Arusha
Wafugaji nchini wameshauriwa kutumia mfumo wa teknolojia
wa simu za mikononi itakayosaidia kuboresha afya ya jamii kwa ujumla
katika kuwasiliana na wataalamu pindi kunapotokea matatizo yakiwaemo
magonjwa katika jamii zao.Hayo yalisemwa na Mtafiti wa Kuboresha na
Ufuatiliaji wa Magonjwa kwa Njia ya Simu kutoka Taasisi ya Utafiti na
Udhibiti wa Magonjwa Ambukizi Kusini mwa Bara la Afrika (SACDS), Profesa
Ezron Karimuribo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa.
Alisema taasisi hiyo imekwisha wapatia elimu ya
kutumia teknolojia hiyo mpya wafugaji pamoja na wataalamu wa afya na
mifugo zaidi ya 30 kutoka Wilaya ya Ngorongoro.
No comments:
Post a Comment