Friday, March 6, 2015

JKT laanza kutoa mafunzo ya ufugaji nyuki

Mkuu wa wilaya ya TABORA SULEIMAN KUMCHAYA
Jeshi la Kujenga Taifa -JKT limeanza kutekeleza agizo la Waziri Mkuu MIZENGO PINDA kwa kutoa mafunzo ya ufugaji nyuki kwa askari wa kudumu wa vikosi mbali mbali vya JKT na JKU kwa lengo la kusambaza ujuzi huo na kuongeza uzalishaji wa Asali nchini. 

Jeshi hilo kupitia kikosi chake cha 823 MSANGE-TABORA limeanza kuendesha mafunzo kwa awamu kwa Askari wa vikosi vya JKT, JKU ZANZIBAR na Wananchi ili kuwapatia ujuzi wa kufuga nyuki kisasa na kuzalisha Asali bora. 

Askari na raia waliopatiwa mafunzo wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuwafundisha askari na wananchi wenzao katika maeneo yao jinsi ya kufuga nyuki kisasa na kupata Asali bora. 

Mkufunzi mkuu wa JKT Kikosi cha 823 MSANGE-TABORA Luteni HANS MWAKANYAMALE na Mkuu wa kikosi hicho Luteni kanali AHMED ABBAS AHMED wamesema madhumuni makubwa ya kuendesha mafunzo hayo ni kusambaza ujuzi huo kwa vikosi vyote vya Tanzania bara na visiwani. 

Akifunga mafunzo hayo, Mkuu wa wilaya ya TABORA SULEIMAN KUMCHAYA amesema Asali ni mali na ni zao lisilotumia gharama kubwa.

No comments:

Post a Comment