Thursday, October 2, 2014
Tuesday, September 23, 2014
Michuzi blog ni chombo muhimu cha habari za huwakika,
Hii ni sehemu ya jangwa ambalo linafanya maajabu sana katika swala zima la kilimo. Nakufanya kuwa tegeneo kubwa sana kwa nchi zenye maeneo makubwa yanayofa kwa kilimo. Hii ni changa moto sana kwa wasomi wetu hasa wa kilimo kwani ni muhimu sana kujifunza kwa walio shinda.
Ndugu wadau habarini za leo! Mungu ni mwema kutupa tena leo, natafuta soko la mayai ya kuku wa kisasa. Tafadhali kama mwenye soko hilo tuwasiliane naye kwa no hii 0655615365. Ahsant
Saturday, September 20, 2014
Hii ndio mitambo ya maji na hali ya hewa ndani ya shamba.
- Mitambo ya kuratibu hali ya hewa pamoja na maji kwenye shamba la kisasa.
Haya ni matokeo bora ya kilimo cha kisasa, kwani yana hitaji hutaalamu wa hali ya juu.Hivyo ndugu zangu Watanzania shime tuweke juhudi sana katika kilimo na ufugaji.
Tunaona mwaka huu ulivyo kuwa wa neema sana 2014 angalia kibaigwa mahindi yalivyo furika.
Tunaona mwaka huu ulivyo kuwa wa neema sana 2014 angalia kibaigwa mahindi yalivyo furika.
Ndugu zangu msiache kutanzama blog kubwa hapa nchini Tanzania [Michuzi blog ] ambao inatarifa nyingi kila baada ya saa.
Friday, September 19, 2014
- TAZANA MAZAO YANAYO PATIKANA KWA NJIA YA KISASA
Wednesday, September 17, 2014
MAONI YA MKULIMA NA MFUGAJI
Ndugu wananchi wenzangu napenda kuchukua fursa hii , Adimu kuweka maoni yangu juu ya kilimo na ufugaji ndani ya taifa letu la Tanzania.Yapo mambo mengi yanasemwa , yanafanywa pia siasa nazo hazikubaki nyuma sana katika jambo hili.
Mimi kama mdau wa kiliomo na ufugaji nimeona mambo mengi yakienda kimyume na utaratibu wa miaka mingi iliyopita, Kwamba utaratibu umebadilika mno na pia sera za nchi zikibadilika hasa unapo ingia uongozi mpya ktk taifa letu. Hii ina maana kwamba hakuna sera ya kudumu ya kuliongoza taifa kwenye maswala muhimu hata katika mfumo mzima wa ardhi na ufugaji.
Hii ina maana kwamba watunga sera wamesahau mambo muhimu kama yafuatayo.
{1} Ardhi tulio nayo aiongezeki.
{2}Watu wanaongezeka
{3} Mifugo nayo inaongezeka tena kwa kasi sana Hili naona halina ubishi kabisa kwani naona haya ni mambo ambayo lazima watunga sera wetu wakayaweka sawa kwani inavyo elekea siku za usoni nchi hii haita kalika kutokana na watu wawili tu, ambao ni ndugu kwa asili.
Mimi ni mdau wa pande zote mbili hivyo ninaelewa nini ninachosema kutokana na uzoefu wangu na kuliona jambo hili kwa jicho la pili., Hivyo wadau na wapenzi wa kilimo na ufugaji ni lazima wakae meza moja na kujenga nchi yao kwani wanategemeana sana katika usawa wa taifa lao.
Napenda sana kuweka maoni yangu haya ili kwamba wadau wenzangu kwa pamoja tushirikiane kuweka mambo yetu sawa ndani ya taifa letu, kwani bado hatuja chelewa ingawa mauji yametokea kwa pande zote twaomba Mungu atusaidie sana tuvuke salama katika jambo hili.
Napenda kutoa RAHI hasa kwa viongozi wetu wasifanye mchezo katika jambo hili kwani huu ni moshi tu ambao upo kwenye shimo ipo siku utatokeza nje hakuna wa kuuzima kwani ilakuwa ni janga kubwa sana katika taifa letu.Maoni yangu ni kwamba toka ngazi ya shina hadi taifa watu washirikishwe katika mambo ya nchi yao na kila jambo likae sawa kwani hatima ya nchi hii ni ya watanzania wenyewe hakuna mgeni atakaye weza kutusaidia katika swala hili.
Naomba kuwakilisha kwenu wadau wa taifa hili, Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
Lema.
Subscribe to:
Posts (Atom)
















































