Pamoja na changamoto nyingi zinazowakabili wakulima wa zao la chai Tanzania ikiwemo kuyumba kwa bei ya zao hilo kwenye soko la dunia lakini limeweza kuzitoa kwenye lindi la umaskini kaya zipatazo 30,000 zilizoko katika wilaya 6 nchini zinazozalisha zao hilo.
Katika mkutano wa uzinduzi wa mradi wa utetezi wa wakulima wadogo wa chai nchini ulifanyika mjini Morogoro inabainishwa kuwa pamoja na zao hili kuuzwa bei ndogo kwa kilo katika soko la dunia, lakini bado limeonesha kuondoa umaskini kwa wakulima wadogo kwani chai huvunwa kila mwezi tofauti na mazao mengine ambayo huvunwa kwa msimu.
Ujio wa sera ya uchumi wa soko katika kuendesha biashara ya chai hapa nchini umeshuhudia changamoto ikwemo bei duni ya majani mabichi ya chai kwa wakulima nchini.
Tangu mwaka 2004 hadi 2013 bei ya majani mabichi ya chai kwa kilo moja imeongozeka kutoka sh.86 hadi sh.206, ongezeko hilo ni dogo sana ikilinganishwa na gharama na uzalishaji wa zao hilo, hata hivyo bado limeonesha kuondoa umaskini kwa wakulima .
Kumeanzishwa mfuko wa wakfu wa maendeleo ya wakulima wadogo wa chai Tanzania , ambao unatakiwa kutatua changamoto za wakulima huku wataalamu wa mfuko huu wakipewa changamoto.
Kutokana na asilimia 80 ya chai ya hapa nchini kuuzwa nje ya nchi moja kwa moja na kupitia mnada wa Mombasa ,Tanzania inaingiza dola za kimarekani milioni 56 kwa mwaka,tofauti na nchi jirani ya Kenya ambayo imekuwa ikijizolea dola za kimarekani milioni 1328.
No comments:
Post a Comment