Tuesday, February 25, 2014
MAHIZA AWAKUNA WAKULIMA WA KOROSHO
Mahiza alitoa agizo hilo kwenye kikao cha ushauri cha mkoa (RCC) kilichofanyika hivi karibuni mjini Kibaha na kubainisha kuwa ni kipindi kirefu aliomba matokeo ya kulipwa kwa madeni ya mikopo hiyo na fedha za wakulima hao suala ambalo usimamizi wake umeonekana sio wa kuridhisha.
"Kauli ya Mahiza kusema kuwa kwasasa hawataki watendaji hao ambao hawana manufaa na mkoa huo hususan wakulima hivyo haina budi kupitia kikao hicho kutamka rasmi hawafukuzi bali hawataki mkoani hapo kwa maslahi ya mkoa ni kauli inayoonyesha uwajibikaji na iwe fundisho kwa watendaji wengine," alisema Malundi.
WAJASIRIAMALI WAPATA MAFUNZO USINDIKAJI MUHOGO
WAJASIRIAMALI 16 kutoka Mikoa ya Mwanza, Pwani na Kagera wamepata elimu ya usindikaji wa zao la muhogo na viwango vinavyozingatia ubora unaokubalika katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EA C).
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, wilayani Misungwi baada ya
mafunzo hayo, mshauri wa usindikaji na masoko wa IITA Dkt. Gabriel Nduguru,
alisema wakulima wasindikaji wa zao la muhogo, hawakuwa na elimu ya kutosha
kuhusu viwango na ubora wa bidhaa zao.
Alisema kuwa mafunzo hayo kwa wasindikaji hao, yalitolewa na Taasisi ya
Kimataifa ya Kilimo cha Kitropiki (IITA) kwa kushirikiana na Shirika la Viwango
nchini (TBS ).
Alisema IITA ilifanya utafiti na kubaini changamoto hiyo kwa wasindikaji wengi
wa zao la muhogo, hivyo ikaamua kutoa elimu inayohusu ubora na viwango kwa
wasindikaji hao ili kuwawezesha kupata masoko ya uhakika.
"Wakulima na wasindikaji hao hawakuwa na elimu, hivyo bidhaa zao hazikuwa
bora na salama na zilitishia afya za walaji.Baada ya kubaini hilo tukaona
tuwafundishe jinsi ya kusindika muhogo salama kwa kuzingatia viwango vya ubora
kulingana na mahitaji ya walaji," alisema Dkt. Ndunguru.
Alisema wanafanya utafiti wa mazao na kusaidia kuainisha viwango vinavyotumika
kwa nchi za EAC, baada ya kuridhiwa na mawaziri wa nchi za Jumuiya hiyo.
Alisema wananchi watafahamu viwango vya ubora baada ya kuwapa mafunzo ya
usindikaji na watazalisha chakula chenye ubora na kuuza katika masoko ya
uhakika na watajiongezea kipato .
Dkt. Ndunguru alisema changamoto kubwa kwa wasindikaji zao la muhogo, ni
vifungashio na mitambo ya kisasa kwani ni kiwanda kimoja tu ambacho
hakitoshelezi mahitaji.
Monday, February 24, 2014
MWAKA WA KILIMO WA AFRIKA WAZINDULIWA MKOANI IRINGA
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh.Dkt Christine Ishengoma akipiga makofi mara baada ya kukata utepe
kuashiria uzinduzi wa ghala la mazao,katika kijiji cha kaning'ombe, wilayani iringa mkoni humo wakati wa uzinduzi wa mwaka wa kilimo
Sehemu ya wadau mbalimbali walio shiriki katika uzinduzi wa mwaka wa kilimo mkoani humo
Mwakilishi wa shirika la afrika one kutoka afrika kusini, Mercy Erhiawarien akitoa ufafanuzi mbele ya wadau wa kilimo kuhusiana ana namna kilimo kinavyoweza kuwasaidia watanzania, hasa kwa vijana na akina mama
Baadhi ya wadau viongozi wakifanya ukaguzi wa shamba la mfano katika kijiji cha kaning'ombe mkoani Iringa.
Wasanii ambao ni mabalozi wa kilimo nchini, Mrisho mpoto na Profesa Jay amabao ni mabalozi wa kampeni ya ''KILIMO KINALIPA,JIKITE'' walikuwepo
Sehemu ya shamba la mfano la mkulima mdogo, Mzee Mbagile
kuashiria uzinduzi wa ghala la mazao,katika kijiji cha kaning'ombe, wilayani iringa mkoni humo wakati wa uzinduzi wa mwaka wa kilimo
Sehemu ya wadau mbalimbali walio shiriki katika uzinduzi wa mwaka wa kilimo mkoani humo
Mwakilishi wa shirika la afrika one kutoka afrika kusini, Mercy Erhiawarien akitoa ufafanuzi mbele ya wadau wa kilimo kuhusiana ana namna kilimo kinavyoweza kuwasaidia watanzania, hasa kwa vijana na akina mama
Pichani juu na chini ni mabalozi wa kilimo nchini, msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Prof Jay pamoja na mchora katuni maarufu nchini, Massoud kipanya wakizungumza mbele ya wadau wa kilimo namna kilimo kinavyoweza kuwakomboa vijana
Wasanii ambao ni mabalozi wa kilimo nchini, Mrisho mpoto na Profesa Jay amabao ni mabalozi wa kampeni ya ''KILIMO KINALIPA,JIKITE'' walikuwepo
Sehemu ya shamba la mfano la mkulima mdogo, Mzee Mbagile
Wednesday, February 19, 2014
KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA MANYARA
FURUSA ZA UWEKEZAJI
KATIKA MKOA WA MANYARA
Mkoa una fursa nyingi za uwekezaji hususani katika huduma za Kiuchumi
(Kilimo na Mifugo, Viwanda, Biashara, Utalii na Madini); Kijamii (Elimu, Afya
na Maji); na Kiutamaduni (Michezo na Utamaduni).
FURSA ZA UWEKEZAJI
KATIKA HUDUMA ZA KIUCHUMI KILIMO
Kuna maeneo makubwa yanayofaa kwa shughuli za kilimo cha kwaida na kilimo
cha umwagiliaji katika Mkoa. Mazao yanayozalishwa kwa wingi ni pamoja na
Mahindi, Alizeti, Mbaazi, Mtama, Ngano, Maharage, Miwa, Vitunguu Maji, Vitunguu
Saumu na Mpunga ambayo hutumika kama mazao ya Biashara na Chakula kwa wakazi wa
Mkoa, Mikoa jirani na Nchi jirani za Kenya, Somalia, Ethiopia, Eritiria na
Sudani. Hivyo wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika sekta hii. MIFUGOMkoa una zaidi ya mifugo milioni 2. Wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika sekta hii hususani katika uanzishaji wa ranchi na viwanda vikubwa na vidogo vya kusindika mazao ya mifugo ambayo ni nyama, maziwa na ngozi. Fursa nyingine ya kuwekeza katika sekta hii ni ujenzi wa majosho na mabwawa kwa ajili ya kuogesha na kunyweshea mifugo.
VIWANDA
Mkoa unawakaribisha wawekezaji ili waanzishe na kuwekeza katika viwanda
Vikubwa, vya kati na Vidogo kwa ajili ya kusindika mazao ya kilimo, mifugo na
sekta nyingine. Kwa sasa Mkoa una Kiwanda kikubwa cha Mbolea cha Minjingu
ambacho husambaza mbolea yake ndani na nje ya Mkoa na Kiwanda cha kusindika
nyama kilichopo Wilayani Simanjiro. Kadhalika, Mkoa unakadiriwa kuwa na viwanda
vidogovidogo 4560 vinavyofanya kazi za: Kusindika Nyama na Maziwa, mafuta ya
Alizeti, Kusaga na kukoboa nafaka na Kutengeneza Mkaa usiotoa moshi wenye
athari.
BIASHARA
Tayari makampuni kadhaa kama vile Kampuni ya Usafirishaji ya Mtei ‘express’,
kampuni za Simu za Vodacom, Airtel, Zantel na Tigo na taasisi za fedha kama
Benki ya Posta Tanzania, NMB, NBC, CRDB, EXIM nk. wanaendelea na shughuli
mbalimbali za biashara ndani ya Mkoa. Hata hivyo bado kuna fursa nyingi za
kuwekeza hususani katika uanzishaji wa maduka makubwa yenye bidhaa mbalimbali,
hoteli za kitalii, vituo vya utamaduni, huduma za usafirishaji, mawasiliano na
shughuli za kibenki. UTALII Mkoa una maeneo mazuri ya vivutio vya utalii
ambavyo ni Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Ziwa Manyara ambako hupatikana aina
mbalimbali za wanyamapori kama Simba, Chui, Chita, Twiga, Pundamilia, Swala,
Nyati, Pofu, Ngiri, Mbuni, Korongo nk. Eneo jingine la utalii ni Yaeda Chini
ambako upatikana jamii ya Wahadzabe ambao huishi kwa kutegemea uwindaji,
matunda, mizizi na asali. Hivyo, Mkoa unawakaribisha wawekezaji kuanzisha na
kuwekeza katika hoteli na vituo vya utamaduni kwa ajili ya kutoa huduma muhimu
kwa Watalii mbalimbali wanaotembelea Mkoa huu.
MISITU
Wawekezaji wanakaribishwa katika Mkoa kuwekeza katika shughuli za Ufugaji
nyuki na uzalishaji Asali. Mkoa una eneo lenye ukubwa wa hekta 927,526 za
hifadhi za Misitu zilizohifadhiwa kisheria ambamo shughuli za ufugaji nyuki na
uzalishaji Asali zinaweza kufanyika. Tayari baadhi ya wananchi wanaendelea na
shughuli hii katika misitu asili na binafsi iliyopo katika maeneo mbalimbali ya
Mkoa.
MADINI
Mkoa una utajiri mkubwa wa madini ya Tanzanite ambayo yanathamani kubwa na
hayapatikani mahali popote duniani isipokuwa Mkoani Manyara Wilaya ya Simanjiro
eneo la Mirerani. Madini mengine yanayopatikana Mkoani hapa ni pamoja na: Ruby,
Green Garnet, Green Tourmaline na Rhodilite. Ukiacha madini ya Tanzanite,
hakuna uwekezaji katika aina nyingine ya madini tajwa hapo juu hivyo Wawekezaji
wanakaribishwa kuwekeza katika Sekta ya Madini.
FURSA ZA UWEKEZAJI
KATIKA HUDUMA ZA KIJAMII
Mkoa unawakaribisha wawekezaji kuwekeza katika Sekta za Elimu, Afya na Maji
kwani huduma zinazoendelea kutolewa kupitia Sekta hizi bado hazitoshelezi na ni
duni katika baadhi ya maeneo. Lengo kuu la Mkoa ni kuimarisha Sekta hizi ili
kusaidia kuleta maendeleo ya haraka na kuondoa umaskini kwa Wananchi.
FURSA ZA
UWEKEZAJI KATIKA HUDUMA ZA KITAMADUNI
Ili kudumisha tamaduni zilizopo, Mkoa kupitia Hospitali ya Rufaa ya Haydom
iliyopo Wilayani Mbulu inajenga kituo cha Utamaduni (4corners) kitakachofanya
utafiti wa mila na desturi za makabila 4 ya Mkoa wa Manyara ambayo ni
Wahadzabe, Wanyaturu, Wairaqw na Wabarbaig. Vilevile, Mkoa unakituo cha Redio
cha kijamii cha ORKENERI RADIO SERVICE 94.40RS FM kilichopo Wilayani Simanjiro
kinachofanya kazi kubwa ya kutangaza utamaduni wa jamii ya Kimaasai. Hata hivyo
Mkoa unawakaribisha wawekezaji kuanzisha vituo vingine vya Utamaduni katika
maeneo mbalimbali kama vile Yaeda Chini ili kuwavutia zaidi Watalii. Aidha,
Mkoa unawakaribisha wawekezaji kuwekeza katika Michezo ya aina mbalimbali kwani
kwa Miaka mingi sasa Mkoa umekuwa chimbuko la Wanariadha maarufu nchini
Tanzania ambao walipeperusha Bendera ya Tanzania katika mashindano mbalimbali
ndani na nje na kuuletea sifa Mkoa na Nchi. Miongoni mwawanariadha hao ni;
Gidamis Shahanga, Joh Bura, John Stephen Akhwari, Zakayo Malekwa na Simon
Robert Naali.
MPYA KUHUSU MATIKITI MAJI - water melon
Ili kulima matikiti maji, inakubidi uwe na sehemu ya kutosha, yenye jua la kutosha, maji mengi na ardhi yenye rutuba ya kutosha, matikiti maji hukua haraka kama mimea mimgine ya jamii yake itambaayo mfano Matango, maboga na maskwash.
Kwa mtu ambaye anaanza kilimo yatampa tabu kidogo tofauti na Yule ambaye ana ujuzi kidogo na mambo ya kilimo kwa sababu yanahitaji umakini kiasi.
HALI YA HEWA
Mimea hii haihimili hali ya joto kali sana, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu, inastawi vizuri kwenye kuanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa machi mpaka wa septemba .
UPANDAJI
Panda kwa kutumia Mbegu zinazouzwa madukani, ukitumia Mbegu kutoka kwenye tikiti ulilonunua linaweza likawa ni hybrid na matokeo yake matikiti yatakayozaliwa hayatakuwa bora kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)
Panda Mbegu yako moja kwa moja kwenye shamba, usinunue miche au kupanda Mbegu kwenyemifuko ya plastiki halafu ndi uhamishie shambani, panda Mbegu mbili sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 2 - 3 kutoka mstari hadi mstari, baada ya siku chache Mbegu zitaanza kuota, baada ya kama wiki 2 katika Mbegu mbili ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi, angalizo using’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki.
Unaweza kupandishia udongo kwenye mashina na hii itasaidia kupunguza maji yasituame kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba.
Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya wa kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda yenye, na wakati wa kuanza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe mimea kwa kuielekezea kwenye waya na kufungia
MCHE ULIOCHIPUKA
UANGALIZI
Miche ikiwa imetambaa kiasi unaweza kuweka matandazo kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu, unaweza kuweka samadi au mbolea za viwandani, mimea ikiwa midogo tumia zaidi mbolea zenye nitrojen na utumie zaidi mbolea za potasiam mara baada ya maua kutokeza hadi matunda kukomaa, matawi yakifikia urefu wa mita 2 kata mbele ilikuruhusu kutoa matawi na hivyo kupata maua mengi zaidi hatimaye mavuno zaidi
MAUA NA MATUNDA
Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja, maua dume ambayo ni madogo zadi hutoka kwanza yakifuatiwa na maua jike ambayo ni makubwa zaidi, usipoona maua dume na jike kuna tatizo mfano maji kidogo yalimwagiliwa, upungufu wa viritubisho kwenye udongo, hali ya hewa ni joto/baridi sana n.k
Uchavushaji kwenye matikiti hufanyika na wadudu, kama huwaoni wakifanya kazi yao unaweza kufanya mwenyewe, muda mzuri ni wa asubuhi, unakata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi
UCHAVUSHAJI KWA MKONO
UVUNAJI MATIKITI
Ili kujua matikiti yamekomaa inahitaji ujuzi kidogo, upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano, pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu, ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake kama tunavyofanya kwenye mafenesi, hii nayo ni shule nyingine. Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi
MAGONJWA NA WADUDU
Wadudu wa matikiti wako wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea, ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kjupata dawa sahii, dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda na FUNGICIDE itasaidia kwa mashambulizi ya fangasi
SOKO LA KATANI YA TANZANIA NCHINI MAREKANI LIMEDORORA
Soko la
Katani ya Tanzania nchini Marekani limedorora kufuatia kuibuka ushindani mkali
kutoka Brazil huku kimbilio la katani ya Tanzania likibaki nchi za Afrika na
Asia.
WADAU WAOMBWA KUDHAMINI MAONYESHO YA KAZI ZA VIJANA WAJASIRIAMALI YATAKAYOFANYIKA DODOMA
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya Aj It Development Bw Jackson Audiface akizungumzia kuhusu Maonyesho ya Tatu ya Kazi za Vijana wajasiriamali Yatakayofanyika Mkoani Dododma Mwezi Aprili mwaka huu.Maonyesho hayo ya kazi za Vijana wajasiriamali Hususani Vijana wanaosoma Vyuo Vikuu vya Dodoma. Lengo la Manonyesho hayo ni Kuzitangaza Kazi za Vijana wajasiriamali Wa Tanzania.Pili kuwapa Muda wadau Mbalimbali Kukutana na Vijana Wajasiriamali Ili kutatua Kero zote zinazowakabili vijana Katika Shuguli zao za Ujasiriamalia .
Baadhi ya Bidhaa Ambazo zinazozalishwa na Vijana wajasiriamali Waliohitimu Vyuo vikuu Mbalimbali hapa Nchini Na Ambao Bado wako Vyuoni kuendelea na Masomo yaoamabzo zitaonyeshwa katika Maonyesho hayo Yatakayofanyika Mkoani Dodoma Yakiwa Ni ya Tatu kuafanyika hapa Nchini kwa Lengo la Kukuza soko la Kazi za Vijana wajasirimali pia Kuzitangaza na Kuatatua Ngangamoto Mbalimbali Zinazowakabili Vijana wa Kitanzania Kama Vile Vibali vya Kufanya Biashara Kutoka Mamlaka Mbalimbali hapa Nchi.Wadau Mbalimbali wa Vijana Mnaombwa Kujitokeza Kudhamini Maonyesho hayo. Bidhaa mbali mbali za kilimo zinazo zalishwa na
Vijana wa Mkoani Dodoma Ambao watazionyesha kwa Wakazi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa ya Jirani.
Jackson Audiface Akielezea Zaidi Kuhusu Maonyesho hayo Yatakayofanyika Mkoani Dodoma.Hapa Akiwa Ameshika Mafuta yanayozalishwa na Vijana wajasirimali wa Mkoani Dodoma jana Wakati wajasiriamali hao walipotembelea Ofisi za Kampuni ya Aj It Development Kwajili ya Kujisajili ili kushiriki Katika Maonyesho ya Kazi za Vijana wajasiriamali Yatakayofanyika Mkoani Dodoma
Subscribe to:
Posts (Atom)







