Tuesday, January 20, 2015

MAMBO YA KUZNGATIA UNAPONUNUA MBEGU ZA VITUNGUU

MAMBO YA KUZNGATIA UNAPONUNUA MBEGU ZA VITUNGUU
• Chanzo cha mbegu
• Tarehe ya uzalishaji
• Tarehe ya kuisha muda wake
• Kifungashio cha mbegu.

Inashauriwa mkulima asipande mbegu zenye umri zaidi ya mwaka mmoja
Mbegu bora za vitunguu zinauzwa na makampuni binafsi kama: ALPHA Seed Co., Popvriend,
Rotian Seed, Kibo Seed, East African Seed Company nk. Wasambazaji wa mbegu ni pamoja na
maduka ya TFA, na maduka ya bembejeo za kilimo katika maduka mbalimbali.

Jinsi ya kuandaa kitalu na kuzalisha miche

• Sehemu ya kitalu iwe wazi, mbali na kivuli na kiwe karibu na chanzo cha maji.
• Tengeneza tuta la kubwa wa 1m x 2m . Urefu na idadi ya matuta hutegemea kiasi cha
mbegu. Kiasi cha mbegu kwa hectare moja ni kilo 6 au 2 kg kwa eka.
• Weka samadi iliyooza vizuri kiasi cha debe moja au mchanganyiko wa mbolea ya TSP na
CAN (200gm) kwa uwiano wa 1:1 kwenye tuta changanya vizuri na udongo.
• Sia mbegu kwenye mistari kwa nafasi ya 1 sm x 20 sm. Tawanya mbegu vizuri wakati
wa kusia ili miche isisongamane.
• Funika mbegu na weka matandazo ya nyasi kavu juu ya tuta na mwagiliwa maji. Udongo
unatakiwa kuwa na unyevu kiasi mpaka mbegu ziote.
• Nyasi ziondolewe mara tu mbegu zikiota (siku7-10 kutegemea hali ya hewa).
• Miche itunzwe vizuri na kitalu kiwe katika hali ya usafi.
• Miche imwagiliwe maji mpaka ifikie umri wa kupandikiza shambani (wiki 5-6)

Matatizo ya miche kitaluni ni kama yafuatayo:

Kuonza kwa mbegu, kunyauka kwa miche kabla na baada ya kuoto. Hali hii inasababishwa na
ugonjwa wa ukungu “Kinyausi” .Dawa za ukungu kama Dithane M45 au Ridomil MZnk
zinatumike kuzuia (changanya dawa na povu la sabuni ili dawa ijishike kwenye majani). Pia
uangalifu uwepo wakati wa kumwagilia maji. Mwagilia maji wakati wa asubuhi au jioni. Epuka
kumwagilia maji wakati wa jua kali kwani unjevunjevu hewani unaongeza na kusababisha
vimelea vya magonjwa.
Wadudu waharibifu ni pamoja na Chawa wekundu.ambao wanashambulia majani, Sota ambao
hukata miche. Dawa za viwandani kama Thiodan , Selecron au Dusrban zinazuia na kudhibiti
hwa wadudu.
 Baada ya wiki 5 au 6, kutegemeana na hali ya hewa miche itakuwa tayari kupandikiza
shambani. Miche iimarishwe kwa kusitisha maji, wiki moja kabla ya kupandikiza.
Kutayarisha shamba
Shamba litayarishwe sehemu usiyokuwa na mwinuko, sehemu ya wazi ambayo haijalimwa
vitunguu kwa muda wa miaka 2 -3. Shamba liwe karibu na chanzo cha maji kwa ajili ya
umwagiliaji. Matuta 1m x 3m au majaruba ya 2mx 3m.yanafaa kwa kupanda miche. Matatu au
majaruba yanarahisisha umwagiliaji, palizi na unyunyiziaji wa dawa.

No comments:

Post a Comment