Wednesday, September 17, 2014

MAONI YA MKULIMA NA MFUGAJI



Ndugu wananchi wenzangu napenda kuchukua fursa hii , Adimu  kuweka maoni yangu juu ya kilimo na ufugaji ndani ya taifa letu la Tanzania.Yapo mambo mengi yanasemwa , yanafanywa pia siasa nazo hazikubaki nyuma sana katika jambo hili.

 Mimi kama mdau wa kiliomo na ufugaji nimeona mambo mengi yakienda kimyume na utaratibu wa miaka mingi iliyopita, Kwamba utaratibu umebadilika mno na pia sera za nchi zikibadilika hasa unapo ingia uongozi mpya ktk taifa letu. Hii ina maana kwamba hakuna sera ya kudumu ya kuliongoza taifa kwenye maswala muhimu hata katika mfumo mzima wa ardhi na ufugaji. 
Hii ina maana kwamba watunga sera wamesahau mambo muhimu kama yafuatayo.

 {1} Ardhi tulio nayo aiongezeki.

 {2}Watu wanaongezeka

 {3} Mifugo nayo inaongezeka tena kwa kasi sana  Hili naona halina ubishi kabisa kwani naona haya  ni mambo ambayo lazima watunga sera wetu wakayaweka sawa kwani inavyo elekea siku za usoni nchi hii haita kalika kutokana na watu wawili tu, ambao ni ndugu kwa asili. 




 Ni lazima hatua zichukuliwe toka sasa kwa kujenga baadaye na wala sio mda ujao, hii inamaana kwamba hatua za makusudi lazima zifuatwe kwa msakabali wa taifa letu sote Kwani kinacho fanyika sasa ni uhuni, rushwa kutawala maeneo mengi na ubaguzi wa fedha kati ya walio nacho, yaani wakulima wakubwa na wafugaji wakubwa. Hii ni vita kubwa sana siku za usoni kwani lazima hatua zichukuliwe sasa .

Mimi ni mdau wa pande zote mbili hivyo ninaelewa nini ninachosema kutokana na uzoefu wangu na kuliona jambo hili kwa jicho la pili., Hivyo wadau na wapenzi wa kilimo na ufugaji ni lazima wakae meza moja na kujenga nchi yao kwani wanategemeana sana katika usawa wa taifa lao.

Napenda sana kuweka maoni yangu haya ili kwamba wadau wenzangu  kwa pamoja tushirikiane kuweka mambo yetu sawa ndani ya taifa letu, kwani bado hatuja chelewa ingawa mauji yametokea kwa pande zote twaomba Mungu atusaidie sana tuvuke salama katika jambo hili.

Napenda kutoa RAHI hasa kwa viongozi wetu wasifanye mchezo katika jambo hili kwani huu ni moshi tu ambao upo kwenye shimo ipo siku utatokeza nje hakuna wa kuuzima kwani ilakuwa ni janga kubwa sana katika taifa letu.Maoni yangu ni kwamba toka ngazi ya shina hadi taifa watu washirikishwe katika mambo ya nchi yao na kila jambo likae sawa kwani hatima ya nchi hii ni ya watanzania wenyewe hakuna mgeni atakaye weza kutusaidia katika swala hili.

Naomba kuwakilisha kwenu wadau wa taifa hili, Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

Lema.

No comments:

Post a Comment