Wednesday, February 19, 2014

KUPE WEKUNDU KWENYE MASIKIO YA NG'OMBE


Ugonjwa huu hushambulia wanyama kama ng'ombe, mbuzi na kondoo na husababishwa na vimelea vijulikanavyo kama Theileria parva ambavyo vusambazwa na kupe wekundu wa kwenye masikio wajulikanavyo kama Rhepicephalus Appendiculatus, ugonjwa huu usipodhibitiwa unaweza kusababisha vifo vya wanyama wengi sana na pia ni aghali kuutibu kulinganisha na magonjwa mengine




DALILI ZA UGONJWA HUU
Homa kali, mnyama kushindwa kupumua vizuri,  kukohoa pamoja na kutoa makamasi, kuharisha na kuvimba matezi

MATIBABU
Mnyama inabidi apigwe sindano ya dawa za  PARVAQUONE au BUTALEX kiasi cha ml 20 (soma kimbatanisho cha dawa kwa maelezo zaidi) na kurudia baada  ya siku moja kupita, yaani ukuchoma leo unarudia dozi kesho kutwa, pia mnyama achomwe dawa ya OTC20% kipindi chote cha matibabu





KINGA
Kinga kubwa ya ugonjwa huu ni kuhakikisha kwamba mifugo yako inaoga mara kwa mara kwenye majosho au kwa kuwanyunyuzia dawa za kuua wadudu wa mifugo


NG'OMBE WAKIOGESHWA KWENYE DAWA 
 
 


KILIMO CHA KUTUMIA MAHEMA CHAINUA UZALISHAJI WA KILIMO NCHINI KENYA



 




Wakikabiliwa na eneo dogo la kulima kutokana na kukua kwa idadi ya watu na hali za hewa zisizotabirika, wakulima wengi wa Kenya wamegeukia teknolojia ya kilimo cha mahema kama njia ya kuongeza uzalishaji na kunyanyua kipato chao.
Kukua kwa umaarufu wa kilimo wa mahema kulioneshwa katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya kila mwaka mjini Nairobi mwezi wa Oktoba ambapo waoneshaji wa kilimo cha kutumia mahema walisema kuwa waliona kuinuka kwa hamu ya umma katika kilimo hicho.
"Wakenya wengi wameanza kufuata kilimo cha kutumia mahema kwa sababu kinahitaji mtaji mdogo ili kuanzisha na wakulima wanaweza kuzalisha zaidi katika shamba dogo," alisema Moses Khaemba wa Kampuni ya Hortipro Limited, iliyoko Nairobi ambayo inatengeneza mahema ya kilimo kwa gharama ndogo.
Pamoja na kuwa inakuwa ya gharama ndogo na rahisi kuyaweka, mahema ya kilimo pia gharama ndogo ya ushughulikiaji, yantumia maji kwa ufanisi na yanaweza kuhamishwa baina ya vitalu, alisema, na kuongeza kuwa wakulima wanaweza kuona faida yake kuanzia mavuno ya kwanza
"Kilimo cha kutumia mahema ya plastiki kina faida nyingi," Khaemba aliiambia Sabahi. "Faida hizi ni pamoja na uzalishaji wa juu zaidi na wa kuendelea kwa kila ekari moja, jambo lenye maana ya kupata faida kubwa zaidi, kujikinga na masuala ya hali ya hewa kama vile ukungu na upepo, kutokuwepo na hatari ya wadudu waharibifu, kupata mwanga asilia na upitishaji wa hewa, miongo mirefu ya upandaji na matumizi madogo ya maji, hasa katika maeneo yenye ukame."
Ukubwa wa mahema ya kilimo unategemea na uwezo wa mkulima wa kuyashughulikia na ukubwa wa shamba, alisema. Wastani wa kila hema moja ni upana wa mita 8 na urefu wa mita 30 na hugharimu shilingi 150,000 (dola 1,800). Kampuni imepokea zaidi ya maombi 1,000 ya mahitaji kutoka kwa wakulima mwaka huu -- ongezeko la asilimia 25 ikilinganishwa na 2011 -- vivyo hivyo na ongezeko la mahema mengi katika shamba hilo hilo, Khaemba alisema.
Mahema ya kulimia yanaweza kuwa ama katika muundo wa jadi kama nyumba au muundo wa upenyo - marefu yakiwa yamefunikwa kwa plastiki juu ya mazao. Wakulima wasema kwa kutumia mahema yenye umbo la upenyo, wanaweza kuzalisha zaidi kuliko katika ardhi ya wazi.
"Mimi ninayo mahema mawili katika shamba langu la ekari tatu huko Karen Estate mjini Nairobi ambako nimepanda nyanya," Margaret Wanjiku, mweny umri wa miaka 54, aliiambia Sabahi.
Wanjiku, ambaye alistaafu miaka mitano iliyopita kutoka shirika moja la kimataifa la msaada, alisema kuwa mmea wa nyanya unaweza kuzalisha kilo 16 hadi 20 za nyanya.
Ingawa bei hubadilikabadilika kutokana na upatikanaji wa bidhaa na mahitaji, alisema kuwa kila mita mraba moja ya nyanya humuingizia kiasi cha shilingi 3,000 (dola 35). "Ninauza nyanya zangu kwenye duka kubwa iliopo karibu na nyingine kwa majirani zangu," alisema.
Amos Karanja ametenga sehemu ya shamba lake la robo ekari huko Kitengela, Jimbo la Kajiado, kwa ajili ya kulima nyanya ndani ya mahema. "Ingawa ninayo kazi ya mchana, ninajaribu aina hii ya kilimo kama njia ya kupata mapato ya ziada ili kuisadia familia yangu," aliiambia Sabahi.
Dan Wanjohi kutoka kampuni Daner Greenhouse Limited huko Ongata Rongai, eneo la makazi ya watu katika Mkoa wa Bonde la Ufa, alisema kuwa kimwonekano aina yoyote ya mboga inaweza kulimwa katika mahema ya kilimo, ikiwa ni pamoja na matango, vitunguu na kabichi.
"Wakulima wengi nchini Kenya wanapendelea kulima nyanya kwa sababu ni mmea unaotoa mazao mengi na mtu hupata faida ndani ya miezi mitatu baada ya kuotesha," aliiambia Sabahi.
Alisema kuwa kampuni yake inatumia chuma cha pua katika ujenzi wa hema la ukubwa wa mita 8 kwa 30 na huuzwa kwa shilingi 200,000 (dola 2,300) kwa moja. Gharama ni pamoja na kulaza bomba kwa ajili ya umwagiliaji maji kwa matone.
Hata hivyo, wakulima ambao hawawezi kumudu gharama za majengo ya chuma cha pua, bado wanaweza kutumia mahema ya vipenyo kwa kutumia mbao kwa gharama ya chini zaidi. "Nililipa shilingi 70,000 (dola 818) kwa kujenga hema langu," Karanja aliiambia Sabahi.

Tuesday, February 18, 2014

MZEE MWINYI AZINDUA MPANGO ENDELEVU KWA WAKULIMA


Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, akizindua  mpango maalumu  na  endelevu wa kumuwezesha mkulima yeyote hapa nchi  kupata trekta  kwa bei nafuu kupitia ushirikiano wa benki ya KCB Tanzania,anaeshuhudia kulia ni Diwani wa Kwadelo wilaya ya kondoa mkoani Dodoma,Bw.Omary Kariati aliefanyikisha mradi huo na kununua trekta(15)kwaajili ya wakulima nchini.Hafla hiyo ilifanyika Mikocheni jijini Dar es Salaam jana.
 
 
 


Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, akiwasha Trekta ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa  mpango maalumu  na  endelevu wa kumuwezesha mkulima yeyote hapa nchi  kupata trekta  kwa bei nafuu kupitia ushirikiano wa benki ya KCB Tanzania, Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam.Anaeshuhudia kulia ni Diwani wa Kwadelo wilaya ya kondoa mkoani Dodoma,Bw.Omary Kariati aliefanyikisha mradi huo na kununua trekta(15)kwaajili ya wakulima  nchini.




Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, akiangalia moja ya  Trekta  kati ya(15) kabla  ya kuzindua mradi endelevu wa kumuwezesha mkulima yeyote hapa nchi  kupata trekta  kwa bei nafuu kwa ushirikiano na benki ya KCB Tanzania na Diwani wa kata ya Kwadelo Bw.Omary Kariati.Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam.
 
 


Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa  mpango maalumu  na  endelevu wa kumuwezesha mkulima yeyote hapa nchi  kupata trekta  kwa bei nafuu kupitia ushirikiano wa benki ya KCB Tanzania na Diwani wa kata ya kwadelo wilaya ya kondoa mkoani Dodoma, Bw.Omary Kariati wapili kushoto. Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya wakuliama wa kata ya Kwadelo wilaya ya kondoa mkoani Dodoma wakimsikiliza Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi,(hayupo pichani)akiongea wakati wa makabidhiano rasmi wa Trekta(15)kuzindua mradi endelevu wa kumuwezesha mkulima yeyote hapa nchi  kupata trekta  kwa bei nafuu kwa ushirikiano na benki ya KCB Tanzania na Diwani wa kata ya Kwadelo Bw.Omary Kariati.
 
 
 
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, akisalimiana na Mkurugenzi wa ushirikiano wa kibenki wa benki ya KCB Tanzania,Bw.Frank Nyabundege(kushoto)wakati wa hafla ya uzinduzi wa  mpango maalumu  na  endelevu wa kumuwezesha mkulima yeyote hapa nchi  kupata trekta  kwa bei nafuu kupitia ushirikiano wa benki ya KCB Tanzania na Diwani wa kata ya kwadelo wilaya ya kondoa mkoani Dodoma, Bw.Omary Kariati(kulia). Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam.

WIZARA KUNUNUA MAZAO YA NAFAKA NCHINI






Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika imetangaza nia yake ya kutaka kununua mazao ya nafaka ili kumwekea mkulima wa hali ya chini soko la uhakika.
Miongoni mwa mazao yatakayonunuliwa kupitia Bodi  ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko  ni mpunga,maharagwe,karanga,choroko,ulezi,ufuta na mahindi,na yatanunuliwa kwa bei ya ushindani ya soko mwaka huu.
Hayo ni kwa mujibu wa Mchumi wa bodi hiyo Bw. Edwin Mkwenda  katika maonesho ya wakulima yaliyofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni Manispaa ya  Dodoma.
Bw. Mkwenda alisema tayari Serikali imeikabidhi bodi hiyo maghala yote yaliyokuwa ya Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC),ambayo hayakubinafsishwa zilizoko  kwenye kanda saba  ili kutunza mazao yatakayonunuliwa.
Kuundwa kwa bodi hiyo ni ukombozi kwa wakulima kwani watakuwa na uhakika wa kupata soko la mazao husika.



UMWAGILIAJI WA MATONE KUONGEZA UZALISHAJI



Serikali imepanga kuendeleza teknolojia ya Umwagiliaji wa Matone ili kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mazao kwa wakulima.
Akizungumza katika kilele cha maonesho ya sikukuu ya wakulima ya Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma, Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddy alisema kuwa umwagiliaji kwa njia ya matone utasaidia katika kukuza  uzalishaji wa mazao ya nafaka na bustani.
“Kutokana na teknolojia hii mpya ya umwagiliaji wa matone serikali imeweza kuvuna tani 16,510 za mazao kwa mwaka’’, alisema Balozi Seif.
Aliendelea kueleza kuwa teknolojia ya umwagiliaji ni lazima ipewe kipaumbele na kutekelezwa nchi nzima ili wakulima waweze kuzalisha mazao kwa wingi na kuuza ndani na nje ya nchi.
Aidha Balozi Seif aliwataka waandaaji na waendeshaji wa maonesho ya Nane Nane (TASO)  waweke utaratibu mzuri wa maonesho hayo ili wakulima waweze kuhamasika na kuhudhuria kwa wingi ili wapate mafunzo ya kilimo na ufugaji

WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA AMESEMA HAPENDI KUONA TASNIA YA SUKARI IKIKOSA MWELEKEO





"Mhe. Eng. Christopher Kajoro Chiza Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika akitoa hotuba kwa Wadau wa Sukari katika Mkutano uliofanyika Mjini Morogoro Mwanzoni mwa Januari 2014.

Mhe. Eng. Christopher Kajoro Chiza (Mb) Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika ameonya kuwa kuwa Serikali haitapenda kuona Tasinia ya Sukari ikikosa mweleleo kutokana na matakwa ya kundi fulani. Alisisitiza kuwa, Tasnia ya sukari ni moja ya tasnia kubwa nchini ikijumuisha wadau muhimu wakiwamo walaji, wakulima, wafanyabiashara na wazalishaji. Kila mdau katika jumuisho hili ana maslahi ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kukinzana na ya mdau mwenzake. Mkulima angependa kuona anauza miwa yake kwa bei ya juu, hali kadhalika mzalishaji kuuza sukari anayozalisha kwa bei yenye faida ya kutosha. Aidha mfanyabiashara angependa kupata faida maradufu na panapokuwa na mwanya kuingiza sukari kutoka nje kwa njia sizizo halali. Lakini kwa upande mwingine mlaji naye angependa kununua sukari kwa bei nafuu.
Serikali haipo tayari kuona tasnia kubwa na muhimu kama hii ya sukari ikipoteza mwelekeo, aidha ingependa kuwepo kwa mazingira mazuri (win - win situation) kwa kila mdau. Kwa maana hiyo nimeona ni jambo jema na muhimu sana kuwakutanisha ninyi wadau ili tuweze kujadili kwa pamoja changamoto zilizopo mbele yetu juu ya sekta hii. Ni matarajio yangu kwamba, mkutano huu utaweka misingi ya kufikia utatuzi wa chamngamoto hizi kwa manufaa ya pande zote
Mhe. Waziri ameyasema hayo katika mkutano wa Wadau wa Sukari uliofanyika Mjini Morogoro mwanzoni wa mwezi Januari
Akitoa picha halisi ya uzalishaji na mahitaji ya sukari hapa nchini Waziri Chiza alisema kuwa, Wakati viwanda vyetu vinabinafsishwa vilikuwa vinazalisha wastani wa tani 120,000 kwa mwaka. Sasa uzalishaji umefikia wastani wa tani 300,000 kwa mwaka.
Aidha uzalishaji wa miwa (siyo sukari) katika mashamba ya wakulima wadogo nao umeongezeka kwa asilimia 61 (hii ni kutoka wastani wa uzalishaji wa tani 439,122 hadi tani 705,176 kwa mwaka). Uzalishaji katika mashamba ya wenye viwanda umeongezeka kutoka wastani wa tani 1,083,738 na kufikia tani 2,229,274 kwa mwaka (ongezeko la asilimia 105).
Pamoja na mafanikio haya bado tasnia ya sukari imegubikwa na changamoto mbali mbali kubwa zaidi ikiwa uzalishaji usiokidhi mahitaji. Mahitaji yetu ni wastani wa tani 590,000 za sukari kwa matumizi ya kawaida na ya viwandani. Viwanda vya sukari nchini huzalisha takribani asilimia sabini tano (75%) ya mahitaji ya sukari ya matumizi ya kawaida. Wastani wa tani 290,000 ni nakisi inayojazwa na uagizaji sukari kutoka nje. Nakisi hii inajumuisha sukari ya matumizi ya kawaida (gap sugar) ya wastani wa tani 120,000 na sukari ya matumizi ya viwandani ya wastani wa tani 170,000 kwa mwaka. Kiasi chote cha sukari ya matumizi ya viwandani kinaingizwa nchini kutoka nje. Aidha uagizaji wa sukari ya matumizi ya kawaida unategemea hali halisi ya soko kwa kipindi husika na kwa hiyo uagizaji halisi unaweza kuwa juu au chini ya nakisi hiyo. Hata hivyo, Kamati ya Ufundi ya Ushauri ya Uagizaji Sukari iliyokutana tarehe 24/12/2013 kujadili hali ya sukari nchini imependekeza kuwa mwaka huu 2013/2014 kusiwe na uagizaji wa sukari kwa sababu kiasi tha tani 257,000 kitapatikana kwa matumizi ya kawaida kuanzia sasa hadi mwishoni mwa 2013/2014.

UKULIMA WA VITUNGUU





 ndugu zangu ambao mnabweteka na kutafuta kazi kuna kilimo cha vitunguu, two years unakuwa mtu mwingine kabisa na huta penda kuajiriwa na kama utakuwa kwenye ajira unaweza acha kabisa na kuamua kuwa mkulima. Tusiwaze kuajiriwa tu tutakufa maskin mwisho wa siku. Mimi nimejaribu na sasa nataka niache kazi na kuwa moja ya wakulima na wafanyabiashara wakubwa wa vitunguu na mazao yote ya shamba kwa ujumla ila pamoja na hilo bado nahitaji muongozo mkubwa kwa watu waliobobea kwenye ukulima pamoja na biashara ya mazao ya shambani ili waweze kunishauri zaidi. Mimi napatikana moshi pamoja na arusha ndiko napofanyia biashara zangu. Please kwa yoyote ambaye amebobea kwenye biashara hii zaidi naomba ani PM ili tuweze kupeana contact ili mkukuza network na bidae kuweza kuanzisha kitu flani kwa manufaa yetu asanteni sana na wakilisha.

MABADILIKO YA HALI YA KIBIASHARA TANZANIA



MABADILIKO YA HALI YA KIBIASHARA TANZANIA







Kama ukiangalia vizuri nchi yetu ya Tanzania inatengeneza mabadiliko fulani ya kibiashara na kiuchumi na mabadiliko haya yatakuwa na athari na faida zake.

1. Kwa sasa serikali imeamua kutengeneza vitambulisho vya utaifa hii ni ili kupata taarifa muhimu za kila mtanzania kuanzia
alikozaliwa hadi aliposasahivi.
2. Wanapitisha dodoso kwa kila nyumba na eneo ili kutambua ni nyumba ngapi zinatumika kama nyumba na sehemu ya
biashara na ngapi zinatumika kama nyumba peke yake au sehemu ya biashara peke yake ( hapa ni lazima uandike na jina
la biashara na biashara unayoifanya katika ofisi yako.
3.Tra kusisitiza matumizi ya EFD
4. TBS kusisistiza matumizi ya nembo zao katika bidhaa.

ukiangalia hivyo ni baadhi tu ya mabadiliko tuliyonayo kwa hivi sasa kitu kikubwa kinachoatafutwa hapo ni kodi na ubora wa biashara,asilimia kubwa ya wanaofanya biashara na wajasiriamali wamekuwa inspired na wajasiriamali wakubwa kutoka nje ya nchi na wengi wametumia baadhi ya njia walizotumia na kuweza kuyaona mafanikio lakini sasa serikali imebadilika inahitaji kila kitu kiwe perfect kama ambavyo ilivyo katika nchi tunazokopi kwao.

kuna watu wengi hufanya vitu bila hata kujua vina umuhimu gani kuna wanaotengeneza Logo kwa kuwa wanajua ili biashara iitwe biashara ni lazima uwe na logo, kuna wanaoprint fliers,posters, nakadhalika bila kujua zina faida gani na zinatoa majibu baada ya muda gani na unaziweka kwa mpango wa muda gani watu hufanya tu kwa mazoea ndio maana hata ukiangalia mabango ya kampuni zetu ni tofauti na mabango ya kampuni za nje.tunafanya vitu kiholela lakini serikali imeamua kututoa huko bila kutuambia kama tunahama kwenye mazoea tunaenda kwenye uhalisia.

kiukweli uhalisia ni mgumu kwa sababu bado watu hawajui faida na hasara au sababu na maana ya kufanya hivyo, lakini Tanzania inageuka kuwa nchi ya uwekezaji siku sio nyingi makampuni mengi yanakuja na kufungua matawi nchini kwetu hivyo tunahamishwa kwa sababu maalum, na kwa kuliona hilo Legacy Impresion Company inatoa ofa kwa wale wote wamiliki wa biashara na ambao wanatarajia kufungua biashara kuja kupata semina ya utambuzi wa matumizi na umuhimua wa vifaa vya kuitambulisha biashara yako kwenye jamii. ( Logo, Fliers,Brochure,Business card, nk) semina hii inatolewa bure kwa kila mfanyabiashara atakaefanya (Branding package) kutoka Legacy amabapo package hii inajumuisha dizaini tofauti tofauti za vifaa vinavyokutambulisha kwenye jamii na mteja unaemtarajia.

Muda wa kufanya kazi kwa mazoea unahesabika badilika sasa, badilika na Legacy,tunapatika Kijitonyama,Dar es salaam,na tunashughulika na kufanya Graphic design, Printing,Webtech,stationery na Brand Consult, mawasiliano ni 0713603699 au info@legacytz.com,website ni .:LEGACY TANZANIA:.



BAADHI YA NJIA UNAZO WEZA KUTUMIA KUPATA WAZO BORA LA BIASHARA



IDEA ya Biashara ni moja ya mambo yanayo waumiza watu wengi sana, Na mara nyingi wazo la biashara linahitaji utafiti wa kina ili kuja na wazo lenye tija kwako na kwa jamii nzima,

HIZI NI MOJA YA NJIA ZA KUPATA WAZO LA BIASHARA


1. TUMIA UJUZI ULIONAO
Ujuzi ulionao ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupata wazo la Biashara, Mfano kama wewe umejiliwa na ni Fundi wa kushona Nguo, why usianze na wewe kuwa na biashara ya aina hiyo? Kama wewe ni fundi magari why usianzishe gereji yako?
Ujuzi ulianao ndo hazina ya kwanza nay a kipekee ya kupata wazo na mara nyingi wajasirimali wengi waliofanikiwa waliacha kazi wanazo fanya na kwenda kuanzisha za aina hiyo na kuzimiliki wenyewe


2. BADILISHA HOBY YAKO KUWA PESA

Hobby ni moja ya maeneo ambayo watu huja kutajilikia, kama wewe hobby yako ni kufuga mbwa kwa nini usianze hiyo biashara ya kufuga mbwa?
Kama Hobby yako ni Kuogelea, kwa nini usinzishe mabwawa ya kuogelea na wengine wakawa wankuja huko kuogelea?
Kam unapenda gardening unaweza anza biashara ya kufanya landscape gardening


3. NUNUA BIASHARA AMBAYO TIYALI IPO
Ukishindwa kabisa kupa wazo mwanana unaweza nunua biashara ya mtu mwingine na kuindeleza, siku hizu kuna biashara kibao zinauzwa kwa sababu mbalimbali so unaweza nunua nu kuendelea nayo


4. Kununua Franchise
Hii ni moja ya njiza zinazo tumika kwa sasa na sehemu nyingi sana, Unaweza nunua Popular Brand na kuifanyia kazi, Ingawa mara nyingi kuna mashariti ya kuambatana ikiwemo kuhakikisha unatoa huduma sawa na Brandi yenyewe, nah ii ni popular sana katika MAHOTELI/MIGAHAWA, MASUPERMARKET NA MADUKA MENGINE
Na usijalibu kutumia Brand ya Kampuni Fulani bila kuwapa Taarifa make inaweza kula kwako na ukajikuta unafilisiwa,
Na ilisha wahi kutokea kwa Kampuni ya Mabasi ya SABENA baada ya kutimia jina la Shirika la Ndege la Ubeligiji, Ila sijui walimalizana vipi, make jamaa bado wanalitumia


5. TUMIA PERSONALITY YAKO
Kuna watu unakuta either ni Mrembo sana, Handsome na kazalika, unaweza utumia huo urembo na uhendsaamu kufanya biashara, either za marketing na kazalika

.
6. NINI KINAKOSEKANA MTAANI?
Tazama ni kitu gani hakipo hapo mtaani and then geuza kuwa opportunity, inaweza isiwe ni mtaani ikawa ni kazini kwako, Kijijini kwenum au maeneo unayo enda kustalehe
-Ni kitu gani huwa kinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia muda mwingi na pesa nyingi?
- Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazo ni za muhimu?
-Ni bidhaa zipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?
-Ni kitu gani, wewe, Ndugu, Majirini huwa wanakilalamikia sana mtaani hapo?


7. UTALII KATIKA MAENEO YAKO
Hii nayo ni moja ya wazo, so unaweza angalia furusa za utalii kwenye maeneo uliyopo au hata kwingine na kuyafanyia kazi.


8. TUMIA TECHINOLOGIA MPYA KUANZISHA BIASHARA
Angalia mfumo wa maisha wa sasa ulivyo, vitu vinavyo tumika kwa sasa na vinavyo tumiwa na watu wengi, so mfumo wa maisha wa watu kwa sasa unaweza kukuongoza kuja na wazo la Biashara


9. ANGALIA MAKAMPUNI MAKUBWA NA TAASISI ZINGINE WANAHITAJI NINI
Unaweza tumia uwepo wa makampuni Fulani au taasisi Fulani maeneo yako kutengeneza wazo la biashara, taasisi kama Shule, vyuo, Hospitali, Makampuni kama Viwanda Migodi na kazalika, angalia ni kipi hawa watu wanaweza kuwa wanahitaji kwa wingi


10. UNAWEZA KUANGALIA KUHUSU KUUZA BIDHAA ZA WENGINE
Unaweza ukawa unauza bidhaa za watu wengine, unachukua na kuuza


11. ANAGALIA NEWS NA MAKALA MBALIMBALI
Kunachaneli huwa zina makala mazuri sana ya kiuchumi na biashara, hata TBC huwa inamakala Fulani nzuri sana, na kuna chaneli za kimataifa siku huzi kazi yao ni hiyo tu, ni kuonyesja ubunifu wa wajasirimali, so TV, radio na magazeti yanaweza toa mchango w akutosha kwa wewe kupata wazo la biashara


12. CPY BUSINESS AIDEA AMBAYO IMEFANIKIWA KWINGINEKO
Hii ni moja ya njia zinazo tumika kwa sasa, unaweza copya aidea kutoka hata India, China, na kwingineko na ukaja kuifanyia kazi huku kwa kufanya marekebisho madogo kulingana na mahitaji ya eneo husika


13. TUMIA NJIZA ZOTE ZA KIUTAFITI KUPATA WAZO LA biashara- maonyesho ya biashara
-Magazeti,
- Kwenye taasisi za uma zinazo husika na biashara
-Kwa marafiki


14. UNAWEZA GUNDUA KITU?Unaweza ukaja na ugunduzi wako kama walivyo fanya wakina Thomas Edson Michael Dell na wengineo, na ikawa ndo mwanzo wa mafanikoa kwako







Wednesday, January 29, 2014



VIDEO YA MTENDAJI MKUU WA SAGCOT AZUNGUMZIA HALI YA UZALISHAJI WA CHAKULA NCHINI


BONYEZA HAPA KUONA


Kenya yapiga jeki kilimo



 Kenya imezindua mradi mwengine tena ambao ikiwa utafanikiwa utapiga jeki na kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya kilimo nchini humo.

Mradi huo 'Galana Kulalu' katika mkoa wa pwani unanuiwa kuziweka katika mpango wa unyunyiziaji maji ekari zaidi ya millioni moja za kilimo hasa cha mahindi na miwa.
Mradi huu unakadiriwa kwamba katika kipindi cha miaka 5 ijayo utagharimu zaidi ya shilingi billioni 250 za Kenya.
Tangu kale maeneo ya bara ya Kenya ndio yamejulikana kuwa na kilimo kinacholisha nchi kutokana na hali nzuri ya hewa na kupata mvua ya kutosha , lakini mpango huu wa Galana Kalula unasemekana utaifanya Kenya kuwa na uwezo wa kujitosheleza kwa chakula na hata kuweka kukiuza nje.
Kila ekari kwa mfano itatarajiwa kuzalisha kati ya magunia 40 na hamsini kutokana na rutuba ya ardhi hiyo na kunyunyiziwa maji kwa kipimo kinachohitajika.
Eneo hilo liko katika majimbo ya Kilifi na Tana river ambayo kwa miaka mingi yamekumbwa na umaskini na yameachwa nyuma kimaendeleo licha ya kuwa na ardhi nzuri ya kilimo.
Hii ilitokana na sera mbovu, ukosefu wa usalama na hivi majuzi kukumbwa na vita kati ya wakulima na wafugaji vilivyochochewa zaidi kisiasa.
Hadi sasa bado kuna hofu miongoni mwa wenyeji kwamba licha ya kuahidi mengi mazuri , huenda wasitendewe haki. Hata hivyo wadadisi wanasema iwapo mradi huo , utatekelezwa kwa haki na uwazi ni fursa nzuri ya kutatua matatizo yanayoilemea kaunti hiyo.

Tuesday, January 28, 2014


 RAIS KIKWETE AFURAHISHWA NA HUDUMA ZA NMB KATIKA MPANGO
WA KILIMO STAKABADHI GHALANI



Rais kikwete akisalimiana na mkuu wa kitengo cha masuala ya kilimo katika benki ya NMB Bw. Robert Pascal alipo tembelea banda lao baada ya kufungua kongamano la kilimo Africa mashariki katika Hoteli ya kilimanjaro.




Rais Kikwete akipata maelekezo juu ya mpango wa stakabadhi ghalani ulivyo na manufaa kwa mkulima toka kwa mkuu wa kitengo cha masuala ya kilimo bw. Robert Pascal





Friday, June 7, 2013

Wakulima 940,800 wafaidi mbolea ya ruzuku

Katika mwaka wa fedha 2012/13, Serikali ilitoa ruzuku ya tani 126,117 za mbolea ambapo jumla ya wakulima 940,783 walinufaika na tani 8,278 za mbegu bora za mahindi huku wakipata mbegu bora za mpunga tani 1,694.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Christopher Chiza ambaye alisema kuwa mipango hiyo imetokana na kukubalika kwa baadhi ya mazao ya chakula kuruhusiwa na kuwa mazao ya biashara.

Alikuwa akijibu swali la Martha Mosesi Mlata (Viti Maalumu-CCM), ambaye alitaka kujua kama Serikali inatambua kwamba kuna baadhi ya mazao ambayo ni chakula lakini yanatumika kama mazao ya biashara hivyo kuna sababu ya kuyapa ruzuku.

Mlata alihoji pia sababu za wakulima wa Mkoa wa Singida kuzuiwa wasilime zao la mahindi licha ya kuwa zao hilo linastawi vizuri mkoani humo.

Waziri alisema Serikali ilijikita katika kutoa mbolea ya ruzuku na pembejeo ili kuboresha uzalishaji wa mazao hayo na kuhakikisha wakulima wanapata chakula cha kutosha na kuwaongezea kipato.

Alisema kuanzia mwaka 2013/14 hadi 2015/16, Wizara kupitia mfumo wa matokeo makubwa imejiwekea malengo ya kuongeza uzalishaji kwa kiasi cha mahindi tani 100,000 na mchele tani 290,000 katika mashamba mapya ya wakulima wakubwa na wadogo.

Kwa mujibu Chiza, katika miradi hiyo Serikali inatarajia kutumia Sh 91.5 bilioni kugharimia ruzuku ya pembejeo za mazao zikiwamo mbolea.

Thursday, June 6, 2013

Teknolojia kuandaa miche ; Mbinu mpya ya kuongeza uzalishaji wa korosho

Wakulima wakitumia teknolojia ya kisasa kubebesha mikorosho katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele mkoani Mtwara hivi karibuni.

Wednesday, June 5, 2013

Wafugaji, wawindaji nchini waridhishwa Rasimu Katiba

Arusha
Mtandao wa Jamii za pembezoni za Wafugaji, Wawindaji wa Asili na Waokota Matunda, umeeleza kuridhishwa na rasimu ya Katiba Mpya iliyotambua uwapo wao na kulindwa rasilimali na tamaduni wao.
Mratibu wa Taasisi ya Katiba-Initiative iliyoundwa na mashirika yanayotetea jamii hizo, William Ole Nasha alisema mapendekezo yao mengi yamechukuliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
“Kimsingi tumeridhishwa na rasimu hii, maombi yetu mengi yameingizwa na sasa haki za jamii hizi, ambazo ni ndogondogo zitalindwa,” alisema Ole Nasha.
Pia, alisema haki za wafugaji ambao wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mengi zimeingizwa na kwamba, sehemu nyingi ya rasimu itakuwa ikijulikana kuwa Tanzania kuna wakulima, wafugaji na wavuvi.
“Siyo kutambuliwa tu bali mifugo imetambuliwa kama zao la uchumi la wafugaji, pia ni maisha na mila,” alisema Ole Nasha.
Naye Mwanasheria wa Mtandao wa Mashirika ya Wafugaji wa Asili na Waokota Matunda (Pingo’s Forum), Emmanuel Saringe alisema wanaunga mkono rasimu hiyo, lakini walitaka wafugaji kuondolewa kwenye kundi dogo katika jamii.
“Wafugaji ni wengi hasa hawa wa asili, tungependa watajwe kama kundi kubwa ambalo linahitaji kutambulika ingawa kwa sasa linatajwa katika rasimu kama sehemu ya makundi madogomadogo,” alisema Saringe.
Alisema wafugaji ni kundi kubwa katika jamii, ambalo lipo nyuma kwa maendeleo, hivyo linapaswa kupewa kipaumbele na katiba.
“Wafugaji ni kundi maalumu, hivyo linapaswa kulindwa katika katiba na kuendelezwa kwani lipo nyuma,” alisema Saringe.

Tuesday, June 4, 2013

Wakulima miwa wataka kulipwa fidia ya hasara


Mvomero. 
Serikali imeshauriwa kuwalipa fidia wakulima wa miwa waliopata hasara na umaskini wa kipato kutokana na soko la miwa lisilo na tija.
Soko hilo linadaiwa kuwafanya wakulima hao kushindwa kuendelea na kilimo hicho, kinachoonekana kukosa msisimko wilayani Mvomero, mkoani Morogoro.
Akizungumza kwenye mkutano wa wanachama, Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Wakulima wa Miwa na Mazao Mengine Turiani (Tucopricos) Wilaya ya Mvomero, Majaliwa Kayanda alisema sheria zinazohusu miwa zinaonekana kumbeba zaidi mwekezaji na kumsahau mkulima mdogo.
Kayanda alishauri Serikali kufanyia kazi haraka mapendekezo yaliyofikiwa kwenye kikao na wakulima, kilichoitishwa na Wizara ya Viwanda na Biashara Machi mwaka huu.
Katika kikao hicho viwanda vinavyonunua miwa ya wakulima nchini vilihudhuria na kukubaliana na kwamba, kila mkulima anafahamu kiwango cha sukari kinachotoka katika muwa wake kabla ya kupelekwa kiwandani. Kwa upande wao, wakulima wa chama hicho walibainisha kuwapo kwa changamoto mbalimbali zinazohitajika kutatuliwa ili kumnusuru mkulima.
Changamoto hizo ni wafugaji kuvamia mashamba, huku Serikali ikishauriwa kuruhusu kuwapo kiwanda kingine cha sukari kuweka ushindani wa bei, badala ya soko kuhodhiwa na kiwanda kimoja.