Sunday, March 8, 2015

UGONJWA WA MIDOMO NA MIGUU (FOOT AND MOUTH DISEASE)


Cow infected with FMD
Huu ni ugonjwa unaowashika ng’ombe, kondoo, mbuzi, pamoja na wanyama wa porini kama mbogo, swala na wakati mwingine tembo.

Ng’ombe anapopatwa na ugonjwa wa miguu na midomo huchechemea na asipotibiwa kwa haraka hushindwa kusimama na kula hatimae hudhoofika na hata kufa.
Ugonjwa wa miguu na midomo husambaa haraka kwenye kundi ukiua ndama na kusababisha wanyama kupoteza uzito na uzalishaji wa wengine kupungua.
Namna unavyoambukizwa
Ugonjwa huu unaambukiza kwa kugusana kwa mnyama mmoja na mwingine. Unaweza vile vile kusambazwa na upepo kwenye umbali hata wa kilometa 250. Pamoja na kusambaa kwa umbali huo, ni nadra kwa binadamu kupata ugonjwa huu.
Kwa muongo mmoja uliopita, wastani ugonjwa huu ulikuwa unashambulia kundi mara moja kwa mwaka. Kwa sasa, katika sehemu nyingi za Afrika Mashariki, ugonjwa unatokea mara tatu kwa mwaka. Aidha, jinsi hali ya hewa inavyokuwa ya joto la juu, yanatokea matabaka mapya ya vimelea visababishavyo ugonjwa huu.

Dalili
• Kuwepo mifugo yenye dalili za mafua, na kuchechemea kwa wakati huo huo.
• Ndama kufa kwa ghafla kutokana na ugonjwa wa moyo.
cow-infected-with-fmd
Tahadhari
Ugonjwa wa miguu na midomo una madhara makubwa kiuchumi hasa ukizingatia kuwa, uzalishaji wa maziwa wa ng’ombe waweza kupungua kwa asilimia 75 kwa maisha yake yote.
Mbali na hayo, ng’ombe badala ya kuzaa kila mwaka au kwa vipindi kama hivyo, anaweza kuzaa kila baada ya miaka miwili au mitatu.

Namna ya kuzuia
Chanjo kwa ajili ya ugonjwa huu husaidia kuzuia isipokuwa gharama yake ni kubwa kwani chanjo hizo zinanunuliwa kutoka nchi za nje na lazima iwe ya kufanyakazi dhidi ya aina nyingi za vimelea. Hata hivyo, jamii inaweza kupanga, na kununua chanjo kwa kushirikiana.
Ugonjwa wa miguu na midomo ni tishio, hasa katika maeneo ambapo mifugo inatumia ardhi ambayo pia inatumiwa na mbogo na nyumbu. Ni vyema kwa wale wanaoishi katika maeneo hayo kuhakikisha kuwa ardhi wanayotumia kulishia mifugo yao si ile inayotumiwa na wanyama pori

No comments:

Post a Comment