Tuesday, February 24, 2015

Waliokopeshwa zana za kilimo watakiwa kuzitumia kwa umakini.

Na Zacharia Mtigandi,
Manyara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji dokta Mary Nagu, amewataka wananchi waliokopeshwa zana mbalimbali za kilimo nchini, kuhakikisha wanaitumia mikopo hiyo kwa umakini ili iweze kuwa chachu ya kuinu hali zao za kiuchumi.

Aidha aliwataka kuhakikisha wanafanya marejesho ya mikopo hiyo kwa wakati kulingana na mikataba waliokubaliana na taasisi zilizowakopesha.

Zana za kilimo zilizokopeshwa kwa wingi kwa wakulima nchini msimu wa mwaka jana ni pamoja na matrekata makubwa na madogo yanii power tiller mbengu na mbolea.
Zana kama vile matreketa yamewanufaisha wakulima hasa wa wilayani Hanang mkoani Manyara ambao wameongeza uzalishaii wa mazao kutoka tani zaidi ya elfu 80 mwaka juzi hadi tani zaidi 120,000 kwa msimu wa mwaka jana.

Matrekta hayo hayawanufaishi wakulima waliokopa pekee bali hata wakulima wa kawaida wamekuwa wakikodi kwa gharama nafuu.

Akiongea na wakazi wa wilaya ya Hanang Waziri Nagu ambaye pia ni Mbunge wa jimbo hilo alisema kuwa serikali imetoa mkopo wa treketa kwa gaharama nafuu ili kuwawezesha wakulima kumudu.

Aidha aliwataka wananchi wa jimbo la Hanang kuanzisha vikundi vitakavyowasaidia kupata mikopo kwa urahisi kutoka taasisi za kifedha.

Uzalishaji aina mpya ya Mgomba, wakulima wapewa darasa.

Na Ramadhani Mvungi, Arusha. 

Kituo cha utafiti na mafunzo ya kilimo cha mazao ya Mboga, Matunda na Maua cha Tengeru Arusha kikishirikiana na taasisi za TAHA na TAPP kimeanza kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu uzalishaji wa aina mpya ya zao la mgomba kupitia mashamba darasa.

Hatua hiyo ni mpango mahususi wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya mbogamboga, matunda na maua katika kuendeleza dhana ya kilimo biashara nchini.
 Ikiwa chini ya Wizara ya Kilimo chakula na Ushirika kituo cha HORTI-TENGERU kinasema, utafiti uliofanywa umebaini aina hiyo mpya ya migomba, kuwa na kiwango cha juu cha uzalishaji wa zao la ndizi, ikiwa na uwezo wa kuvunwa migomba 1450 katika heka tofauti na ile ya awali yenye uwezo wa kuzalisha migomba 400 pekee katika kipindi cha mwaka mzima.

Mkuu wa kituo cha utafiti cha HORTI-TENGERU Juma Shekidele pamoja naye meneja uzalishaji kutoka taasisi ya TAPP kanda ya Kaskazini Milton Chitanda,wametoa mwito kwa wakulima kuzitumia teknolojia mpya zinazoibuliwa na watafiti, ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya mbogamboga na matunda yanayoonekana kuhitajika sakoni kwa wingi.

Chama cha wakulima wa mboga na maua nchini TAHA, kupitia kwa afisa mawasiliano wake Likati Thomas kimesema lengo la kutoa fursa kwa wakulima kutembelea mashamba darasa na kujionea teknolojia mpya ni kutoa hamasa kwa wadau wa sekta hiyo hususani vijana ili waweze kujihusisha na kilimo cha Hortculture lengo likiwa ni kupunguza adha ya ukosefu wa ajira.

Uwekezaji wenye thamani ya shilingi milioni thelathini na tano unatajwa kuweka katika mashaba darasa yaliyopo eneo la Horti-Tengeru ambapo wakulima takribani mia saba wamepatiwa mafunzo ya teknolojia za usambazwaji wa miundombinu ya umwagiliaji kwa matone na matumizi ya mbolea

Wajasiriamali waaswa kuendesha biashara zao kitaalamu.

Na Amina Saidi, Mbeya.
Wajasiriamali nchini wametakiwa kujifunza mbinu za kuendesha biashara zao kitaalamu ili kukuza mitaji.
Hatua hiyo itazijafanya biashara hizo kuwa endelevu na zenye tija.
Ni katika uzinduzi wa kitabu cha Mjasiriamali kinacholenga kutoa elimu itakayowasaidia wajasiriamali wadogo na wa kati kukuza mitaji ya biashara zao kitaalamu badala ya kuendesha biashara za kuiga ama kufuata mkumbo ambazo mara nyingi si endelevu.
Mtunzi wa kitabu hicho mjasiriamali mdogo anayejishughulisha na uuzaji wa viatu jijini Mbeya David Mbukwa anawaasa wajasiriamali wenzake kutokuogopa mikopo inayotolewa na taasisi za fedha na badala yake wakope na kuitumia mikopo hiyo kwa malengo mahususi.

Serikali kutoa elimu kwa wakulima wadogo wa Pamba.

Na Gloria Matola,
Pwani Bagamoyo.
Serikali imejipanga kuendelea kuwaelimisha wakulima wadogo wadogo wa zao la pamba waliopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ili wafikie hatua ya kulifanya zao hilo kuwa la kibiashara zaidi ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na hali ya umasikini uliokithiri kwenye ukanda wa Mashariki.
Hayo yameelezwa kwenye ziara ya Bodi ya Pamba kwa kushirikiana na Chama kikuu cha Ushirika mkoa wa Pwani CORECU na TACOGA lengo likiwa ni kuwahamasisha wakulima wa zao hilo kurejea kwenye kilimo hicho.
Walipozungumza na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi wakulima hao wamesema kumekuwepo na tatizo la muda mrefu la soko la uhakika hivyo kuitaka Serikali kueleza mipango yake katika kukabiliana na tatizo hilo.
Mkurugenzi wa Huduma za Usimamizi Bodi ya Pamba Tanzania James Shimbe amesema Serikali imejipanga vizuri kutatua matatizo yote yaliyopo ikiwa ni pamoja na kufungua kiwanda cha kuchambua pamba cha Bagamoyo.
Naye Meneja wa chama kikuu cha Ushirika mkoa wa Pwani Seif Upalla amewahakikishia wakulima hao kupata soko la uhakika ikiwa ni pamoja na chama hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi amewataka wakulima hao kuitikia mwito wa kuanza kulima zao la pamba kwa kuwa tayari wamehakikishiwa mazingira bora ya masoko.

Benki ya DCB yatoa mikopo kwa wajasiliamali wanawake

Benki ya DCB imetoa mikopo yenye thamani ya Sh. bilioni 47.5 kwa wanawake wajasiliamali 79, 464 katika kipindi cha mwaka jana, ikiwa ni jitihada za benki hiyo kuwainua kiuchumi na kupunguza umaskini.

Mikopo hiyo ilitolewa kati ya Januari na Desemba 31, 2014, kupitia huduma za mikopo ya vikundi, kwa wanawake katika wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Bidhaa na Masoko wa Benki ya DCB,  Boyd Mwaisame, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake na Vijana Tanzania, uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na kuhudhuriwa na wanachama, maafisa wa benki na wajasiliamali.

Alisema benki hiyo inatoa huduma mbalimbali za mikopo kwa wajasiliamali wadogo na wa kati, huku akiwasihi watumie fursa hiyo kuomba mikopo ili kuendeleza shughuli zao.

“Tathmini ya kina imefanywa kuhusu huduma ya mikopo ili kuhakikisha inakidhi mahitaji ya waombaji (wajasiliamali wadogo na wa kati),” alisema Boyd.

Akielezea alisema mikopo kutoka benki ya DCB ina riba nafuu, hivyo kuwafanya wajasiliamali wadogo na wa kati kuweza kurejesha mikopo yao kwa muda na kuendeleza biashara zao kwa upande mwingine.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake na Vijana Tanzania, Sophia Mwakagenda, aliipongeza benki ya DCB kwa kudhamini  mkutano huo na kuweka mikakati inayolenga kuboresha shughuli za
wajasiliamali wadogo na wa kati nchini.

inetolewa na ipp media

Monday, February 23, 2015

Kilimo cha chai Morogoro chaonesha tija.

Pamoja na changamoto nyingi zinazowakabili wakulima wa zao la chai Tanzania ikiwemo kuyumba kwa  bei ya zao hilo kwenye soko la dunia lakini limeweza  kuzitoa  kwenye lindi la  umaskini kaya  zipatazo  30,000 zilizoko katika wilaya 6 nchini zinazozalisha zao hilo.

Katika mkutano wa uzinduzi  wa mradi wa utetezi  wa wakulima wadogo  wa chai  nchini  ulifanyika mjini Morogoro  inabainishwa kuwa  pamoja na zao hili kuuzwa bei ndogo kwa kilo  katika soko la dunia, lakini bado limeonesha kuondoa umaskini kwa wakulima wadogo kwani chai huvunwa kila mwezi tofauti na mazao mengine ambayo  huvunwa kwa msimu.

Ujio wa sera ya uchumi wa soko katika kuendesha biashara ya chai hapa nchini umeshuhudia changamoto ikwemo bei duni ya majani mabichi ya chai  kwa wakulima nchini.
Tangu mwaka 2004 hadi 2013 bei ya majani  mabichi ya chai   kwa kilo moja imeongozeka kutoka sh.86 hadi sh.206, ongezeko hilo ni dogo sana ikilinganishwa na gharama na uzalishaji wa zao hilo, hata hivyo bado limeonesha kuondoa umaskini kwa wakulima .
Kumeanzishwa mfuko wa  wakfu  wa maendeleo ya  wakulima  wadogo wa chai  Tanzania  , ambao unatakiwa kutatua changamoto za wakulima  huku wataalamu wa mfuko huu wakipewa changamoto.
Kutokana na  asilimia 80 ya chai ya hapa nchini kuuzwa nje ya nchi  moja kwa moja  na kupitia mnada wa  Mombasa ,Tanzania inaingiza  dola  za kimarekani milioni 56 kwa mwaka,tofauti na nchi  jirani ya  Kenya ambayo imekuwa ikijizolea dola za kimarekani milioni 1328.

KILIMO CHA VITUNGUU SWAUMU- garlic

UDONGO
Vitunguu twaumu vinahimili aina nyingi za udongo, ila vinastawi zaidi katika udongo usiotuamisha maji kabisa na wenye mbolea asili, kama mbolea si ya kutosha kwenye udongo, tumia samadi iliyokwisha oza vizuri usitoe samadi bandani na kuipeleka shambani moja kwa moja kwenye shamba la vitunguu thwaumu, labda kama utaliacha shamba bila kulimwa kwa zaidi ya miezi 6, pia unaweza kutumia mbolea za viwandani kama ammonium nitrate, ammonium sulphate, urea n.k wakati wa kupanda na kila baada ya wiki 4 – 6 mara mbili zaidi



MAKAKARA - PASSION FRUITS


Ni mimea inyotambaa na kuhimili hali nyingi za hewa (sio ukame) mme huu hustawi zaidi ukanda usio na baridi wastani wa 20c – 30c na kiasi cha mvua 1500mm za ujazo kwa Mwaka, tunda huwa na ukubwa wa sentimeta 10 kwa kipenyo na uzito gramu 90, kuna aina kadhaa za matunda haya lakini yale ya kijani/manjano hustawi zaidi ukanda wa pwani na yale yenye wekundu Fulani hustawi zaidi maeneo ya misitu, hupendelea udongo wa kichanga wenye mbolea na usiotuamisha maji, pia udongo usiwe na chumvi nyingi na pia kusiwe na mwamba chini kasi cha mita moja tu.



UPANDAJI
Mbegu zipandwe kwanza kwenye mifuko ya plastiki yenye udongo wenye rutuba ya kutosha , kiasi cha Mbegu 3 kwa kila mfuko na mara zinapoota mimea ikingwe na jua kali na ikifikia urefu wa sentimeta 30, huweza kuhamishiwa shambani
Kwenye shamba lako hakikisha kuna nguzo zenye waya mmoja kwa ajili ya mimea kutambaa juu yake, sehemu ya juu baada ya nguzo kuzikwa chini ibakie kama mita mbili na kati ya msatari na mstari iwe ni mita 2 (ukanda wa pwani ) na mita 3 ukanda wa juu kiasi, na umbali kati ya nguzo na nguzo kwenye mstari ni mita 6, na mimea ipandwe umbali wa mita 3 kati ya nguzo na nguzo kufuata mstari.



UANGALIZI
MBOLEA

Mbolea za viwandani ziwekwe kutokana na hali ya udongo, muone afisa ugani kilimo ili afanye vipimo kujua mahitaji na upungufu wa udongo,

MAGONJWA WADUDU
Wadudu kama chawa wa mimea na mchwa wekundu ndio adui wa makakara, pia fangasi husshambulia sana maua ya makakara. Dawa za jamii ya kopa zitumike mara dalili za magonjwa au wadudu kuonekana, kiasi cha kilo 2.8 – 3 hutosha kwa hekta moja au gramu 225 kwa ajili ya dumu moja la lita 20

MAGUGU
Makakara yanatakiwa yawe kwenye shamba safi lisilo na majani na magugu, jembe la Mkono au madawa kama ROUND-UP na GRAMOXONE ynaweza kutumika mimea ikishaefuka na kuwa juu kwenye waya

KUFUNDISHA MIMEA
Ni lazima kuyafundisha matawi mawili ya kwanza kwa kuyaelekeza kutambaa kwenye waya kila moja likielekea upande wake na matawi yatakayoota kutokana na matawi makuu nayo yaelekezwe juu kwenye waya yakifikia ukubwa wa sentimeta 30 – 40



KUPUNGUZA MATAWI
Silazima kupunguza matawi kwa sababu mmea mkubwa zaidi ndio hutoa matunda mengi zaidi, labda kama kuna matatizo katika uchumaji ndio unaweza kupunguza baadhi ya matawi kiasi.

UVUNAJI

Uvunaji huanza baada ya miezi 8 – 9 baada yam mea kupandwa na matunda hukusanywa baada ya kudondoka yenyewe chini baada ya kuiva kila baada ya wiki moja, matunda yahifadhiwe sehemu kavu na isiyo na joto , kiasi cha tani 5 – 10 huweza kupatikana katika hakta moja kwa msimu

JINSI YA KULIMA BUSTANI KWENYE ENEO LENYE MAJIMAJI



1- Lima na tifua udongo kwa kutumia trekta la mkono (power tiller) kiasi cha inchi 12 chini, udongo mwingine unaweza kuujaza kama matuta na kuweka mifereji pande zote la eneo lako. Kama huna trekta hili pia unaweza kutumia jembe la kukokotwa na ng’ombe (plau)

2- Jaza majani makavu, vijiti, maranda ya mbao n.k kiasi cha inchi 5 -6 halafu mbolea vunde au samadi kiasi cha inchi 4 halafu rudishia udongo wako juu yake na hapo utakuwa umeinyajua ardhi yako kiasi cha inchi 8 juu (kumbuka maranda na mbolea vitadidia kidogo) kisha pitisha harrow au jembe la kukokotwa na ng’ombe ili kuweza kuchanganya vitu hivi
3- Acha udongo wako ukauke kiasi cha siku 3 kisha pitisha harrow au jembe la kukokotwa na ng’ombe tena ili kuvunja vunja mabonge ya udongo yaliyotokea wakati wa udongo kukauka na pia kuchanganya mchanganyiko huu zaidi

4- Weka tena mbolea vunde au samadi kiasi cha nchi mbili juu ya mchanganyiko huu kisha panda mbegu au miche yako na uizungushie udongo kiasi

5- Mwagia maji kadri inavyo hitajika kama udongo utakuwa mkavu, na uendelee kufuata kanuni za kilimo bora kama inavyoshauriwa kitaalamu

Sunday, February 22, 2015

Mbiringanya ni mkombozi kiuchumi na kiafya:FAO Kusikiliza / Hamishia


Tunda la mbiringanya. (Picha:FAO)
Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limetangaza Mbiringanya kuwa  zao la asili kwa mwezi huu wa Januari.FAO inasema majani machanga ya mbiringanya huchanganywa kwenye supu au na mboga nyingine na pia kuliwa mabichi. Halikadhalika tunda lake linaweza kutengenezwa achali au kuliwa bichi na hata kuchanganywa na nyama.
Licha ya kwamba kuna aina mbili za mbiringanya moja yenye tunda refu na nyingine tunda la mviringo, FAO inasema aina zote ni mkombozi kwa wakulima wadogo mijini na vijijini kwani hutoa mazao mengi kwenye bustani ndogo.
Tovuti ya FAO pamoja na kuelezea mapishi ya biringanya, inataja matumizi yake kiafya ikisema mizizi na matunda yake hutumika kupunguza maumivu, shinikizo la damu ilhali juisi itokanayo na majani huweza kutibu matatizo ya njia ya mkojo.

Saturday, February 21, 2015

MILIBAGI - MDUDU MHARIBIFU WA MIKOROSHO

Milibagi (Pseudococcus longispinus) ni wadudu waharibifu katika zao la korosho, waliojitokeza kuwa maarufu sana katika miaka ya tisini. Hawa ni wadudu wanaoonekana katika maeneo mengi ulimwenguni, lakini hushamiri na kuleta athari kubwa katika mazingira ya Tropikali. Mnamo mwaka 1990, milibagi walionekana kushambulia mikorosho katika maeneo ya mjini Masasi. Mwaka 1993, walionekana kuenea hadi wilaya za Nachingwea na Tunduru. Hivi leo, wadudu hawa wameenea karibu sehemu nyingi za kanda ya kusini, ingawa mashambulizi makubwa yapo wilayani Masasi, Tunduru, Nachingwea na Liwale.   Milibagi ni moja ya wadudu waharibifu wanaoishi na kuponea mimea. Wadudu hawa hutengeneza utando mweupe (scale) juu ya miili yao kwa ajili ya kinga na kujihami dhidi ya adui zao.



UBWIRI UNGA - UGONJWA MKUU WA MIKOROSHO

Moja ya matatizo makubwa ya uzalishaji wa  zao  la korosho ni ugonjwa wa Ubwiri unga.Ugonjwa huu unasababishwa  na vimelea aina ya uyoga (fungus) viitwavyo Oidium anacardii. Ugonjwa huu ni muhimu sana, kiasi kwamba kama haukuthibitiwa,  unaweza kupunguza mavuno kwa zaidi ya asilimia 70.       Ugonjwa huu umeenea katika  mikoa  yote inayolima zao hili Tanzania.  Hapo awali ugonjwa huu ulikuwa unaitwa kwa jina la“ukungu” kutokana na uhusiano wake mkubwa na haliya hewa ya ukungu  (litabwe  kwa  Kimakonde) unaoonekana  alfajiri/asubuhi katika miezi ya Juni - Septemba.  Hivyo  basi,  jina la Ubwiri unga linatumika sasa ili kuwawezesha wakulima wasichanganye vitu hivyo viwili.


MASHAMBULIZI
Ugonjwa huu unashambulia maeneo yote machanga na teketeke  katika  mti wa mkorosho, hasa machipukizi, majani, maua, mabibo na korosho changa (tegu). Athari kubwa  ya ugonjwa  huu inatokana na mashambulizi ya maua, ambayo hushindwa kufunguka  na  kuwezesha chavua kufanya kazi yake,  hatimaye  hunyauka  na kukauka.



SUKUMA VUTA -Njia bora ya kupambana na kiwavi mshambulia mabua ya mahindi (maize stalk borer)


Kiwavi anayeshambulia mabua ya mahindi anajulikana pia kama maize stalk borer(Sesamia fusca) kiwavi huyu hutokana na vipepeo weupe wanao onekana kwenye mashamba ya mahindi, vipepeo hawa hutaga na baada ya mayai yao kuanguliwa ndipo viwavi hawa waharibifu hutokea na kuanza kushambulia mahindi shambani



Viwavi hawa hushambulia katikati ya mabua na kusababisha mmea kudumaa na kisha kufa, hali huwa mbaya zaidi kama mashambulizi yatatokea wakati mimea ikiwa bado michanga maana mkulima hatavuna kabisa katika mimea iliyoshambuliwa na pia hupunguza mavuno kwenye mimea iliyokomaa na kutoa mbelewele



Njia hii ya sukuma vuta ni njia yenye mafanikio kwa asilimia kupambana na viwavi hawa kama utafuata maelekezo kwa usahihi, na hii itakusaidia kupambana na viwavi hawa kwa njia ya kibaiolojia bila kutumia kemikali zozote shambani mwako
 Ilikupambana na viwavi hawa waharibifu kwenye shamba lako la mahindi, panda mimea ya desmodium kila baada ya mistari mitano ya mahindi, desmodiuM husaidia kufukuzavipepeo na viwavi kutokana na harufu yake kali na wakati huo huo kuongeza nitrjeni kwenye udongo shambani

Panda majani aina ya napier kuzunguka shamba lako, kwani majani haya huwavutia pia vipepeo na viwavi hawa waharibifu, wakati desmodium inawafukuza nje ya shamba lako viwavi hawa, majani ya napier yanakuwa yanawavuta nje ya shamba lako na ndio maana njia hii ya kibaiolojia hiutwa SUKUMA VUTA

NG'OMBE ALIYE KWENYE JOTO - JINSI YA KUMTAMBUA

Kwa kawaida ng'ombe jike aliyebalehe huingia kwenye joto kila baada ya siku 14 - 24 au wastani wa siku 21 kama hatapandwa na kushika mimba, hii hutegemea na aina ya ng'ombe, mazingira, lishe na hali ya hewa. kuna masaa kati ya 6 - 10 kabla hajaingia vizuri kwenye joto (pre heat) na joto lenyewe huchukua kati ya masaa 4 - 30 pia kutegemeana na aina ya ng'ombe, mazingira, lishe na hali ya hewa na yai hupevuka kwa wastani wa masaa 10 - 12 baadae


Kama utataka kumpandisha ng'ombe jike wako kwa kutumia madume bora ya kuazima au kwa kutumia  kupandisha kwa njia ya chupa, basi ni muhimu kuzijua dalili kuu ambazo huonekana ng'ombe jike anapokuwa kwenye joto, dalili hizi zinaweza kuonekana kabla ya joto, wakati wa joto ana hata baada ja joto kupita kidogo, kwa hiyo ni muhimu kuzitambua mara zinapoanza ili usiweze kupitiliza na kulikosa joto halisi

DALILI KUU

  1. Sehemu ya nje ya kizazi/uke huwa kubwa zaidi kama imeumuka na kutuna zaidi ya ile saizi yake ya kawaida.
  2. Sehemu ya nje ya kizazi/uke huwa na rangi nyekundu inayoelekea kukooza zaidi ya kawaida yake.
  3. Ute ute hutoka kwenye kizazi na huwa mzito wenye kunata nata.
  4. Ng'ombe huwa hatulii, mwenye kuzunguka zunguka na hata kulia lia zaidi ya kawaida yake.
  5. Ingawa ni jike lakini pia hujaribu kuyapanda majike mengine yaliyopo bandani, kana kuna mabanda mengine zaidi, ukimuhamisha hali hii ya kuwapanda wenzie hizi.
  6. Hunyanyua nyanyua mkia na kwenye ncha mkia huwa imevurugika (rough)
  7. Ukimgandamiza mgongoni kwa kutumia mikono sehemu ya nyuma kabisa karibu na mkia hutulia na kusikilizia kama anapandwa, mwanzo hatatulia ila ukifikia wakati sahihi atatulia na hapo ndipo unapoweza kumuwekea mbegu kwa njia ya chupa na kama unatumia dume lenyewe litatambua hali hii kwa hiyo ukiona dalili tu zinaanza mpeleke kwa dume na lenyewe litapanda kwa wakati sahihi.

KILIMO BORA CHA KARANGA

Karanga ni mojawapo ya mazao yanayotoa mafuta. Katika Tanzania zao hili hustawi zaid katika mikoa ya Kusini Mashariki, Dodoma na Morogoro. Pamoja na kutoa mafuta vile vile zao hutumika kwa njia nyingine mbali mbali, nazo ni pamoja na: 


1. Chakula cha wanyama (Mashudu na majani)
2. Kurutubisha ardhi
3. Chakula cha binadamu (Confectionary)

Kwa ujumla zao hili hutumika na wakulima kama zao la biashara.



HALI YA HEWA
Karanga hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye miinuko chini ya mita 1500, toka usawa wa bahari katika Tanzania, na hustawi zaidi katika maeneo ambayo yanapata mvua za wastani wa mm 750 hadi mm 1200 kwa mwaka.
Vile vile karanga hustawi vizuri kwenye udongo wa kichanga, inashauriwa kutopanda karanga kwenye udongo mzito (mfinyanzi) hii ni kutokana na sababu kwamba, karanga hazistawi kwenye sehemu zinazo simama maji, na udongo mzito huleta hasara wakati wa uvunaji.


KILIMO BORA CHA VIAZI VITAMU

Watu wengi wamekuwa wakiulizia umuhimu wa madini kwenye udongo na namna ya asili ya kuongezea kosefu wa madini kama potasiam, fosforas, kalsiam na mengineyo, njia rahisi ya kuongeza baadhi ya madini kwenye udongo ni kwakutumia majivu


UMUHIMU
Majivu yanakiwango cha wastani wa madini kifuatacho potasiam 5% - 7%, kalsiam 25% - 50%, fosforas 1.5% - 2% na madini mengine kwa kiasi kidogo pia mabaki mabaki ya chenga za mkaa kwenye majivu pia yanasaidia kwenye kunyonya baadhi ya sumu kwenye ardhi, kumbuka mkaa ni kaboni halisi (pure carbon)

KIASI CHA KUTUMIA
Kiasi cha kilo 2.5 mpaka 5 kitumike kwenye eneo la mita za mraba 33 au futi 100 za mraba, na majivu yamwagwe wiki 3 - 4 kabla ya kupanda kitu chochote ardhini.

MADHARA
Kila kitu kikitumiwa zaidi ya kiasi kina madhara na majivu pia yana madhara kwenye udongo kwa sababu yana hali ya kuwa alkaline zaidi (10 - 12 pH)  kwa sababu baadhi ya mchanganyiko wake hauyayuki kwenye maji, kama utahitaji kuongezea kwenye mimea yenye upungufu wa madini kama fosforas na potasiam basi hakikisha majivu hayagusi mashina kwani yanaweza kuuungua haya kama mimea ni michanga.

Pia majivu yanan kiasi kidogo sana cha naitrojeni ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya mmea wowote ule, kwa hiyo hakikisha pia unatumia vyanzo vingine kwa ajili ya naitrojeni, vyanzo kama mimea jamii ya mikunde, marejea, lukina, na alfal

-KILIMO BORA CHA MATUFAA - APPLES


Viazi vitamu ni moja kati ya mazao makuu ya mizizi nchini Tanzania ambalo hulimwa kwa ajili ya chakula. Zao hili ni moja kati ya mazao ya kinga ya njaa kutokana na sifa yake ya kuvumilia ukame. Zao la viazi vitamu, asilia yake ni Amerika ya Kati na ya Kusini. Nchini Tanzania, zao hili hulimwa zaidi katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Morogoro,Kagera,Arusha na Ruvuma.

Matumizi 
Viazi vitamu hutumika kama chakula kwa kutayarishwa katika njia mbalimbali kama vichembe, na Matobolwa. Pia Unga wa viazi vitamu hutumika kutengeneza vyakula kama keki, maandazi, kalimati na tambi. Majani ya viazi huliwa kama mboga pia hutumika katika kutayarisha mboji.

Aina za viazi vitamu
Kuna aina nyingi za viazi vitamu zinazolimwa ulimwenguni. Hapa nchini Tanzania aina zinazolimwa zaidi ni Ukerewe, Simama, Kakamega, Karoti C, Mwananjemu, Ali mtumwa mayai, Mavuno, Pananzala, Kibakuli, Sinia,Vumilia na Polista

Uzalishaji 
Zao hili hustawi maeneo mengi Nchini Tanzania. Viazi hustawi vizuri katika maeneo ya tambarare yenye udongo tifutifu, unaoruhusu maji kupenya kwa urahisi. Udongo wa mfinyazi na wenye kokoto nyingi haufai kwani huzuia mizizi kupenya na kupanuka.

Shamba jipya litayarishwe vizuri kwa kufyeka vichaka na kung’oa visiki. Majani yafukiwe wakati wa kutengeneza matuta ili kuongeza rutuba ya udongo.

Viazi vipandwe kwa kutumia Marando yenye urefu wa sentimita 30 kwa mavuno bora. Inashauriwa kutumia sehemu ya juu ya shina kwa mavuno zaidi. Marando yapandwe katika umbali wa sentimita 25 hadi 30 kutoka mmea hadi mmea na sentimita 60 hadi 75 kutoka tuta hadi tuta. Viazi pia vyaweza kupandwa kwa kutumia viazi vyenye afya vyenye uzito wa kati ya gramu 20 hadi 30. Hata hivyo inashauriwa kutumia marando ili kupata mavuno zaidi na kuepuka kuenea kwa magonjwa.

Kutunza shamba
Ni muhimu kupalilia viazi vitamu katika miezi miwili ya mwanzo ili kuupa mmea nguvu ya kutambaa vizuri. Baada ya muda huo, viazi huweza kufunika ardhi na hivyo huzuia uotaji wa magugu.

Viazi hushambuliwa na wadudu mbalimbali wakiwemo kipepeo, mbawa kavu, fukusi na minyoo fundo.Pia hushambuliwa na magonjwa yakiwemo magonjwa yanayotokana na virusi kama Sweet Potato Chlorotic Stunt virus (SPCSV). Magonjwa na wadudu yaweza kudhibitiwa kwa kuzingatia usafi wa shamba, kubadilisha mazao, na kuzingatia udhibiti sango.

Uvunaji
Viazi vitamu huwa tayari kuvunwa miezi mitatu hadi minne tangu kupanda kutegemea hali ya hewa. Viazi vinaweza kuvunwa kidogo kidogo kwa kutumia mikono, vijiti, jembe, au rato kadri vinavyohitajika. Aidha inashauriwa viazi visiachwe ardhini muda mrefu bila kuvunwa kwani vitakomaa sana na kuwa na nyuzi, na hivyo kuharibu ubora wake. Pia kuacha viazi muda mrefu hukaribisha mashambulizi ya wadudu kama fukusi na kuoza. Kwa maeneo makubwa zaidi, inashauriwa kutumia mashine ya kukokotwa na ng’ombe. Uvunaji ufanywe kwa uangalifu ili kuhakikisha viazi visikatwekatwe wala kuchubuliwa wakati wa kuvuna.

Mavuno ya viazi hutofautiana kulingana na aina, hali ya hewa, na udongo. Mavuno ya viazi yanakadiriwa kufikia tani 20 kwa hekta

Friday, February 20, 2015

Soya zao lenye manufaa lukuki kwa jamii

Soya zao lenye manufaa lukuki kwa jamii



Maharagwe ya soya ni moja ya mazao muhimu katika jamii ya mikunde katika nyanja za uzalishaji wa kibiashara kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha protini (35-40%). Soya inatumika katika kuandaa vyakula vinavyoliwa vikiwa vibichi, vinavyovundikwa na vyakula nikavu, mfano maziwa, tofu, mchuzi pamoja na kimea.


Hali ya hewa, udongo na maji


Soya hulimwa katika ukanda wa Ikweta. Soya hukomaa katika kipindi cha siku 180 (miezi 6) lakini inaweza kuwa na baadhi zinazokomaa mapema zaidi. Joto chini ya nyuzi joto 21 na juu ya 32 inaweza kuathiri ushavushaji na utengenezaji wa viriba. Na joto zaidi ya nyuzi 40 ni hasara kwa uzalishaji wa mbegu.


Endapo maji yanapatikana, Soya inaweza kulimwa kwa kipindi chote cha mwaka. Soya huhitaji milimita 400-500 za maji kwa msimu ili kupata mazao bora. Kiwango cha juu cha unyevu kinahitajika sana wakati wa kuota, kuchanua na kuunda viriba. Hata hivyo majira ya kiangazi ni muhimu kwa ajili ya kukomaza. Soya inaweza kuvumilia maji yaliyotuama lakini mvua ikizidi ni tatizo kubwa kwa uzalishaji wa mbegu.




ZIFAHAMU MBEGU BORA ZA MAHARAGE

mbegu_za_maharage_selian_39c9e.jpgNa. Josephine MkudeNi vema kwa wakulima kuzingatia mbegu bora katika kilimo ili kupata mazao bora yatakayowapa faida baada ya mavuno.  Kituo cha Utafiti wa Kilimo Selian Arusha ambacho ni makao makuu ya utafiti ya kanda ya Kaskazini kwa miaka mingi imekuwa ikitafiti aina bora za maharage ambazo hutoa mazao mengi, ambazo pia zinastahimaaili ukame na magonjwa. Kwa kufuata kanuni bora za kilimo wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji wa zao la maharage kwa kutumia mbegu bora kama vile Jesica, Lyamungu na Selian. Mbegu hizi zimeshasambazwa kwa wakulima na wanazitumia kwa uzalishaji

KILIMO CHA MICHUNGWA NA MACHENZA

Ndugu Ali Kalufya alitaka kujua kwa kina ukuliama wa michungwa na jamii yake, aliuliza swali hili katika mtandao wa Dada Subi nami najaribu kumweleza haya...

Michungwa na Jamii yake hustawi zaidi ukanda wa pwani wenye joto kiasi, mvua nyingi na udongo wenye rutuba, kwa Tanzania mikoa kama Pwani, Dar es salaam, Tanga, Mtwara, Lindi, na Morogoro ni maarufu kwa kilimo hiki

MBEGU
Kwa kuanzia unakusanya mbegu za mlimao kutoka katika malimao yaliyokomaa na ikiwezekana yawe yameiva yakiwa mtini, kausha mbegu zake na kisha unaweza kutolea ganda la nje ili ziweze kuota vizuri.

KITALU
Mwaga mbegu zako kwenye kitali na uzifukie kwa udongo kiasi cha nusu sentimeta, mwagia maji kilasiku na baada ya wiki 3 - 6 mbegu zitaanza kuchipua,

MICHE YA MILIMAO TAYARI KWA KUUNGWA




WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA ZIARANI KATIKA JIMBO LA ISIMANI NA KALENGA MKOANI IRINGA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua matrekta madogo maarufu kwa jina la Power Tiller yanayotumika katika shamba la kilimo cha umwagiliaji la Magozi katika jimbo la Ismani wakati alipolitembelea shamba hilo akiwa katika ziara ya mkoawa Iringa Februari 19, 2015. Watatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza.

Thursday, February 19, 2015

UKOSEFU WA WATAALAMU MBALI MBALI KATIKA SEKTA YA KILIMO CHA MIWA NI KIKWAZO KIKUBWA KWA WAKULIMA WA MIWA KILOMBERO


UKOSEFU WA WATAALAMU MBALI MBALI TATIZO KWA WAKULIMA WA MIWA KILOMBEROUkosefu wa Wataalamu wa Uchumi , Mizani na Sheria ni baadhi ya changamoto zinazovikabili vyama vya Wakulima wa Miwa katika Bonde la Kilombero.Akizungumza katika mahojiano na mwandishi wetu Katibu wa Chama Cha Wakulima wa Miwa cha Msolwa Ujamaa (MUCGA) Modestus Chitemi amesema ili kuwezesha ongezeko la bei kwa Wakulima kwa Uwiano kama ilivyo kwa Nchi Jirani Wataalamu zaidi wanahitajika.Akitolea mfano wa Nchi ya Malawi, Bwana Chitemi amesema kuwa Wakulima wa Miwa waNchi hiyo wana uwiano wa kupata asilimia Sitini (60) wakati Viwanda vya Sukari vinapata asilimia Arobaini(40).Ameongeza kuwa kutokuwepo kwa mgao na Ruzuku ya pembejeo kutoka Serikalini katika zao la Miwa ingawa Mahitaji ya mbolea na dawa za magugu ni makubwa sana ni changamoto nyingine inayoikabili vyama vya Wakulima wa Miwa katika Bonde laKilombero




Mfanyakazi katika shamba la miwa akiendelea na zoezi la ukataji miwa..(picha juu)Changamoto nyingine ni ukosefu wa Mtaji kuanzisha na kuendeleza Kilimo cha bega kwa bega na Umwagiliaji na kukosa kasi kubwa ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara na mifereji mashambani.Mbali ya changamoto hizo katibu huyo amesema kuwa Ajira kwa Wananchi, Idadi ya Wakulima na pato la Mkulima, limeongezeka baada ya ubinafsishaji wa Viwanda na matumizi ya mfumo Mauzo ya miwa kwa uwiano wa mapato.

Shamba la miwa wilayani kilombero..

KILIMO BORA CHA MUHOGO



O

·        UANDAAJI WA SHAMBA
Zao la muhogo ni  muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia chakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani
Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750  - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.

MBEGU BORA ZA MUHOGO  

     i.   Mbegu bora za muhogoMpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimathibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.                               ·        

                                                       

1 .     Kiroba - Huzaa tani 25 – 30  kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.