Friday, March 20, 2015

serikali yaomba wakulima kuhama katika vyanzo vya maji

Waziri wa maji prof JUMANNE MAGHEMBE
Waziri wa maji prof JUMANNE MAGHEMBE ameagiza kuwa watu wanaoishi au kulima katika vyanzo vya maji waondoke ili kutekeleza sheria ya maji ya mwaka 2009 inayoeleza kuwa shughuli zozote za kibinadamu zisifanyike katika vyanzo ili viwe endelevu . 


Akizungumza na wakazi wa vijiji vya MUMAGUNGA, LIGAMBA na KITARAMAKA wilayani BUNDA mkoani MARA kwa nyakati tofauti, waziri MAGHEMBE amesema serekali haitawafumbia macho watu watakaokaidi agizo hilo na kuagiza viongozi kusimamia utekelezaji wake. 



Awali akimkaribisha Mgeni rasmi, mkuu wa wilaya BUNDA JOSHUA MIRUMBE ameeleza kuwa Halmashauri ipo katika hatua za mwisho kukamilisha miradi miwili ya maji ambapo hadi kufikia Desemba mwaka huu zaidi ya asilimia 58 ya wakazi wa BUNDA watakuwa wamepata maji safi na salama. 



Katika ziara hiyo prof MAGHEMBE amezindua miradi miwili ya maji iliyogharimu zaidi milioni mia saba na kuwaeleza wananchi kuwa miradi hiyo ni mali yao hivyo wailinde.

No comments:

Post a Comment