Friday, February 6, 2015

KILIMO BORA CHA NYANYA- MAGONJWA NA WADUDU




Nyanya ni zao la chakula na biashara. Kilimo cha zao hili hufanyika majira yote
(masika na kiangazi), na faida hupatikana haraka na ni ya kuridhisha ikilinganishwa
na mazao mengine. Pamoja na umuhimu wa zao hili, wadudu waharibifu na
magonjwa huathiri uzalishaji na ubora wa matunda. Ili mkulima aweze kupata faida
na kuongeza pato la kaya yake ni vema kuzingatia udhibiti wa magonjwa na wadudu
wa zao hili. Kipeperushi hiki kinatoa maelezo ya udhibiti wa magonjwa na wadudu
muhimu ya zao la Nyanya.

MAGONJWA YA NYANYA
Bakajani chelewa (Late blight)
Ugonjwa huu huenenzwa na vimelea vya fangasi. Husababishwa na hali ya hewa hasa
ya unyevunyevu, na huenezwa na upepo. Majani, shina, matunda hushambuliwa.
Majani huwa na ukungu mweupe na kijivu, na baadaye hukauka. Matunda huwa na
mabaka ya kikahawia na baadaye kuoza. Mashina pia huwa na mabaka ya kikahawia.


Wednesday, February 4, 2015

KILIMO BORA CHA UFUTA

    KILIMO BORA CHA UFUTA

Ufuta (sesamum indicum)ni zao linalolimwa kwa wingi katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani, Morogoro, Dodoma, Tanga na ukanda wa chini katika mikoa ya Rukwa na Mbeya. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. Mbegu za zao hili huwa na wastani wa mafuta kiasi cha asilimia 45.
  MAMBO YA KUZINGATIA WA KATI WA KUZALISHA MBEGU •
 Chagua aina ya mbegu inayotoa mazao mengi na bora, inayovumilia mashambulizi ya magonjwa na wadudu, inayokomaa mapema na kutoa mafuta mengi.
 • Chagua mbegu inayokomaa kwa pamoja ili kurahisisha uvunaji na pia kuepuka upotevu wa zao shambani. • Aina nyeupe ya mbegu ya ufuta hupendelewa zaidi kuliko aina nyeusi.


Tuesday, February 3, 2015

Magimbi, mkombozi wakati wa njaa

Hello Mkulima Mbunifu, naomba maelezo jinsi ya kuzalisha zao la magimbi hali ya hewa, ardhi, mvua au umwagiliaji na mda gani tangu kupanda hadi kuvuna. Asante – David Kilangi. yamMagimbi ni chakula muhimu chenye kiwango kikubwa cha wanga kinachohitajika katika mwili wa binadamu na moja kati ya mazao makuu ya chakula kama vile viazi mviringo, mihogo na viazi vitamu. Zao hili hulimwa katika sehemu mbalimbali duniani kama barani Afrika, Caribbean, Asia, America na Pacific. Kwa nchi za Afrika, zao hili hutumika zaidi kunapokuwa na uhaba wa chakula, kwani lenyewe hupatikana msimu wote wa mwaka na katika majira yote.
 Matumizi Magimbi hutumika kama chakula kikuu na huweza kupikwa kwa kuchanganya na ndizi, nyama, viazi, kupika kwa kukaanga, kuchemsha, kuchoma au kwa namna yoyote ila ambayo mlaji ataamua kutengeneza mlo wake.
  Pia hutumika kutengenezea unga wa ugali kwa kukatakata na kukausha kisha kuchanyanga na mahindi pamoja na mtama. Kulingana na kukua na kuongezeka kwa njia nyingi za ujasiriamali, zao hili kwa sasa hutumika kwa kutengenezea kaukau (crisps) kama ilivyo kwa viazi mviringo, viazi vitamu, ndizi na mihogo.

Papai, zao linalozalishwa kwa urahisi

Papai ni tunda lenye ladha nzuri, na rahisi kuliwa. Aina hii ya tunda ni chanzo cha virutubisho muhimu mwilini, ambavyo husaidia kujenga mwili. Zao hili asili yake ni ukanda wa kitropiki ambao hauna baridi kali na joto kiasi. 

Udongo pawpaw 2Mipapai hustawi vizuri kwenye udongo usiotuhamisha maji. Endapo maji yakituama kwenye eneo lililopandwa mipapai kwa muda wa siku mbili, mpapai unaweza kuoza kwa haraka na kufa. Kwa kuwa mipapai haina mzizi mkuu, inahitaji udongo wenye rutuba ya kutosha. Halikadhalika, zao hili halihitaji udongo wenye kina kirefu, hivyo ni muhimu kumwagilia mipapai wakati wa kiangazi. Wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hali hiyo huongeza ubora wa papai ikiwamo kutooza mapema baada ya kuvunwa. 

Kupanda Mipapai ipandwe sehemu ambazo hazina upepo mkali. Hii itasaidia mipapai kukua vizuri bila kuvunjika kwani mti wa mpapai huvunjika kirahisi. Inashauriwa kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka shamba la mipapai. Ili kuwa na tija zaidi, unaweza kupanda aina nyingine ya miti ya matunda kama vile miparachichi, na miembe. Hakikisha miti ya kukinga upepo inakuwa mirefu kuzidi mipapai. Miti hiyo inaweza kutangulia kupandwa miezi kadhaa kabla ya kupanda mipapai.

Sunday, February 1, 2015

ZANA ZA KISASA KUWAINUA WAKULIMA

Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika chini ya Idara ya Zana za Kilimo imeandaa mkakati wa kuboresha sekta ya kilimo ili wakulima waondokane na jembe la mkono na kutumia zana za kisasa ikiwa ni moja ya sababu zinazoweza kuleta tija kwenye sekta ya kilimo nchini.
Zana ambazo zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa na kutumia mafuta ya dizeli zinaweza kutumika katika mazingira mbalimbali ya kilimo nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya zana za kilimo ya Savoy Farm Ltd Bw. Omari  Issa akizungumza katika maonesho ya Nane Nane , viwanja vya Nzuguni alisema mashine aina ya ‘palleting’ zimetengenezwa kwa ajili ya kuwakomboa wajasiriamali wadogo wanaojishughulisha na kilimo ili wazitumie katika shughuli zao.



Tuesday, January 27, 2015

Kuanzisha mradi wa mbuzi wa maziwa

Kuanzisha mradi wa mbuzi wa maziwa

Watu wengi hutemea mifugo kwa riziki.Ufugaji wa wanyama humpa mkulima nyama na maziwa kwa matumizi ya nyumbani na mapato kutokana na mauzo ya ziada. Mifugo pia ni chanzo cha samadi. Bidhaa zingine za wanyama zinazoweza kuuzwa ili kupata pesa zinajumulisha ngozi,samadi ya kuongeza rutuba kwenye ardhi ya kupanda mimea na pia kutoa kawi ya biogas, pembe, kwato na midomo ya ndege. Kuna aina mingi ya wanyama ambao mkulima anaweza kuwafuga kuanzia kwa ng’ombe, mbuzi, kondoo, ngamia na vile vile ndege wa nyumbani kama kuku, bata bukini, bata na mbuni.

Mbuzi wa Maziwa (Dairy Goats)

ufugaji wa mbuzi wa kisasa wa maziwa moja ya faida ya ufugaji wa mbuzi wa maziwa
NDIZI AINA YA FIA 16

UFUGAJI WA NYUKI


Chumba cha nyuki 1

Ufugaji wa nyuki ni kazi ambayo imekuwepo na kudumu kwa karne nyingi sana. Shughuli ya ufugaji wa nyuki nchini Tanzania hasa katika mkoa wa Tabora ambao ni maarufu kwa uzalishaji wa asali, ilianza kutambulika rasmi tangu mwaka 1884, wakoloni kama vile Rebman na Craft walipofika katika eneo hilo.
Katika kipindi hicho, jamii ya eneo hilo walikuwa wanafuga nyuki kwenye magome ya miti, vibuyu, vyungu, mapango, vichuguu na kwenye miamba. Baada ya muda ufugaji ulipiga hatua kidogo na watu wengi wakawa wanafuga kwa kutumia mizinga iliyochongwa kutoka kwenye magogo ya miti. Ufugaji wa aina hii umedumu kwa karne nyingi kote nchini Tanzania.
Kutokana na uhitaji na ongezeko la matumizi ya bidhaa za nyuki, kulifanyika tafiti mbalimbali ambazo ziliweza kuboresha ufugaji wa nyuki kwa kuwa na mizinga ya kisasa ambayo imewezesha uzalishaji wa asali kuwa mkubwa na kuongeza pato la wafugaji tofauti na ilivyokuwa hapo awali. Tafiti hazikuishia kwenye kuboresha mizinga tu, ila siku hadi siku kunavumbuliwa namna bora zaidi za kuimarisha uzalishaji wa nyuki. Katika makala hii, tutazungumzia namna ambavyo unaweza kuwajengea nyuki nyumba ili kuboresha mazingira yao ya uzalishaji, na hatimae kupata ufanisi zaidi.
Nyumba ya nyuki
Hii ni aina mpya ya ufugaji wa nyuki ambapo unaweza kujenga kibanda au nyumba kisha kuweka mizinga idadi unayohitaji.
Ni kwa nini kujenga nyumba au kibanda?

• Ni muhimu kufuga nyuki kwenye kibanda au kwenye nyumba kwa sababu inasaidia kudhibiti wizi wa mizinga, pamoja na wanyama wanaokula asali na kudhuru nyuki.
 • Inarahisisha utunzaji wa mizinga na kuwafanya nyuki wasihame kwenda sehemu nyingine.
• Inasaidia watu wengi kujifunza namna nzuri ya ufugaji wa nyuki, ikiwa ni pamoja na watoto, jambo ambalo linafanya shughuli hii kuwa endelevu.
• Ufugaji wa aina hii unasaidia kuwak inga nyuki dhidi ya majanga kama vile moto, na mafuriko.
• Inawaepusha nyuki na usumbufu unaoweza kuwafanya wasizalishe kwa kiwango kinachotakiwa.
• Uzalishaji unaongezeka. Hii ni kwa sababu mizinga inayotumika ni ile ya kibiashara. Mzinga 1 unapata asali kilo 30 sawa na lita 20.

Chumba cha nyukiAina ya nyumbaUnaweza kujenga nyumba yenye upana wa futi 3 na urefu wa futi 9. Nyumba hii inaweza kuchukua mizinga hamsini. Halikadhalika, unaweza kujenga kibanda chenye ukubwa sawa na huo.
Eneo linalofaa
• Ili kuwa na ufanisi mzuri, nyumba hii inafaa kujengwa nje kidogo ya makazi ya watu.
• Kusiwe na mifugo karibu.
•Iwe sehemu ambayo watoto hawawezi kufika.
• Isiwe karibu na njia ambayo watu wanapita mara kwa mara.
• Kusiwe na aina ya mimea ambayo nyuki hawapendi.
• Kuwe na maji karibu.
Mavuno

Baada ya kujenga nyumba, kuweka mizinga na nyuki kuingia, unaweza kuvuna kwa mara ya kwanza baada ya miezi mitatu. Utaweza kupata mavuno mazuri endapo utavuna kabla nyuki na wadudu wengine hawajaanza kula asali.
Ni muhimu kuhakikisha kuwa wadudu waharibifu kama vile sisimizi, mende na wengineo wanadhibitiwa ili kutokuathiri uzalishaji wa asali. Hakikisha unavuna kitaalamu ili kuepuka upotevu wa asali. Endapo nyuki wametunzwa vizuri na kwenye mazingira mazuri, unaweza kuvuna asali mara tatu kwa mwaka. Katika mzinga mpya nyuki wana uwezo wa kutengeneza masega kwa siku tatu na kuanza uzalishaji wa asali.
Ni nini umuhimu wa asali
• Asali inatumika kama chakula
• Inatumika kama tiba ya magonjwa mbalimbali
• Hutumika kutibu majeraha
• Ni chanzo kizuri cha kipato
• Hutumika katika kutengeneza dawa za binadamu
*Asali inaweza kuhifadhiwa kwa miaka mingi sana bila kuharibika. Hii inatokana na wingi wa dawa maalum iliyo nayo inayofanya isiharibike.

Bidhaa zinazotokana na asali

Chumba cha nyuki 2Kuna aina nyingi ya bidhaa zinatokana na asali, kwa kutengenezwa na nyuki wenyewe na nyingine zikitengenezwa na binadamu kutokana na tafiti mbalimbali. Miongoni mwa bidhaa hizo ni:
• Asali yenyewe
• Royal jelly : Hii ni aina ya maziwa yanayotengenezwa na nyuki, ambayo hutumika kama tiba.
• Gundi: Hii hutumika kutengeneza bidhaa za aina mbalimbali kulingana na mahitaji ya mtumiaji.
• Nta: hutumika kutengenezea mishu maa, kulainisha nyuzi, kutengeneza dawa ya viatu, mafuta ya kupaka, pamoja na dawa ya ngozi.
Kwa maelezo zaidi juu ya ufugji wa kisasa wa nyuki wasiliana na Kinanda Kachelema kutoka SEED Tabora kwa simu +255 783 212 263

AINA YA NYUKI WAKUFUGWA

Monday, January 26, 2015

Kilimo Biashara katika shughuli ya ufugaji nyuki na uvu...

kijana ambaye amejitita katika kilimo biashara amejitika katika ufugaji wa nyuki
Hao ni baazi ya kuku chotara kuku hao chotara ni wazuri sana kwa nyama na wanasoko zuri sana ni kuku ambao wanampa mfugaji faida nzuri sana.Chotara hao wana miezi Tisa mfugaji wetu anaweza kuwauza kwa sh 15000/=kwa jogoo moja au sh 20000/= kwa mtetea mfugaji anaweza akauza kwa sh 20000/= hiyo ndio faida ya mfugaji wa kuku wa aina ya chitara hii ni moja ya utajili wa mfugaji
Hili ni moja ya banda bora lililojengwa kwa ubora zaidi banda hili lina vyumba vitatu chumba cha kwanza wana kaa kuku wa kawaida ambao hawatagi chumba cha mwisho wanakaa kuku wanao lalia mayai na wametenganisha sehemu ya kukuzia vifaranga

Wednesday, January 21, 2015

JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI

Tengeneza chakula cha samaki mwenyewe

PAGE 7Mfugaji anaweza kupunguza gaharama za kununua chakula kwa ajili ya samaki, kwa kutengeneza chakula mwenyewe kwa kutumia malighafi ulizo nazo katika eneo lako. Tumia resheni rahisi ambayo itakupatia chakula cha kutosha na kwa gharama nafuu.


Mahitaji


• Pumba ya mahindi sadolini 1.
• Pumba ya ngano au mpunga sadolini 1.
• Dagaa sadolini 1.
• Kilo moja ya soya.
• Robo kilo ya mashudu ya pamba au alizeti.

Namna ya kuandaa


• Changanya malighafi hizo kwa pamoja.
• Saga hadi zilainike.
• Kanda kama vile unga wa kutengenezea chapati.
• Weka kwenye mashine ya kusaga nyama au kutengenezea tambi.
• Anika kwenye jua la wastani.
• Baada ya kukauka, vunja vunja kwenye vipande vidogo vidogo hasa kwa kuzingatia umri wa samaki unaokusudia kuwalisha.
• Tumia lishe hiyo kwa samaki mara tatu kwa siku.

SAMAKI AINA YA SATO



Samaki aina ya Sato ni wazuri katika kufuga na nimoja ya samaki mwenye soko

MABWAWA YA SAMAKI

 Moja ya bwawa la samaki la kisasa

Bwawa la samaki lililo jegwa vizuri sana