Friday, July 28, 2017

Ndugu wanablog wa wakulima na wafugaji

Habari ya siku nyingi!! Kwa kweli tumepotea kwa muda mtatuwia radhi wadau wetu wa kilimo na wafugaji.

Tuna mambo mazuri sana ndugu zetu tunataka kuwaletea ambayo ni kilimo na ufugaji,Tukianza na kilimo, mwaka huu baadhi ya maeneo ya nchi yetu.yamepata mvua nzuri na mengine ya wastani na mengine hayakupata kabisa. Hivyo basi tunakila sababu ya kumshukuru Mungu kwani mwaka jana msimu kama huu hali ikikuwa tete kidogo ya chakula, sasa basi ninaipongeza serikali kwa uhamuzi wake kwa kuliona hilo tatizo iliyotupata mwaka jana ya kuchukua hatua ya kuzibiti chakula kisitoke nje ya nchi bila kibali.

Napenda kuchukua fursa hii kwa kuwakumbusha wadau wote wa kilimo kutunza hii kitu kilicho kipata mwaka kwa uangalifu mkubwa, Hivyo basi shime wadau wa kilimo tushirikiliane na serikali katika tafiti mbalimbali za kilimo cha kisasa pamoja na umwangiliaji,  hitatusaidia kuwa na mazao mengi kwa technology ya kisasa kwa mfano sasa zipo taasisi nyingi zinazoamasisha matumizi ya green house

Napenda wadau wote wa kilimo tushirikiane kwa pamoja ili tuwe na chakula cha ziada hata kuweza kuuza nje ya nchi yetu na kuachana na dhana ya kutengemea mvua za masika nk.

Kwa upande wa mifugo nayo lazima tutumie technology ya kisasa ya ufugaji wa zero graize ambao huu utamzuia mfugaji kuzungunga na mifungo toka kaskazini hadi kusini na kufanya kutulia sehemu moja.

Na hii itafanya kuwa na mifugo yenye tija na ufugaji wenye tija  sana kwa maendeleo ya mfugaji na taifa pia.Sisi kama taasisi isiyo kuwa ya kiserikali tupo tayari kutoa elimu na kuonganisha wadau wote wa pande zote mbili wa wakulima na wafugaji tukishirikiana na serikali.

Friday, February 12, 2016

Hii ni kambuni ya mbegu , wapo morogoro na Arusha tafadhali wasiliana nao kwa faida yako mwenyewe.

Hiyo ni kampuni nzuri sana ya mbegu za mboga mboga tafadhali wasiliana  nao kwa matokeo mazuri zaidi.
Kwa mweli wapo vizuri simu zao zipo hapo.



Tuesday, February 9, 2016

Kwa wale ndugu zangu wapenda mauwa karibuni moshi utapata mauwa
Mazuri na kwa  bei nzuri , tafadhali wasiliana nasi. (Kwa simu au email zetu)
0655615365.
Hii ni kampuni ya uchimbaji visima  vya maji hapa nchini kwa bei  nzuri. Unaweza
Kuwasiliana nao kwa no zao zipo hapo.
Tunapenda kuwatangazia wadau wetu wate wa kilimo pamoja na ufugaji  mambo sasa
Yamekuwa mazuri zaidi kwani zipo  anm sasa zi a saidia sana menye kilimo.
Wapendwa wateja wetu mashine za kisasa kutoka uk tafathali wasiliana nasi ili uwe wakisasa











Wednesday, February 3, 2016





Hili ni godwn lipo boko ni sq 800 karibu sana bei kwa sq ni maelewanno tafadhali karibu.




Hili gari linauzwa bei poa sana ni shs 25 mil. Tu karibu sana waweza wasiliana nasi no 0655615365.

Saturday, January 23, 2016


HERI YA MWAKA MPYA WADAU WETU WA KILIMO:

TUNA PENDA KUWAPONGEZA SANA KWA KUCHAGULIWA NA KUONA MWAKA HUU MPYA.

KWA NEEMA ZAKE MUNGU TUNA YAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ATUWEZESHAYE.

 

Mwaka huu tumejipnga kuweza kuwaletea yale yote mlio kuwa mkiyatazania kwa miaka mingi , hivyo wapenzi wetu napenda kuchukua nafasi hii kuomba radhi sana kwa kutokuwepo hewani muda mrefu, sasa tumerudi na mambo mapya kabisa.

VIPAOMBELE VYETU:

(a) Elimu.

(b)Elimu.

(c)Elimu.

Haya ni mambo matatu naomba niyatoelee maelezo, kwanini ni elimu mara tatu(3) hii maana ni kubwa sana kwani kwenye elimu hutakosea ndio mwanga wa kila siku.

Elimu (a) Maswala yote yanayo husu kilimo na ufugaji wa kisasa, hii ni pamoja na matayarisho ya shamba au eneo pamoja na mbegu bora. Hilo ni eneo moja amabalo ni muhimu sana kulizigatia.

Elimu(b) Ni maswala la masoko nalo ni eneo muhimu linahitaji elimu ya hali ya juu ili kupishana na majanga ya hasara na haswa swala la wakati gani na ni sehemu gani.

Elimu(c). Upatikanaji wa taarifa sahii na wakati sahii na hii ni muhimusana kuwa na elimu hii kwani , hapa nyuma mbambo mengi yamekwenda ndiyo siovyo kwa kusosa muongozo sahii au taarifa sahii na wakati sahii.

 Mambo haya matatu ni maswala ya Elimu kwani elimu ndio kioo cha uchumi kwa taifa letu, Hivyo wadau wetu nomba sana tushirikiane kwa kila hali ili tunapo elekea uchumi wa kati mambo haya hayana budi tushirikiaane sote kwa pamoja.

Hii ndio maana kila moja wetu ni mdau kwa mna moja au nyingine.

Shime jamii ya watanzania na wasio watanzania kwani leo dunia ni kijiji kimoja twabadilishana uzoefu. Napenda kutoa shukurani zangu kwenu wadau niwatakie kila la kheri,

Lema Dennis.


 


Friday, April 10, 2015

Wafanyabiashara wagoma kununua mazao ya kilimo

Wafanyabiashara wagoma kununua mazao ya kilimo


Wafanyabiashara wagoma kununua mazao ya kilimo
Wafanyabiashara ya mazao ya kilimo wilayani mpwapwa wamegoma kununua mazao mbali mbali kutoka kwa wakulima kutokana na kile wanachodai kuwa tabia ya viongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kupandisha tozo za ushuru wa mazao kiholela bila kuwashirikisha.

Mgomo huo umekuja mara baada ya Halmashauri ya MPWAPWA kupandisha ushuru wa mazao kutoka shilingi elfu moja hadi elfu tano kwa gunia moja la mahindi na shilingi elfu moja hadi tatu kwa mazao mengine hali ambayo imezua malalamiko kutoka kwa wakulima.

NJOMBE waanza kutumia mbegu mpya za viazi mviringo

NJOMBE waanza kutumia mbegu mpya za viazi mviringo
Mbegu Bora Nne za Viazi Mviringo zimeanza kutumika katika wilaya ya WANGING’OMBE, Mkoani NJOMBE, kufuatia utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, UYOLE, na kubaini kuwa mbegu hizo ni bora kwa kilimo.

Afisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya hiyo , HENRY VAHAYE amesema wakulima wamekuwa na mwitiko katika matumizi ya mbegu hizo ambazo zinatajwa kuhimili magonjwambalimbali ya mazao.

Watalaam wa kilimo katika Halmashauri ya wilaya Mpya ya Wanging’ombe, wamesema kugunduliwa kwa mbegu hizo Nne za Viazi Mviringo,yawezekana ikawa suluhisho la adui Umaskini katika wilaya hii Mpya.

Pamoja na Mbegu hizo mpya za Viazi Mviringo ambazo zimeanza kutumiwa na wakulima wa wilaya tano za mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya, inadaiwa magonjwa mengine yamedhibitiwa isipokuwa Ugonjwa wa Mnyauko ambao umekuwa ni sumu kwa mimea ya mizizi nchini.

HANANG watakiwa kupanga matumizi bora ya ardhi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Dkt. MARY NAGU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Dkt. MARY NAGU, amevitaka vijiji vyote wilayani HANANG mkoani MANYARA, kupanga matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro miongoni mwa makundi mbalimbali katika jamii

Dkt. NAGU ametoa wito huo wakati wa ziara yake katika vijiji vipya vilivyosajiliwa mwaka jana na kuwataka wananchi kushirikiana na viongozi wao kudumisha amani miongoni mwao.

Waziri NAGU amewaeleza wananchi hao kuwa uamuzi wa serikali wa kuanzisha vijiji vingi zaidi umelenga kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi.

Hata hivyo ameonya kuwa bila kupanga matumizi bora ya ardhi katika vijiji ili kuyapanga makundi mbalimbali yaweze kuishi kwa usalama, upendo na mshikamano, maendeleo ya haraka yaliyokusudiwa hayawezi kufikiwa kwa wakati.

Viongozi wa vijiji hivyo kwa upande wao, wameiomba serikali na Mbunge huyo wa Jimbo la HANANG, kuwasaidia kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika maeneo yao ikiwemo maji, elimu na baadhi ya barabara za vijiji.

Katika ziara hiyo pia ambayo mpaka sasa imehusisha vijiji vipya 30, DOKTA NAGU amewahimiza wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, kujiunga katika mfuko wa afya ya jamii-CHF ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya wilayani humo pamoja na kuipigia kura katiba inayopendekezwa wakati utakapofika.

Wednesday, April 8, 2015

ULIMAJI WA VITALU VYA BUSTANI BIASHARA RAHISI YENYE FAIDA



ULIMAJI WA VITALU VYA BUSTANI BIASHARA RAHISI YENYE FAIDA

ULIMAJI WA VITALU VYA BUSTANI BIASHARA RAHISI YENYE FAIDA
Katika falsafa ya Kilimo kwanza nchini Tanzania, baadhi ya watanzania wengi wameitikia kauli hiyo na baadhi ya wafanya biashara na wakulima mbalimbali kusahau suala la ulimaji na utunzaji wa vitalu Bustani kama Maua, miche ya matunda, miti, nyanya na mazao yoyote ya bustani ni biashara rahisi na yenye faida.
Ukulima wa vitalu vya Bustani ni biashara ambayo inafanya vizuri na kupata mwitikio mkubwa katika nchi mbalimbali hususani Kenya nchi jirani na Tanzania ambapo wanawake wamewekeza katika biashara hii na kupata mafanikio kwa urahisi kama mwanamama Loyce ambaye pia ni msomkama anavyvo elezea katika kidokezo hapo chini.
Aidha teknolojia hii ni chanya kwa watanzania kuanza kuitumia kwani Tanzania ni nchi yenye rutuba nzuri kwa kilimo na asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima wakitegemea kilimo kama uti wa Mgongo. Hata hivyo Njia Mpya inalitazama suala hili kwa jicho pana na faida kwa mkulima au mfanyabiashara wa ulimaji na utunzaji wa vitalu na kuiona ni fursa muhimu kwa mfanyabiashara kupitia njia hii kupata kipato na hatimaye kupunguza na kuondoa kabisa umasikini katika familia na nchi kwa ujumla. Kuna maadui watatu ambao ni hatari sana kwa maendeleo katika jamii nao ni “Umasikini, Ujinga na Maradhi” ni wakati sasa wa kupambana na umasikini huu tujitokeze na kuiona fursa hii. Biashara hii haibagui wanaume wala wanawake 

Vijana waaswa kutumia Fursa wazipatazo

WAZIRI wa habari vijana utamaduni na michezo FENELLA MKANGARA
WAZIRI wa habari vijana utamaduni na michezo FENELLA MKANGARA,amewashauri vijana kote nchini kuwa wabunifu na kutumia fursa zinazojitokeza mbele yao ili kujiletea maaendeleo

Hayo ameyasema katika mkusanyiko wa magari hamsini na pikipi 10 za vijana wa BONGO RIDE wakiwa tayari kufanya msafara unaotwa BONGO CHARITY CRUIZE kutoka DAR hadi MORO.

mkurugenzi wa makapuni ya TSN GROUP, FAROUQ BAGHOZA anaeleza kwa nini amedhamini msafara huo kuwa ni kuwaleta vijana pamoja na kuibuwa vipaji vya vijana hapa nchini.

Msafara huo wa MAGARI na PIKIPIKI kutoka DAR HADI MOROGORO, utatembelea kikundi cha watu wanaoshi na virusi vya ukimwi mkoani morogoro,WAVUMO ili kujua shida zao na kuzitafutia ufumbuzi.