Na Mkombe Zanda,
Mbeya.
Serikali imetenga shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kuwalipa wakulima waliouza mazao yao kwa Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula NFRA kwenye mikoa mbalimbali nchini.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema fedha hizo zitalipwa kwa Wakulima katika awamu mbili za shilingi bilioni 15 ili kumaliza malalamiko yanayotokana na kuchelewa kwa malipo hayo.
Hayo yalibainishwa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda, katika siku ya kwanza ya ziara ya wiki moja mkoani Mbeya akiwa wilayani Mbarali, ambapo pia alipata fursa kufungua maabara za sayansi katika shule ya sekondari ya Igomelo na kusomewa taarifa ya kazi ya wilaya hiyo.
Katika mkutano wa hadhara, Waziri Mkuu alibainisha kuwa Serikali imetenga shilingi Bilioni 30 kwa ajili ya kuwalipa wakulima waliouza mazao yao kwa Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula, NFRA.
Kuhusu mgogoro wa mpaka unaotenganisha Hifadhi ya Bonde la Ihefu na makazi ya watu wilayani Mbarali, Waziri Mkuu amesema Serikali itapitia upya sheria ndogo inayohusu mpaka huo ili kuondoa kasoro zilizopo.
Katika kukabiliana na uhaba wa Walimu wa Sayansi, Pinda, alisema Serikali imeongeza ajira za wakulimu hao.
Hii ni ziara ya kwanza kwa Waziri Mkuu Pinda mkoani Mbeya kwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment