Je unaweza kula nyama ya mifugo waliolishwa Funza? Kufuga Nguruwe, Kuku, Samaki kwa kuwalisha funza, kunatarajiwa kubadili tunavyo fuga mifugo.
Haya hufanyika katika sehemu moja ya kufanyia majaribio inayomilikiwa na kampunib ya AgriProtein nchini Africa Kusini.
Kampuni hiyo inatengeneza litakalokua shamba kubwa kabisa duniani , linalofuga Nzi. Ufaransa, Kanada, Uholanzi, na Marekani pia wana mipango hiyo.
Mamia ya watu walishiriki kikao cha 'Funza kulisha Ulimwengu' , kilichofanyika huko Wageningen, Uholanzi, mapema mwezi huu.
Wengi waliridhika kuwa Funza na Buu wanaweza kutupa lishe mbadala kwa lishe ile ya kawaida ya Soya na Samaki ambayo yanazidi kuwa ghali.
Shirika la chakula na kilimo duniani linabashiri kuwa kuongezeka kwa idadi ya watu duniani kutaongeza na mahitaji ya proteni inayotokana na Nyama na Samaki.
Hivyo basi kutakuwa na ushindani kati ya wanyama na binadamu, hususan katika mahitaji ya Proteni.
Kwa upande wa wanyama ongezeko la mahitaji ya proteni litafika asilimia 70 ifikapo mwaka 2050.
Hili litapunguza ardhi inayoweza fanyiwa ukulima na pia hifadhi za Samaki. Vyakula vya Samaki na Ng'ombe vyazidi kuwa ghali. Nafaka hutumika kutupa protini, lakini protini katika mimea haitoshi.
Soya ina protini za kutosha ila tu bei yake imekua ghali.
'Twahitaji vyakula mbadala.'
Aina tofauti ya Nzi, waweza kutumika kutengeza aina tofauti ya vyakula kwa kila hatua ya kukua katika maisha ya mnyama yeyote yule.
AgriProtein ilitangaza kuwa ilikua imekwisha changisha dola milioni 11, kwa matumizi ya ujenzi wa mashamba mawili ya kwanza ya kufuga nzi wa kuuzwa. Shamba la kwanza huko Cape Town litakua na Uwezo wa kutoa tani 20 ya buu na tani 20 za mbolea kila siku.
Wao hutumia aina tatu za Nzi akiwemo Yule wa kawaida wa nyumba, kila aina akiwa na aina tofauti ya vyakula anavyovila. Nzi wa kike na wale wa kiume hufugwa katika vizimba vikubwa na mayai yao kuchukuliwa kisha kuchanganywa na vyakula vyao.
Kilo moja ya mayai yao hugeuka kuwa takriban kilo 380 ya buu, katika muda wa siku tatu tuu. Buu hawa hutolewaa kisha kukaushwa na kusiagwa na kinachobakia hua ni mbolea iliyo na Naitrojini.
'Bidhaa za nzi'
Enterra Feed Corporation, kampuni ya huko Vancouver, ina mipangilio ya kuzalisha bidhaa za nzi weusi, mara tatu zaidi. Bidhaa hizi zitatumika kulisha wanyama wanaofugwa na kisha kuwa vyakula vya wanyama wa majini baadaye.
EnviroFlight, ya huko Ohio, Marekani, pia yatoa vyakula vya samaki waliofugwa.Karibu na Paris, Ufaransa, Ynsect, yatarajiwa kufuga Nzi hao pia kwa kiwango kikubwa itimiapo mwaka 2016.
Protix Biosystems ya Uholanzi pia ina mipangilio ya kupanua ufugaji wao wa nzi na kuuza buu kwa maumizi ya vyakula vya wanyama nap protini.
Sheria katika sehemu zingine hata hivyo zinazuia ufugaji wa Nzi kwa ajili ya kutengeneza vyakula. Katika Muungano wa nchi za Uropa, Nzi huchukuliwa kama mifugo wanapouawa na kukaushwa au kutengenezwa kwa njia nyingune yoyote ile.
Hili lamaanisha kuwa protini yao yaweza kulishwa tu kwa wanyama ambao si wa kuliwa na binadamu. Wanyama wanaofugwa pia hawawezi lishwa kwa minajili ya kutoa mbolea tu.
Sheria hizi zilizotengenezwa katika miaka ya 1990, hazikutarajiwa kuhusisha nzi.
Je, watumizi watakubali vyakula kutoka kwa wanyama waliolishwa buu na funza? Binadamu hula kuku na samaki.
Kuku hula wadudu hawa na pia samaki wanaovuliwa majini hula wadudu hawa. Miaka 10 au 15 kutoka sasa, hili litakua tasnia kubwa ulimwenguni.
No comments:
Post a Comment