Migogoro ya wakulima na wafugaji imekuwa ikijitokeza mara kwa mara hapa nchini na sehemu nyingine nchini Afrika. Sababu kubwa imekuwa ni kugombania ardhi na hasa uhalali wa kutumia ardhi kwa manufaa ya mfugaji au mkulima. Migogoro hii imekuwa ikisababishwa mara nyingi na wafugaji na kwa upande mwingine serikali ikichangia. Wafuagji wamekuwa wakihamahama kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa manufaa ya kutafuta malisho na maji au kukimbia maeneo yenye vijimelea vya magonjwa kwa wingi vinavyoweza kusababisha mifugo yao kutoweka. Wakulima nao waekuwa wakitafuta maeneo mazuri kwa ajili ya kuzalisha mazao yatakayo wasaidia wajipatie chakula na kipato cha kuwa kimu maisha yao. Katika harakati zote hizi za mfugaji na mkulima, kwa sehemu moja au nyingine zimekuwa zikiwagonganisha na kupelekea kwenye migogoro baina ya wafugaji na wakulima.
Wakati wafugaaji wakihaha kutafuta malisho mazuri mifugo yao wakati fulani imekuwa ikipita kwenye mashamba ya wakulima. Wakulima nao wamekuwa wakienda kulima kwenye maeneo ambayo wafugaji wamekuwa wakiyatumia tangu enzi. Hii imesababisha mtafaruku, wakulima wamekuwa wakiwapiga na kuwadhuru mifugo na hata kuwapotezea uhai na kwa upande mwingine wafugaji nao wamekuwa wakivamia nyumba za wakulima kulipiza kisasi. Vita hii imekuwa haiishi, hakuna mtatatuzi kwa muda mrefu sasa.
Wakati fulani serikali nayo imekuwa ikichangia kupelekea kwenye migogoro hii badala ya kutatua, chukulia mfano uhamishwaji wa mifugo kutoka bonde la Usangu. Hakukuwa na utaratibu mzuri, wafugaji hawakuwekewa utaratibu wa kuhakisha mifugo yao inafika maeneo waliyoelekezwa bila kuleta madhara maeneo wanayopitia. Mifugo ilihitaji kusafiri ikiwa inakula kwani ilikuwa safari ndefu mno, ilihitaji siku nyingi kidogo. Lakini wafugaji hawakuelekezwa wanafikaje huko na njia za kupitia na maeneo ambayo wangekuwa wakilisha mifugo yao humo njiani pamoja na maji. Waliondolewa wakiwa hawajajipanga na hata hawakujua wakifika huko utaratibu wa kuanza maisha utakuwaje huko. Hivyo walikuwa na hofu na ndo maana wengine badala ya kwenda huko waliweka makazi njiani na kusababisha migogoro na wakazi wa maeneo hayo. Moja ya maeneo hayo ilikuwa ni Pawaga huko Iringa na Kilosa huko Morogoro.
Serikali bila ya kufikiri kwa kina waliwatoza faini wafugaji hao walioweka makazi njiani tena fani kubwa. Wafugaji wengi walipoteza mifugo yao njia kwa kuuza walipe faini, mingine ilipotea na mingine ilikufa. Kimsingi uhamaji ule haukuwa na manufaa kwa mfugaji zaidi ya serikali pamoja na mkulima. Wafugaji walijiona kama hawana msaada maana serikali iliwatelekeza na hata kuwanyanyasa sana walipokutwa wameweka makazi njiani. Wafugaji hawakupewa fidia kwa uhamishwaji ule ukizingati waliondolewa kwa nguvu na serikali.
Lakini hata katika maeneo ambapo wafugaji wameamua kuweka makazi yao ya kudumu, hawatengewi maeneo ya kulishia wanyama wao. Samani kubwa ipo kwa wakulima zaidi, wafugaji wanaweza wakatengewa maeneo lakini yasiwe na maji ya kunyweshea mifugo. Kwa vyovyote vile watahitaji kufunga safari kwenda kutafuta maji sehemu za mbali. Na hapo ndipo wanaweza pitisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima kwa maana njia haijatengwa kwa ajili ya mifugo yao.
Tuesday, March 3, 2015
CHANZO CHA MIGOGORO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment