Tuesday, January 27, 2015
Kuanzisha mradi wa mbuzi wa maziwa
Chaguo la mnyama wa kufuga hutegemea mambo mengi. Hata hivyo wakulima wengi hufuga wanyama ambao wana ujuzi wa kuwasimamia na wanawapatia mapato mazuri. Mbuzi wa maziwa hummtolea mkulima maziwa ya kunywa na kuuza,na samadi ya kurutubuisha ardhi na mbuzi wenyewe wanaweza kuuzwa. Na kipato cha ziada,wakulima wanaweza kulipa ada za nyumbani; kuwapeleka bwatoto wao shuleni ama kuwekeza mara nyingine kwa shamba na biashara zingine. Uchunguzi kifani unaofuata unaonyesha jinsi ya kufuga mbuzi wa maziwa,yaani kwa minajili ya utoaji wa maziwa.Msingi wake ni mradi unaoendelea katika divisheni ya Kibwezi katika wilaya ya Makueni ambao unafanywa na wenyeji na usaidizi wa shirika lisiilo la kiserikali linaloitwa Farm-Africa. Shirika hili lisiilo la kiserikali lilianzisha mradi uliotoa kizazi cha mbuzi kilichoboreshwa kinachoitwa Toggenburgs. Mbuzi hawa ambao ni wa kiume ni wa uzalishaji mtambuka na vizazi vya mbuzi wa kienyeji. Mradi huu pia umewapa mafunzo wakulima na wafanya kazi wa nje kuhusu ujuzi wa kufuiga mbuzi na kuwasimamia.Mafunzo haya yanajumlisha sehemu zifuatazo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment