Wakulima wa zao la mpunga wilayani SAME mkoani KILIMANJARO wamesema kilimo cha mpunga wilayani humo kimekuwa kikiathiriwa na uwepo wa magadi chumvi yanayoathiri rutuba katika mashamba yao na kupunguza uzalishaji wa zao hilo.
Wakizungumza katika kikao cha wadau wa kilimo cha mpunga kilicho fanyika katika kijiji cha NDUNGU wilayani SAME wakulima hao wamesema magadi chumvi hayo yamekuwa ni changamoto kubwa jambo ambalo linaweza kupunguza kabisa uzalishaji wa mpunga katika kipindi cha miaka 20 ijayo.
Daktari SOPHIA KILLENGA ambaye ni mtafiti kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo ARI-KATRIN ameeleza athari za magadi chumvi katika kilimo cha mpunga pamoja na jia ambazo zinawezatumika kupunguza magadi chumvi katika udogo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa HALMASHAURI ya wilaya ya SAME CHRISTOPHER MICHAE ameeleza mikakati aliyoweka kutokana na kutambua uwepo wa tatizo hili.
Zao la mpunga ni miongoni mwa mazao yanayolimwa kwa wingi hapa nchini ambapo utafiti unaonesha kuwa Tanzania ni ya pili kwa kilimo cha mpunga katika nchi zilizochini ya jangwa la sahara ikitanguliwa na nchi ya MADAGASCA.
No comments:
Post a Comment