Tuesday, January 27, 2015
UFUGAJI WA NYUKI
Ufugaji wa nyuki ni kazi ambayo imekuwepo na kudumu kwa karne nyingi sana. Shughuli ya ufugaji wa nyuki nchini Tanzania hasa katika mkoa wa Tabora ambao ni maarufu kwa uzalishaji wa asali, ilianza kutambulika rasmi tangu mwaka 1884, wakoloni kama vile Rebman na Craft walipofika katika eneo hilo.
Monday, January 26, 2015
Kilimo Biashara katika shughuli ya ufugaji nyuki na uvu...
kijana ambaye amejitita katika kilimo biashara amejitika katika ufugaji wa nyuki
Hao ni baazi ya kuku chotara kuku hao chotara ni wazuri sana kwa nyama na wanasoko zuri sana ni kuku ambao wanampa mfugaji faida nzuri sana.Chotara hao wana miezi Tisa mfugaji wetu anaweza kuwauza kwa sh 15000/=kwa jogoo moja au sh 20000/= kwa mtetea mfugaji anaweza akauza kwa sh 20000/= hiyo ndio faida ya mfugaji wa kuku wa aina ya chitara hii ni moja ya utajili wa mfugaji
Hili ni moja ya banda bora lililojengwa kwa ubora zaidi banda hili lina vyumba vitatu chumba cha kwanza wana kaa kuku wa kawaida ambao hawatagi chumba cha mwisho wanakaa kuku wanao lalia mayai na wametenganisha sehemu ya kukuzia vifaranga
Saturday, January 24, 2015
Thursday, January 22, 2015
JINSI YA KULIMA SEHEMU YA MLIMA
Wednesday, January 21, 2015
JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI
Tengeneza chakula cha samaki mwenyewe
Mahitaji
• Pumba ya mahindi sadolini 1.
• Pumba ya ngano au mpunga sadolini 1.
• Dagaa sadolini 1.
• Kilo moja ya soya.
• Robo kilo ya mashudu ya pamba au alizeti.
Namna ya kuandaa
• Changanya malighafi hizo kwa pamoja.
• Saga hadi zilainike.
• Kanda kama vile unga wa kutengenezea chapati.
• Weka kwenye mashine ya kusaga nyama au kutengenezea tambi.
• Anika kwenye jua la wastani.
• Baada ya kukauka, vunja vunja kwenye vipande vidogo vidogo hasa kwa kuzingatia umri wa samaki unaokusudia kuwalisha.
• Tumia lishe hiyo kwa samaki mara tatu kwa siku.
UFUGAJI WA SAMAKI
Ufugaji wa samaki kama ilivyo shughuli nyingine yoyote ya kiuchumi inahitaji usimamizi mzuri ili uweze kuwa na faida. Mbali na hilo, mfugaji wa samaki anatakiwa kuzingatia vigezo vingi kabla ya kuanza ufugaji. Moja ya vigezo hivyo ni soko. Si jambo la busara kuanza shughuli yoyote kabla haujafanya uchunguzi na kujua kama kuna mahitaji ya bidhaa unayokusudia kuzalisha. Wafugaji wengi wameanzisha ufugaji wa samaki lakini wakaishia kupata hasara kutokana na ukosefu wa soko. Na wengine wameanguka kutokana na utunzaji mbovu wa mabwawa ya samaki.
Maji
Upatikanaji wa maji na ubora wake ni kigezo muhimu katika ufugaji wa samaki. Mtiririko wa maji ni njia rahisi kwa mfugaji. Maji machafu hayatakiwi kwa ufugaji wa samaki. Wafugaji ni lazima wasaidiwe na maafisa kilimo katika eneo lao kama maji yanayopatika yana ubora kwa ajili ya ufugaji wa samaki. Kwa wakazi wa Dar es
Salaam, inawezekana pia kufuga samaki kwenye bwawa, endapo maji yana chumvi ya wastani, na kwa kiwango kinachoshauriwa kitaalamu, basi samaki wanaweza kustahimili, na kukua vizuri.
Bwawa
Bwawa la samaki linahitaji nafasi kubwa ya ardhi, yenye mwinuko pamoja na eneo la samaki kukimbilia. Hii ni njia rahisi ya ufugaji endapo ardhi na maji havina gharama kubwa. Eneo kubwa zaidi linaruhusu uzalishaji usiohitaji nguvu ya ziada na wenye tija.
Utengenezaji wa bwawa la samaki kwa maeneo yenye udongo wa kichanga kama Dar es Salaam, mfugaji atalazimika kuchimba na kuweka karatasi ya nailoni. Hii, itasaidia kuzuia upotevu wa maji pamoja na kuzuia bwawa kuporomoka.
Ni vyema upande mmoja wa bwawa ukawa na kina kirefu kuliko mwingine. Upande mmoja unaweza kuwa na kina cha mita moja na nusu, na mwingine mita moja. Hii itamsaidia mfugaji kuweza kulihudumia bwawa vizuri, hata kama ni kuingia na kufanya usafi.
Utunzaji wa bwawa
Hivyo, kila unapoona uchafu, safisha mara moja.
Ulishaji
Wafugaji walio wengi, wamekuwa hawazingatii kanuni za ulishaji wa samaki. Kwa kawaida inatakiwa kuwalisha samaki mara mbili hadi mara tatu kwa siku.
Aina ya chakula
Samaki wanaweza kulishwa kwa kutumia pumba ya mahindi, mashudu ya pamba na alizeti, soya, mabaki ya dagaa. Haishauriwi kulisha chakula kilichoko kwenye mfumo wa vumbi, bali kiwe mabonge madogo madogo, kwa wastani wa tambi.
Magonjwa
Kwa kawaida samaki hawana magonjwa mengi sana yanayowashambulia, ila kuna baadhi ya yaliyozoeleka kama vile magonjwa ya ukungu (fangasi), magonjwa yatokanayo na virusi, pamoja na minyoo.
Samaki wanaposhambuliwa na fangasi, huonekana kwa macho kwa kuwa huwa na madoa madoa. Samaki aina ya kambale hushambuliwa zaidi kuliko perege.
Pia unaweza kutambua kuwa samaki ni mgonjwa kwa kuwa huzubaa sehemu moja kwa muda mrefu. Magonjwa kwa samaki pia yanaweza kutokana na mrundikano kwenye bwawa. Hivyo, ni muhimu kuwapunguza kila wanapoongezeka.
Tiba
Tiba iliyozoeleka kwa samaki ni kwa kuweka chumvi kwenye maji, kasha kuwatumbukiza samaki unaowaona kuwa ni wagonjwa, kisha kuwatoa na
kuwarudisha bwawani.
Upatikanaji
Unaweza kupata vifaranga wa samaki kutoka katika kituo cha kuzalisha na kufuga samaki Kingolwira Morogoro. Bei ya kifaranga cha Perege ni shilingi 50, na Kambale ni shilingi 150.
Tuesday, January 20, 2015
MAMBO YA KUZNGATIA UNAPONUNUA MBEGU ZA VITUNGUU
MAMBO YA KUZNGATIA UNAPONUNUA MBEGU ZA VITUNGUU
• Chanzo cha mbegu
• Tarehe ya uzalishaji
• Tarehe ya kuisha muda wake
• Kifungashio cha mbegu.
Inashauriwa mkulima asipande mbegu zenye umri zaidi ya mwaka mmoja
Mbegu bora za vitunguu zinauzwa na makampuni binafsi kama: ALPHA Seed Co., Popvriend,
Rotian Seed, Kibo Seed, East African Seed Company nk. Wasambazaji wa mbegu ni pamoja na
maduka ya TFA, na maduka ya bembejeo za kilimo katika maduka mbalimbali.
• Tengeneza tuta la kubwa wa 1m x 2m . Urefu na idadi ya matuta hutegemea kiasi cha
mbegu. Kiasi cha mbegu kwa hectare moja ni kilo 6 au 2 kg kwa eka.
• Weka samadi iliyooza vizuri kiasi cha debe moja au mchanganyiko wa mbolea ya TSP na
CAN (200gm) kwa uwiano wa 1:1 kwenye tuta changanya vizuri na udongo.
• Sia mbegu kwenye mistari kwa nafasi ya 1 sm x 20 sm. Tawanya mbegu vizuri wakati
wa kusia ili miche isisongamane.
• Funika mbegu na weka matandazo ya nyasi kavu juu ya tuta na mwagiliwa maji. Udongo
unatakiwa kuwa na unyevu kiasi mpaka mbegu ziote.
• Nyasi ziondolewe mara tu mbegu zikiota (siku7-10 kutegemea hali ya hewa).
• Miche itunzwe vizuri na kitalu kiwe katika hali ya usafi.
• Miche imwagiliwe maji mpaka ifikie umri wa kupandikiza shambani (wiki 5-6)
ugonjwa wa ukungu “Kinyausi” .Dawa za ukungu kama Dithane M45 au Ridomil MZnk
zinatumike kuzuia (changanya dawa na povu la sabuni ili dawa ijishike kwenye majani). Pia
uangalifu uwepo wakati wa kumwagilia maji. Mwagilia maji wakati wa asubuhi au jioni. Epuka
kumwagilia maji wakati wa jua kali kwani unjevunjevu hewani unaongeza na kusababisha
vimelea vya magonjwa.
Wadudu waharibifu ni pamoja na Chawa wekundu.ambao wanashambulia majani, Sota ambao
hukata miche. Dawa za viwandani kama Thiodan , Selecron au Dusrban zinazuia na kudhibiti
hwa wadudu.
Baada ya wiki 5 au 6, kutegemeana na hali ya hewa miche itakuwa tayari kupandikiza
shambani. Miche iimarishwe kwa kusitisha maji, wiki moja kabla ya kupandikiza.
Kutayarisha shamba
Shamba litayarishwe sehemu usiyokuwa na mwinuko, sehemu ya wazi ambayo haijalimwa
vitunguu kwa muda wa miaka 2 -3. Shamba liwe karibu na chanzo cha maji kwa ajili ya
umwagiliaji. Matuta 1m x 3m au majaruba ya 2mx 3m.yanafaa kwa kupanda miche. Matatu au
majaruba yanarahisisha umwagiliaji, palizi na unyunyiziaji wa dawa.
• Chanzo cha mbegu
• Tarehe ya uzalishaji
• Tarehe ya kuisha muda wake
• Kifungashio cha mbegu.
Inashauriwa mkulima asipande mbegu zenye umri zaidi ya mwaka mmoja
Mbegu bora za vitunguu zinauzwa na makampuni binafsi kama: ALPHA Seed Co., Popvriend,
Rotian Seed, Kibo Seed, East African Seed Company nk. Wasambazaji wa mbegu ni pamoja na
maduka ya TFA, na maduka ya bembejeo za kilimo katika maduka mbalimbali.
Jinsi ya kuandaa kitalu na kuzalisha miche
• Sehemu ya kitalu iwe wazi, mbali na kivuli na kiwe karibu na chanzo cha maji.• Tengeneza tuta la kubwa wa 1m x 2m . Urefu na idadi ya matuta hutegemea kiasi cha
mbegu. Kiasi cha mbegu kwa hectare moja ni kilo 6 au 2 kg kwa eka.
• Weka samadi iliyooza vizuri kiasi cha debe moja au mchanganyiko wa mbolea ya TSP na
CAN (200gm) kwa uwiano wa 1:1 kwenye tuta changanya vizuri na udongo.
• Sia mbegu kwenye mistari kwa nafasi ya 1 sm x 20 sm. Tawanya mbegu vizuri wakati
wa kusia ili miche isisongamane.
• Funika mbegu na weka matandazo ya nyasi kavu juu ya tuta na mwagiliwa maji. Udongo
unatakiwa kuwa na unyevu kiasi mpaka mbegu ziote.
• Nyasi ziondolewe mara tu mbegu zikiota (siku7-10 kutegemea hali ya hewa).
• Miche itunzwe vizuri na kitalu kiwe katika hali ya usafi.
• Miche imwagiliwe maji mpaka ifikie umri wa kupandikiza shambani (wiki 5-6)
Matatizo ya miche kitaluni ni kama yafuatayo:
Kuonza kwa mbegu, kunyauka kwa miche kabla na baada ya kuoto. Hali hii inasababishwa naugonjwa wa ukungu “Kinyausi” .Dawa za ukungu kama Dithane M45 au Ridomil MZnk
zinatumike kuzuia (changanya dawa na povu la sabuni ili dawa ijishike kwenye majani). Pia
uangalifu uwepo wakati wa kumwagilia maji. Mwagilia maji wakati wa asubuhi au jioni. Epuka
kumwagilia maji wakati wa jua kali kwani unjevunjevu hewani unaongeza na kusababisha
vimelea vya magonjwa.
Wadudu waharibifu ni pamoja na Chawa wekundu.ambao wanashambulia majani, Sota ambao
hukata miche. Dawa za viwandani kama Thiodan , Selecron au Dusrban zinazuia na kudhibiti
hwa wadudu.
Baada ya wiki 5 au 6, kutegemeana na hali ya hewa miche itakuwa tayari kupandikiza
shambani. Miche iimarishwe kwa kusitisha maji, wiki moja kabla ya kupandikiza.
Kutayarisha shamba
Shamba litayarishwe sehemu usiyokuwa na mwinuko, sehemu ya wazi ambayo haijalimwa
vitunguu kwa muda wa miaka 2 -3. Shamba liwe karibu na chanzo cha maji kwa ajili ya
umwagiliaji. Matuta 1m x 3m au majaruba ya 2mx 3m.yanafaa kwa kupanda miche. Matatu au
majaruba yanarahisisha umwagiliaji, palizi na unyunyiziaji wa dawa.
UZALISHAJI WA VITUNGUU
Uzalishaji wa vitunguu
Zao la vitunguu linazalishwa kutokana na mbegu na miche inakuzwa kwenye kitalu kabla ya
kupandikizawa shamban. Miche inakuwa na kuzaa vitunguu.Vitunguu vikikomaa, vinavunwa na
kuhifadhiwa vikiwa katika hali ya kulala bwete. Katika hali hii vitunguu vinaweza kuhifadhiwa
kwa muda mrefu aitha kwa ajili ya kuzalisha mbegu msimu unaofuata au kuuza.
Wingi na ubora wa zao la vitunguu hutegemea; hali ya hewa, aina ya vitunguu, upatikanaji wa
mbegu bora, kilimo bora, uangalifu wakati wa kuvuna, usafirishaji na hifadhi bora.
Uzalishaji
Hali ya hewa na maji
Hali ya hewa na maji ni vipengele muhimu sana vya kuzingatia katika uzalishaji wa vitunguu.Vitunguu vinastawi vizuri katika hali ya ukavu kwa kutumia umwagiliaji. Maji mengi hasa
wakati wa masika inasababisha magonjwa mengi hasa ukungu, vitunguu haviwezi kukomaa
vizuri, hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa mazao. Jua na hewa kavu ni muhimu sana wakati
wa kukomaa na kuvuna vitunguu.
Aina za vitunguu
Aina bora za vitunguu ni pamoja na Mang’ola red, Red creole na Bombay Red. Hizi ni mbegubora ambazo zinatoa mazao mengi kuanzia 40-60kgs kwa hekta ikiwa kilimo bora
kitazingatiwa.Mkulima anaweza kuchagua mbegu kwa kuzingatia:-
• mahitaji ya soko (vitunguu vyekundu hupendwa zaidi)
• musimu wa kupanda
• uwezo wa kuzaa mazao mengi
• uwezo wa vitunguu kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
Mbegu bora
Ubora wa mbegu ni muhimu sana, kwani ndiyo chanzo cha mazao bora. Mbegu bora inatoamiche yenye afya na kuzaa mazao mengi na bora. Mbegu za vitunguu inapoteza uoto wake upesi
baada ya kuvunwa (mwaka1). Mbegu nzuri zina sifa zifuatazo:-
• Uotaji zaidi ya 80%
• Mbegu safi zisiyo na mchanganyhiko
• Zimefungwa vizuri kwenye vyombo visivyopitisha hewa na unjevu.
NAMNA BORA YAKULISHA NA KUNYWESHA KUKU
NAMNA BORA YAKULISHA NA KUNYWESHA KUKU.
Maji ni muhimu sana kwa kuku wawapo bandani. Wape maji ya kutosha kila wakati unapoona yanapungua/kuisha ili waendelee kuyeyusha chakula wanachokula Nna kupunguza joto mwilini. Kuku 1 anaweza kunywa hadi robo lita ya maji kwa siku. Kwa hiyo utawawekea kulingana na wingi wao. Pata chombo kizuri ili uwaning’inizie juu kidogo kutoka usawa wa ardhi. Hii itasaidia kupunguza uchafuzi wa maji na magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya maji.
ZINGATIA= hakikisha kuwa maji ni safi na salama.
Ni vema kutafuta vifaa vizuri kwaajili ya kuwawekea chakula. Tafuta vyombo ambavyo utaweza kuning’iniza/tundika juu kidogo kutoka chini kulingana na umri wa kuku. Hii itasadia sana kupunguza uwezekano wa kutosambaa kwa magonjwa hasa yale yanayoenezwa kupitia viatu tunvyo vaa tunapoingia bandani. Pia itasaidi sana kupunguza chakula kinacho mwagika chini wakati kuku wanapokula.
Kwa mfugaji yeyote wa kuku anapaswa kuelewa kuwa chakula cha kuku ni ghali. Hivyo ni vema kufuata taratibu vizuri katika ulishaji na kutengeneza/kununua vyombo ambavyo kuku hataweza kumwaga chakula. Kumbuka kwamba kama vyombo siyo vizuri basi vitamwaga chakula kingi na hivyo kukuletea hasara.
Ili kuweza kupata mazao mazuri yenye faida, ni vema ununue chakula cha kuku madukani au utengeneze wewe mwenyewe kama nitakavyoeleza hapa chini ili uwape kuku wako chakula chenye viini lishe vyote muhimu kwa kuzingatia umri wa kuku ulionao. Kwa vifaranga, unaweza kuwawekea chakula chini kwenye magazeti/mifuniko ya ndoo/sahani. Baada ya siku 10 unaweza kuwawekea kwenye chombo maalum.
Namna ya kuandaa chakula cha kuku.
Vyakula vya kuku vinapaswa kuwa na aina/viini lishe muhimu kama vile Protini, Wanga, madini na Vitamini.
Vyakula hivyo vimegawanyika kama ifuatavyo;
Ukosefu wa madini kama fosforasi na kalsiam husababisha matege, vidole kukunjamana, kufyatuka kwa misuli ya magoti, kuwa kilema na kupofuka macho kwa kuku.
- MAJI.

- CHAKULA.

- Vyakula vya kujenga mwili ni; Jamii ya kunde,samaki, dagaa,mashudu ya ufuta/alizeti/pamba,
- Vyakula vya kulinda mwili ili usipatwe na maradhi ni; Mafuta ya samaki na majani mabichi kama vile; kabichi, mchicha,majani ya mpapai na nyasi mbichi.
- Vyakula vinavyojenga mwili/mifupa ni kama vile; Aina za madini, chokaa, chumvi na mifupa iliyosagwa.
- Vyakula vilivyotajwa vinaweza kumkuza vizuri kuku hadi uuzwaji/kuliwa kwake. Surghum Larrymeal huzuia kudonoana, huboresha kiini cha yai na kuongeza mayai. Changanya kg 1 kwa kg 50 za pumba.
Ukosefu wa madini kama fosforasi na kalsiam husababisha matege, vidole kukunjamana, kufyatuka kwa misuli ya magoti, kuwa kilema na kupofuka macho kwa kuku.
Monday, January 19, 2015
KUCHI WEKUNDU CHOTARA
Kuchi chotara wekundu : Hawa ni kuchi
chotara wekundu siza zake hapati magonjwa kama kuku wengine na ni
watagaji wazuri pia.karibu kuwa mfugaji utafurahia mifugo yako.
Black Australorp (Weusi/Malawi)
Black Australorp (Weusi/Malawi) ;
ni kuku weusi na wenye maumbo makubwa kama wanavyoonekana kwenye
picha.sifa ya kuku hawa ni watagaji sana kuliko kuku mwingine
yoyote.mayai yake ni madogo kuliko kuku wengine,siyo mzito kama kuku
wengine lakini watagaji wazuri
KUCHI
KUCHI
Ni kuku warefu kwa umbo na wenye kusimama mgongo ukiwa wima. Wana manyoya machache mwilinini na hasa kifuani, vilemba vyao ni vidogo. Majogoo huwa na wastani wa uzito wa Kg. 2.5 na mitetea kg 1.5 mayai ya kuchi yana uzito wa wastani wa gm 45. Ni moja ya jogoo mzuri sana

FAIDA ZA KUKU WA KIENYEJI
FAIDA ZA KUKU WA KIENYEJI.
Faida ni nyingi na zinafahamika lakini nitaeleza zile ambazo kwa wengine huenda zikawa ni ngeni kwao.
- Mayai huweza kutumika kwa tiba. (Pata maelezo jinsi yai la kuku wa kienyeji linavyoweza kutumika kwa tiba kutoka kwa wataalam wa tiba mbadala)
- Kiini cha njano cha yai kinaweza kutumika kutengenezea mafuta ya nywele (shampoo)
- Manyoya yake yanaweza kutumika kama mapambo.
Fuga kuku upate faida kwa kuzingatia:
Chanjo ya mdondo kila baada ya miezi mitatu na chanjo ya ndui mara mbili kwa mwaka
Zuia viroboto, utitiri na minyoo.
Chagua mayai bora kwa ajili ya kuatamiza
Panga kuuza kuku kwa makundi uongeze kipato
Kula mayai na kuku kadri uzalishaji unavyoongezeka.
Kipato unachokipata utenge pia na kiasi kwa ajili ya uendelezaji wa kuku
UTAGAJI WA MAYAI
Kwa kawaida kuku huanza kutetea(Kutoa mlio wa ishara ya kutaga) anapofikisha miezi sita hadi minane. Hivyo ni vyema viota viandaliwe mapema wakiwa na umri wa miezi mitano. Kuku anapoanza kutaga akifikisha mayai matatu mfugaji anashauriwa kuondoa kila yai linalozidi hayo matatu kila siku linapotagwa na kuliweka alama ya tarehe au namba kwa kutumia penseli ili kumfanya kuku aendelee kutaga kwa lengo la kufikisha mayai 15 mpaka 20. Mayai yanayoondolewa yawekwe kwenye chombo kikavu kinachopitisha hewa ni vizuri pia kuweka mchanga ndani ya chombo hicho.
Hakikisha ya fuatayo.
Sehemu iliyochongoka iwe chini na pana iwe juu.
Hifadhi sehemu yenye hewa ya kutosha na isiyohifadhi joto
Mayai yasikae kwenye hifadhi hiyo zaidi ya wiki mbili toka siku ya kuanza kutagwa.
UATAMIAJI WA MAYAI NA UANGUAJI WA VIFARANGA
Uatamiaji na uanguaji wa kubuni - Mfumo huu hutumia mashine za kutotoleshea vifaranga (Incubators) hutumika kuangua mayai mengi kati ya 50 hadi 500 kwa wakati mmoja Mashine zinazotumika kutotoleshea vifaranga wa kisasa zinaweza kutumika pia kutotoleshea wa kienyeji.
Uatamiaji na uanguaji wa asili
KUCHAGUA MAYAI YA KUANGUA.
Hili nalo ni muhimu kuzingatia. Ni vizuri kuchagua mayai ya kuatamia ili mayai yasiyofaa yaweze kuuzwa au kutumiwa nyumbani kwa chakula. Mayai ya kuatamia yawe na sifa zifuatazo
Yasiwe na uchafu yawe masafi
Yasiwe na nyufa
Yatokane na kuku aliyepandwa na jogoo
Yasiwe madogo wala makubwa bali yawe na ukubwa wa wastani kulingana na umbile la kuku.
Yasiwe mviringo kama mpira pia yasiwe na ncha kali sana.
Yasiwe yamekaa muda mrefu zaidi ya wiki mbili toka yalipotagwa
Yasiwe yaliyohifadhiwa kwenye sehemu yenye joto.

Friday, January 16, 2015
JINSI YA KUMTAMBUA KUKU ANAYE UMWA NA KUKU MWENYE AFYA
TOFAUTI ZA MUONEKANO YA KUKU MWENYW AFYA NA KUKU MGONJWA
KUKU MWENYE AFYA
Macho na sura angavu
Hupenda kula na kunywa maji
Pua zilizo safi, upanga na undu mwekundu, manyoya
laini na yaliyopangika vizuri
Hupumua kwa utulivu
Sehemu ya kutolea haja huwa kavu
Kinyesi kikavu, cheupe na kisicho na rangi
Hutaga mayai kawaida
KUKU ASIYE KUWA NA AFYA NZURI(MGONJWA)
Huonekana mchovu na dhaifu
Hula na kunywa kidogo au zaidi ya kawaida
Hutoa kamasi puani, ute na matongotongo; manyoya
yaliyovurugika
Hupumua kwa shida na kwa sauti
Sehemu ya kutolea haja inakuwa na unyevunyevu na
kinyesi kuganda
Huharisha, kinyesi huwa na damu au minyoo
Hutaga mayai machache au husimama kutaga kabisa
Huwa na tabia ya kujitenga na wenzake katika kundi
NAMNA YA KUBORESHA UFUGAJI WA KUKU
Wafugaji wengi wa Tanzania wanafuga kuku wa kienyeji. Ndege hawa kwa kawaida wanafugwa sehemu za vijijini ambapo wanaachiwa huru kuzurura.
Mfugaji anayetaka kufanikiwa katika ufugaji wa kuku wa kienyeji ni lazima achanganye mbinu za kienyeji na za kisasa. Hii inajumuisha njia zifuatazo:
Kuchagua aina/mbegu
Kuchagua mbegu inamaanisha: Mtetea au jogoo mwenye ubora wa hali ya juu , akiwa na sifa kama uzalishaji wa juu wa mayai au uzalishaji wa nyama, wanachanganywa na aina mfugaji alionayo, au kuboresha mbegu ambayo ni dhaifu. Kuna makundi matatu ya aina za kuku;
• Kuku wenye umbo dogo ni wazuri zaidi kwa uzalishaji wa mayai.
• Kuku wenye umbo kubwa ni wazuri zaidi kwa uzalishaji wa nyama.
• Mbegu iliyochanganywa ni nzuri kwa uzalishaji wa mayai na nyama.
Endapo mfugaji anataka kufuga kuku kwa ajili ya mayai, basi anaweza kuchanganya mbegu ya kienyeji aliyonayo na mbegu yenye umbo dogo ambao wana historia nzuri ya uzalishaji wa mayai, na kama anataka kuzalisha kwa ajili ya nyama, basi anaweza kuchagua wenye umbo kubwa. Na ambae anahitaji kwa ajili ya mayai na nyama, basi anaweza kuchanganya mbegu.
Chagua mbegu kwa umakini
Wafugaji wenye uzoefu huchanganya mbegu tofauti ambazo zina ubora na sifa maalumu, kama vile uwezo wa kukabiliana na magonjwa, ukubwa wa mayai, umbo, na kiasi cha chakula wanachohitaji.
Vigezo vifuatavyo vinaruhusu uchaguzi sahihi:
1. Mtetea au jogoo kati ya kilo 1 mpaka 2, anahesabiwa kuwa kwenye kundi la umbo dogo.
2. Kuku wote wenye uzito wa kilo 3 au zaidi wanahesabiwa kwenye umbo kubwa.
Kuku wenye kilo 2 mpaka 3 wanahesabiwa kuwa mbegu mchanganyiko (Chotara).
Uzalishaji mzuri wa kuku ni pamoja na kuhakikisha kuwa, kila baada ya mzunguko mmoja, jogoo anabadilishwa, au kuku wote pamoja na mayai yake wanauzwa na kuleta aina nyingine ili kuzuia kizazi kujirudia. Ruhusu jogoo mmoja kuhudumia kuku 10 tu. Mfugaji pia anaweza kuzuia uwezekano wa kizazi kujirudia kwa kuweka kumbukumbu rahisi, kwa mfano, unaweza kuweka viota na kufahamu ni kuku yupi yupo kwenye kiota kipi na kwa muda upi.
Kumbukumbu ni muhimu
Uwekaji wa kumbukumbu ni lazima! Kumbukumbu humsaidia mfugaji kufahamu kizazi na tabia za kila kuku ambaye amechaguliwa kwa ajili ya uzalishaji, kiasi kwamba anaweza kuelezea kuhusu kila kuku aliye naye bandani, kwa kuzingatia uzalishaji wa mayai na nyama
Thursday, January 15, 2015
UFUGAJI WA KUKU: BANDA LA KUKU WA KIENYEJI
UFUGAJI WA KUKU: BANDA LA KUKU WA
KIENYEJI
Sifa za banda bora la Kuku
. Banda bora la kuku
linatakiwa kuwa kama ifuatavyo:
Liwe jengo imara
• Pasiwe na sehemu zilizo wazi kwenye msingi na kati ya ukuta na
paa.
• Banda lijengwe na vifaa vinavyopatikana katika mazingira yako
ili liwe na gharama utakayoweza kumudu.
• Unaweza kutumia matofali ya udongo, udongo, miti, fito,n.k.
Ukitumia fito au mabanzi ondoa maganda ili kuthibiti mchwa.
• Jengo mara litazuia maadui kama panya, vicheche, paka, nyoka na
wezi kuingia ndani ya banda na kuwadhuru au kuwaiba kuku.
Liwe rahisi kusafisha
• Kuta na sakafu visiribwe zisiwe na nyufa ili kurahisisha
kusafisha.
• Pia itadhibiti kusiwe na wadudu wa kujificha katika nyufa kama
papasi, viroboto n.k.
• Sakafu ya banda lazima iwekewe matandazo kama pumba ya mpunga au
maranda ya mbao au mabaki ya mazao au nyasi kavu kutegemeana na kinachopatikana
kwa urahisi katika mazingira yako.
• Matandazo haya husaidia kunyonya unyevu unaotokana na kinyesi
cha kuku au maji yanayomwagika katika banda.
• Banda hubakia kavu bila kuwa na harufu mbaya na wadudu kama inzi
hata vimelea vya magonjwa hudhibitiwa.
Eneo la nje kuzunguka banda kuwe na usafi wa
kudumu
Hali ya usafi nje ya banda itafanya wadudu
kama siafu au mchwa na wanyama kama panya na paka mwitu wakose maficho. Nje ya
banda ndani ya uzio kuwe na miti midogo na mimea mingine midogo kwa ajili ya
kivuli.
Ufugaji wa nusu huria
|
Banda liwe na nafasi ya kutosha kwa kuku
waliopo: Kwa kawaida eneo la mita mraba moja hutosha kuku wanne wanaotaga au
kuku 8 wa nyama. Nafasi ya mita mraba 1 inatosha vifaranga 16 hadi kufikia umri
wa majuma manne.
Liweze kuingiza hewa na mwanga wa kutosha:
Banda linaloweza kuingiza hewa safi na kutoka ndani yake hubaki kavu. Harufu
mbaya hutoka na kuku huweza kupumua hewa safi. Hii husaidia pia kudhibiti
kuzaliana kwa vimelea vinavyosababisha magonjwa,hivyo hudhibiti magonjwa.
Lisiwe na joto sana au baridi sana: Panda miti
ya kuzunguka banda lako ili eneo liwe na kivuli cha kutosha na pia lisiwe na
upepo mkali.Kama hali halisi ya eneo la kufugia ina joto kubwa kwa vipindi
virefu paa la banda wakati wa ujenzi liinuliwe juu zaidi kuruhusu mzunguko
zaidi wa hewa na joto la paa ( kama ni la bati) liwe mbali juu ya kuku.
Joto kwenye banda linaweza kusababishwa na
msongamano wa kuku, hivyo mfugaji aangalie aweke idadi ya kuku inayowiana na
ukubwa wa banda lake.
Paa lifunike ukuta kwa sehemu kubwa
|
Liwe imara na lisilovuja. Waweza kutumia
mabati, nyasi, madebe, makuti n.k. kutegemeana na upatikanaji wa vifaa vya
kuezekea.Wakati wa kuezeka paa lisiishie karibu sana na ukuta bali liwe na
sehemu kubwa iliyozidi ukuta kuzuia mvua kuingia ndani kama ni ya upepo (
angalia mchoro hapa chini).
Vifaa vinavyohitajika katika banda la kuku
Kuku wakifugwa kwa mtindo wa nusu ndani na
nusu nje wanahitaji huduma mbalimbali ndani ya banda na ndani ya wigo. Ili
kutoa huduma hizi vifaa vifuatavyo ni muhimu viwe katika banda:
Kinywesheo cha
kujitengenezea
|
Kuna njia nyingi za kutengeneza vyombo vya
kuwekea maji ya kuku ya kunywa.
• Aina ya mojawapo unayoweza kutumia ndoo au debe la lita kumi au
ishirini ya plastiki. Kata ndoo hiyo pande nne kutoa nafasi ya kuku ya kunywea
kama kielelezo kinavyoonyesha. Tengeneza idadi ya vyombo hivi inayowiana na
wingi wa kuku ulionao.
• Au waweza kutumia sufuria au beseni pana kiasi. Hii huwekewa
tofali au jiwe safi pana baada ya kuwekewa maji ya kunywa ili kuzuia kuku
wadogo wasizame na maji yasichafiliwe kirahisi.
• Vifaa maalum vya kunyweshea kuku vinapatikana katika maduka ya
pembejeo za kilimo.
Kilishio |
Vyombo hivi ni muhimu viwe vimetengenezwa
vizuri ili visiwe chanzo cha upoteaji wa chakula. Unapotengeneza kilishio cha
kuku kumbuka kuwa kuku wana tabia ya kuchakura. Husambaza au kupekua chakula
kwa miguu hata kwa midomo ili kupata chakula cha chini.
Tabia hii husababisha kumwagwa kwa chakula
kingi chini na kusababisha hasara. Unaweza kudhibiti tatizo hili kwa
kutengeneza vyombo visivyoruhusu kuku kuchakura kama inavyoonyeshwa kwenye
kielelezo hapa chini.
Unaweza kutengeneza kilishio hiki wewe
mwenyewe au fundi seremala waliopo katika eneo unaloishi. Inafaa kilishio kiwe
chembamba ili kuku wasiweze kuingia. Pia kinatakiwa kiwe kirefu ili kuku waweze
kula bila kusongamana.
Muunganiko wa Viota
|
Zipo aina tofauti za viota ambazo hutumika kwa
ajili ya kutagia. Ipo aina ya ambayo ni ya kutagia kuku mmoja mmoja. Vipimo
vinavyopendekezwa kwa kila kiota ni upana wa sentimita 30, urefu sentimita 30
na kina sentimita 35. Upande wa mbele uachwe wazi ila sentimita 10 za kwanza
kutoka chini zizibwe na ubao ( angalia kielelezo). Weka idadi ya viota
inayotosheleza kuku ulio nao.
Pia ipo aina nyingine inayoweza kutumiwa na
kuku zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Ni kama kiota kimoja kilichogawanywa
katika vyumba kadhaa. Ila kila chumba kina vipimo kama vya kiota kimoja(
angalia picha hapa chini).Aina hii ya kiota ina upana wa sentimita 30 na kina
sentimeta 35 na urefu wake unategemea idadi ya viota.
Viota vinatakiwa kuwa na giza ili kuku
wasiogope kuingia kutaga ndani yake. Pia giza husaidia kupunguza tabia ya kuku
kula mayai na kudonoana. Kiota kinafaa kuwekwa mahali ambako ni rahisi kuku
kuingia na kutoka. Vile vile iwe ni sehemu itakayorahisisha usafishaji wa kiota
chenyewe.
Tuesday, January 13, 2015
Friday, January 9, 2015
Hii ni sehemu tu ya kilimo cha mboga mboga, na muda sio mrefu tutaingia kwenye ufugaji wa kuku kuanzia kwenye yai hadi kuku kamili.
1, Matayarisho ya Banda
2, Usafi wa mazingira, kuondoa wadudu waharibifu
3, Maji na vyakula.
Hili ni zoezi endelevu la kufundisha wahitaji mambo muhimu kuhusu kuku.
1, Matayarisho ya Banda
2, Usafi wa mazingira, kuondoa wadudu waharibifu
3, Maji na vyakula.
Hili ni zoezi endelevu la kufundisha wahitaji mambo muhimu kuhusu kuku.
- MAENDELEO YA KILIMO DUNIANI: Utunzaji mzuri wa aridhi hasa swala la kumomonyoka kwa eneo.Hii inna maana kwamba
- jinsi ya utunzji ardhi kwa maaendeleo.
Monday, January 5, 2015
HERI YA MWAKA MPYA WANA MTANDAO.
Napenda kuchukua fusahi kumshukuru Mungu kwa neema zake na kutufikisha leo hii, hii ni neema ya kipekee sana kwa kila mwanadamu. 2015 ni mwaka wa kuchapa kazi sana kulioko ule ulio pita.
Mungu atusaaidie sana na watakia kila la kheri wana mtandao.

Subscribe to:
Posts (Atom)