Friday, March 6, 2015

UFUGAJI WA SAMAKI: VITUO VYA SERIKALI KWA AJILI YA KUPATA VIFARANGA WA SAMAKI


Hawa ni vifaranga wa samaki kwa ajili ya kupandikiza kwenye bwawa la samaki.
Serikali ya Tanzania ina vituo vya ukuuzaji wa samaki maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa samaki, ajira na kipato kwa wananchi wake. Vituo vya kuzalisha vifaranga wa maji baridi nchini ni Kingolwira (Morogoro), Ruhila (Songea), Mtama (Lindi), Nyamirembe (Chato) na Mwamapuli (Igunga). Serikali bado inaendelea na jitihada zake za kujenga na kuviimarisha vituo vya Chongoleani (Tanga), Nyamirembe (Chato), Kingolwira (Morogoro), Ruhila (Songea), Karanga (Moshi) pamoja na kuanzisha vituo vipya vya Chihiko (Mtwara) na Kibirizi (Kigoma). Yote hii ni kutaka kuongeza upatikanaji wa vifaranga vya samaki kwa wafugaji. Kama unafuga au unadhamiria kufuga basi fika karibu na vituo hivi ili uweze kupata ushauri wa namna ya kufanya ufugaji wenye tija na ununue vifaranga wa samaki kwa ajili ya kuanza ufugaji wako. 
Huu ni mtambo rahisi wa kuzalisha vifaranga wa samaki iliotengenezwa na Watanzania. Mtambo huu upo katika kituo cha uzalishaji wa samaki cha Serikali kilichopo Kingolwira (Morogoro).

1 comment:

  1. Naomba mawasiliano ya kituo cha uzalishaji samaki kingolwira

    ReplyDelete