Tuesday, March 3, 2015

MAHITAJI YA NG’OMBE ILI AONGEZE MAZIWA


Wape ng’ombe wako lishe kamili, yenye nguvu, protini, na vitamin pamoja na maji ya kutosha.

Kulisha ng’ombe kwa kutumia aina yoyote ya malisho haitoshi kukuhakikishia ng’ombe anakuwa na afya nzuri na kutoa maziwa ya kutosha. Kama ilivyo kwa binadamu, ng’ombe anahitaji mlo kamili. Malisho ni lazima yawe na uwiano sahihi wa viungo.


Mifugo inahitaji chakula kitakachowapa nguvu, protini, madini, na vitamin ili kujenga miili yao, kuzalisha maziwa, na kuzaliana. Wanyama wadogo wanahitaji virutubisho vya kutosha, ili wakuwe na kuongeza uzito. Ng’ombe wa maziwa wanahitaji virutubisho zaidi ili kuweza kuzalisha maziwa kwa wingi hasa katika kipindi cha miezi 3-4 ya mwanzo baada ya kuzaa, wakati ambao uzalishaji wa maziwa unakuwa juu.
Malisho ya kijani ni mlo mkuu kwa mifugo

KUKU WEUSI KUTOKA MALAWI TEGEMEO KWA WAJASIRIAMALI


NA ADAM MALINDA
*Wanakua na kufikia uzito wa kilo 4
UJASIRIAMALI ni jambo jema katika mapambano dhidi ya umasikini, lakini pia ili kuweza kuwa mjasiriamali, yanahitajika maarifa ya ziada, ikiwamo ubunifu katika kuboresha shughuli unazozifanya ili ziwe na tija.
Nilipomtembelea kijana Peter Kitembe nyumbani kwao Mburahati Jijini Dar es Salaam, aliniambia anamiliki kampuni ya kifamilia iitwayo Peace Poultry Farm, ambapo alinisimulia kilichomsukuma kuingia katika ujasiriamali wa kufuga kuku wa kienyeji.

“Nilikuwa katika kampuni moja ya kutengeneza chakula cha kuku ambayo ilinipa changamoto za kimawazo, nikajiuliza, kwa nini nami nisiwe mmoja wa wafugaji wanaoweza kuinua hali ya kipato na kuupiga vita umasikini,” alianza kueleza kijana huyo.

Kitembe alisema amekuwa akisukumwa na hali ya umasikini ambayo Watanzania wengi wamekuwa wakiamka asubuhi na mapema kuwahi maeneo mbalimbali kujitafutia fedha za kujikimu, lakini wakirudi nyakati za usiku wanakuwa hoi, hali inayowafanya baadhi yao kukata tamaa na wengine wanaamua kukaza buti hadi kupata mafanikio.

UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE WAENDELEA KULETA HASARA KUBWA KWA WAFUGAJI WA TANZANIA


Ugonjwa wa homa ya nguruwe unaosababishwa na virusi umeenedelea kuwa tishio kubwa kwa wafugaji wa nguruwe nchini. Ni ugonjwa unaoongoza kwa kuleta madhara makubwa sana kwa wafugaji wa nguruwe kwani unaweza kuteketeza nguruwe wote wa mfugaji ndani ya siku chache. Walaji nao huathirika kwa kukosa kitoweo/kitimoto kwani unapogundulika ugonjwa huu katika eneo moja, basi nji ya kuzuia usisambae maeneo mengine ni kuzuia usafirishaji na uchinjaji wa nguruwe katika eneo lenye ugonjwa au kuwatoa nguruwe kwenda sehemu ambayo haina ugonjwa. 
Jitihada za wataalamu wa mifugo wakishirikiana na serikali (soma kiambatanisho mwisho) hasa katika eneo husika ili kupambana na ugonjwa huu hasa pale unapojitokeza zimekuwa zikifanywa. Wananchi wamekuwa wakihamasishwa ili waweze kushiki vema katika kuhakikisha njia za kuutokomeza ugonjwa zinafanikiwa. Hata hivyo jitihada hizo hazijaweza kuzaa matunda kwani ugonjwa huu umekuwa ukijitokeza karibu kila mwaka katika maeneo mbalimbali ya nchi. Mwaka jana (2012) maeneo ya mikoa ya Mbeya, Rukwa, Iringa (Matukio daima) na Morogoro yalikumbwa na ugonjwa huu. Sambuli zilizochukuliwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Kitivo cha Tiba Mifugo zilithibitisha uwepo wa ugonjwa huu. Mara nyingi ugonjwa huu umekuwa ukianzia maeneo ya Mbeya na Rukwa kisha kuenea maeneo ya Iringa na Morogoro na mara chache kufika Dar es Salaama. Mwaka huu (2013) pia ugonjwa umeripotiwa maeneo ya Sumbawanga (Tarehe 11/4/2013 
Hivi sasa ugonjwa upo maeneo ya Kilimanjaro ukisambaa kuelekea maeneo ya Korogwe na huu unasemekana kutokea maeneo ya Kenya tofauti na ilivyozoeleka kuwa chanzo cha ugonjwa huwa maeneo ya Mbeya na Rukwa. Sampuli zilizopelekwa SUA, Kitivo cha Tiba Mifugo na kufanyiwa uchunguzi kwa njia za kisasa (PCR) umebaini uwepo wa ugonjwa huu. Hii inafanya sasa kuwa na vyanzo viwili ambapo ugonjwa unaanzia na hii ni hatari kwa waafugaji na nchi kwani ugonjwa unaweza kuenea nchi nzima na kuleta hasara kubwa sana kwa wafugaji na taifa kwa ujumla. 








Monday, March 2, 2015

ZIFAHAMU TOFAUTI YA ASALI YA NYUKI WADOGO NA ASALI YA NYUKI WAKUBWA

Asali za NYUKI WAKUBWA na WADOGO zina tofautiana katika mambo kadhaa na hvyo ni muhimu kujua tofauti hizo kabla hujanunua ili kua na uhakika.

NYUKI WADOGO
1. Ni nyepesi zaidi kwani ina kiwango cha maji kuanzia asilimia 24

2. Ina ladha ya UCHACHU ingawa ni tamu sana.
3. Mara nyingi ina rangi ya KAHAWIA ILIYOKOLEA inayoenda kwenye WEUSI

NYUKI WAKUBWA
1. Ni nzito kuliko ya nyuki wadogo kwani ina kiwango cha maji kuanzia asilimia 17 hadi 20.
2. Ni tamu moja kwa moja bila kua na ladha ya uchachu kama nyuki wadogo
3. Ina rangi nyingi kuanzia NYEUPE, NYANO, KAHAWIA ILIYOPOA, KAHAWIA ILIYOKOZA n.k

Hizo ni tofauti za muhimu kuzijua kwani zitakuwezesha kupata asali unayoitaka na kuepuka kuibiwa

Jikinge na Kansa kwa Kula Vyakula Asilia


Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  duniani, ugonjwa  wa  kansa  unatajwa  kuwa  ndio  ugonjwa  wa  hatari  zaidi  pengine  kuliko  ugonjwa  mwingine  wowote  uliowahi  kutokea  katika  historia  ya  mwanadamu. Nchini   Tanzania  pekee  kiasi cha watu 100 hufariki dunia KILA SIKU kutokana na magonjwa ya saratani, hii  ni  kwa  mujibu  wa  taarifa  ya  Taasisi  ya  Saratani  ya  Hospitali  ya  Ocean  Road a  jijini  Dar  es  salaam  kupitia  Mkurugenzi  wake  Dk. Twalib  Ngoma.
Hali ni  mbaya  zaidi katika  nchi  zilizoendelea   ambako  tunataarifiwa  ya  kwamba   kuna  idadi  kubwa  sana  ya  watu  wanaopoteza  maisha  yao  kila  siku  kutokana  na  magonjwa  ya  kansa ambayo  kimsingi  yanasababishwa na  na ulaji wa vyakula tunavyokula kila siku. Mfano  nchini  Marekani  pekee  karibu  theluthi  moja  ya  wagonjwa  wa  kansa  inasababishwa  na  vyakula  wanavyokula  kila  siku, na  hii  ni  kwa  mujibu  wa Taasisi  ya  Saratani  ya  nchini  Marekani. 
Pamoja na kuwepo habari hiyo mbaya na ya kusikitisha ya kupoteza mamia ya ndugu zetu kila siku, kuna habari njema pia kuwa unaweza kabisa kujikinga na ugonjwa huu hatari kwa kula vyakula vinavyostahili na kuepuka vinavyochangia saratani.

Kwa leo hebu tuangalie orodha ya baadhi ya vyakula ambavyo vinaaminika kuwa na uwezo mkubwa wa kupambanana seli zinazosababisha saratani mwilini. Mwenyekiti wa Taasisi ya Kuzuia na Kutibu Saratani, DK. Richard Béliveauwa Chuo Kikuu cha Québec, Montreal Canada, anasema kuwa tafiti zote zinaonesha kuwa kinga ya saratani iko kwenye ulaji wa vyakula vitokanavyo na mimea (Plant-based foods).
Unachotakiwa kufanya ili kuupa mwili wako kinga dhidi ya saratani, kula matunda na mboga za majani za aina mbalimbali kila siku, hasa hizi zifuatazo:

BROKOLI (BROCCOLI)
Brokoli
Hii ni aina fulani ya mboga ya majani, iko kama maua ya maboga au uyoga, inapatikana katika masoko mengi makubwa nchini. Aina hii ya mboga inaelezwa kuwa na kiasi kingi cha kirutubisho aina ya ‘sulforaphane’ ambacho uwezo wake wa kutoa kinga ni mkubwa. Inatoa kinga dhidi ya saratani ya matiti, ini, mapafu, kibofu, ngozi, tumbo na kizazi.

BERI (BERRIES)
Beri
Haya ni matunda maarufu ambayo hujulikana pia kama matunda ya kuongeza damu au ‘matunda damu’ kutokana na kuwa na rangi nyekundu na mengine meusi na kijani. Ulaji wa matunda haya hutoa kinga dhidi ya saratani ya utumbo, koo, mdomo na ngozi.

NYANYA (TOMATOES)
Nyanya
Wengi tunaidharau nyanya na kuipuuzia kwa kutoila katika milo yetu ya kila siku, wakati nyanya ziko nyingi kiasi zingine zinaoza mitaani. Nyanya inaelezwa kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ ambacho kina uwezo mkubwa wa kuzuia saratani ya kizazi ambayo nchini Marekani inaua zaidi ya watu 8,000 kila mwaka, kwa Tanzania hali ni mbaya zaidi. Nyanya huzuia pia saratani ya mapafu, tumbo na kibofu.

KITUNGUU SAUMU (GARLIC)
Saumu
Faida za kitunguu saumu zipo nyingi, lakini miongoni mwa hizo faida ni kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani. Kwa kuweka mazoea ya kula mara kwa mara, kwa kuchanganya katika mlo wako au saladi yako utakuwa umejijengea kinga mwilini. Hutoa kinga dhidi ya saratani ya utumbo, matita, koo na tumbo kwa ujumla.

MAHARAGE (BEANS)
Beans
Wengi wetu hatupendi kula maharage tukiamini ni mboga ya kimaskini! Ukweli ni kwamba maharage ni mboga muhimu na ina faida nyingi mwilini, ikiwemo kutoa kinga dhidi ya saratani ya utumbo na matiti. Utafiti kuhusu faida za maharage uliofanywa na Chuo Kikuu cha Michigan nchini Marekani umethibitisha faida hizo.

Kwa ujumla, magonjwa ya saratani yanaweza kuepukwa iwapo mtu atazingatia ulaji wa mboga na matunda asilia kila siku na kujiepusha na ulaji wa vyakula vya ‘kutengeneza’. Wiki ijayo nitakuletea orodha ya vyakula vinavyosababisha saratani ambavyo unatakiwa kuviepuka kama ukoma!

Asali na Mdalasini

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kutokana na asali. Sasa hivi kuna makala nyingi zilizo andikwa zikielezea kuhusu uwezo wa asali katika tiba ya magonjwa mbalimbali.Warusi na Wafaransa wanafahamika sana katika kufanya utafiti katika maabara kuhusu uwezo wa asali katika tiba mbalimbali.
index
Katika makala hii tutaangalia tiba ya asali na mdalasini na namna ya kuitumia kutibu maradhi mbalimbali (asali tunayoizungumzia hapa ni asali safi yaani asali mbichi ya nyuki wakubwa na wadogo).
YAFUATAYO NI BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIKA KWA ASALI NA MDALASINI:
1. UGONJWA WA VIUNGO/MAUMIVU NA UVIMBE
-Chukua maji kiasi vuguvugu na ongeza mdalasini, unga kijiko cha chai na asali vijiko 2 vya chakula na kuchua sehemu zenye maumivu.
-Vilevile waweza kutengeneza kikombe kimoja cha chai kwa kuweka kijiko kimoja cha unga wa mdalasini na kuongeza asali vijiko viwili vya chakula na kisha kunywa ikiwa ya moto kutwa mara mbili.
2. KUKATIKA KWA NYWELE
-Asali ikichanganywa na mdalasini na mafuta vuguvugu ya mzeituni hutia kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele.
-Tumia mchanganyiko huo vuguvugu kwa kupaka na kusugua kichwani na acha kwa dakika 15 kisha uoshe.
3. UKUNGU WA MIGUU AU FUNGUS
-Changanya kijiko cha chakula cha asali na vijiko viwili vya chai vya mdalasini na acha kwa muda wa nusu saa kisha safisha (rudia hivyo mpaka upone).
4. MAAMBUKIZI KWENYE KIBOFU CHA MKOJO
-Changanya maji ya uvuguvugu na vijiko 2 vya chai vya mdalasini na kijiko1 cha asali huondoa bakteria kwenye kibofu.
5. MAUMIVU YA JINO
-Changanya sehemu tano za asali na sehemu moja ya mdalasini na dondoshea kwenye jino linalouma hadi maumivu yatakapotoweka.
6. VIDONDA VITOKANAVYO NA MAGONJWA YA KULALA KWA MUDA MREFU
-Paka saladi iliyochanganywa asali na mdalasini.Vilevile tumia chai ya roseberry nyekundu kwa kuondoa aina hii ya maumivu.
7. LEHEMU
-Changanya asali safi mbichi vijiko 2 vya chakula na unga wa mdalasini vijiko 2 vya chakula na kikombe cha chai cha maji ya moto na unywe kutwa mara 3
8. MAFUA
-Tumia mchanganyiko wa kijiko 1 cha chakula cha asali vuguvgugu na robo kijiko cha unga wa mdalasini kuondoa chafya na kuvimba koo.
9. UGUMBA
-Asali inaaminika kuamsha hamu ya mapenzi. Wapenzi wa jinsia zote wanashauriwa kunywa walau vijiko 2 vya chakula kila siku kabla ya muda wa kulala. Mdalasini imetumika muda mrefu katika dawa za kichina na kihindi kuongeza uwezo wa uzazi kwa akina mama wenye kuhitaji kuzaa
-Changanya mdalasini na kiasi cha asali na kufanya mgando (paste) na upake kwenye fizi na meno na kuacha inyonywe na kuingia mwilini taratibu na hii ni kwa akina mama wasio na sababu za kimsingi za kuwakosesha kuzaa.
10. MCHAFUKO WA TUMBO
-Asali kwa muda mrefu imetambulika kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko wa tumbo na kichefuchefu. Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali pia hupunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.
11. GESI au ASIDI
-Kula asali pamoja na mdalasini kuondoa mchafuko wa tumbo uletwao na gesi (acid) na huu ni uchunguzi ulio fanywa na Japan na India
12. UGONJWA WA MOYO
-Unaweza kujikinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara kwa kupakaa kama jam wakati wa kula mkate wa ngano wenye nyuzinyuzi nyingi iliyopakwa kijiko 1 cha chakula cha mchanganyiko huo (asali na mdalasini) kila siku.
13. SHINIKIZO LA JUU LA DAMU
-Shinikizo la damu pamoja na matatizo yaambatanayo na maumivu ya kifua na kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya kupata dozi ya mara kwa mara ya asali iliyochanganywa na mdalasini.
14. KINGA YA MWILI
-Kinga yako ya mwili itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini kwa pamoja. Utafiti unaonyesha kuwa hazina kubwa ya vitamini (virutubisho), madini pamoja na mchanganyiko wa mdalasini na asali iondoayo magonjwa na kinga itolewayo na chembechembe nyeupe za damu husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea na bakteria.
15. UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME
-Asali ina historia ndefu ya kuamsha nguvu ya uume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi kutokana na uwezo wake kama kiamshaji/chaji. Asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za mashariki za dunia. Watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba asali inauwezo wa kupelekea mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo mdalasini.
-Katika Afrika na dunia ya kusini mabaharia wamekuwa wakipaka asali katika sehemu zao za nje ya uume ili kuongeza nguvu ya kufanya mapenzi.
16. MATATIZO KATIKA MMENG’ENYO WA CHAKULA
-Kula vijiko 2 vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo huondoa kiungulia na wataalam wanasema asali husaidia kutolewa kwa juisi zinazotumika kuchaguliwa kwa chakula tumboni na mdalasini unaongeza kasi ya kuchaguliwa kwa chakula.
17. FLU
-Tafiti moja ya Kihispania imethibitisha kwamba aina ya dawa iliyopo katika asali ni dawa moja asilia ya ajabu ambayo huharibu vimelea(virus)waletao flu.
18. KUONGEZA UMRI WA KUISHI
-Unaweza kuishi hadi miaka 100 na kufurahia maisha ya afya na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai ya mdalasini na asali.Kutengeneza kinywaji hiki kitamu weka vijiko 4 (vikubwa) vya mdalasini na vijiko 4 vya asali,vikombe 3 vya maji na koroga kwa dk 10 kisha kunywa robo kikombe mara 3 au 4 na hivyo utakuwa na kinywaji kingi.
19. KUONDOA CHUNUSI
-Changanya vijiko 3 vikubwa vya asali na kijiko 1 kikubwa cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi.Uwezo wa asali wa kuua bakteria unafanya uso kuwa wa kawaida katika muda wa wiki 2.
20. KUUMWA NA WADUDU WENYE SUMU
-Changanya asali na mdalasini kisha pakaa moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia tena hadi uvimbe uishe.
21. MAAMBUKIZI KATIKA NGOZI
-Fanya kama ilivyoandikwa namba ishirini hapo juu.
22. KUPUNGUZA UZITO.
-Waweza kufurahia vyakula vyote unavyovipenda kuwa na afya nzuri na kupunguza uzito wa mwili ambao hauhitajiki kwa kula chakula chenye nguvu na ladha nzuri kilichojaa vitu muhimu viwili ambavyo ni asali na mdalasini.
-Unachohitajika kufanya ni kuhakikisha unavitumia vyote kwa kiasi katika mapishi yako.Vilevile wataalam wanasema unaweza kuondoa mabonge ya uvimbe wa nyama nyama nje ya mwili kwa kuanza siku yako kwa kutumia vijiko 2 vikubwa vya asali na kijiko 1 cha mdalasini.Rudia mchanganyiko huo kabla ya kulala.Wataalam wamethibitisha kuwa inapunguza hamu ya kula na kuleta joto mwilini.
23. SARATANI
-Utafiti uliofanyika huko Australia na Japan umeonyesha kuwa asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya magonjwa kwa anaetumia madawa ya kutibu saratani.Katika tafiti iliyofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua saratani ya mifupa na utumbo ambao walikuwa wanatumia kila siku dozi ya asali na mdalasini walionyesha kupata nafuu maradufu kuliko wale waliokuwa wanatumia madawa ya kutibu saratani peke yake.Dr.HIROKI OWATA alisema waliwapa mchanganyiko wa asali na mdalasini kijiko kimoja kutwa mara 3 kwa mwezi 1 na wengine waliendelea kama kawaida.
24. KUONDOA UCHOVU SUGU
-Uko ushahidi kwamba sukari asilia iliyopo katika asali inauwezo wa kuongeza nishati mwilini. Ikitumika ipasavyo sukari hii inaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu.Wataalam wanapendekeza kuchanganya nusu kijiko cha asali katika nusu kikombe cha maji yaliyonyunyiziwa mdalasini kunywewa masaa mawili baada ya kuamka.Rudia kunywa saa 9 alasiri wakati nishati (nguvu) inapoanza kuisha kufuatia ushauri wa Dr. MILSTON ABBOZZA ambaye kazi zake kuhusu asali na mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa.
25. KUVIMBA NYAYO
-Changanya asali na mdalasini katika maji vuguvugu na uchue miguu(nyayo)zilizoathirika baada ya siku ndefu ya kazi au baada ya mazoezi marefu.Rudia kila asubuhi na unawe nyayo kwa maji baridi na vaa viatu.
26. HARUFU MBAYA MDOMONI
-Chukua maji ya vuguvugu changanya na asali na mdalasini kisha sukutua kila asubuhi.Katia Asia ya kusini mashariki watu hula kijiko cha asali na mdalasini ili kuondoa harufu mbaya(halitosis).Wataalam wanaamini uwezo wa kuua bakteria uliopo kwenye asali ndio unaopigana na harufu mbaya toka mdomoni.
27. KUPUNGUA KWA USIKIVU
-Dozi za kila siku za asali na mdalasini hufanya hali ya usikivu kuwa makini kama ilivyogunduliwa na Wagiriki zamani.
-Kutumia mdalasini na asali kutakufanya uonekane kuwa na afya nzuri.
ANGALIZO KUHUSU ASALI FEKI
Ndugu msomaji napenda kukufahamisha kuwa miaka ya karibuni kumejitokeza baadhi ya wafanyabiashara kutengeneza asali feki kwa kutumia maji ya miwa na sukari guru au kuongeza maji na vimiminika vingine ndani ya asali ili wajipatie faida kubwa, endapo utatumia asali ya namna hii basi utakuwa ukiihatarisha afya ya mwili zaidi badala ya kujitibu.
Zifuatazo ni mbinu za kuitambua asali ambayo ni salama kwa maana ya kwamba haijachakachuliwa:
• Weka maji kwenye glasi na kisha mimina asali ndani yake na kwamba ikikaa chini ya glasi bila kuchanganyana na maji basi hiyo ni asali asilia na inakuwa haijachanganywa na chochote.
• Njia ya pili ni kuiweka asali kwenye njiti ya kibiriti na kisha kuiwasha ikiwa njiti hiyo itawaka basi asali haijachakachuliwa kwa kuchanganywa na chochote lakini njiti ya kiberiti isipowaka inakuwa ni feki.
• Njia nyingine ni kuionja bidhaa hiyo na kwamba iliyokachuliwa kwa kuchemshwa hutoa harufu ya moshi tofauti na ambayo ni halisi.
Ikiwa utahitaji asali safi, nzuri,  na ambayo haijachakachuliwa wasiliana na mimi kwenye whatsapp kwa namba hii +255769142586.
Zifuatazo ni picha mbalimbali za Asali na Mdalasini, bonyeza juu ya picha ili kuikuza na iwe kubwa zaidi.

Sunday, March 1, 2015

Tanzania sasa yagundua mbegu mpya ya mahindi

Kilosa. Wataalamu wa kilimo nchini wamegundua aina tatu mpya za mbegu za mahindi ambazo zina uwezo wa kuvumilia ukame.
Mratibu wa Mradi wa Utafiti wa Mahindi Yanayohimili Ukame Afrika (Wema) Tawi la Tanzania, Dk Alois Kulaya alisema ugunduzi huo ni ukombozi kwa wakulima wadogo ambao ndiyo wanaathirika zaidi na ukame.
“Lengo letu wakulima wadodogo wawe na uwezo wa kuzalisha zaidi,” alisema Dk Kulaya.
Alisema katika majaribio yaliyofanyika sehemu mbalimbali nchini, yalionyesha mvua zikinyesha inavyotakiwa mkulima akitumia mbegu hizo anaweza kuvuna wastani wa tani nane kwa hekta moja.
“Lakini kama kutakuwa na mvua kidogo watavuna wastani wa tani nne kwa hekta,” alisema Dk Kulaya.
Dk Kulaya alizitaja mbegu hizo mpya kuwa ni WE2113, WE2109 na WE2112 na wanatarajia zitawafikia wakulima 
“Tunatarajia wakulima wataanza kuzitumia msimu wa kilimo mwaka 2015,” alisema.
Alisema hivi sasa mbegu hizo zinapelekwa kwa kampuni za uzalishaji mbegu, ambazo zitazizalisha na kuzifunga kitaalamu tayari kusambazwa kwa wakulima nchini.
Akizindua mbegu hizo, Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Dk Fidelis Myaka aliahidi Serikali kuendelea kuwa na watafiti wa kilimo ili kufanikisha uboreshaji kilimo nchini.
Dk Myaka alisema tangu Tanzania ianze kuathirika na Mabadiliko ya Tabianchi, wakulima wengi wamekuwa wakiyumba kutokana na kutegemea kilimo cha mvua.
Kwa sababu hiyo, alisema ugunduzi huo utasaidia kuinua hali ya maisha ya wakulima hasa kukabiliana na tatizo la ukame ambalo limekuwa likisababisha ukosefu wa chakula nchini mara kwa mara.
Alisema lengo ni kumkwamua mkulima ili kuongeza uzalishaji.

Saturday, February 28, 2015

MASHINE YA KUKAMULIA MAZIWA YA NG'OMBE

Moja ya mashine za kukamulia maziwa ya NG'OMBE

NG'OMBE JAMII YA ANKOLE


  • Ng'ombe hawa wanapatikana kwa wingi Uganda, lakini pia wapo wilaya zinazopakana na Uganda

Friday, February 27, 2015

Matrekta 3000 kuingizwa nchini

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, PHILIP MARMO
KAMPUNI ya kutengeneza Matrekta iitwayo ARSUS ya nchini POLAND, inatarajia kuingiza Matrekta elfu tatu (3,000) kwa kushirikiana na kampuni ya SUMA JKT ili kukuza sekta ya kilimo hapa nchini

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, PHILIP MARMO ameiambia TBC mjini BERLIN UJERUMANI, kuwa uwekezaji huo mkubwa katika sekta ya kilimo, ni matokeo ya kuvutia uwekezaji wa eknolojia na mitaji kutoka nje unaofanywa kupitia uwakilishi wa diplomasia ya kiuchumi

Sekta ya kilimo nchini Tanzania inaajiri zaidi ya asilimia 85 ya watanzania hususani waishio vijijini.

Changamoto kubwa inayoikabili sekta hiyo ni pamoja na matumizi duni ya zana za kilimo hali iliyoifanya Tanzania kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika kuimarisha sekta hiyo.

Akizungumzia sekta ya utalii, BALOZI PHILIP MARMO amesema kuwa idadi ya watalii kutoka nchi za Ulaya wanaotembelea Tanzania imeongezeka hadi kufikia wastani wa watalii laki nne kila mwaka

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na rais Dokta JAKAYA KIKWETE, imekuwa ikisisitiza mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje kuimarisha utendaji wao wa kazi kwa kuendeleza diplomasia ya kiuchumi badala ya uwakilishi wa kisiasa pekee ili kukuza uchumi wa nchi

COCA-COLA YAZINDUA UPYA MAJI YA DASANI


Kutoka kushoto ni Meneja wa Coca- Cola, Yebeital Getachew, Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola Kwanza, Basil Gadzios, Meneja Masoko wa Coca-Cola Kwanza, Hettiarachchi na Msimamizi wa Masoko Coca-Cola Kwanza, Josephine Msalilwa wakionyesha muonekano mpya wa chupa ya maji ya Dasani baada wakati wa uzinduzi. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola Kwanza, Basil Gadzios akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kuzindua upya maji ya Dasani.
Chupa ya Dasani inavyoonekana baada ya kuzindua upya maji ya Dasani.
Maji ya Dasani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola Kwanza, Basil Gadzios akizungumza wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa ya maji ya Dasani katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi huo.
 Wageni waalikwa.
Wafanyakazi wa Coca-Cola Kwanza wakijumuika na wageni waalikwa katika uzinduzi huo.
 Wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Muonekano wa maji ya Dasani katika chupa mpya.

Wanamuziki wa bendi ya Odama THT wakitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa muonekano wa Chupa mpya ya maji ya Dasani jijini Dar es Salaam.

Wakulima wadogo wabadili mwelekeo wao wa kilimo

SIMU za mkononi ni muhimu zaidi hivi sasa kwa wakulima katika wilaya za Mbeya, Mbarali na Morogoro baada ya kuanza kuzitumia kupata taarifa mbalimbali za masuala ya kilimo.
Matumizi hayo ya wakulima kwa baadhi ya vijiji katika wilaya hizo yanabainisha kuwapo kwa mahitaji ya vipindi vya kilimo katika vyombo vya habari nchini, kutokana na uwepo wa wafuatiliaji wa karibu kwa vipindi hivyo.
Katika baadhi ya vijiji ndani ya wilaya hizo tatu, wakulima hufuatilia vipindi vya kilimo vinavyotolewa katika redio maalumu walizochagua na hutumia simu za mkononi kuwasiliana na waendeshaji vipindi hivyo au wataalamu wao wa kilimo kwa ajili ya kupata taarifa za kilimo anazozihitaji.
Farm radio ni vipindi vinavyorushwa redioni kupitia mradi maalumu wa kuwajengea uwezo wagani katika kuendeleza matumizi ya mikunde kurutubisha udongo nchini, unaotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA).
Kupitia mradi huo, baada ya wagani hao kupatiwa taaluma ya kurutubisha udongo huisambaza kwa wakulima katika maeneo yao kupitia vipindi vya redio na simu za mkononi na kisha, wakulima nao hupata nafasi  kuwasiliana na wataalamu hao kuhusu masuala mbalimbali ya kilimo kupitia vyombo hivyo.
Kwa mujibu wa Ofisa Mradi huo, Christopher Mkondya, wakulima 260 kutoka vijiji vya Nsongwi, Ifiga na Nsongwi Juu, katika Wilaya ya Mbeya Vijijini wameunganishwa na redio ya Baraka FM kupitia vikundi vyao vya wasikilizaji, na kwa Wilaya ya Mbarali wakulima 160 wameunganishwa na redio Bomba FM.
Wilayani Mbarali, mradi huo unafanya kazi na wakulima waliojiunga katika vikundi vya skimu za umwangiliaji kwa ajili ya kilimo cha mpunga, ambazo ni pamoja na Majengo, Maendeleo na Ruanda Manjenje, ambazo zinahudumia vikundi vya Majengo, Hamasa, Maendeleo na Ruanda Manjenje.
Mbali ya Mbeya, mradi huo pia unahudumia wakulima 160 katika Wilaya ya Kilosa wanaounganishwa na redio ya Aboud FM. Wakulima hao ni kutoka kwenye vijiji vya  Kondoa, Chanzuru na Ludewa.
Hata hivyo, wakulima walioko kwenye masafa ya redio hizo nao wamekuwa wakifuatilia, na hivi sasa mahitaji yanaongezeka kwa kasi ambapo wakulima wengi zaidi kutoka vijiji visivyofikiwa na huduma hiyo, wanashinikiza kuingizwa kwenye mradi ili nao wanufaike na elimu ya kilimo bora inayotolewa kupitia vifaa hivyo vya elekroniki.
“Mwitikio wa wakulima ni nzuri, wanashirikishwa katika vipindi, hujisajili kwenye orodha ya simu ili kupata taarifa mpya za vipindi na taarifa za kilimo,” anasema Mkurugenzi wa Baraka FM, Henry Mazunda.
Watayarishaji wa vipindi hivyo wanathibitisha kuwepo kwa mahitaji makubwa ya taarifa za kilimo, ambapo wakulima wenye kubahatika kunasa mawimbi ya vipindi hivyo huwapigia simu kuomba kushirikishwa kwenye mpango huo pamoja na kupatiwa elimu ya mazao mengine zaidi ya mahindi na yale ya jamii ya mikunde.
“Wakulima wengi zaidi kutoka nje ya mradi wanafuatilia na kuuliza maswali, nao wanataka kushirikishwa kwenye mradi,” anasema Lina Mwambungu, mmoja wa watayarishaji wa vipindi hivyo vya wakulima.
Lina anazitaja taarifa zinazopatikana kupitia ujumbe mfupi wa simu kuwa ni pamoja kukumbushwa siku na muda wa kipindi, elimu kuhusu kilimo bora cha mahindi na mazao jamii ya mikunde, wakulima hutuma maswali kuhusu taarifa wanazohitaji au maombi ya kurudiwa kwa kipindi.
Ofisa ugani kutoka Kijiji cha Mantanji, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Abubakar Ramadhan anauona mradi huo kuwa wenye tija kwa wakulima na kubainisha kuwa kwa mkulima mwenye kushiriki kikamilifu kwenye mradi huo huongeza wingi na ubora wa mazao yake.
Anasema shamba lenye mchanganyiko wa mahindi na mikunde huongeza tija katika uzalishaji kutokana na virutubisho vinavyotengezwa na mazao jamii ya mikunde na wakati huo huo hutunza udongo, hauchakai na kupoteza uwezo wake wa kuzalisha.
Katika msimu wa kilimo wa 2012/2013, mkulima kutoka Kikundi Faida Mwandaji, Jela Mandewela alikuwa na ekari moja ya kilimo mseto ambapo alipanda mahindi na maharage, na katika mavuno yake amevuna maharage kilo 300, mahindi ikiwa ni kati ya gunia 22 hadi 26.
Hali hiyo anasema ni tofauti na huko nyuma alipovuna gunia kati ya tatu na saba katika ekari ile ile moja, na wakati huo huo akikosa maharage ambayo alilazimika kuyalima kwenye eneo jingine hivyo kutokuwa na matumizi mazuri ya ardhi.
“Tunapata elimu kutoka kwa ofisa ugavi na vipindi vya redio, tunarekodi mambo yetu ya kilimo, tunatumia simu kuwasiliana na wataalamu wetu na watangazaji,” anasema Mandewele kisha anaongeza akisema; “redio inatusaidi kupata elimu, tunatambulika na watu, wanatusikiliza.”
Rozina Mohamed kutoka Kijiji hicho cha Mantanji anakielezea kilimo mseto kuwa na faida zaidi kwao ambapo anasema tangu aingie kwenye kilimo hicho ameweza kuongeza kipato cha familia yake na sasa anamudu kusomesha watoto wake walioko shule za sekondari.
Manufaa mengine aliyopata ni pamoja na kuezeka bati kwenye nyumba yake, kuweka maji ya bomba na amenunua mifugo ikiwemo ng’ombe na mbuzi, akisisitiza kwamba kilimo kina faida kuliko uchuuzi.
Hata hivyo mradi huo unakabiliwa na changamoto kubwa ya mahitaji kuzidi uwezo uliopo sasa. Mradi unaelekeza darasa moja la maofisa ugani kuwa na watu 40 kwa chuo, lakini kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji wamejikuta wakifika hadi 70 lakini wakihudumiwa na rasilimali zile zile za watu 40.
Vyuo vinavyohusika na utoaji elimu hiyo kwa wagani ni MATI Uyole na Igurusi vilivyopo mkoani Mbeya na kile cha Ilonga mkoani Morogoro.
Katika mfumo wa uendeshaji mradi huo, kila chuo kimekuwa kikihudumia vijiji vitatu vinavyokizunguka na kwamba ni wakulima wenyewe ambao huchagua redio ambazo wangependa zitumike kuwarushia matangazo hayo.
Mkondya anasema, uandaaji wa vipindi hivyo hufanywa kwa kushirikiana kati ya wakulima, wagani na watangazaji ambao huwatembelea wakulima kwenye vijiji vyao na kuandaa nao vipindi. 
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/wakulima-wadogo-wabadili-mwelekeo-wao-wa-kilimo#sthash.O55W8xaH.dpuf

Thursday, February 26, 2015

FAIDA ZA UFUGAJI WA NG'OMBE

FAIDA ZA UFUGAJI WA NG'OMBE

Ufugaji wa ng'ombe umekuwa ukifanywa tangu enzi za mababu zetu na haiwahi tokea mfugaji kujua kwa nini anafanya ufugaji. Sababu kubwa ni faida ziletwazo na ufugaji, ng'ombe kwa mfano amekuwa akimletea mfugaji faida zifuatazo:

1. Hutoa Nyama
Nyama ya ng'ombe ni chanzo kizuri cha protini kwa binadamu na kila siku duniani kote huchinjwa nyama ya ng'ombe na huliwa na asilimia kubwa sana ya binadamu duniani. Mabucha mengi makubwa duniani ni kwa ajili ya uchinjaji wa ng'ombe na pengine ndo mabucha ya kwanza kuanzishwa. Hapa Tanzania machinjio yote makubwa ni kwa ajili ya ng'ombe. Hii inaonyesha namna gani nyama ya ng'ombe huhitajika na binadamu.
Nyama ya ng'ombe ikiwa imening'inizwa

Banda bora la kufugia ndama

Banda la ndama wakubwa upande wa mbele kukiwa na ndoo kwa ajili ya chakula.
Ndama wamepumzika ndani ya banda lao

KILIMO KWANZA: KILIMO CHA KUTUMIA JEMBE LA KUKOKOTWA NA NG'OMBE

  • Ulimaji huu wa kutumia jembe linalokokotwa na ng'ombe ni kilimo cha tangu enzi za mababu, na kiasi kikubwa ndicho kimekuwa kikitumiwa na wakulima wadogo ukiachilia mbali wale wanaotumia jembe la mkono. Hii ni faida mojawapo anayoipata mfugaji wa ng'ombe katika kujiongezea kipato kinachosaidia maisha yake. Pengine upandaji wa mazo kwa kufuata mistari inayotengezwa na jembe la kukokotwa na ng'ombe ndio unaopaswa kuboreshwa kwa kupanda kwa njia ya mistari inayonyooshwa na kamba.

Wakulima wa kahawa KAGERA washauriwa kujiunga vyama vya ushirika

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya MULEBA Mkoani KAGERA limeshauri wakulima wa zao la kahawa wilayani humo kujiengua kutoka katika Chama cha Ushirika mkoani KAGERA (KCU), na kuunda ushirika wao. 

Katika kikao hicho baadhi ya madiwani wamesema KCU hakijafanya jitihada za kumkomboa mkulima, ikiwa ni pamoja na kumpatia bei nzuri hususani ya zao la kahawa na hivyo kusababisha mkulima kujitafutia masoko nje ya nchi ili kujipatia unafuu wa bei. 

Azimio hilo limetokana na na taarifa ya mapato na matumizi iliyosomwa mbele ya madiwani hao na Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo GEORGE KATOMERO , kuwa halmshauri hiyo imeshindwa kukusanya asilimia hamsini ya mapato ya ndani kama makisio ya nusu mwaka, kutokana na sababu kadhaa ikiwemo usafirishwaji wa magendo ya kahawa nje ya nchi. 

Hoja ya njia ipi itumike kuzuia magendo ya kahawa ikawasilishwa na baadhi ya madiwani ,wengi wao wakidai sababu kubwa ni bei ya chini inayotolewa na Chama kikuu cha ushirika mkoani Kagera (KCU) 

Katika mkutano Mkuu wa Chama cha ushirika mkoani Kagera (KCU) Mwenyekiti wa Chama hicho FRANK MUGANYIZI amekiri kuwepo kwa bei ndogo katika soko la kahawa ,lakini Mkuu wa Mkoa wa Kagera JOHN MONGELLA akitoa ilani kwa wale wote wanaojihusisha na biashara ya magendo ya kahawa kuwa mkono wa sheria itawakabili. 

Licha ya Hivi karibuni Chama cha Msingi MAGATA KURUTANGA kilichopo wilayani MULEBA, kujiondoa kutoka chama kikuu cha ushirika mkoani KAGERA (KCU)Madiwani hao wanataka kuwepo na muundo wa chama kikubwa cha ushirika kitakachojumuisha wakulima wote kutoka katika wilaya hiyo.

Serikali yatenga Sh. Bil. 30 kuwalipa wakulima.

Na Mkombe Zanda,
Mbeya.

Serikali imetenga shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kuwalipa wakulima waliouza mazao yao kwa Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula NFRA kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema fedha hizo zitalipwa kwa Wakulima katika awamu mbili za shilingi bilioni 15 ili kumaliza malalamiko yanayotokana na kuchelewa kwa malipo hayo.

Hayo yalibainishwa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda, katika siku ya kwanza ya ziara ya wiki moja mkoani Mbeya akiwa wilayani Mbarali, ambapo pia alipata fursa kufungua maabara za sayansi katika shule ya sekondari ya Igomelo na kusomewa taarifa ya kazi ya wilaya hiyo.
Katika mkutano wa hadhara, Waziri Mkuu alibainisha kuwa Serikali imetenga shilingi Bilioni 30 kwa ajili ya kuwalipa wakulima waliouza mazao yao kwa Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula, NFRA.

Kuhusu mgogoro wa mpaka unaotenganisha Hifadhi ya Bonde la Ihefu na makazi ya watu wilayani Mbarali, Waziri Mkuu amesema Serikali itapitia upya sheria ndogo inayohusu mpaka huo ili kuondoa kasoro zilizopo.

Katika kukabiliana na uhaba wa Walimu wa Sayansi, Pinda, alisema Serikali imeongeza ajira za wakulimu hao.

Hii ni ziara ya kwanza kwa Waziri Mkuu Pinda mkoani Mbeya kwa mwaka huu.

UFUGAJI KWA UJUMLA


Ufugaji : ni neno linalotumika kumaanisha wanyama wanaofugwa na binadamu kwa malengo ya kumpatia chakula au faida Fulani. Mifugo inaweza kufugwa kwa ajili ya kukidhi mahitaji madogo madogo au ufugaji wa faida wenye kuinua uchumi wa mfugaji. Wanyama wanaoweza kufugwa na binadamu ni pamoja na ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, kuku, bata na aina zake, njiwa, punda, farasi, kware, kanga, ngamia, na mbogo maji. Mbwa nap aka hufugwa na binadamu kwa ajili ya kumsaidia ulinzi lakini pia siku hizi hufugwa kama rafiki wa binadamu


MADHUMUNI YA UFUGAJIYapo madhumuni makubwa mawili yanayoweza kumvuta mtu fulani apende kufuga;
a) Thamani ya kiuchumi itokanayo na ufugajii.     Nyama- Nyama ni muhimu kwa ajili ya kupata protini na nguvu, mfugaji akiuza nyama au mfugo wenyewe ukiwa mzima anajipatia kipato.ii.    Maziwa na mazao yake- Kut okana na ufugaji wa ng’ombe, mbuzi, kondoo, ngamia na mbogo maji, mfugaji anaweza kujipatia maziwa na mazao yake kama mtindi, jibini, na siagi/samuli. Maziwa na mazao haya anaweza kuyatumia katka familia lakini pia akauza kujiongezea kipato chake.iii.   Nyuzi- baadhi ya mifugo manyoa yake yanaweza kutumika kwa kazi mbalimbali kama kutengenezea nguo mfano manyoa ya kuku, mbuzi, kondoo, ng’ombe. Hivyo yakiuzwa yanasaidia kuongeza kipato.iv.  Mifupa, pembe na Ngozi- Ngozi ya mifugo kama ng’ombe, mbuzi na kondoo hutumika kutengeneza viatu, nguo. Mifupa hutumika kutengenezea viatu, gundi, kuwambia ngoma, na chakula cha mifugo, wakati pembe hutumika kwa mabaragumu yanayopigwa kwenye ngoma za jadi, kutoa taarifa fulani katika jamii.v.    Mbolea ya mifugo- Hutumika mashambani kuongeza uzalishaji, kukandikia nyumba, kuchomea matofali na vyungu, pia hutumika kama kuni, na kuzalishia gesi. Mbolea inaweza ikauzwa na kumpatia mfugaji pesa kwa matumizi yake mbalmbali.vi.  Nguvu kazi-Mifugo mingi hutumiwa  na binadamu kumsaidia kufanya kazi ulani, mfano ngombe na punda  hutumika kwa ajili ya kulima, kukota mikokoteni, kuvuta miti na mizigo mingine. Punda, farasi na ngamia hutumika kama usafiri wa kusafisha watu au mizigo kutoka sehemu moja kwenda nyingine au wakati mfugaji anahama kutoka eneo moja kwenda eneo jingine.


b) Thamani isiyo ya kiuchumii.     Ufahari- Kuwa na mifugo kunamletea mfugaji ufahari na hivyo kumfanya awe na amani kwani hana hofu hata akiwa na matatizo anayosehemu ya kukimbilia kwa haraka bila ya kupata msongo wa mawazo.ii.    Kuwa sehemu ya familia- Wapo watu wanaofuga wanyama kwa lengo la kuwa marafiki wa karibu au kuwa sehemu ya familia, wanyama wanaofugwa kwa jinsi hii hawauzwi wala hawaliwi. Tena mnyama akiugua au kufa huduma yake inafanana sana ya mwanadamu mwenye mfugo hupata huzuni.iii.   Imani ya kidini- Wapo wanaofuga wanya kwa lengo la kuabudu kama miungu wao, mfano dini ya kihindi huabudu ng’ombe. Lakini pia mifugo hutumika kwenye imani za kimila wanapofanya matambiko au kutoa kafara kwa waganga wa kienyeji au wanapofanya mazindiko ya mali, mashamba, nyumba, au magari. Wanya wamekuwa wakitumika kwa kazi hii tangu karne nyingi zilizopiata.iv.  Kusafisha mashamba- Mifugo pia hutumika kwa lengo la kusafisha mashamba kwa kulishia mifugo kwenye mashamba ili yawe safi. Wakati mifugo inakula nyasi na majani ya shamba pamoja na kukanyaga huasidia kuua magugu na kuzuia yasiote. Njia hii si nzuri kwa upande mwingine kwa vile huharibu pia virutubisho vya shamba na kufanya litoe mazao duni.


AINA ZA UFUGAJIZipo aina kuu mbili za ufugaji, ufugaji wa kuhamahama na ufugaji wa kutulia eneo moja. Wafugaji wa jamii ya kuhamahama huhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa lengo la kuatafuta chakula, maji na kukimbia magonjwa ya mifugo. Uhamaji huu hutegemea kipindi cha mwaka, wakati wa mvua wafugaji husogea karibu na sehemu ambapo kuna makazi ya kudumu ya watu wengine kwa ajili ya urahisi wa mahitaji mengine ya kijamii. Wakati wa mvua huwa hakuna shida ya maji na chakula maeneo mengi. Wakati wa kiangazi maeneo haya majani huwa yameisha nap engine maji hakuna, hivyo huhama kwenda sehemu ambapo watapata mahitaji hayo. Ufugaji wa aina hii hufanywa kwa ng’ombe wa kienyeji tu kwani ndio wanaoweza kuvumilia joto, magonjwa na shuruti nyingine nyingi zinazopatikana wakati wa uhamaji. Wafugaji wanaofanya ufugaji huu ni wa jamii ya kimasai, kisukuma, na kibarbeiji, hawa wameshazoea kuishi porini na hawanatabia ya kujenga makazi ya kudumu kwa sababu ya kuhamahama. Hasara kubwa ya ufugaji huu ni kukosa huduma za msingi kama shule, hospitali, makanisa na misikiti. Lakini kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa, ongezeko la watu linalofanya maeneo ya kulishia kupungua kunafanya wafugaji hawa sasa wanze kuhama kutoka aina hii ya ufugaji kuingia ile ya kutokuhamahama.Ufugaji usio wa kuhamaha unafanywa na watu wanaoishi sehemu moja kama kijiji na kufanya ufugaji wao ndani ya jamii. Hawa hufuga mifugo yao kwa kuifungia ndani muda wote na kuwaletea majani au kwa kuwachunga mchana na jioni kuwafungia ndani. Wale wanaowafungia ndani wanahitaji wakati mwingine kulima majani yatakayotumika kuwalisha mifugo yao. Hapa ufuagaji wa kisasa na wa kienyeji hufanyika kwa njia zote mbili, kuwafungia ndani muda wote au usiku tu. Huu ndiyo ufugaji wenye tija, kwani mfugaji atakuwa na mifugo michache na ataihudumia kirahisi zaidi kwa kuwapa huduma zinazotakiwa.