Wednesday, March 25, 2015

MANYARA yakumbwa na ukame

Mkuu wa mkoa wa MANYARA, DOKTA JOEL BENDERA
Wakati hayo yakiendelea jijini DSM, huko Mkoani MANYARA hali ya ukame imekuwa tishio kwa wakulima Mkoani humo na kuwasababishia hofu ya kukabiliwa na njaa kutokana na uhaba wa mvua kwa kipindi kirefu. 

Baadhi ya wakulima wamesema uhaba huo wa mvua umesababisha mazao yaliyoko shambani hususan mahindi kunyauka. 

Katika msimu wa kilimo wa mwaka 2014/2015, mkoa wa MANYARA umefanikiwa kuwa na mavuno ya uhakika ya mazao mbalimbali kutokana na mvua za wastani zilizonyesha kwa mpangilio 

Lakini katika msimu huu, kila mahali mkoani Manyara, wakulima wanapaza sauti zao za kukosa matumaini ya kuvuna chochote baada ya jitihada kubwa walizowekeza katika kilimo kuonekana kugonga mwamba. 

Wataalamu wa idara ya kilimo katika wilaya ya HANANG wameielezea hali hiyo ya ukame kutishia upatikanaji wa chakula 

Mkuu wa mkoa wa MANYARA, DOKTA JOEL BENDERA, amesema katika mahojiano maalumu na TBC, mabadiliko ya tabia nchi yanachangia hali hiyo ya ukame 

Makundi mbalimbali ya kijamii yameanza kufanya ibada za aina mbalimbali zikiwemo za kimila na kwenye makanisa kuombea mvua inyeshe ili kunusuru hali hiyo

imetolewa na TBC 1


No comments:

Post a Comment