Tuesday, March 3, 2015

UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE WAENDELEA KULETA HASARA KUBWA KWA WAFUGAJI WA TANZANIA


Ugonjwa wa homa ya nguruwe unaosababishwa na virusi umeenedelea kuwa tishio kubwa kwa wafugaji wa nguruwe nchini. Ni ugonjwa unaoongoza kwa kuleta madhara makubwa sana kwa wafugaji wa nguruwe kwani unaweza kuteketeza nguruwe wote wa mfugaji ndani ya siku chache. Walaji nao huathirika kwa kukosa kitoweo/kitimoto kwani unapogundulika ugonjwa huu katika eneo moja, basi nji ya kuzuia usisambae maeneo mengine ni kuzuia usafirishaji na uchinjaji wa nguruwe katika eneo lenye ugonjwa au kuwatoa nguruwe kwenda sehemu ambayo haina ugonjwa. 
Jitihada za wataalamu wa mifugo wakishirikiana na serikali (soma kiambatanisho mwisho) hasa katika eneo husika ili kupambana na ugonjwa huu hasa pale unapojitokeza zimekuwa zikifanywa. Wananchi wamekuwa wakihamasishwa ili waweze kushiki vema katika kuhakikisha njia za kuutokomeza ugonjwa zinafanikiwa. Hata hivyo jitihada hizo hazijaweza kuzaa matunda kwani ugonjwa huu umekuwa ukijitokeza karibu kila mwaka katika maeneo mbalimbali ya nchi. Mwaka jana (2012) maeneo ya mikoa ya Mbeya, Rukwa, Iringa (Matukio daima) na Morogoro yalikumbwa na ugonjwa huu. Sambuli zilizochukuliwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Kitivo cha Tiba Mifugo zilithibitisha uwepo wa ugonjwa huu. Mara nyingi ugonjwa huu umekuwa ukianzia maeneo ya Mbeya na Rukwa kisha kuenea maeneo ya Iringa na Morogoro na mara chache kufika Dar es Salaama. Mwaka huu (2013) pia ugonjwa umeripotiwa maeneo ya Sumbawanga (Tarehe 11/4/2013 
Hivi sasa ugonjwa upo maeneo ya Kilimanjaro ukisambaa kuelekea maeneo ya Korogwe na huu unasemekana kutokea maeneo ya Kenya tofauti na ilivyozoeleka kuwa chanzo cha ugonjwa huwa maeneo ya Mbeya na Rukwa. Sampuli zilizopelekwa SUA, Kitivo cha Tiba Mifugo na kufanyiwa uchunguzi kwa njia za kisasa (PCR) umebaini uwepo wa ugonjwa huu. Hii inafanya sasa kuwa na vyanzo viwili ambapo ugonjwa unaanzia na hii ni hatari kwa waafugaji na nchi kwani ugonjwa unaweza kuenea nchi nzima na kuleta hasara kubwa sana kwa wafugaji na taifa kwa ujumla. 








No comments:

Post a Comment