Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi-CCM, ABDULRAHMAN KINANA ameishauri serikali kufanya thamthni juu ya mashamba ya baadhi ya wananchi yaliyochukuliwa na wawekezaji ambao wameshindwa kuendeleza wakati wa kipindi cha ubinasfsishaji ili kuruhusu wigo mpana wa wananchi kupata fursa ya kumiliki ardhi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika mji wa SANYAJUU, wilayani SIHA mkoani KILIMANJARO, KINANA amesema baadhi ya wawekezaji wakubwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo TANGA, ARUSHA na KILIMANJARO wamehodhi maeneo makubwa ya ardhi ambayo wamekuwa wakiyakodisha kwa wafanyabishara, mashamba ambayo hapo zamani yalikuwa yakimilikiwa na wananchi.
Akiwa ziarani mkoa wa KILIMANJARO, katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ABDULRAHAMN KINANA, akatembelea katika bwawa la umwagilaiji katika kijiji cha KASHISHI wilayani SIHA, mradi ambao unatajwa kuwa chachu ya wananchi kujipatia kipato na kupitia sekta ya kilimo.
(imetolewa na tbc1)
No comments:
Post a Comment