Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi imesema ukosefu wa malisho na maji umefanya mifugo mingi kuhamia katika mikoa ya MOROGORO, PWANI na NYANDA ZA JUU ambayo yanafaa kwa shughuli za kilimo na hivyo kusababisha migongano ya wakulima na wafugaji.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo KAIKA SANING’O OLE TELELE amemesema hayo wakati wa ufunguzi wa siku ya Nyanja za malisho iliyofanyika mjini MOROGORO ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Naibu waziri huyo pia akawataka watafiti wagani na mameneja wa mashamba ya mbegu za malisho kuhakikisha wanaweka mkazo katika kufanya tafiti na kutoa ushauri unaolenga uendeshaji na uboreshaji nyanda za malisho ili kuongeza tija na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa kuhamahama kwa wafugaji ili kuondoa migongano kati ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi hususani wakulima.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro akizungumza kabla ya kumakaribisha mgeni rasmi amesema licha ya kuwepo kwa wataalamu na watafiti katika sekta ya mifugo wanao jishughulisha na uboreshaji katika nyanda za malisho bado kunachangamoto .
Nae ANGELO MWILAWA kutoka taasisi ya utafiti na uhifadhi wa mifugo anasisitiza umuhimu wa matumizi ya matokeo ya tafiti mbalimbali zinazotolewa na wataalamu ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima kwa wafugaji na wakulima.
No comments:
Post a Comment