Monday, April 22, 2013

Wakulima wa korosho wapata hasara ya Sh10 bilioni

 Wakulima wa zao la korosho mkoani Lindi wamepata hasara ya jumla ya Sh10 bilion kutokana na kuuza korosho kwa bei ya chini ya dira ya Sh1200.
Kufuatia hasara hiyo wakulima hao wameitaka Serikali iwafidie wakulima hao wa korosho kama ilivyo kwa wakulima wengine ambao huwa wanapata hasara nchini.
Hayo yalibainishwa mkoani hapa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Abdallah Chikawe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa wa Mkoa wa Lindi (ALAT), wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma.
Chikawe alisema wakulima wa zao la korosho wa Mkoa wa Lindi hawana imani na Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Lindi cha Ilulu pamoja na COASCO.
Hata hivyo walimtaka Mkuu wa Mkoa wa Lindi afunge akaunti zote za Chama cha Ushirika cha Ilulu cha mkoani Lindi hadi hapo ukaguzi utakapofanywa .

No comments:

Post a Comment