Uzalishaji wa vitunguu
Zao la vitunguu linazalishwa kutokana na mbegu na miche inakuzwa kwenye kitalu kabla ya
kupandikizawa shamban. Miche inakuwa na kuzaa vitunguu.Vitunguu vikikomaa, vinavunwa na
kuhifadhiwa vikiwa katika hali ya kulala bwete. Katika hali hii vitunguu vinaweza kuhifadhiwa
kwa muda mrefu aitha kwa ajili ya kuzalisha mbegu msimu unaofuata au kuuza.
Wingi na ubora wa zao la vitunguu hutegemea; hali ya hewa, aina ya vitunguu, upatikanaji wa
mbegu bora, kilimo bora, uangalifu wakati wa kuvuna, usafirishaji na hifadhi bora.
Uzalishaji
Hali ya hewa na maji
Hali ya hewa na maji ni vipengele muhimu sana vya kuzingatia katika uzalishaji wa vitunguu.Vitunguu vinastawi vizuri katika hali ya ukavu kwa kutumia umwagiliaji. Maji mengi hasa
wakati wa masika inasababisha magonjwa mengi hasa ukungu, vitunguu haviwezi kukomaa
vizuri, hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa mazao. Jua na hewa kavu ni muhimu sana wakati
wa kukomaa na kuvuna vitunguu.
Aina za vitunguu
Aina bora za vitunguu ni pamoja na Mang’ola red, Red creole na Bombay Red. Hizi ni mbegubora ambazo zinatoa mazao mengi kuanzia 40-60kgs kwa hekta ikiwa kilimo bora
kitazingatiwa.Mkulima anaweza kuchagua mbegu kwa kuzingatia:-
• mahitaji ya soko (vitunguu vyekundu hupendwa zaidi)
• musimu wa kupanda
• uwezo wa kuzaa mazao mengi
• uwezo wa vitunguu kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
Mbegu bora
Ubora wa mbegu ni muhimu sana, kwani ndiyo chanzo cha mazao bora. Mbegu bora inatoamiche yenye afya na kuzaa mazao mengi na bora. Mbegu za vitunguu inapoteza uoto wake upesi
baada ya kuvunwa (mwaka1). Mbegu nzuri zina sifa zifuatazo:-
• Uotaji zaidi ya 80%
• Mbegu safi zisiyo na mchanganyhiko
• Zimefungwa vizuri kwenye vyombo visivyopitisha hewa na unjevu.
No comments:
Post a Comment