Thursday, February 27, 2014
WAJASIRIAMALI WAPATA MAFUNZO USINDIKAJI MUHOGO
cha Kitropiki (IITA) kwa kushirikiana na Shirika la Viwango nchini (TBS ).
Dkt. Ndunguru alisema changamoto kubwa kwa wasindikaji zao la muhogo, ni vifungashio na mitambo ya kisasa kwani ni kiwanda kimoja tu ambacho hakitoshelezi mahitaji.
Wednesday, February 26, 2014
USIMAMIZI HAFIFU WACHANGIA SAMAKI KUPOTEA MKOANI MARA
IMEELEZWA kuwa usimamizi hafifu wa kanuni na sheria za uvuvi ndani ya Ziwa Victoria ndio chanzo kinachochangia kupotea kwa samaki mkoani Mara. Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mfawidhi ulinzi na rasilimali za uvuvi Mkoa wa Mara, Braison Meela wakati akitoa taarifa katika kikao cha wadau wa uvuvi katika ziwa hilo kilichofanyika kwenye ukumbi wa uwekezaji uliopo katika Ofisi ya mkuu wa mkoa huo.
Meela alisema kuwa kumekuwepo na wasimamizi wabovu katika kusimamia kanuni na sheria ya uvuvi kuanzia ngazi ya kata hadi Taifa hali inayochangia kupungua kwa rasilimali hiyo ambayo ndiyo inayoingiza pato kubwa katika nchi hii .
Alisema kuwa lengo ni kuchukua hatua stahiki ili kuwa na rasilimali endelevu ya samaki katika ziwa hilo litakalofikiwa iwapo hatua sahihi na za makusudi zitachukuliwa dhidi ya wanaosababisha kupungua wingi wa samaki hao ndani ya ziwa.
Akizungumzia kuhusu changamoto zilizopo katika sekta hiyo alisema kuwa ongezeko la matumizi ya mbinu haramu ya uvuvi kama vile matumizi ya dawa za kilimo ya kuvulia samaki, usimamizi hafifu wa sheria na kanuni zake kama vile wataalam, BMU, wanasiasa na serikali ya vijiji ambapo matokeo yanaachwa yanaenda kama yalivyo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maadili na ukiukwaji wa miiko ya utumishi kwa baadhi ya watendaji.
"Nyavu za timba ni nyavu ambazo zimekuwa zikitumiwa mara kwa mara kuvulia samaki kwa njia ya uvuvi haramu na nyavu hizi zinatokea nchi za nje kwani wanaozingiiza ni wenzetu kwa kuwa wanajua bidhaa hiyo ina soko hapa kwetu hivyo tunapaswa kila mmoja kuwa mlinzi wa rasilimali hii," alisema Meela.
Akizungumzia viashiria vya kupungua kwa
samaki alisema kuwa viwanda vya samaki vinazalisha kwa kiwango cha chini ya asilimia
hamsini ya uwezo wake, hivyo kushindwa kukidhi mahitaji ya wateja wao.
Mmoja wa wadau hao ambaye ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Butiama Magina Magesa
alisema kuwa inashangaza sana kuona hapa nchini hakuna viwanda vinavyozalisha
nyavu hizo, lakini nyavu hizo zimezagaa katika maeneo mbalimbali ndani ya nchi
huku vyombo vya dola vimeshindwa kudhibiti uingizwaji wa nyavu hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa akifungua kikao hicho alisema kuwa BMU ambao ndio kama ya kufuatilia matumizi mabaya ya zana hizo lakini hao ndio wanaowakingia kifua wavuvi haramu kwa kuwaambia wafiche zana hizo wakati wa oparesheni ili wakimaliza waendelee na shughuli zao kama kawaida.
Alisema nchi jirani zinazozungukwa na ziwa hilo wananufaika na mazao ya ziwa hilo lakini Mkoa wa Mara umeshindwa kunufaika na mazao yanayotokana na ziwa hilo kwa sababu ya watu wa BMU kutokuwa na maadili ya utendaji kazi kama dhamana yao.
WAKULIMA NCHINI WATAKIWA KUTUMIA MAOFISA UGANI
WAKULIMA nchini wameshauriwa kuwatumia maofisa ugani wa Kata kwa ajili
ya kupata ushauri kuhusu kilimo cha kitaalamu ili wajipatie mavuno mengi
kulingana na shamba walilolima.
Ushauri huo ulitolewa juzi na Ofisa Masoko wa Kampuni ya Kuuza Mbegu za
Nafaka (SEED.CO) mkoani Morogoro, Silas Ngowe, wakati akizungumza na waandishi
wa habari ofisini kwake mkoani hapa. Alishauri wakulima wa Mkoa wa Morogoro
kupanda mbegu za muda mfupi kutokana na mvua kupungua ikilinganishwa na miaka
iliyopita.
Mbali na ushauri huo, Ngowe aliwataka wakulima kuwafanya maofisa ugani
kama waganga wao kwa kuwapatia ushauri na kwamba wasiwapuuze kwa sababu ndiyo
msaada wao."Kwa kawaida mgonjwa anapoumwa hukimbilia kumtafuta daktari hivyo na hawa
wakulima nawashauri wawe wanawatafuta mara kwa mara maofisa ugani kwa ajili ya
maelezo ya mashamba yao," alisema Ngowe .
Kuhusu pembejeo za vocha, alisisitiza kuwa wakulima wachukue mbegu na mbolea kwenye maduka waliyopangiwa na Serikali. Kuhusu tatizo la wakulima kuuza vocha zao ameshauri wasiziuze badala yake wazitumie kama Serikali ilivyoagiza na kwamba mkulima ambaye hana shida na vocha hizo awaachie wenye shida na si kuuza kwa bei nafuu.
"Unakuta mkulima anapata vocha kwa bei nafuu halafu anaamua kuuza kwa bei ya chini kitu ambacho si sahihi, ni vizuri kama mkulima huyo hahitaji vocha awaachie wakulima wanaohitaji na si kuuza kwa bei rahisi," alisema. Ngowe alisisitiza wakulima kuchukua kiwango kilichoandikwa kwenye vocha kiwe ndicho kiwango mwafaka na si vinginevyo .
Tuesday, February 25, 2014
ZAO LA MIWA LIINGIZWE KATIKA MFUMO WA PEMBEJEO ZA KILIMO
ZAO LA MIWA

UMOJA wa Wakulima wa Kilimo cha Miwa mkoani
Kagera (KASGA) wameiomba serikali kuliingiza zao la miwa
katika mfumo wa pembejeo za kilimo ili
kupunguza gharama za kununua dawa ambazo ni kubwa na
kuwasababishia kushindwa kumudu.
Mmoja wa wakulima hao, Anasi Swaibu
alibainisha hayo hivi karibuni mjini Kyaka wakati akizungumza
na mwandishi wa habari hizi juu ya changamoto
zinazowakabili katika kilimo hicho.Swaibu alisema sasa wakati
umefika Serikali kuliingiza zao hilo katika
mfumo wa pembejeo ili kuondoa ukiritimba ambao upo kwa sasa katika
maduka ya wauzaji binafsi wa dawa au pembejeo
zinazotumika katika kilimo hicho.
Alisema mfano dawa ya kuulia magugu ambayo
huuzwa zaidi ya Sh 16,000 kwa lita moja hapa Tanzania wakati
nchini Uganda dawa hiyo hiyo huuzwa kwa
gharama ya Sh 10,000 jambo ambalo linasababisha wakulima hao
kushindwa kulima kilimo chenye tija kilicho
bora.
Gharama hiyo ni kubwa kwa mkulima wa kawaida
kama sisi itakuwa vigumu kuendelea, basi Serikali ilione hili la
kuweka zao hili katika mfumo wa pembejeo kama
yalivyo mazao kama korosho maana tunajikuta asilimi 90 ya
faida hiyo inaishia katika ununuzi wa
dawa,”alihoji Swaib.
Mkulima mwingine wa miwa, Ahmed Kajubi
alishauri kama Serikali haiwezi kuweka utaratibu wa pembejeo za
ruzuku katika zao hilo basi viwanda vya
sukari nchini viweke utaratibu wa jinsi ya kukopesha pembejeo kwa
wakulima hao pale wakipeleka miwa waweze
kurejesha au kuwauzia wakulima wadogo pembejeo hizo kwa bei ya
kawaida ili waweze kumudu gharama hizo na
kufanya kilimo cha miwa kuwa cha uhakika na kupendwa na
wakulima wengi.
Subscribe to:
Posts (Atom)


