Tuesday, March 3, 2015

Kamati ya mbegu ya taifa yaidhinisha aina 65 za mbegu

Naibu Katibu Mkuu wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika,YAMUNGU KAYANDABILA
Kamati ya Taifa ya mbegu nchini imeidhinisha aina 65 za mbegu mbali mbali ambapo kwa upande wa mahindi kutakuwa na aina KUMI na SITA zinatarajia kuleta mabadiliko makubwa kwa wakulima.

Naibu Katibu Mkuu wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika YAMUNGU KAYANDABILA, akitangaza mbegu hizo jijini ARUSHA, amesema lengo ni kuongeza tija na kipato kwa wakulima kutokana na kupata mbegu zenye uhakika.

Wataalamu wa masuala ya mbegu ambao wako katika kamati ya Taifa ya mbegu wamekutana jijini ARUSHA kutangaza mbegu mbele ya waandishi wa habari ambazo zinataraji kuleta mabadiliko makubwa kwa wakulima.

Naibu Katibu Mkuu toka wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika,YAMUNGU KAYANDABILA,amesema iwapo wakulima wakitumia kikamilifu mbegu hizo wataweza kuvuna kwa wingi bila kupata hasara kutokana na mbegu walizozitangaza kuwa na uwezo mkubwa.

Kaimu Murugenzi mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa mbegu nchini TOSCI Dk HAMISI MTWAENZI amekiri kuwepo kwa mbegu bandia ambazo hudhoofisha juhudi za wakulima.

Aina hizo za mbegu zitaanza kuzalishwa na mawakala wa mbegu nchini ambapo mbegu zinatarajiwa kuwafikia wakulima kuanzia mwaka 2016 hadi 2017.

No comments:

Post a Comment