Friday, April 10, 2015

NJOMBE waanza kutumia mbegu mpya za viazi mviringo

NJOMBE waanza kutumia mbegu mpya za viazi mviringo
Mbegu Bora Nne za Viazi Mviringo zimeanza kutumika katika wilaya ya WANGING’OMBE, Mkoani NJOMBE, kufuatia utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, UYOLE, na kubaini kuwa mbegu hizo ni bora kwa kilimo.

Afisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya hiyo , HENRY VAHAYE amesema wakulima wamekuwa na mwitiko katika matumizi ya mbegu hizo ambazo zinatajwa kuhimili magonjwambalimbali ya mazao.

Watalaam wa kilimo katika Halmashauri ya wilaya Mpya ya Wanging’ombe, wamesema kugunduliwa kwa mbegu hizo Nne za Viazi Mviringo,yawezekana ikawa suluhisho la adui Umaskini katika wilaya hii Mpya.

Pamoja na Mbegu hizo mpya za Viazi Mviringo ambazo zimeanza kutumiwa na wakulima wa wilaya tano za mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya, inadaiwa magonjwa mengine yamedhibitiwa isipokuwa Ugonjwa wa Mnyauko ambao umekuwa ni sumu kwa mimea ya mizizi nchini.

No comments:

Post a Comment