FAIDA ZA KUKU WA KIENYEJI.
Faida ni nyingi na zinafahamika lakini nitaeleza zile ambazo kwa wengine huenda zikawa ni ngeni kwao.
- Mayai huweza kutumika kwa tiba. (Pata maelezo jinsi yai la kuku wa
kienyeji linavyoweza kutumika kwa tiba kutoka kwa wataalam wa tiba
mbadala)
- Kiini cha njano cha yai kinaweza kutumika kutengenezea mafuta ya nywele (shampoo)
- Manyoya yake yanaweza kutumika kama mapambo.
Fuga kuku upate faida kwa kuzingatia:
Chanjo ya mdondo kila baada ya miezi mitatu na chanjo ya ndui mara mbili kwa mwaka
Zuia viroboto, utitiri na minyoo.
Chagua mayai bora kwa ajili ya kuatamiza
Panga kuuza kuku kwa makundi uongeze kipato
Kula mayai na kuku kadri uzalishaji unavyoongezeka.
Kipato unachokipata utenge pia na kiasi kwa ajili ya uendelezaji wa kuku
UTAGAJI WA MAYAI
Kwa kawaida kuku huanza kutetea(Kutoa mlio wa ishara ya kutaga)
anapofikisha miezi sita hadi minane. Hivyo ni vyema viota viandaliwe
mapema wakiwa na umri wa miezi mitano. Kuku anapoanza kutaga akifikisha
mayai matatu mfugaji anashauriwa kuondoa kila yai linalozidi hayo matatu
kila siku linapotagwa na kuliweka alama ya tarehe au namba kwa kutumia
penseli ili kumfanya kuku aendelee kutaga kwa lengo la kufikisha mayai
15 mpaka 20. Mayai yanayoondolewa yawekwe kwenye chombo kikavu
kinachopitisha hewa ni vizuri pia kuweka mchanga ndani ya chombo hicho.
Hakikisha ya fuatayo.
Sehemu iliyochongoka iwe chini na pana iwe juu.
Hifadhi sehemu yenye hewa ya kutosha na isiyohifadhi joto
Mayai yasikae kwenye hifadhi hiyo zaidi ya wiki mbili toka siku ya kuanza kutagwa.
UATAMIAJI WA MAYAI NA UANGUAJI WA VIFARANGA
Uatamiaji na uanguaji wa kubuni - Mfumo huu hutumia mashine za
kutotoleshea vifaranga (Incubators) hutumika kuangua mayai mengi kati ya
50 hadi 500 kwa wakati mmoja Mashine zinazotumika kutotoleshea
vifaranga wa kisasa zinaweza kutumika pia kutotoleshea wa kienyeji.
Uatamiaji na uanguaji wa asili
KUCHAGUA MAYAI YA KUANGUA.
Hili nalo ni muhimu kuzingatia. Ni vizuri kuchagua mayai ya kuatamia ili
mayai yasiyofaa yaweze kuuzwa au kutumiwa nyumbani kwa chakula. Mayai
ya kuatamia yawe na sifa zifuatazo
Yasiwe na uchafu yawe masafi
Yasiwe na nyufa
Yatokane na kuku aliyepandwa na jogoo
Yasiwe madogo wala makubwa bali yawe na ukubwa wa wastani kulingana na umbile la kuku.
Yasiwe mviringo kama mpira pia yasiwe na ncha kali sana.
Yasiwe yamekaa muda mrefu zaidi ya wiki mbili toka yalipotagwa
Yasiwe yaliyohifadhiwa kwenye sehemu yenye joto.
No comments:
Post a Comment