Wednesday, March 4, 2015

Mvuvi katika kisiwa cha Yozu wilaya ya Sengerema Aibuka na Toyota IST

Kaimu Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa wa Airtel Bwana David Wankuru akimkabithi gari aina ya Toyota IST bwana Kijiji Gweso ambaye ni Mvuvi na mkazi wa wilaya ya Sengerema Mwanza mara baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel,Bi. Jane Matinde.
Mshindi wa gari kupitia promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Bwana Kijiji Gweso akifungua gari mara baada ya kukabidhiwa gari na Airtel mara baada ya kuibuka mshindi, Bwana Gweso ni Mvuvi na mkazi wa wilaya ya Sengerema Mwanza. akishuhudia ni Kaimu Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa wa Airtel David Wankuru.
Mshindi wa gari kupitia promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Bwana Kijiji Gweso akiwa ndani ya gari yake mara baada ya kukabidhiwa gari na Airtel mara baada ya kuibuka mshindi, Bwana Gweso ni Mvuvi na mkazi wa wilaya ya Sengerema Mwanza.



Kaimu Katibu wa Wilaya ya Sengerema Bwana Aaron L Laizer ( wa pili kushoto) akimkabithi gari aina ya Toyota IST bwana Kijiji Gweso ambaye ni Mvuvi na mkazi wa wilaya ya Sengerema Mwanza mara baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde na Kaimu Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa wa Airtel Bwana David Wankuru.

Mkazi wa wilaya ya sengerma na mvuvi katika kisiwa cha Yozu bwana Kijiji Gweso Jana amekabithiwa gari aina ya Toyota IST na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mara baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Airtel yatosha zaidi.

Akiongea wakati wa halfa ya kukabithiwa gari lake Bwana kijiji Gweso alisema” nilipopigiwa simu na Airtel nilipuuzia sikuamini kabisa kama nimeshinda gari mpaka ndugu zangu waliponipigia na kunihakikishia kuwa mimi nimetangazwa mshindi ndipo nilipoenda ofisi za Airtel na kukuta kweli nimejishindia. Mimi ni mvuvi na mke na watoto wawili na nilinunua kifurushi cha Airtel yatosha cha mia tano tu na furahi sana kushinda gari hili kupitia promosheni hii”.

“Sijawahi kumiliki gari hivyo usafiri huu utanisaidia katika shughuli zangu za uvuvi, za kifamilia na kiuchumi kwa ujumla, nachukua fulsa hii kuwaambia watanzania wenzangu waamini kuwa Airtel inatoa magari na kwamba wao pia wanaweza kuwaibuka washindi. Nawashukuru sana Airtel kwa kuboresha maisha yangu na yawatanzania wengine walioshinda kama mimi”aliongeza Gweso.

Akiongea wakati wa kukabithi gari kaimu katibu wa wilaya ya sengerema bwana Aaron L Laizer alisema” nampongeza sana bwana Kijiji Gweso kwa kuibuka mshindi, ushindi huu umetuthihirishia wakazi wa sengerema kuwa promosheni hii ya ya ukweli na zawadi zinatolewa. Tunawashukuru sana Airtel kwa kutoa huduma bora za mawasiliano nchini ambazo zimerahisisha shughuli za kiuchumi, kijamii na kiusalama lakini pia kuanzisha promosheni inayowazawadia wateja wake, na kwa wananchi wa sengerema na wa mwanza kwa jumla hii nifulsa kwetu tuendelee kutumia huduma za Airtel na kupata nafasi ya kushinda”.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa kanda ya Airtel Bwana David Wankuru alisema “ promosheni hii bado inaendelea mpaka sasa ni washindi 24 tumeshapatikana , magari bado yapo hivyo natoa wito kwa wakazi wa kanda yangu na watanzania kwa ujumla kuweza kushiriki. Tunafurahi kuwa na washindi wane mpaka sasa kutoka katika kanda ya ziwa washindi hawa ni pamoja na Bi Ester Mathias Mashauri muuguzi bugando, Bi kajala kokutima said mkulima na mkazi wa bukoba, Seleman Daudi Onesmo mkazi wa nyakato Mwanza na leo tunamkabithi gari bwana Kijiji Gweso mkazi wa Sengerema’.

Wankuru aliongeza kwa kusema “kujishindia unatakiwa kujinga na kifurushi chochote cha Airtel yatosha cha siku, wiki au mwenzi kwa kupiga *149*99# au kununua vocha ya Airtel yatosha au kwa kununua kupiita huduma ya Airtel Money, baada ya kununua kifurushi chako namba yako moja kwa moja itaingizwa kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia gari aina ya Toyota IST kila siku”.

Promosheni ya Airtel yatosha Zaidi ilizinduliwa na kampuni simu za mkononi ya Airtel Mwanzoni mwa mwenzi wa Februari, watanzania wengi kutoka katika mikoa mbalimbali wameweza kujishindia magari na kubadili maisha ya kupitia promosheni hii. Magari 24 yameshapata washindi toka promosheni hii ianze hadi sasa.

No comments:

Post a Comment