Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya MULEBA Mkoani KAGERA limeshauri wakulima wa zao la kahawa wilayani humo kujiengua kutoka katika Chama cha Ushirika mkoani KAGERA (KCU), na kuunda ushirika wao.
Katika kikao hicho baadhi ya madiwani wamesema KCU hakijafanya jitihada za kumkomboa mkulima, ikiwa ni pamoja na kumpatia bei nzuri hususani ya zao la kahawa na hivyo kusababisha mkulima kujitafutia masoko nje ya nchi ili kujipatia unafuu wa bei.
Azimio hilo limetokana na na taarifa ya mapato na matumizi iliyosomwa mbele ya madiwani hao na Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo GEORGE KATOMERO , kuwa halmshauri hiyo imeshindwa kukusanya asilimia hamsini ya mapato ya ndani kama makisio ya nusu mwaka, kutokana na sababu kadhaa ikiwemo usafirishwaji wa magendo ya kahawa nje ya nchi.
Hoja ya njia ipi itumike kuzuia magendo ya kahawa ikawasilishwa na baadhi ya madiwani ,wengi wao wakidai sababu kubwa ni bei ya chini inayotolewa na Chama kikuu cha ushirika mkoani Kagera (KCU)
Katika mkutano Mkuu wa Chama cha ushirika mkoani Kagera (KCU) Mwenyekiti wa Chama hicho FRANK MUGANYIZI amekiri kuwepo kwa bei ndogo katika soko la kahawa ,lakini Mkuu wa Mkoa wa Kagera JOHN MONGELLA akitoa ilani kwa wale wote wanaojihusisha na biashara ya magendo ya kahawa kuwa mkono wa sheria itawakabili.
Licha ya Hivi karibuni Chama cha Msingi MAGATA KURUTANGA kilichopo wilayani MULEBA, kujiondoa kutoka chama kikuu cha ushirika mkoani KAGERA (KCU)Madiwani hao wanataka kuwepo na muundo wa chama kikubwa cha ushirika kitakachojumuisha wakulima wote kutoka katika wilaya hiyo.
Nitawezaje kuupata uongozi wa chama cha ushirika cha pamba KAGERA?
ReplyDeleteNina shida nao sana