Friday, March 6, 2015

UFUGAJI WA KUKU: ULISHAJI WA CHAKULA KWA KUKU NA MATUNZO MENGINE


Kama unafugia ndani kwa kuwa unaeneo dogo basi kitu kikubwa cha kukumbuka ni kuwapa majani kwa njia hii ya kuning'iniza. Njia hii inasaidia sana hata kupunguza tabia mbaya ya kuku ya kudonoa ambayo inaweza kuwapelekea kuku wapoteze maisha.

Namna nzuri ya kulisha na kunywesha kuku maji ndani ya banda lako. Chombo cha chakula na maji lazima kiwe juu kidogo ili kuzuia kuku waichezea chakula au maji. Kuku wanatabia ya kupanda juu ya chakula au maji na hivyo kuchafua kwa miguu yao au hata kwa kinyesi chao. Hivyo tabia hii huzuiwa kwa kuweka vyombo kama inavyooneka kwenye picha hapo juu.




Kuku hawa wamewekwa ndani ya uzio ili wajitafutie chakula wenyewe ikiwa ni pamoja na kula majani ya kijani. Kuku hawa wamefugwa kwa njia ya nusu asili. Wanajitafutia chakula chao wenyewe lakini ndani ya fenzi na hupewa ziada kidogo pamoja na maji.

Kuku hufurahia sana kucheza kwenye mchanga wakipewa uhuru na nafasi hiyo, huchimba kwa miguu yao na kutengeneza bonde ambao hulala. Hupenda kufanya hizi hasa wakiwa wanaotea jua ambalo si kali kiasi cha kuwachoma. Pamoja na kula wadudu wanaowaona udongoni kuku hawa hunufaika na vitamini D inayozalishwa mwilini baada ya kuota jua. Kumbe mwanga na jua/joto pia vinaumuhimu sana kwa ufugaji wa kuku. Kama unafanya ufugaji wa ndi zingatia kuwapa joto, hewa na mwanga wa kutosha ili kuku wako waweze kukupa maza
o unayo tarajia.

No comments:

Post a Comment