ZAO la mhogo ni miongoni mwa mazao yasiyopewa kipaumbele kikubwa hapa nchini, huku likitajwa kuwa ni sawa na dhabu nyeupe inayooza ardhini.
Msimu wa kilimo unapowadia wakulima wengi huanza kufikilia kulima mahindi kama zao la chakula na biashara kisha hufuatiwa na mazao mengine ya biashara, mhogo ukionekana kama la ziada.
Hata hivyo imebainika kuwa kama wazalishaji wa viwanda wakiamua kukaa na wakulima wakapeana elimu ya kusindika unga wa mhogo unaotakiwa kwenye viwanda vyao Tanzania inaweza kumaliza tatizo la njaa na umasikini kwa wakati mmoja.
Hiyo ni kutokana na utafiti uliofanyika nchini Italia kuhusiana na zao hilo na kuonyesha kuwa zao la muhogo linaweza kutumika kwa matumizi mbalimbali zaidi ya 300 yakiwemo chakula na bidhaa kama tambi, bisukuti, mafuta ya lishe, keki, sabuni ya unga, kuni, mboga, huksi pamoja na bidhaa nyingine nyingi.Matumizi yote yaliyotajwa yanatakikana hapa nchini na viwanda vyake vipo, lakini cha kusikitisha kama sio usaliti wa wenye viwanda hivyo wamekuwa wakiagiza unga huo kutoka nje ya nchi.
Lakini pia wakati zao hilo kwa wananchi walio wengi linachukuliwa kama zao la kinga ya njaa hali iliyosababisha mikoa yenye chakula kingi kuliacha likiozoea shambani wakisubiri kipindi cha njaa imefahamika kuwa linaweza kumuingizia mkulima kipato cha haraka kama soko lake likitangazwa vizuri.
“Kikwazo kikubwa sio upatikanaji wa unga wake bali ni namna wanavyouandaa ili sumu yake iweze kutoka ndani ya masaa 12 uwe umepatikana unga mweupe”anasema Julias Wambura ambaye ni msambaza wa nafaka kwenye masoko.
No comments:
Post a Comment