatizo ya mkandamizo wa mawazo, shinikizo la damu, matatizo ya mfumo wa chakula, matatizo ya uvimbe mwilini, vidonda vya tumbo, kisukari, matatizo ya ini, shinikizo la damu, pumu, upungufu wa damu, aleji za aina mbalimbali, matatizo ya mgozi, eczema, matatizo ya moyo, magonjwa ya mapafu. Mayai ya KWALE yanajulikana kuchochea ukuaji wa mwili, kuongeza hamu ya mapenzi na uzalishaji wa homoni, kuchochea kazi ya ubongo ambaayo inaboresha akili na kasi ya kufikiri na kwa ujumla mayai husaidia kutunza ngozi ya mwili (kupunguza kasi ya uzee). Ni wazi kwamba hakuna apendekezaye kwamba mayai yak wale ni aina yoyote ya dawa ya ajabu au kuwa dawa ya tiba kwa magonjwa makubwa kama vile kansa, lakini athari yao chanya juu ya mwili wa binadamu imekuwa kuthibitika na watumiaji mbalimbali

Matumizi ya Mayai
Matumizi ya mayai ya KWALE yanapendekezwa kutumika kama sehemu ya chakula. Kwa afya zaidi inapendekezwa kuyala mabichi. Watu wengi hawapendi wazo hili hivyo kurahisisha matumizi unashauriwa kuchanganya yai bichi katika maziwa au matunda ama uji, Ili kuimarisha mfumo wa kinga na kuboresha ubora. Damu inapendekezwa kutumia kuanzia mayai 60, Awali mayai 3 kwa siku na kasha mayai 5 kwa siku

Jedwali lifuatalo linaonyesha pendekezo la ratiba ya matumizi kwa mayai ya KWALE, Matumizi haya yameandaliwa kulingana na umri wa mwanadamu:


UmriMayaiSikuSiku ya KwanzaSiku ya PiliSiku ya TatuSiku ya nne nakuendelea
Mtu mzima (Tiba)240493345
Mtu Mzima120253345
Miaka 16-18120253345
Miaka 11-15120323334
Miaka 8-1090303333
Miaka 4-760203333
Miezi 1-360302222
Miezi 3 – Mwaka 130301111


Magonjwa yanayotibika
Watumiaji wa dawa za asili wamependekeza matumizi yafuatayo ya mayai ya KWALE kulingana na magonjwa mbalimbali;
Kwa Watoto : Matumizi ya mayai yak wale yamependekezwa kwa watoto yakiwa yamepikwa au mabichi kwa ukuaji mzuri wa mwili na akili. Mayai husaidia kuboresha ufanisi wa kufikiri (IQ)
Kuchochea ukuaji wa mwili, kusisimua na kuboresha shughuli za kimetaboliki mwiliniMayai 100
Kuimarisha mishipa na mfumo mkuu wa mishipaMayai 120
Kwa wazee: Mayai ya KWALE yana athari chanya katika kuimarisha mwili kwa hiyo inapendekeza kwa ajili ya wazee na yanaweza kutuliza na / au kutibu magonjwa mengi kuhusishwa na uzee, upungufu au virutubisha zaidi mwilini
Mayai ya KWALE husaidia kuleta hali mpya ya afya na huleta mwili kwa usawa, yanapingana na kupambana na maradhi ya mwiliMayai 240
Yanafufua kumbukumbu na kulinda seli za mwiliMayai 120
Yanaongeza ufanisi katika tendo la ndoa na kuongeza uzalishaji bora wa homoni husikaMayai 120
Yanaongeza ufanisi wa viungo vilivyo choka kutokana na kazi na msongo wa mawazoMayai 240
Yanaimarisha mwiliMayai 240
Matibabu ya aleji
PumuMayai 240
Mwasho wa Ngozi na fangasiMayai 120
Mchafuko wa mfumo wa chakulaMayai 240
Yanasaidia vidonda vya tumboMayai 240
Yanaboresha mmeng’enyo mbovu wa chakulaMayai 120
Yanadhibiti uzalishaji wingi wa asidi za tumboniMayai 120
Mfumo wa Ini
Yanaboresha utendaji kazi wa kiungo iniMayai 240
Matibabu ya magonjwa ya figoMayai 240
Yanaboresha utendaji kazi wa kiungo figoMayai 240
Matibabu ya magonjwa ya moyoMayai 240
Yanaimarisha utendaji kazi wa moyoMayai 240
Matibabu ya magonjwa ya mzunguko wa damuMayai 240
Upungufu wa damuMayai 240
Shinikizo la damuMayai 240
Magonjwa ya mfumo wa kimetabolikiMayai 240
GautiMayai 240
Uzito wa mwili uliokithiliMayai 240
KisukariMayai 240
Magonjwa ya mfumo wa mishipaMayai 240
Hali ya wasiwasiMayai 240
Faida ya mayai yak wale wakati wa ujauzito na wakati wa kunyonyesha
Matumizi ya mayai ya KWALE kwa kuutia nguvu mwili wa mwanamke wakati wa kipindi cha kabla na baada ya kujifungua hasa yanapendekezwa zaidi kama baada ya upasuaji au mionzi. Pia yana manufaa juu ya kiumbe hai kiichopo tumboni (kuboresha uwiano wa mwili na akili) na kwa mama baada ya kujifungua (kimwili kukarabati na kuimarisha utengenezwaji wa seli). Mayai ya KWALE pia huboresha ubora wa maziwa ya mama.Mayai 240
Magonjwa ya Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI)
Matumizi ya mayai ya KWALE husaidia wagonjwa wenye upungufu wa kinga mwilini na kuongeza CD4Mayai 240

Taarifa zote hapo juu zimetokana na vyanzo kutoka katika machapisho mbalimbali ya kisayansi ya lishe na sisi hatuta chukuwa jukumu la kuthibitisha ukweli au usahihi wa yoyote ya hapo juu. 
Chanzo : quailfarm(dot)co(dot)uk

1 comment:

  1. Nanawashukuru waandaaji wa makala hii. Niko mbioni kutafuta mtaji nianze biashara hii mara moja. Asanteni.

    ReplyDelete